Mke wangu amekutwa HIV+

Mke wangu amekutwa HIV+

Ilikuwa aibu kubwa,maana harusi ilishatangazwa kwa jamiijamii utaidanganya vipi ikuelewe?

Bi dada kalia weeh hadi amezoea.
Harusi kwahio ilikuwa cancelled na michango mkarudisha ama? Hio ni pigo kubwa kisaikolojia aisee😅 kwahio aliona bora hata aolewe week tu ilimradi kuondoa gundu jmaa akachomoa
 
Harusi kwahio ilikuwa cancelled na michango mkarudisha ama? Hio ni pigo kubwa kisaikolojia aisee kwahio aliona bora hata aolewe week tu ilimradi kuondoa gundu jmaa akachomoa
Harusi ilifutwa...michango haikurudishwa

Mdada alikuwa anataka akaishi japo wiki kuficha iwe siri,watu tusijue kama kaathirika,lakini mwanaume akachomoa

,,,,huyo mwanaume sasa alikuwa anamtangaza bi dada balaa

Maana mama wa bi dada,alifosi wakapime,alikuwa na mashaka na mkaka labda anao
 
Harusi ilifutwa...michango haikurudishwa

Mdada alikuwa anataka akaishi japo wiki kuficha iwe siri,watu tusijue kama kaathirika,lakini mwanaume akachomoa

,,,,huyo mwanaume sasa alikuwa anamtangaza bi dada balaa

Maana mama wa bi dada,alifosi wakapime,alikuwa na mashaka na mkaka labda anao
Dah hii kiboko aisee
 
brother wait for three months ukapime tena! sina la kusema, pole ndugu ndo ya dunia..
 
Pole sana kaka huo ni mtihani ila sekta ya Elimu na Maaskari ni janga la taifa ki ukweli hawana tofauti na wafanya Scrub wa Saloon.
Hawa watu wa saloon ni noma sana, Kuna mmoja nilimpata nikamshaur tupime kwanza, weee alikuwa mkali balaa! hataki kusikia Mambo ya kupima

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana Mkuu hzo ni changamoto tu unaptia kikubwa huyo mwanamke alitakiwa kukuweka waz kwamba tayar yeye anatumia dawa sababu ni vitu vya kawaida tu

Mfano mim na miaka 17 natumia ARVs tangu kuzaliwa na najikubal na kujpenda sana
Binafsi nilikuwa nafikiria hichi kitu, inawezekana binti alizaliwa na HIV toka kwa Mama yake na amekuwa nayo wakati wote ndio maana haikumshtua, pia huenda alianza kunywa dawa muda mrefu, nina kesi ya mtoto wa mdogo wangu ambaye alizaliwa HIV Positive,mpaka leo anatumia ARV na yuko sekondari anendelea vizuri ukimuona huwezi kuamini kuwa ni mgonjwa.
 
Pole sana
Ila na wewe ulikaa muda mrefu bila kushiriki tendo wakati ana mimba hiyo pia ni changamoto.
Kuna Rafik yangu mmoja alikuwa anamla dada wa saloon alikuwa ana mimba, mmeo mwenye mimba alikuwa ashiriki tenda kuogopa mimba isije kuaharibika.
Mdada anajipeleka mwenye kwa mchepuko wake, michepuko wanapiga kavu kavu wanawaamni sana wanawake walioolewa
Tena ukipiga wakati wa mimba unamsaidia kutanua njia, ukisusa wahuni wanamkunja na mimba yake
 
Ukimwi uko manageable,aisee bora ukimwi kuliko kisukari au sijui moyo au figo utajuta..

Shida ya ngoma ni vile watu wanakunyanyapaa but ukipata elimu sahihi sio kesi Sana.
Hiv mnaongeaga kwa sifa au....hiv ukimwi ni ugonjwa wa kuchkulia poa kihivyo mkuu..daah..ukimw ni hatar ndugu..yaan acha kabisa huo ugonjwa haufai
 
Duh
Habari za wakati huu JF?

Ndugu zangu Nina kisa cha kusikitisha ambacho ningependa kupata mawazo kutoka kwenu.

