Mke wangu amekutwa HIV+

Mke wangu amekutwa HIV+

Bro muda wako ni muhimu Sana kwa Sasa ...hao wanao kuambia uchunguze Sasa uchunguze Nini.....? Huo muda nenda kafanye maisha mengine kwa ajiri ya badae yako
 
Nimesoma, kuna uwezekano huyu dada watu wanamnanga na kumtusi lakini ukute ugonjwa alionao si HIV, halafu hizi rapid hata wanawake wenye ujauzito ni common sana kutokea false ve+...
mi naona aende mbele zaidi katika vipimo na pia akae aongee na mkewe kiutu uzima, sababu cha kuangalia sasa ni namna ya kutatua shida na si kulaumiana cause hakuna faida zaidi ya hasara na kumletea mtoto mazingira magumu...

Na kweli inawezekani huyo ana Hepatitis (ambayonayo ni virus) ndio maaana amepata jaundice maana liver function imekuwa impaired.
 
Habari za wakati huu JF?

Ndugu zangu Nina kisa cha kusikitisha ambacho ningependa kupata mawazo kutoka kwenu.

Nitajitahidi kuandika Kwa ufupi kadiri iwezekanavyo. Jitahidi tu usome upate cha kuniambia Yani.

Iko hivi, ninaishi na binti ambaye tumebahatika kupata mtoto mmoja wa mwaka na miezi miwili sasa.

Kisa chenyewe ni kwamba Tangu mwenzangu Huyu akiwa mjamzito wa miezi mitano (April/2020) sikuwahi kushiriki naye mapenzi hata romance yaani Hadi hivi leo mtoto ana mwaka mmoja na miezi miwili. Hii ilikuwa ni kumfanya apate nafasi ya kupumzika Hadi atakapojifungua, na hili tulikubaliana kabisa.

Sasa miezi kadhaa baada ya kujifungua bado akawa hataki hata nimguse yani. Alikuwa anasema ni Kwa sababu Hana hisia kabisa za mapenzi kutokana na kumbukumbu za maumivu wakati wa kujifungua. ( Ikumbukwe alijifungua kawaida kabisa uzao wake huu wa kwanza). Kutokana na Mimi kuwa mtu wa kusafiri huku na kule kutafuta riziki sikuwa na nafasi yakuweza kujua mienendo yake nikiwa mbali. (Yeye ni mwalimu wa primary school).

Hali imeendelea hivyo,, hataki kabisa hata nimguse. Ukimgusa tu ni ugomvi mkubwa. Sasa Kama mwezi mmoja umepita nilitoka kwenye mishe zangu huko kusini mwa nchi yetu,, nikiwa home jioni moja nikaona anameza dawa ambazo sikuwahi ziona kabla, nikashtuka kidogo maana alikuwa anameza Kwa kuibia hivi! Nikamuuliza vipi unaumwa? Akajibu ni kichwa ndo maana anameza paracetamol. Lakini ukweli hazikuwa paracetamol! Nikasubiri nilipopata nafasi kuziangalia zile dawa nikakuta ni " ISONIAZID" ambazo haraka niliingia mtandaoni nikagundua ni za Tuberculosis (TB).

Nilipomuuliza akasema walipita watu shuleni kwao ( yeye ni mwalimu) wanagawa eti wamepewa Kama prevention! Kama wanavyofanyaga Kwa dawa za minyoo n.k

Japo nilishashutuka,, nikaamua kukaa kimya kwanza ili nisivuruge uchunguzi wa kina. Sasa wiki iliyopita tukiwa tumelala usiku (taa zinawaka chumbani Kwa ajili ya mtoto), nilishtuka tu baada ya mtoto kuanza kulia bila Shaka ilikuwa ni njaa. Lakini mwenzangu hakushtuka labda kutokana na uchovu wa siku mzima. Hapo ndipo niliona ngozi za mapaja yake zikiwa na njano kabisa Kama ndizi mbivu!

