Mke wangu amekutwa HIV+

Mke wangu amekutwa HIV+

Hapa ndiyo unaona umuhimu wa uwepo wa imani za kidini hata kama hakuna chochote baada ya kifo. Neither heaven nor Hell.

Jamaa baada ya kupatwa na mshituko, hasira na hofu kakimbilia kanisani kwanza kwenda kujipa matumaini na kujituliza kidogo ingawa sala zake hazi muhakikishii kubadili tukio baya lililomkuta kifamilia.

Religions serves as placebos to the ones who are in need or in trouble, and for emotionally weak people.

Twendeni misikitini na makanisani wadau.
Most definetely..Dini ni placebo moja kali sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kajuaje kama ni muathirika ndani ya muda mfupi ? hadi na dawa anatumia au alijua kipindi cha ujauzito ? we hukwenda nae hospital ? mengine ntauliza baada ya kujibiwa
 
Mwanamke akishajifunguwa ile arobaini ya mtoto lazima uzibuwe masikio ili mtoto asikie vizuri, yani kula mzigo hakuna cha kusubili.

Unaweza kuishi mke na mume na mkafanya tendo la ndoa kila siku lakini mkapima mmoja akaonekana hana maambukizi inatokea sana.

Kilichobaki hapa kama unampenda mkeo nenda kwa wataalam wa hizi mambo watakupa elimu ya kuishi naye bila tatizo.

Kwa sasa ugonjwa unaosumbuwa ni covid, cancer na figo.

Ukimwi umeshapitwa na wakati hauna chati tena.

Jaribu kumuuliza mgonjwa wa figo kati ys ukimwi na figo anachaguwa ugonjwa gani? Ndio utaelewa somo.
Shida pia ni kwamba ukiwa kwenye ART plan kupata shida ya figo na ini ni kawaida..

So tusiubeze sana UKIMWI..complication zake bado zinasumbua sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninavyowajua wanawake kama angekuhisi tu kwa 100% kwamba wewe ni chanzo cha hayo matatizo mpaka muda huu unapo-type hapa angekuwa ameshaitisha vikao siyo chini ya 10 upande wa familia yako na familia yake na angekutishia hata kukupeleka mahakamani,nikupe pole kwa matatizo haya na upo uwezekano hata mtoto unayelea siyo damu yako.

Mshukuru Mungu umetoka salama kama uchumi unaruhusu mpime mtoto DNA kama siyo damu yako mwambie ampelekee baba yake na huyo huyo amuowe.
 
Habari za wakati huu JF?

Ndugu zangu Nina kisa cha kusikitisha ambacho ningependa kupata mawazo kutoka kwenu.

Nitajitahidi kuandika Kwa ufupi kadiri iwezekanavyo. Jitahidi tu usome upate cha kuniambia Yani.

Iko hivi, ninaishi na binti ambaye tumebahatika kupata mtoto mmoja wa mwaka na miezi miwili sasa.

Kisa chenyewe ni kwamba Tangu mwenzangu Huyu akiwa mjamzito wa miezi mitano (April/2020) sikuwahi kushiriki naye mapenzi hata romance yaani Hadi hivi leo mtoto ana mwaka mmoja na miezi miwili. Hii ilikuwa ni kumfanya apate nafasi ya kupumzika Hadi atakapojifungua, na hili tulikubaliana kabisa.

Sasa miezi kadhaa baada ya kujifungua bado akawa hataki hata nimguse yani. Alikuwa anasema ni Kwa sababu Hana hisia kabisa za mapenzi kutokana na kumbukumbu za maumivu wakati wa kujifungua. ( Ikumbukwe alijifungua kawaida kabisa uzao wake huu wa kwanza). Kutokana na Mimi kuwa mtu wa kusafiri huku na kule kutafuta riziki sikuwa na nafasi yakuweza kujua mienendo yake nikiwa mbali. (Yeye ni mwalimu wa primary school).

Hali imeendelea hivyo,, hataki kabisa hata nimguse. Ukimgusa tu ni ugomvi mkubwa. Sasa Kama mwezi mmoja umepita nilitoka kwenye mishe zangu huko kusini mwa nchi yetu,, nikiwa home jioni moja nikaona anameza dawa ambazo sikuwahi ziona kabla, nikashtuka kidogo maana alikuwa anameza Kwa kuibia hivi! Nikamuuliza vipi unaumwa? Akajibu ni kichwa ndo maana anameza paracetamol. Lakini ukweli hazikuwa paracetamol! Nikasubiri nilipopata nafasi kuziangalia zile dawa nikakuta ni " ISONIAZID" ambazo haraka niliingia mtandaoni nikagundua ni za Tuberculosis (TB).

Nilipomuuliza akasema walipita watu shuleni kwao ( yeye ni mwalimu) wanagawa eti wamepewa Kama prevention! Kama wanavyofanyaga Kwa dawa za minyoo n.k

Japo nilishashutuka,, nikaamua kukaa kimya kwanza ili nisivuruge uchunguzi wa kina. Sasa wiki iliyopita tukiwa tumelala usiku (taa zinawaka chumbani Kwa ajili ya mtoto), nilishtuka tu baada ya mtoto kuanza kulia bila Shaka ilikuwa ni njaa. Lakini mwenzangu hakushtuka labda kutokana na uchovu wa siku mzima. Hapo ndipo niliona ngozi za mapaja yake zikiwa na njano kabisa Kama ndizi mbivu!

Nikashtuka sana! Yeye aliposhtuka, baada ya muda kidogo Ile njano ikapotea akawa kawaida tu. Nikahisi labda ni Maruweruwe ya usingizi, hivyo sikumuuliza nikakausha.

Usiku uliofuata nikafanya sasa kuvizia nione Kama lilikuwa wenge au lah! Mambo yakawa vile vile! Nikasema ngoja nione tena na leo siku ya tatu,, Mambo yakawa vile vile rangi ya ngozi hasa huko mapajani ni njano kabisa na safari hii Hadi sehemu za mgongoni. Nikavunja ukimya, nikamuuliza lakini alinijibu Kwa kunibeza; "....eti haaa, mi najua umeniamsha kuna Jambo la maana kumbe ni...."

Hapo sasa akili ikanikaa nikajua rasmi anafahamu vema juu ya hilo. Asubuhi nikachelewa kutoka nyumbani lengo nifanye msako mkali labda kuna dawa Zaidi na labda anaumwa lakini anaficha..

Kwa bahati nzuri nikakutana na dawa kwenye mfuko wa kawaida tu ( zimeandikwa " LA 75". nika-googgle chap nikaambiwa ni Lamivudine! Aina mojawapo ya ARVs! Moyo ukapasuka! Nilitoka nikaenda kwanza kanisani akili itulie.

Jioni baada ya yeye kurudi nikamwita chumbani Kwa Sura ya kigaidi na mkanda mkononi,, (sikuwahi kamwe kumpiga) lakini ilibidi nivae Sura hiyo.. baada ya kumuuliza akawa mkali anabisha, nikafungua mkoba wenye hizo dawa nikamwonesha kisha nikashika vema mkanda mkononi. Kabla ya kuanza kichapo akaomba nisimpige atanieleza kila kitu. Basi Akafunguka..kwamba amegundua ameathirika huu ni mwezi wa sita sasa! Na alijua ni Mimi ndo nimemuambukiza ndiyo sababu ya kunichukia Kwa kipindi chote kile hata asitake nimguse!

Jioni hiyo hiyo nikaenda kupima,, Niko negative. Nikapita pharmacy moja hapa mjini pia nikanunua vile vipimo nikaja navyo nyumbani akanipima yeye mwenyewe maana ameshakuwa mtaalamu.. nikakuta negative pia.

Mengine yaliyoendelea siyo muhimu ,,lakini anasema hajawahi kuchepuka Kwa kipindi chote hicho. Sasa nikabaki na maswali inawezekana vipi mtu apimwe mara tatu wakati wa ujauzito awe negative, hajachepuka halafu miezi kadhaa baada ya kujifungu awe positive? Na Mimi mwenyewe sina maambukizi?!!