Nitajitahidi kuandika Kwa ufupi kadiri iwezekanavyo. Jitahidi tu usome upate cha kuniambia Yani.

Iko hivi, ninaishi na binti ambaye tumebahatika kupata mtoto mmoja wa mwaka na miezi miwili sasa.

Kisa chenyewe ni kwamba Tangu mwenzangu Huyu akiwa mjamzito wa miezi mitano (April/2020) sikuwahi kushiriki naye mapenzi hata romance yaani Hadi hivi leo mtoto ana mwaka mmoja na miezi miwili. Hii ilikuwa ni kumfanya apate nafasi ya kupumzika Hadi atakapojifungua, na hili tulikubaliana kabisa.

Sasa miezi kadhaa baada ya kujifungua bado akawa hataki hata nimguse yani. Alikuwa anasema ni Kwa sababu Hana hisia kabisa za mapenzi kutokana na kumbukumbu za maumivu wakati wa kujifungua. ( Ikumbukwe alijifungua kawaida kabisa uzao wake huu wa kwanza). Kutokana na Mimi kuwa mtu wa kusafiri huku na kule kutafuta riziki sikuwa na nafasi yakuweza kujua mienendo yake nikiwa mbali. (Yeye ni mwalimu wa primary school).

Hali imeendelea hivyo,, hataki kabisa hata nimguse. Ukimgusa tu ni ugomvi mkubwa. Sasa Kama mwezi mmoja umepita nilitoka kwenye mishe zangu huko kusini mwa nchi yetu,, nikiwa home jioni moja nikaona anameza dawa ambazo sikuwahi ziona kabla, nikashtuka kidogo maana alikuwa anameza Kwa kuibia hivi! Nikamuuliza vipi unaumwa? Akajibu ni kichwa ndo maana anameza paracetamol. Lakini ukweli hazikuwa paracetamol! Nikasubiri nilipopata nafasi kuziangalia zile dawa nikakuta ni " ISONIAZID" ambazo haraka niliingia mtandaoni nikagundua ni za Tuberculosis (TB).

Nilipomuuliza akasema walipita watu shuleni kwao ( yeye ni mwalimu) wanagawa eti wamepewa Kama prevention! Kama wanavyofanyaga Kwa dawa za minyoo n.k

Japo nilishashutuka,, nikaamua kukaa kimya kwanza ili nisivuruge uchunguzi wa kina. Sasa wiki iliyopita tukiwa tumelala usiku (taa zinawaka chumbani Kwa ajili ya mtoto), nilishtuka tu baada ya mtoto kuanza kulia bila Shaka ilikuwa ni njaa. Lakini mwenzangu hakushtuka labda kutokana na uchovu wa siku mzima. Hapo ndipo niliona ngozi za mapaja yake zikiwa na njano kabisa Kama ndizi mbivu!

Nikashtuka sana! Yeye aliposhtuka, baada ya muda kidogo Ile njano ikapotea akawa kawaida tu. Nikahisi labda ni Maruweruwe ya usingizi, hivyo sikumuuliza nikakausha.

Usiku uliofuata nikafanya sasa kuvizia nione Kama lilikuwa wenge au lah! Mambo yakawa vile vile! Nikasema ngoja nione tena na leo siku ya tatu,, Mambo yakawa vile vile rangi ya ngozi hasa huko mapajani ni njano kabisa na safari hii Hadi sehemu za mgongoni. Nikavunja ukimya, nikamuuliza lakini alinijibu Kwa kunibeza; "....eti haaa, mi najua umeniamsha kuna Jambo la maana kumbe ni...."

Hapo sasa akili ikanikaa nikajua rasmi anafahamu vema juu ya hilo. Asubuhi nikachelewa kutoka nyumbani lengo nifanye msako mkali labda kuna dawa Zaidi na labda anaumwa lakini anaficha..

Kwa bahati nzuri nikakutana na dawa kwenye mfuko wa kawaida tu ( zimeandikwa " LA 75". nika-googgle chap nikaambiwa ni Lamivudine! Aina mojawapo ya ARVs! Moyo ukapasuka! Nilitoka nikaenda kwanza kanisani akili itulie.

