Mke wa Lowassa azindua kitabu

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Mke wa Lowassa azindua kitabu

Na Mwandishi Wetu,
MTANZANIA, Aprili 15, 2009.

Watu mbali mbali jana jioni walimiminika nyumbani kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kushuhudia uzinduzi wa kitabu kilichotungwa na mkewe Regina, uliofanywa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Regina aliandika kitabu hicho wakati akiwa katika matembezi binafsi inchini Israel, siku chache baada ya mumewe kujiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka jana kutokana na sakata la Richmond.

Kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kiitwacho “Walk The Path With Diary in Israel, The Holy Land” kina kurasa 15 na dibaji yake imeandikwa na Monsinyori Julian Kangalawe kutoka Kanisa la Mtakatifu Joseph la Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. “Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo,” alisema.

Mhubiri maarufu mwenye makazi yake mjini Arusha, Christopher Mwakasege, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema ni yeye aliyetoa wazo kwa Lowassa na mkewe kutembelea Israel baada ya matatizo yaliyowakuta.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, aliwahimiza watu kujenga moyo wa kupendana ili kujenga nchi yenye maelewano.

Mbali na Mlasasusa, Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ni Pwani, Elinaza Sendoro, pia alihudhuria hafla hiyo, na akatumia nafasi hiyo kuwashawishi watu kutembelea Israel kujionea namna watu wa dini tofauti wanavyoishi.

Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.
 
Mhmmm!! yaani viongozi woote hao wa dini walikuwepo kuzindua kitabu cha Page15 !? Msisulubu watu!? Lowasa kama umeokoka naomba urudishe mali zoote ambazo unaona hujapata kihalali ndipo nitajua kweli umeamua kuacha mali na fedha na kumfuata Bwana.
 
Duh it sound like somebody is trying to get cleaned, lakini kama sio mchafu huitaji kuoga au vipi. Mbona Simba wa vita pamoja na malawama kibaoooo sikuwahi kumsikia akikusanya mashekhe wamsafishe! I think he was clean. Lowassa atubu tu hadharani then other things can follow otherwise mtatunga sana vitabu vya pg 15, hiko ni kitabu au kijarida?
 
15-page BOOK! We may need to go back to the definition of a book! What were all these big folks celebrating! A book? Jokes in all walks of life continue...! A dinner would have done better!
 
Nchi hii bwana, mafisadi wana enziwa mpaka na watu wanao jiita 'Watu wa Mungu,' utata mtupu,kazi tunayo.
 
Nimeamini hii ndo tanzania zaidi ya uijuavyo!! Kijarida cha pg 15 kinakusanya maaskofu na mapadre wote hao! Kweli huu ni wakati wakusafishana kuelekea uchaguzi mkuu. Hivi kweli viongozi wa dini wa namna hii tunawahitaji kweli??? Ndio makanisa na misikiti imeanza kupoteza waumini kwa kasi kubwa hapa Tz, angalia makanisa ya RC, Lutheran na Moravian jinsi yanavyozidi kuwa upu siku hadi siku, these are some of the reasons wana JF!
 
Mbona hatukuwaona kwenye tamasha la wanazuoni (kuenzi fikra za Nyerere) pale chuo kikuu. Ningekuwa EL ningesoma alama za nyakati na kutulia na kusimamia miradi niliyokwishawanyonya walala hai wa tz. Shame on them all!!
 
Hongera familia ya Lowassa kwa kuokoka na kumrudia muumba wenu.ila zile mali zilizokusanywa isivyo halali kwa ujumla wake wapeni maskini na wahitaji ili mungu azidi kuwabariki zaidi

tutakitafuta hichi kijarida cha msiwasulubu watu,tukisome halafu tutatoa mawazo yetu

bwana asifiwe
 
Sishangai kwanini watanzania tunaingia kwenye mikataba mibovu sio kwa rushwa tu, HATA UVIVU WA KUSOMA, tumeanza kujudge a book by its pages, mnajuaje may be wametubu kupitia kitabu hicho, ebu tuleteeni copy tusome ndio tumponde vizuri, msiwalaumu mapadri na wachungaji, kwa wale wana biblia mnakumbuka story ya mwanakondoo mmoja aliyepotea toka kwenye kundi la kondooo? Muchungaji alifanyanye????? mnakumbuka Bwana Yesu alivyoenda kupata Lunch kwa mtoza ushuru? Nini Kilifuata baadae????????
 
