Mazee sidhani kabisa kama nimepotoka, naamini kabisa mtetea mafisadi nae ni fisadi, hawa viongozi wa dini nadhani wanaelewa fika ujambazi na ufisadi wa Lowassa na wao bila ya aibu wakaamua kwenda kubariki uzinduzi wa hiki kitabu na wengine hadi kufikia kukemea mambo ya kusulubiana yanayoendelea nchini akimaanisha kama vile Lowassa ni mtu safi ambaye amechafuliwa na wabaya wake. Sijawadhalilisha kabisa nadhani wenyewe ndio wamejidhalilisha mbele ya jamii ya Watanzania kwa kuamua kwenda kubariki kitabu cha Mke wa Fisadi Lowassa hasa ukichukulia wao ni viongozi wa dini wanaoheshimiwa nchini.
Msimamo wangu wa kupinga wote wanaotetea mafisadi hautobadilika hata huyo mhusika awe Kadinali, Sheikh Mkuu, Mchungaji, Rabbi au Askofu. Fisadi ni Fisadi tu na mnatetea mafisadi nae ni fisadi tu.
HYPOCRISY OF THE HIGHEST ORDER, basi tukana kila kiongozi wa Tanzania kuwa ni fisadi. Badala ya kutumia forum constructively unakuja kutukana watu? Woooooote!
Mke gani wa kiongozi Tanzania ameandika hata kitabu cha pg 2?? Leta evidence moja ya ufisadi wa lowassa, mimi nitakulipia gharama zote mahakamani, tuache huu unafiki wa siasa. Tunabaki kusema kila mtu amenunuliwa, tunalidhalilisha taifa letu, hamna kingine tuna-achieve. Lets discuss issues.
Watu wanthubutu hata kutukana viongozi wa dini, wao wanatujua wote matatizo yetu, na kufanya waliyofanya ni ujumbe wa kutafakari, siyo matusi.
JF mnamsulubu Regina kwa "dhambi" ya Edward. Regina ni Mwanakondoo wa Kardinali Pengo. Ni Mkatoliki anayefuata dini yake kwa jitihada kubwa. Mchungaji Mwema huenda kwenye hafla ya mwanakondoo wake, hata kama hafla yenyewe ni ya kuzindua kitabu kidogo sana. Mnamsulubu Pengo kwa kumtembelea Muumini wake?
Kuna viongozi ambao wako safi na si majambazi wala hawafanyi ufisadi lakini wote tunajua kwamba Lowassa ni Jambazi na Fisadi Mkuu nchini Tanzania nadhani hilo hata wewe unajua. Ni bora angeitumia hiyo nafasi ya kwenda nchi takatifu ya Israel kutubu dhambi zake ambapo pia ingehusisha kurudisha mali zote za watanzania ambazo kwa miaka mingi amekuwa akiwaibia ili kushibisha tumbo lake na familia yake. Hatuna shida ya kusoma kitabu chake na mke wake, bali tunachotaka na urudishwaji wa mali zote na rasilimali za Tanzania ambazo amejilimbikizia.HYPOCRISY OF THE HIGHEST ORDER, basi tukana kila kiongozi wa Tanzania kuwa ni fisadi. Badala ya kutumia forum constructively unakuja kutukana watu? Woooooote!
Mke gani wa kiongozi Tanzania ameandika hata kitabu cha pg 2?? Leta evidence moja ya ufisadi wa lowassa, mimi nitakulipia gharama zote mahakamani, tuache huu unafiki wa siasa. Tunabaki kusema kila mtu amenunuliwa, tunalidhalilisha taifa letu, hamna kingine tuna-achieve. Lets discuss issues.
Watu wanthubutu hata kutukana viongozi wa dini, wao wanatujua wote matatizo yetu, na kufanya waliyofanya ni ujumbe wa kutafakari, siyo matusi.
Kuna vitu vinachanganywa hapa,ni kama kuna baadhi wanataka kurestrict mjadala ubakie kwa mtunzi wa kitabu na maudhui yake.Wanasahau kuwa thread zina behavior ya ku_evolve.Na katika hili what catches majority attention ni matamko waliyoyatoa hao 'walisha kondoo'.Hapo ndipo palipoanza utata.Na hizo kurasa 15 si ni kama karatasi 8 hivi given that they are printed on both pages!
Kuna haja ya kutohamaki. Gazeti limeandika kilikuwa na kurasa 15. Inawezekana sana kwamba walikosea wakaandika 15 badala ya 150. It would not be the first time. Ni vema kuthibitisha kurasa zake kabla ya kumdharau Mwandishi.
JF mnamsulubu Regina kwa dhambi ya Edward. Regina ni Mwanakondoo wa Kardinali Pengo. Ni Mkatoliki anayefuata dini yake kwa jitihada kubwa. Mchungaji Mwema huenda kwenye hafla ya mwanakondoo wake, hata kama hafla yenyewe ni ya kuzindua kitabu kidogo sana. Mnamsulubu Pengo kwa kumtembelea Muumini wake?
Jiulizeni kama aliyeandika dibaji ni mjinga. Lazima kuna kitu kizito sana kwenye hicho kitabu au kijarida.
I would advise caution. Why insult the prelates before knowing anything about what is written in the book, encyclical, poster, letter or whatever? Dont be quick to throw mud at others
Mama kaandika kitabu chake kwa nia njema, na badala ya kumpongeza wengine wameamua kumsakama. Hiki kitabu kina kurasa 41 zilizochapishwa pande zote, zikiwemo 1.5 ya acknowledgements, 2 za foreword, 2 za preamble na 37 ndiyo zenye maudhui: chapter 1 hadi chapter 6. Mpongezeni kajitahidi. Nahitimisha kwa kuqote vision ya kitabu hiki, kwa maono ya muandishi: "Regina's delight and insipiration is to illuminate desires of readers of this book and hopefully inspire them"
..kwani ameandika nini kwenye kitabu chake?
..nadhani tunakuwa na haraka kidogo kuhukumu kabla ya kusoma kitabu chenyewe.
kitabu ni kidogo tu ukurasa 6, page 37 tu.
The Lowasa's have money other than what Edward may or may not have taken from the people. Is it not possible that they used those funds to visit the Holy Lands?
Kosa la Kardinali Pengo, Askofu Malasusa na viongozi wengine wa dini waliohudhuria hiyo hafla ni lipi hasa? Ni kosa kwa Askofu kuhudhuria sherehe ya muumini wake ya kuzindua kitabu cha dini?
Sidhani kama Kardinali alimaanisha watu wanamsulubu Mheshimiwa Lowasa "kwa dhambi ya wengine" kama baadhi yenu mnavyosema. Alimaanisha kwamba wako watu wanaomsulubu Mama Regina kwa "dhambi" ya wengine (possibly Edward).
Wanandoa ni mwili mmoja lakini sio roho moja. Akitenda dhambi mmoja sio kwamba wote wametenda dhambi. Kwa mfano, mmoja anaweza kuwa mwasherati wakati mwenziye hana hiyo dhambi.
Be humble fellows and apologies for all the nasty things that you have said about this woman of God.