Jioni baada ya yeye kurudi nikamwita chumbani Kwa Sura ya kigaidi na mkanda mkononi,, (sikuwahi kamwe kumpiga) lakini ilibidi nivae Sura hiyo.. baada ya kumuuliza akawa mkali anabisha, nikafungua mkoba wenye hizo dawa nikamwonesha kisha nikashika vema mkanda mkononi. Kabla ya kuanza kichapo akaomba nisimpige atanieleza kila kitu. Basi Akafunguka..kwamba amegundua ameathirika huu ni mwezi wa sita sasa! Na alijua ni Mimi ndo nimemuambukiza ndiyo sababu ya kunichukia Kwa kipindi chote kile hata asitake nimguse!

Jioni hiyo hiyo nikaenda kupima,, Niko negative. Nikapita pharmacy moja hapa mjini pia nikanunua vile vipimo nikaja navyo nyumbani akanipima yeye mwenyewe maana ameshakuwa mtaalamu.. nikakuta negative pia.

Mengine yaliyoendelea siyo muhimu ,,lakini anasema hajawahi kuchepuka Kwa kipindi chote hicho. Sasa nikabaki na maswali inawezekana vipi mtu apimwe mara tatu wakati wa ujauzito awe negative, hajachepuka halafu miezi kadhaa baada ya kujifungu awe positive? Na Mimi mwenyewe sina maambukizi?!!

Hebu tieni neno wakuu. Nahisi kuvurugwa kabisa yaani. Kuhusu mtoto wanadai hawezi kupimwa Hadi afikishe miezi 18. Lakini Kwa mwonekani dogo yupo na afya njema.

Mnadhani possibility ya kuambukizwa ipo wapi Kama hakuchepuka?

Dah! Mungu nisaidie.
View attachment 1964380
Duh! Hapo lazima alichepuka hakutaka tu kusex na wewe kwa hofu ya kukuambukiza au kuficha sehemu zake za Siri zenye mabaka kwa kuwa alijua ungegundua, pole saana ila okba Mungu mwanao awe mzima tu.
 
Ulitakiwa uendelee kumnyandua mapaka mimba inafika miezi tisa, baada ya kujifungua ungeanza mara tu alipopona maungo yake.

Kuna sehem kaupata kipindi ulipokuwa humkuli.
 
Na unakuta kuna watu wanakubandua kavu....jamani!!!!! Eee Mungu tuepushe waja wako



Sent using Jamii Forums mobile app
Tena huyo bora hana uwezo wa kuambukiza.Mtu akiwa kwenye dawa zaidi ya miezi sita uwezekano wa kusambaza ni mdogo sana au haupo.
Waliopo kwenye nafasi kubwa ni wale ambao hata hawajijui kama wameathirika.
 
Ndugu hao virus wana mambo meng..w
1.saikolojia...utateseka sana

2.ukiwa na hao wadudu..kupata weakmess zingne/magonjwa mengne ni rahis sanaa
Yaan kupata hayo magonjwa uliyosema inakua rahis sana..tena figo ndo znakufa mapema sana

Kwahyo hakuna unafuu....kwanza mahusiano utakua unajiuliza sana..yaan kuchakata mtu inakua na mawazo sanaa..kula dawa maisha yako yote..simchezo

Etc etc...
Utateseka kama hujielewi mbona hata ukiachwa huwa unateseka na hadi mnajinyonga?

Msipopata elimu sahihi ya kujitambua ndio utapata shida,mimi mara kadhaa huwa najioeleka kupima ngoma wala sihitaji kusukumwa kwa sababu nafahamu wanaoteseka na hayo magonjwa unayosema wewe ni wale ambao wana ngoma afu hawajui kama wanao afu wanakuja kugundulika too late cd4 ziko chini Sana na kuja kuziridisha sio leo.
 
huyo dada hajachepuka,hakuna kitu kinaitwa hiv ni propaganda tu
 
Muongo huyo. Kama kaweza kukuficha ni mgonjwa atashindwaje kusema kuwa hajachepuka ?
 
Pole, ila nimegundua mnaishi maisha ya Mtu na Kimada sio kama Mume na Mke, na hapo ndio tatizo lilipoanzia
 
Back
Top Bottom