Mke wangu amekutwa HIV+

Mke wangu amekutwa HIV+

Pole sana mkuu kitu cha maana apo unatakiwa ww ndo uwe faraja yake kwa mda huu mpe moyo ili akukuzie mtoto na malengo yake yatimie

huu sio wakati wa kujilaumu mpe nafasi na ushauri ili awe huru kuihudumia afya yake bila kikwazo kutoka kwako

zingatia ushauri wa wataalamu na epuka ushauri wa mitaani

na mwisho mshukuru Mungu kwa kukuepusha na hili huku ukijipanga kwa yajayo
 
Habari za wakati huu JF?

Ndugu zangu Nina kisa cha kusikitisha ambacho ningependa kupata mawazo kutoka kwenu.

Nitajitahidi kuandika Kwa ufupi kadiri iwezekanavyo. Jitahidi tu usome upate cha kuniambia Yani.

Iko hivi, ninaishi na binti ambaye tumebahatika kupata mtoto mmoja wa mwaka na miezi miwili sasa.

Kisa chenyewe ni kwamba Tangu mwenzangu Huyu akiwa mjamzito wa miezi mitano (April/2020) sikuwahi kushiriki naye mapenzi hata romance yaani Hadi hivi leo mtoto ana mwaka mmoja na miezi miwili. Hii ilikuwa ni kumfanya apate nafasi ya kupumzika Hadi atakapojifungua, na hili tulikubaliana kabisa.

Sasa miezi kadhaa baada ya kujifungua bado akawa hataki hata nimguse yani. Alikuwa anasema ni Kwa sababu Hana hisia kabisa za mapenzi kutokana na kumbukumbu za maumivu wakati wa kujifungua. ( Ikumbukwe alijifungua kawaida kabisa uzao wake huu wa kwanza). Kutokana na Mimi kuwa mtu wa kusafiri huku na kule kutafuta riziki sikuwa na nafasi yakuweza kujua mienendo yake nikiwa mbali. (Yeye ni mwalimu wa primary school).

Hali imeendelea hivyo,, hataki kabisa hata nimguse. Ukimgusa tu ni ugomvi mkubwa. Sasa Kama mwezi mmoja umepita nilitoka kwenye mishe zangu huko kusini mwa nchi yetu,, nikiwa home jioni moja nikaona anameza dawa ambazo sikuwahi ziona kabla, nikashtuka kidogo maana alikuwa anameza Kwa kuibia hivi! Nikamuuliza vipi unaumwa? Akajibu ni kichwa ndo maana anameza paracetamol. Lakini ukweli hazikuwa paracetamol! Nikasubiri nilipopata nafasi kuziangalia zile dawa nikakuta ni " ISONIAZID" ambazo haraka niliingia mtandaoni nikagundua ni za Tuberculosis (TB).

Nilipomuuliza akasema walipita watu shuleni kwao ( yeye ni mwalimu) wanagawa eti wamepewa Kama prevention! Kama wanavyofanyaga Kwa dawa za minyoo n.k

Japo nilishashutuka,, nikaamua kukaa kimya kwanza ili nisivuruge uchunguzi wa kina. Sasa wiki iliyopita tukiwa tumelala usiku (taa zinawaka chumbani Kwa ajili ya mtoto), nilishtuka tu baada ya mtoto kuanza kulia bila Shaka ilikuwa ni njaa. Lakini mwenzangu hakushtuka labda kutokana na uchovu wa siku mzima. Hapo ndipo niliona ngozi za mapaja yake zikiwa na njano kabisa Kama ndizi mbivu!

Nikashtuka sana! Yeye aliposhtuka, baada ya muda kidogo Ile njano ikapotea akawa kawaida tu. Nikahisi labda ni Maruweruwe ya usingizi, hivyo sikumuuliza nikakausha.