Hebu tieni neno wakuu. Nahisi kuvurugwa kabisa yaani. Kuhusu mtoto wanadai hawezi kupimwa Hadi afikishe miezi 18. Lakini Kwa mwonekani dogo yupo na afya njema.

Mnadhani possibility ya kuambukizwa ipo wapi Kama hakuchepuka?

Dah! Mungu nisaidie.
View attachment 1964380
Pole sana. Nimewai siku moja kuongea na mtaharamu wa Virus na tabia zao. Aliniambia kuwa kuna case nyingi Africa watu kuonekana kuwa wana Virus vya HIV wakati sio Kweli. Hivi vipimo vya Rapid Test (un gold na jamaii yake) utoa majibu as if ni HIV+ ata kwa magonjwa mengine yaani kuna aina ya magonjwa ambayo kama mtu anayo akipima HIV ataonekana anao.Yeye kwa Ushauri alisema kuna aja Serikali ya Tanzania kuwa na mahabara mahususi ya Virology ambayo ingesaidia kuondoa kadhia hii.Yeye kwa maoni yake amesema kuna mamia ya watu wanaishi na hofu/,kula Dawa za HIV japo kiukweli awana HIV .bali ni ufinyu wa Vipimo vinavyotumika hapa nchini .Ata hapa hawa watafiti wamethibitisha hilo futialia hapa
 
Mkuu hio ya yellowish skin ni dalili ya Hepatitis, jaribuni kwenda kupima na Hepatitis...
pole sana mkuu...
 
kajuaje kama ni muathirika ndani ya muda mfupi ? hadi na dawa anatumia au alijua kipindi cha ujauzito ? we hukwenda nae hospital ? mengine ntauliza baada ya kujibiwa
Kwa maelezo yake Amegundu miezi sita iliyopita ( Yaani mwezi wa Nne huko). Miezi nane baada ya kujifungua?!
 
Hapa ndiyo unaona umuhimu wa uwepo wa imani za kidini hata kama hakuna chochote baada ya kifo. Neither heaven nor Hell.

Jamaa baada ya kupatwa na mshituko, hasira na hofu kakimbilia kanisani kwanza kwenda kujipa matumaini na kujituliza kidogo ingawa sala zake hazi muhakikishii kubadili tukio baya lililomkuta kifamilia.

Religions serves as placebos to the ones who are in need or in trouble, and for emotionally weak people.

Twendeni misikitini na makanisani wadau.
pamoja na kukimbilia huko hakuna alichopata zaid ya kupotezewa muda na kuombewa maombi ya uongo(which is useless) lkn chaajabu kaona JF ndio sehem sahihi ameomba ushaur na kwel anasaidika(sehem sahihi),/pia ilimpasa awatafte wanasaikolojia, ama wazee anaowaheshimu, hawa wangeweza pia kumpa somo na kumtia moyo..kanisa&msikit ni sehem hatar kwa maisha ya mtu(ukwel mchungu)
 
Hapana.
Kwa kufanya hivi amepunguza kidogo mzigo wa moyoni na kichwani.

Anahitaji counselling haraka sana. Anaweza kufanya kitu kibaya muda wowote.

Kuna vitu kama havijakufika unaweza usivielewe. Nilifanya tukio natamani kuongea na mwanangu wa miaka mitatu nimwelezee anishauri ( kuongea inasaidia sana) japo kuna wengine ukiwaelezea utajutia sana hicho kitendo na kuongeza maumivu.

Heaven Sent njoo utoe ushauri na Faraja huku!!!
 
Pole sana, usichukue maamuzu ya haraka kwani mwenzio baada ya kugundua kaathirika aliamua kukulinda angeweza kuhakikisha na wewe update ili muwe ngoma draw ingawa alifanya makosa kukuficha

Ktk hili hakuna excuses obviously kuna mazingira ya kuvunja uaminifu kwenye mahusiano yao aliyofanya huyu mwanamke,inaumiza sana kama mwanaume unatoka kutafuta maisha ya kesho ya familia yako huku nyuma mwanamke anafanya upumbavu huu.

Maamuzi ni muhimu yachukuliwe mapema apime mtoto kama wake siyo wake amfukuze aende kwa aliyemzalisha.
 
Back
Top Bottom