Nikashtuka sana! Yeye aliposhtuka, baada ya muda kidogo Ile njano ikapotea akawa kawaida tu. Nikahisi labda ni Maruweruwe ya usingizi, hivyo sikumuuliza nikakausha.

Usiku uliofuata nikafanya sasa kuvizia nione Kama lilikuwa wenge au lah! Mambo yakawa vile vile! Nikasema ngoja nione tena na leo siku ya tatu,, Mambo yakawa vile vile rangi ya ngozi hasa huko mapajani ni njano kabisa na safari hii Hadi sehemu za mgongoni. Nikavunja ukimya, nikamuuliza lakini alinijibu Kwa kunibeza; "....eti haaa, mi najua umeniamsha kuna Jambo la maana kumbe ni...."

Hapo sasa akili ikanikaa nikajua rasmi anafahamu vema juu ya hilo. Asubuhi nikachelewa kutoka nyumbani lengo nifanye msako mkali labda kuna dawa Zaidi na labda anaumwa lakini anaficha..

Kwa bahati nzuri nikakutana na dawa kwenye mfuko wa kawaida tu ( zimeandikwa " LA 75". nika-googgle chap nikaambiwa ni Lamivudine! Aina mojawapo ya ARVs! Moyo ukapasuka! Nilitoka nikaenda kwanza kanisani akili itulie.

Jioni baada ya yeye kurudi nikamwita chumbani Kwa Sura ya kigaidi na mkanda mkononi,, (sikuwahi kamwe kumpiga) lakini ilibidi nivae Sura hiyo.. baada ya kumuuliza akawa mkali anabisha, nikafungua mkoba wenye hizo dawa nikamwonesha kisha nikashika vema mkanda mkononi. Kabla ya kuanza kichapo akaomba nisimpige atanieleza kila kitu. Basi Akafunguka..kwamba amegundua ameathirika huu ni mwezi wa sita sasa! Na alijua ni Mimi ndo nimemuambukiza ndiyo sababu ya kunichukia Kwa kipindi chote kile hata asitake nimguse!

Jioni hiyo hiyo nikaenda kupima,, Niko negative. Nikapita pharmacy moja hapa mjini pia nikanunua vile vipimo nikaja navyo nyumbani akanipima yeye mwenyewe maana ameshakuwa mtaalamu.. nikakuta negative pia.

Mengine yaliyoendelea siyo muhimu ,,lakini anasema hajawahi kuchepuka Kwa kipindi chote hicho. Sasa nikabaki na maswali inawezekana vipi mtu apimwe mara tatu wakati wa ujauzito awe negative, hajachepuka halafu miezi kadhaa baada ya kujifungu awe positive? Na Mimi mwenyewe sina maambukizi?!!

Hebu tieni neno wakuu. Nahisi kuvurugwa kabisa yaani. Kuhusu mtoto wanadai hawezi kupimwa Hadi afikishe miezi 18. Lakini Kwa mwonekani dogo yupo na afya njema.

Mnadhani possibility ya kuambukizwa ipo wapi Kama hakuchepuka?

Dah! Mungu nisaidie.
View attachment 1964380
I am very sorry.....yataisha
 
Uwiiiiii Moyo wanguuu mimi... Polee kakaa. Ila sector ya Elimu na Ulinzi huwa siamini kabisa hawa watu...
 
Mshukuru sana huyo mwanamke kukukazia kitobo manunda wangepiga kimya tu upambane na hali yako. Inamaanisha ana kupenda ama bado ana utu/ ubinadamu.. Chochote utakachoamua busara itumike kuliko hasira..
 
Labda ushauri wangu unawez kuw umechelewa ila la kwanza kubwa embu

muonyeshe upeupendo na shukran kwakuw alichepuka na alijigundua kuw n HIV+ ,hakukuuzia mechi ambayo lazm ingekuumza wew

Kwa sasa nazan umeshafany maamuz fulan na maisha yanaendelea

Tuwe makn wandugu.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Mpime na mtoto Dna kama ni wako kweli huna mke hapo ukijiona kwenye maisha hujatulia ni mtu wa kusafiri safiri tena muda mrefu bora uendelee kuwa single
 
Comment zingine ni za kujiaibisha,yaani kupitia comment mtu anaeza jua we ni aina gani
Yes! Unapofungua mdomo unaongea kuwa makini Sana Mana unayatoa yaliyo moyoni mwako ama they describe you,they tell us who are you,what kind of person are you , zamani watu waliishi kijamaa karibu kusaka Ile human comfort ili wakivamiwa na wanyama iwe rahisi kumchangia na kumshinda.
Nowdays hizi Teknlojia zimetutenganisha na ingawa tunaishi hata nyumba moja Ila ila Ile humanity bond imelegea Sana.
Unaenda kumsalimia mtu anawakuwashia tv ama redio iku keep busy Mana Hana Cha kuongea na wewe.
Binafsi kwangu Sina tv Ila Nina library ya vitabu mbalimbali.

Yaani natumia muda mwingi Sana kwa simu sema nakuwa najisomea kuliko natumia na wanangu Ila Kuna muda naiweka pembeni tunacheza pamoja na kufanya mazoezi pamoja kidogo Ina create bond.
Nowdays mtt 4yrs eti boarding school Ila hakuna namna.
Am seeking personal freedom a lot and financial freedom
 
Habari za wakati huu JF?

Ndugu zangu Nina kisa cha kusikitisha ambacho ningependa kupata mawazo kutoka kwenu.

Nitajitahidi kuandika Kwa ufupi kadiri iwezekanavyo. Jitahidi tu usome upate cha kuniambia Yani.

Iko hivi, ninaishi na binti ambaye tumebahatika kupata mtoto mmoja wa mwaka na miezi miwili sasa.

Kisa chenyewe ni kwamba Tangu mwenzangu Huyu akiwa mjamzito wa miezi mitano (April/2020) sikuwahi kushiriki naye mapenzi hata romance yaani Hadi hivi leo mtoto ana mwaka mmoja na miezi miwili. Hii ilikuwa ni kumfanya apate nafasi ya kupumzika Hadi atakapojifungua, na hili tulikubaliana kabisa.

Sasa miezi kadhaa baada ya kujifungua bado akawa hataki hata nimguse yani. Alikuwa anasema ni Kwa sababu Hana hisia kabisa za mapenzi kutokana na kumbukumbu za maumivu wakati wa kujifungua. ( Ikumbukwe alijifungua kawaida kabisa uzao wake huu wa kwanza). Kutokana na Mimi kuwa mtu wa kusafiri huku na kule kutafuta riziki sikuwa na nafasi yakuweza kujua mienendo yake nikiwa mbali. (Yeye ni mwalimu wa primary school).

Hali imeendelea hivyo,, hataki kabisa hata nimguse. Ukimgusa tu ni ugomvi mkubwa. Sasa Kama mwezi mmoja umepita nilitoka kwenye mishe zangu huko kusini mwa nchi yetu,, nikiwa home jioni moja nikaona anameza dawa ambazo sikuwahi ziona kabla, nikashtuka kidogo maana alikuwa anameza Kwa kuibia hivi! Nikamuuliza vipi unaumwa? Akajibu ni kichwa ndo maana anameza paracetamol. Lakini ukweli hazikuwa paracetamol! Nikasubiri nilipopata nafasi kuziangalia zile dawa nikakuta ni " ISONIAZID" ambazo haraka niliingia mtandaoni nikagundua ni za Tuberculosis (TB).

Nilipomuuliza akasema walipita watu shuleni kwao ( yeye ni mwalimu) wanagawa eti wamepewa Kama prevention! Kama wanavyofanyaga Kwa dawa za minyoo n.k

Japo nilishashutuka,, nikaamua kukaa kimya kwanza ili nisivuruge uchunguzi wa kina. Sasa wiki iliyopita tukiwa tumelala usiku (taa zinawaka chumbani Kwa ajili ya mtoto), nilishtuka tu baada ya mtoto kuanza kulia bila Shaka ilikuwa ni njaa. Lakini mwenzangu hakushtuka labda kutokana na uchovu wa siku mzima. Hapo ndipo niliona ngozi za mapaja yake zikiwa na njano kabisa Kama ndizi mbivu!

Nikashtuka sana! Yeye aliposhtuka, baada ya muda kidogo Ile njano ikapotea akawa kawaida tu. Nikahisi labda ni Maruweruwe ya usingizi, hivyo sikumuuliza nikakausha.

Usiku uliofuata nikafanya sasa kuvizia nione Kama lilikuwa wenge au lah! Mambo yakawa vile vile! Nikasema ngoja nione tena na leo siku ya tatu,, Mambo yakawa vile vile rangi ya ngozi hasa huko mapajani ni njano kabisa na safari hii Hadi sehemu za mgongoni. Nikavunja ukimya, nikamuuliza lakini alinijibu Kwa kunibeza; "....eti haaa, mi najua umeniamsha kuna Jambo la maana kumbe ni...."

Hapo sasa akili ikanikaa nikajua rasmi anafahamu vema juu ya hilo. Asubuhi nikachelewa kutoka nyumbani lengo nifanye msako mkali labda kuna dawa Zaidi na labda anaumwa lakini anaficha..

Kwa bahati nzuri nikakutana na dawa kwenye mfuko wa kawaida tu ( zimeandikwa " LA 75". nika-googgle chap nikaambiwa ni Lamivudine! Aina mojawapo ya ARVs! Moyo ukapasuka! Nilitoka nikaenda kwanza kanisani akili itulie.

Jioni baada ya yeye kurudi nikamwita chumbani Kwa Sura ya kigaidi na mkanda mkononi,, (sikuwahi kamwe kumpiga) lakini ilibidi nivae Sura hiyo.. baada ya kumuuliza akawa mkali anabisha, nikafungua mkoba wenye hizo dawa nikamwonesha kisha nikashika vema mkanda mkononi. Kabla ya kuanza kichapo akaomba nisimpige atanieleza kila kitu. Basi Akafunguka..kwamba amegundua ameathirika huu ni mwezi wa sita sasa! Na alijua ni Mimi ndo nimemuambukiza ndiyo sababu ya kunichukia Kwa kipindi chote kile hata asitake nimguse!

Jioni hiyo hiyo nikaenda kupima,, Niko negative. Nikapita pharmacy moja hapa mjini pia nikanunua vile vipimo nikaja navyo nyumbani akanipima yeye mwenyewe maana ameshakuwa mtaalamu.. nikakuta negative pia.

Mengine yaliyoendelea siyo muhimu ,,lakini anasema hajawahi kuchepuka Kwa kipindi chote hicho. Sasa nikabaki na maswali inawezekana vipi mtu apimwe mara tatu wakati wa ujauzito awe negative, hajachepuka halafu miezi kadhaa baada ya kujifungu awe positive? Na Mimi mwenyewe sina maambukizi?!!

Hebu tieni neno wakuu. Nahisi kuvurugwa kabisa yaani. Kuhusu mtoto wanadai hawezi kupimwa Hadi afikishe miezi 18. Lakini Kwa mwonekani dogo yupo na afya njema.

Mnadhani possibility ya kuambukizwa ipo wapi Kama hakuchepuka?

Dah! Mungu nisaidie.
View attachment 1964380
Muongo huyo. Anajua alikolitoa hilo jinamizi

Angekutilia shaka kuwa wewe ndiye umemwambukiza, siku hiyo hiyo aliyopimwa na kubainika kuwa yu + nyumbani pasingekalika.

Vumilia mkuu hayo ndiyo matokeo ya kuoa mke mwenye uzoefu wa ngono. Huwa hawawasahau waanzilishi.
 
Back
Top Bottom