Usiku uliofuata nikafanya sasa kuvizia nione Kama lilikuwa wenge au lah! Mambo yakawa vile vile! Nikasema ngoja nione tena na leo siku ya tatu,, Mambo yakawa vile vile rangi ya ngozi hasa huko mapajani ni njano kabisa na safari hii Hadi sehemu za mgongoni. Nikavunja ukimya, nikamuuliza lakini alinijibu Kwa kunibeza; "....eti haaa, mi najua umeniamsha kuna Jambo la maana kumbe ni...."

Hapo sasa akili ikanikaa nikajua rasmi anafahamu vema juu ya hilo. Asubuhi nikachelewa kutoka nyumbani lengo nifanye msako mkali labda kuna dawa Zaidi na labda anaumwa lakini anaficha..

Kwa bahati nzuri nikakutana na dawa kwenye mfuko wa kawaida tu ( zimeandikwa " LA 75". nika-googgle chap nikaambiwa ni Lamivudine! Aina mojawapo ya ARVs! Moyo ukapasuka! Nilitoka nikaenda kwanza kanisani akili itulie.

Jioni baada ya yeye kurudi nikamwita chumbani Kwa Sura ya kigaidi na mkanda mkononi,, (sikuwahi kamwe kumpiga) lakini ilibidi nivae Sura hiyo.. baada ya kumuuliza akawa mkali anabisha, nikafungua mkoba wenye hizo dawa nikamwonesha kisha nikashika vema mkanda mkononi. Kabla ya kuanza kichapo akaomba nisimpige atanieleza kila kitu. Basi Akafunguka..kwamba amegundua ameathirika huu ni mwezi wa sita sasa! Na alijua ni Mimi ndo nimemuambukiza ndiyo sababu ya kunichukia Kwa kipindi chote kile hata asitake nimguse!

Jioni hiyo hiyo nikaenda kupima,, Niko negative. Nikapita pharmacy moja hapa mjini pia nikanunua vile vipimo nikaja navyo nyumbani akanipima yeye mwenyewe maana ameshakuwa mtaalamu.. nikakuta negative pia.

Mengine yaliyoendelea siyo muhimu ,,lakini anasema hajawahi kuchepuka Kwa kipindi chote hicho. Sasa nikabaki na maswali inawezekana vipi mtu apimwe mara tatu wakati wa ujauzito awe negative, hajachepuka halafu miezi kadhaa baada ya kujifungu awe positive? Na Mimi mwenyewe sina maambukizi?!!

Hebu tieni neno wakuu. Nahisi kuvurugwa kabisa yaani. Kuhusu mtoto wanadai hawezi kupimwa Hadi afikishe miezi 18. Lakini Kwa mwonekani dogo yupo na afya njema.

Mnadhani possibility ya kuambukizwa ipo wapi Kama hakuchepuka?

Dah! Mungu nisaidie.
View attachment 1964380
Hayo mapaja ya njano ni njano iliyokolea au iliyofifia?

I mean ni njano ile ya jezi ya Yanga au ya CCM?

Pole Mkuu ila sikuwahi kujua kuwa hiyo yellowish kwny mapajaz ni dalili pia ya HIV
 
kajuaje kama ni muathirika ndani ya muda mfupi ? hadi na dawa anatumia au alijua kipindi cha ujauzito ? we hukwenda nae hospital ? mengine ntauliza baada ya kujibiwa
Hata mimi nimewaza namna hii halafu mpaka dawa zianze kubadilisha rangi ya ngozi sio issue ya miezi huwa Inachukua muda hapo kuna mawili huyo dada ameupata muda mrefu na ameanza kutumia Dawa siku nyingi Ila huenda jamaa damu yake haiwezi kupata virus majibu sahihi yatapatikana wakimpima mtoto

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Ninavyowajua wanawake kama angekuhisi tu kwa 100% kwamba wewe ni chanzo cha hayo matatizo mpaka muda huu unapo-type hapa angekuwa ameshaitisha vikao siyo chini ya 10 upande wa familia yako na familia yake na angekutishia hata kukupeleka mahakamani,nikupe pole kwa matatizo haya na upo uwezekano hata mtoto unayelea siyo damu yako.

