Mke wa "President" Ashiriki Shindano Clouds!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,

Mwanamke kutoka Zanzibar kwa jina la Bi Nasra, aliyejitambulisha kama mke wa kwanza wa president wa kwanza wa Zanzibar, anashiriki shindano la Bibi Bomba la Clouds FM!

Mwanamke huyo emedai kufanikiwa kupata mtoto mmoja na rais huyo wa kwanza na kusema yupo na mtoto yupo!

Kwa wale wajuzi wa mambo ya Zanzibar, jee ni kweli president wa kwanza wa Zanzibar alikuwa na mke mkubwa? Kama ni kweli, is it proper kwa mke wa president kushiriki shindano na kujiexpose kuwa yeye alikuwa ndiye mke wa kwanza wa president wa kwanza?!

Namfahamu huko Zanzibar kuna mtoto wa nje wa Sultan aliyezaa na mjakazi wa mkewe na baada ya kupata ujauzito ikafanywa siri kubwa kumuozesha huyo mjakazi haraka haraka kabla siri haijafichuka!. Mwana mfalme huyo yupo na amejinyamazia kimya!

Kama ni kweli rais wa kwanza wa Zanzibar atakuwa alikuwa na mke mkubwa, basi urais Zanzibar haushi vibwanga!

Kimbwanga kingine ni kuna watoto wawili wa kiume wa rais, kaka mkubwa akawa rais kwa kipindi cha miaka 10, alipokaribia kumaliza mdogo mtu nae akautaka urais, akashauriwa yeye asigombee kwa sababu aliyemaliza ni kaka yake wa damu, hivyo urais wa Zanzibar ungeonekana kama usultani!. Mdogo mtu aligoma kujitoa kwa hoja kuwa mtoto halali wa rais aliyepaswa kuchukua urais ni yeye!, eti kakaye ni mtoto wa kufikia!

Visa vya marais wa Zanzibar havikuishia hapo. Kuna rais mmoja mpenda warembo, ila alikuwa akioa na kuacha, alipoa mke wa 5, aliporwa huyo mke na rafiki yake ambaye alikuwa ni rais wa nchi nyingine hapa hapa barani Afrika. Sasa ana mke wa 6 na ndio katulia kutokana na umri!
 
Kwani ukiangalia ndevu za hao marais ndugu unaona zina fanana?

Watu siku hizi ni aibu tu ndo maana wanakaa miaka kumi lakini siku aibu ikiwaisha utasikia mimi ntatawala hadi zanzibar itakapo jenga daraja la kutuunganisha na bara. hamna Kiongozi africa anaye tamani kutoka madarakani. Na akisha ingia madarakani familia yake yote inajiona ni familia ya kifalme na kuongoza nchi ni haki yao wote. Mfano Mzuri angalia rais wa sasa, hadi mke wake ana escort kama rais. Hata mtoto anataka salute akipita. Mia
 
aaah ndio maana hata wenzake wanamsema anajidai na anajiona ye ni msomi kuliko wenzake kumbe alikuwa ni mke prezdar
 
Wanabodi,
Mwanamke kutoka Zanzibar kwa jina la Bi Nasra, aliyejitambulisha kama mke wa kwanza wa president wa kwanza wa Zanzibar, anashiriki shindano la Bibi Bomba la Clouds FM!.

Mwanamke huyo emedai kufanikiwa kupata mtoto mmoja na rais huyo wa kwanza na kusema yupo na mtoto yupo!.

Kwa wale wajuzi wa mambo ya Zanzibar, jee ni kweli president wa kwanza wa Zanzibar alikuwa na mke mkubwa?. Kama ni kweli, is it proper kwa mke wa president kushiriki shindano na kujiexpose kuwa yeye alikuwa ndiye mke wa kwanza wa president wa kwanza?!.
Wanabodi,
Swali hili niniliuliza mwaka mmoja na nusu uliopita, jibu ndio nimelipata leo na ni hili hapa.
Kwa mara ya kwanza Sheikh Abeid Karume alifunga ndoa na Bibi Pili binti Ahmed Ambari mwanzoni mwa miaka ya Arubaini. Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara. Baada ya kutengana na wake hao wawili, Sheikh Karume alifunga ndoa na Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944 mwishoni mwa mwezi wa Novemba, harusi ambayo ilifanyika huko Bumbwini Misufini. - Ali Shaaban Juma.

Isitoshe, si Fatma tu na Ashura ambao ni wakizazi cha "mabwana", pia kuna wengine ambao waliolewa na Bwana Karume ni Bibi Nasra, Bibi Helemu na Bibi Fadya ambao kila mmoja alizaa nae mtoto mmoja wa kike.

Unawajua khabari zao hawa mabibi Nasra, Helemu na Fadya?

Pasco Zanzibar huijui. Waachie Wazanzibari wenyewe japo kidogo na sie wa pwani, kwani kwetu pia mpaka wa hii leo ni himaya ya Zanzibar na khulka zetu hazijapishana kihivyo, si kama wewe wakuja. Unalijuwa hilo?

"Sisi mambo twayajua" - Khadija Kopa.

Situmai majibu kutoka kwako lakini nna uhakika somo umelipata.

Asante Mkuu Zomba, kiukweli hayo mengine yote sikuyajua zaidi ya Bi. Nasra kushiriki shindano la Bibi bomba hapa bara.

Naomba kuuliza very genuinely, hivi Karume alikuwa na wake wangapi jumla?, hawa ulinitajia hapa ni wake 7!. Jee alikuwa na watoto wangapi?!, wako wapi sasa?!, vipi hali za hao wake wengine?!.
Pasco.
 
Wanabodi,
Swali hili niniliuliza mwaka mmoja na nusu uliopita, jibu ndio nimelipata leo na ni hili hapa.

Asante Mkuu Zomba, kiukweli hayo mengine yote sikuyajua zaidi ya Bi. Nasra kushiriki shindano la Bibi bomba hapa bara.

Naomba kuuliza very genuinely, hivi Karume alikuwa na wake wangapi jumla?, hawa ulinitajia hapa ni wake 7!. Jee alikuwa na watoto wangapi?!, wako wapi sasa?!, vipi hali za hao wake wengine?!.
Pasco.



Interesting,naomba unitag siku atakayokujibu japo na mimi niambulie mawili matatu....
 
Wanabodi,
Mwanamke kutoka Zanzibar kwa jina la Bi Nasra, aliyejitambulisha kama mke wa kwanza wa president wa kwanza wa Zanzibar, anashiriki shindano la Bibi Bomba la Clouds FM!.

Mwanamke huyo emedai kufanikiwa kupata mtoto mmoja na rais huyo wa kwanza na kusema yupo na mtoto yupo!.
Leo ni Karume Day, nami naomba kujiunga na Watanzania wenzetu maadhimisho mema ya Karume Day na kuwatakia mapumziko mema.

Katika kumuenzi Karume, tuwadurusu kidogo na wale wanamhusu wana hali gani, ikibidi nao pia waangaliwe na ikibidi watunzwe!.

RIP Abedi Amani Karume.
Paskali
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom