Mke wangu amekutwa HIV+

Mke wangu amekutwa HIV+

Ulifanya kosa kubwa sana kutokumtombra kwa kipindi chote hicho pole sana.kama unampenda utashea nae vidonge akiend Kuchua akuchukulie na wewe, ukimtreat vibaya atajiua so kaa nae vizur
 
Habari za wakati huu JF?

Ndugu zangu Nina kisa cha kusikitisha ambacho ningependa kupata mawazo kutoka kwenu.

Nitajitahidi kuandika Kwa ufupi kadiri iwezekanavyo. Jitahidi tu usome upate cha kuniambia Yani.

Iko hivi, ninaishi na binti ambaye tumebahatika kupata mtoto mmoja wa mwaka na miezi miwili sasa.

Kisa chenyewe ni kwamba Tangu mwenzangu Huyu akiwa mjamzito wa miezi mitano (April/2020) sikuwahi kushiriki naye mapenzi hata romance yaani Hadi hivi leo mtoto ana mwaka mmoja na miezi miwili. Hii ilikuwa ni kumfanya apate nafasi ya kupumzika Hadi atakapojifungua, na hili tulikubaliana kabisa.

Sasa miezi kadhaa baada ya kujifungua bado akawa hataki hata nimguse yani. Alikuwa anasema ni Kwa sababu Hana hisia kabisa za mapenzi kutokana na kumbukumbu za maumivu wakati wa kujifungua. ( Ikumbukwe alijifungua kawaida kabisa uzao wake huu wa kwanza). Kutokana na Mimi kuwa mtu wa kusafiri huku na kule kutafuta riziki sikuwa na nafasi yakuweza kujua mienendo yake nikiwa mbali. (Yeye ni mwalimu wa primary school).

Hali imeendelea hivyo,, hataki kabisa hata nimguse. Ukimgusa tu ni ugomvi mkubwa. Sasa Kama mwezi mmoja umepita nilitoka kwenye mishe zangu huko kusini mwa nchi yetu,, nikiwa home jioni moja nikaona anameza dawa ambazo sikuwahi ziona kabla, nikashtuka kidogo maana alikuwa anameza Kwa kuibia hivi! Nikamuuliza vipi unaumwa? Akajibu ni kichwa ndo maana anameza paracetamol. Lakini ukweli hazikuwa paracetamol! Nikasubiri nilipopata nafasi kuziangalia zile dawa nikakuta ni " ISONIAZID" ambazo haraka niliingia mtandaoni nikagundua ni za Tuberculosis (TB).

Nilipomuuliza akasema walipita watu shuleni kwao ( yeye ni mwalimu) wanagawa eti wamepewa Kama prevention! Kama wanavyofanyaga Kwa dawa za minyoo n.k

Japo nilishashutuka,, nikaamua kukaa kimya kwanza ili nisivuruge uchunguzi wa kina. Sasa wiki iliyopita tukiwa tumelala usiku (taa zinawaka chumbani Kwa ajili ya mtoto), nilishtuka tu baada ya mtoto kuanza kulia bila Shaka ilikuwa ni njaa. Lakini mwenzangu hakushtuka labda kutokana na uchovu wa siku mzima. Hapo ndipo niliona ngozi za mapaja yake zikiwa na njano kabisa Kama ndizi mbivu!

Nikashtuka sana! Yeye aliposhtuka, baada ya muda kidogo Ile njano ikapotea akawa kawaida tu. Nikahisi labda ni Maruweruwe ya usingizi, hivyo sikumuuliza nikakausha.

Usiku uliofuata nikafanya sasa kuvizia nione Kama lilikuwa wenge au lah! Mambo yakawa vile vile! Nikasema ngoja nione tena na leo siku ya tatu,, Mambo yakawa vile vile rangi ya ngozi hasa huko mapajani ni njano kabisa na safari hii Hadi sehemu za mgongoni. Nikavunja ukimya, nikamuuliza lakini alinijibu Kwa kunibeza; "....eti haaa, mi najua umeniamsha kuna Jambo la maana kumbe ni...."

Hapo sasa akili ikanikaa nikajua rasmi anafahamu vema juu ya hilo. Asubuhi nikachelewa kutoka nyumbani lengo nifanye msako mkali labda kuna dawa Zaidi na labda anaumwa lakini anaficha..

Kwa bahati nzuri nikakutana na dawa kwenye mfuko wa kawaida tu ( zimeandikwa " LA 75". nika-googgle chap nikaambiwa ni Lamivudine! Aina mojawapo ya ARVs! Moyo ukapasuka! Nilitoka nikaenda kwanza kanisani akili itulie.

Jioni baada ya yeye kurudi nikamwita chumbani Kwa Sura ya kigaidi na mkanda mkononi,, (sikuwahi kamwe kumpiga) lakini ilibidi nivae Sura hiyo.. baada ya kumuuliza akawa mkali anabisha, nikafungua mkoba wenye hizo dawa nikamwonesha kisha nikashika vema mkanda mkononi. Kabla ya kuanza kichapo akaomba nisimpige atanieleza kila kitu. Basi Akafunguka..kwamba amegundua ameathirika huu ni mwezi wa sita sasa! Na alijua ni Mimi ndo nimemuambukiza ndiyo sababu ya kunichukia Kwa kipindi chote kile hata asitake nimguse!

Jioni hiyo hiyo nikaenda kupima,, Niko negative. Nikapita pharmacy moja hapa mjini pia nikanunua vile vipimo nikaja navyo nyumbani akanipima yeye mwenyewe maana ameshakuwa mtaalamu.. nikakuta negative pia.

Mengine yaliyoendelea siyo muhimu ,,lakini anasema hajawahi kuchepuka Kwa kipindi chote hicho. Sasa nikabaki na maswali inawezekana vipi mtu apimwe mara tatu wakati wa ujauzito awe negative, hajachepuka halafu miezi kadhaa baada ya kujifungu awe positive? Na Mimi mwenyewe sina maambukizi?!!

Hebu tieni neno wakuu. Nahisi kuvurugwa kabisa yaani. Kuhusu mtoto wanadai hawezi kupimwa Hadi afikishe miezi 18. Lakini Kwa mwonekani dogo yupo na afya njema.

Mnadhani possibility ya kuambukizwa ipo wapi Kama hakuchepuka?

Dah! Mungu nisaidie.
View attachment 1964380
Sijaelewa vizuri.... Hapa mwisho umemalizia kuwa mlinunua vipimo pharmacy mkapima na wote mkawa negative?? Sijaelewa vizuri hapo....
 
Ww uko sawa kabisa. NI HIV NEGATIVE. ACHANA KABISA NA HUYO MWANAMKE. ATAKUCHOMA HATA SINDANO YENYE VIRUSI ILI NA WW UATHIRIKE. NI MUUAJI HUYO. Inawezekana kabisa kwa mwanaume kutoambukizwa vizuri na mwanamke wake aliyeathirika kwa sababu kadhaa hivi. Moja ni ugumu wa mwanaume kupata HIV ukilinganisha na mwanamke sababu ya maumbile. Pili ni U=U kama amekuwa anatumia hizo dawa. LAKINI KAA KABISA MBALI NA HUYO AISEE. ACHANA NAYE KABISA NI MWONGO WA HATARI KABISA. ALIPEWA VVU NA MTU NA HATAKI KUKIRI HILO. AMEKUWA ANAKUDANGANYA SIKU NYINGI SANA AKIKUFICHA UKWELI.. ETI LEO ANASEMA UONGO MWINGINE KWAMBA HAJACHEPUKA NA WW UNAMWAMINI????
Kama haja chepuka basi atakuwa kazaliwa nao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona tupooo


Inshu hapa ni unakulaje??


Tena kama nyie mnaojifanya , unatongozwa mwezi mzima, jamaa anakumwagia mwagia vipesa,


Siku ukienda kumtunuki tu..na ngoma unayo


Kwa sababu, muda wote huo ulomzungusha, ulijikuta unajenga imani juu yake na kumuaminiiiiii
Hebu niambie wewe unakula kwa stail gani kuepuka huu ugonjwa
 
Nyie si ndo mnasemaga walimu na manesi ndo wife material? Imekuaje tena?
Hakuna kitu Walimu ni wahoovyo sana tena ni wahuni kuliko hata hao dada wa kona bar. Siku hizi wameibuka na wazimu wa kumiliki motokaa ni shida. Yaani ukipiga tafiti ndogo tu wengi sana ni single mama.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Tulia kwanza mkuu, umesahau kuku anapokua amekamatwa na kicheche jambo la kwanza unamuokoa kwanza mikononi mwa kicheche kisha unamuonya kwamba sio vizuri kuchunga vichakani?...acha kwanza mzuka wa vipimo vya hiv na madawa utulie. Hiyo topic nyingine iache kwanza kapteni.
Natulia

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Uzi fikirishi sana huu na stajabishi
Pole Sana kwa mkasa mkuuu muombe sana Mungu
 
Nimesoma, kuna uwezekano huyu dada watu wanamnanga na kumtusi lakini ukute ugonjwa alionao si HIV, halafu hizi rapid hata wanawake wenye ujauzito ni common sana kutokea false ve+...
mi naona aende mbele zaidi katika vipimo na pia akae aongee na mkewe kiutu uzima, sababu cha kuangalia sasa ni namna ya kutatua shida na si kulaumiana cause hakuna faida zaidi ya hasara na kumletea mtoto mazingira magumu...
Ndugu unazifahamu stages za kuconfirm diagnosis ya HIV. Mpaka kashaanzishiwa ARV uje ni HIV. Diagnosis ya HIV sio a single test.
 
Back
Top Bottom