Mshukuru Mungu umetoka salama kama uchumi unaruhusu mpime mtoto DNA kama siyo damu yako mwambie ampelekee baba yake na huyo huyo amuowe.
Huu ndio ukweli

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Kwa maelezo yake Amegundu miezi sita iliyopita ( Yaani mwezi wa Nne huko). Miezi nane baada ya kujifungua?!
Sio kweli ndugu itakuwa ni muda mrefu halafu kawaida ya hizo dawa mpaka ifikie hatua yakumbadilisha ngozi ameanza kutumia muda mrefu sema labda ww damu yako haishiki virus

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Uliposema wyf wako ni mwalimu wa shule ya msingi nikasimama kusoma story nikaja kukomenti kwanza. Infwakiti waalimu wana muda mwingi wa kupumzika baada ya kazi licha ya idadi kubwa ya wanafunzi na uchache wa vifaa kazi katika utendaji wa kazi zao ambao unaweza waweka bize masaa hata ya ziada. Lakini ukweli ni kwamba waalimu wa Tanzania wapo free sana.
 
Kuna dadaangu,hadi tarehe ya harusi ilipangwa,baada ya wiki moja ya ndoa,mama wa bidada akasema hapa mkapime kwanza yaani alikuwa amuamini mkaka...........oooooh kwenda kupima,bidada kakutwa nao mkaka yupo safi......asee mdada alilia balaa,akamwambia mkaka tufunge ndoa tu nikakae ata wiki moja nitudi ngumbanmkaka alijaza no ndoa,japo alitoa kila kitu alisamehe.
Heheheheh hii ilikuwa kasheshe na huyo maza nae duh😅 sahizi atakuwa wanalia na mwanae hapo nyumbani😅
 
Na huyo mwanamke kwa kumsaidia, mwambie wabadilishe madawa. Hayo madawa yanaharibu Liver (maini) yake. Yanamuongezea bilirubin mwilini ambayo inaharibu zaidi maini. Na ndio maana ni wa njano hivyo kwa ngozi. Baadhi ya Hizo dawa za ARVs yani zina side effects mbaya sana sana acha tu. Atapata liver failure mwisho wa siku. Wamtafutie madawa mengine mbadala.
Asee huu ugonjwa dawa zinakuua taratibu kupitia organ failures! Ukiacha dawa nayo wanasema hutoboi dah! Mchana tochi usiku magogo.
 
Kuna rafiki yangu alikuwa anamchumbia binti ikafika mda wa harusi ,Kama kawaida kuna baadhi ya makanisa huwezi kufunga bila vipimo,jamaa akaonekana ameathirika,akaachwa na mwanamke hapo hapo ,jamaa kidogo afe kwa mawazo ,baada ya Kama miezi 6 akapima tena ikaonekana hajaathirika ,akafululiza kupima kila baada ya miezi 3 jamaa bado anaonekana si mwathirika .
Mbwa kala mbwa... Mizimu au Mungu wa jamaa alimuokoa na huyo jinamizi alietaka kumuoa.... Hehehehehehe... Dadeki... Maisha bana Yana namna yake yakufanya miujiza yake.

Sent from my GIONEE S11 lite using JamiiForums mobile app
 
Cha kushangaza baada ya Kama miezi 6 msichana akaolewa na jamaa mwingine ,hiyo kidogo ilitushtua kwamba imekwaje gafla hivo ,inawezekana maruweruwe au daktari katoa vipimo feki
Au dokta kapewa hongo, Ili jamaa mwengine abebe mzigo. Everything and anything is possible

Sent from my GIONEE S11 lite using JamiiForums mobile app
 
Kuna dadaangu,hadi tarehe ya harusi ilipangwa,baada ya wiki moja ya ndoa,mama wa bidada akasema hapa mkapime kwanza yaani alikuwa amuamini mkaka...........oooooh kwenda kupima,bidada kakutwa nao mkaka yupo safi......asee mdada alilia balaa,akamwambia mkaka tufunge ndoa tu nikakae ata wiki moja nitudi ngumbanmkaka alijaza no ndoa,japo alitoa kila kitu alisamehe.
Hatari tupu

Sent from my GIONEE S11 lite using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom