Ipo hivi jamaa yangu anaishi na mke ambaye tayari Wamejaaliwa kupata watoto wawili ,sasa anasema mwaka jana waliingia kwenye mgogoro mkubwa baada ya kugundua mke wake alikuwa akimsaliti japo huo usaliti ulitokea kipindi cha nyuma hili suala limefika pabaya jamaa aliamua kumufukuza waifu nyumbani kwake Ila mke amegoma kuondoka na amemsihi jamaa kuwa alishaachana na usaliti anaomba amsamehe waendelee kuishi.mme anagoma sasa mwanamke yupo pale kwake ana mawazo mengi amekonda sana kibao kimegeuka lawama zimehamia up upande wa mwanaume watu wanasema anamnyanyasa mke wake jamaa yupo njia panda napia inaonekana mtoto wa kwanza jamaa alipakaziwa hivyo amegoma kusamehe anacho omba ushauri ni kuhusu mke kuonekana kama ananyanyaswa maana amekonda baada ya mme kuujua usaliti wake