Okei okei inachosha sasa.
Haya mtutajie aliyechapisha hicho kitabu i mean printer and publisher ili tuwazomee pia.
Nipo katika book sector for decades now sijapata kuona serious chapisho la pages 15. sana sana ni hadithi za watoto unaweza hata kuchapa page kumi ila size huzingatiwa sana ktk hilo. Inawezekana Regina Lowasa alidhamiria kutunga children book lakini morani akamshawishi kitumike kisiasa.
Kwa kuwa ni masuala ya dini tuseme hajatunga kitabu, ameandaa booklet (nadhani kijarida) cha kiimani kwania ameelezea masaibu ya safari yake Mji Mtakatifu.

Nashindwa kuamini wasomi kama Pengo. Malasusa, Mwakasege n.k walikuwa na picha ya uzinduzi wa kitabu kumbe uhalisia ni booklet kisha wasihoji.....

Lakini kwa kuwa fedha za ufisadi ndizo hupokelewa na nyumba za ibada basi si haba waliohudhuria walimegewa ka-fungu kalikobaki kutoka Richmonduli.. teh tih toh tuh!
 
Sishangai kwanini watanzania tunaingia kwenye mikataba mibovu sio kwa rushwa tu, HATA UVIVU WA KUSOMA, tumeanza kujudge a book by its pages, mnajuaje may be wametubu kupitia kitabu hicho, ebu tuleteeni copy tusome ndio tumponde vizuri, msiwalaumu mapadri na wachungaji, kwa wale wana biblia mnakumbuka story ya mwanakondoo mmoja aliyepotea toka kwenye kundi la kondooo? Muchungaji alifanyanye????? mnakumbuka Bwana Yesu alivyoenda kupata Lunch kwa mtoza ushuru? Nini Kilifuata baadae????????

..nakuona kama sauti ya mtu aliye nyikani.....
Je watakaa tumnyooshee mapito bwana mkubwa atakapoanza kupita kuelekea 2015? No way!
Kumbuka Baada ya Yesu kula na mtoza ushuru nini kilitokea baada ya hapo? jamaa alilipa dhuluma yoote kwa riba ya asilimia 400 kwa kila senti ya EPA. Mnapotetea watu kwa kutumia vitabu vitakatifu basi msiwe wavivu wa kusoma aya ili unapotafsiri uelewe unasema nini.
Kumbukeni yule kijana tajiri aliyeambiwa na Yesu kuwa akauze kila alichonacho kisha mafuate. Yesu alijua kuwa mali zote za yanki yule zilitokana na dili feki na dhuluma.
 
Salaam Wana JF
Ninacho shangaa badala ya kumpa KUDO'S huyu mama kwa kuwa mmoja wa waandishi angalau kazi ambayo wasomi wetu pale HILL wameshindwa na kubaki kufuga kuku na kufungua Glosary mitaani watu wanaanza kubeza kuwa mara kijarida,mara kajitabu.

A book,or kitabu can not be defined kwa kuangalia Number of pages alone,but wana JF mm kilichonifanya nichangie hapa hasa ktk mada hii ni DELEGATION, NA UJUMBE HASA WA MUHASHAMU POLLY.

The mesaje waz veri clia huyu mzee kasema na hapa amenikumbusha kumbe huu mtindo wa kusulubiana orijin yake ni mateso alofanyiwa yesu,na a good mesaje hapa ni kuwa HATA YESU ALIPOSULUBIWA HAKUWA NA DHAMBI but as per christian teaching alisulubiwa kwa dhambi za wengine,na hapa tunapata fundisho na kwa Mwenye MACHO,NA MASIKIO ameelewa LOWASA ALISULUBIWA KWA DHAMBI ZA WENGINE.

Whoever aliekuwa anafatilia mchakato kama si ushabiki basi aliliona hilo na dhambi hii haitaisha italitafuna taifa hili mpaka hapo watu watakapo tubu.
 
Katika kauli yake kwenye hafla hiyo Kardinali Pengo ali-omit maneno ambayo mimi nimemsaidia kuyaweka kwenye brackets: “Yesu alikuja duniani, akasulubiwa (bila kosa) na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana (bila makosa). Tuache mchezo huo."

Kwa maneno mengine ni vyema tu angesema "Lowassa hakuwa na kosa," na angeeleweka, kuliko kuleta kigugumizi.
 
Duh...hi kweli kali...nashindwa kuamini yaani hadi Kardinali Pengo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Elinaza Sendoro na Mch Mwakasege wote walihudhuria na kupewa nafasi ya kutoa natoa nasaha zao....hicho "kijarida" kimeandikwa nini wajameni..??!!!

Hakuna mwana JF aliyekisoma atupe japo summary...
 
Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.
Hii sijaipenda kabisa, Kumgeukia Mungu ni kwenda Israeli kutembelea maeneo takatifu? Mie nadhani kuna zaidi ya hapo kwa Lowasa kufanya ili asamehewe na Muumba (maana kauli yake inaonyesha kesha jua madhambi yake) Akiri hadharani na kurudisha kile aonacho hajakipata kihalali ili asamehewe, kwenda Israeli hayo ni matembezi ya kitalii tuu tena kwa fedha zilezile za kifisadi.
 
Jamani Yebo Yebo ushishangae sana. Hao ndiyo walikuwa na wanaendelea kulipwa mafungu ya kumi manono. Umesahau ni kiasi gani Lowasa family wanatoa michango ya ufadhili kwa makanisa, kumbe ni mihela ya wizi?? Nakuambia hivi, ingeuwa ni makanisa yanayoongozwa na wachugaji wale wa zamani ambao wengi ni marehemu au hawawezi kabisa kuamka ni kwamba Lowasa asingeruhusiwa kotoa sadaka kanisani tena baada ya kugundulika kuwa ni mwizi. Yes ni kwamba wapo wezi wa aina mbalimbali makanisani lakini angalao hawajajulikana kwa public ufisadi wao.

Mimi binafsi nimeshuhudia viongozi wa dini wakikiumbatia matajiri tu sasa maana ndiyo wenye fedha za kutoa kwa maaskofu na mapadre, wachungaji, you name all. Makanisa siku hizi ni biashara tena naaita haramu, hawajali michango wala sadaka inatoka wapi. Hapo zamani kidogo hata ikijulikana muumini ametalikiana au kutengana na familia, au kuwa na nyumba ntobo (ndogo) au kuwa na mahusianao nje ya ndoa, alikuwa anafungiwa sacrament kanisani na alikua anazuiwa kupata huduma zote za kiroho kaninisani ikiwa pia ni kwamba hata akifa au akipata msiba wa familia kanisa halitatoa huduma ya maziko. Je leo hii haya yanafanyika???? Kama yangekuwa yanafanyika ndugu Reginald Mengi asingeruhusiwa kuingia Azania Front na kwingineko kabla ya kurekebisha mitafaruku ya ndoa yake na kuachana na vimada ambao ni umri na wanawe. Kwa mantiki hiyo basi, kinachomweka Lowassa, Mengi, n.k katika kiti cha mbele kanisani ni pesa yao. Naweza kusema hivi makanisa ya leo na uongozi wa theme ni kuwa "Fedha mbele, Mungu nyuma" hapa hapendwi mtu ila fedha yake.

Tabia hii ipo pia kwa makanisa au makundi ya kiroho yanayoibuka siku hizi. Huko ndiko utakuta uozo wa kila namna. Matajiri wanawekwa kiti cha mbele kwa kuwa ndiyo wanavaa vizuri na kuwa pesa yake ndiyo inamweka mbele. Mshirika tajiri asipoonekana kanisani ni lazima mchungaji atampigia simu, ili asipotee maana kupotea ni kupoteza sadaka nono, fungu la kumi, shukrani,, michango, you name all. Asipoonekana maskini hakuna hata wa kumtafuta. Narudia makanisa ya leo ni biashara tu, hapendwi mtu bali pesa yake. Ole wako, ikitokea ukifilisika yaani mchungaji atabalidli hata namba ya simu maana anaogopa usije ukamdai pesa yako.

Lowassa na mke wake wasituletee uchuro hapa wa kutaka kufunika maovu kwa kajitabu kao. Kwanza wauze kila kitu maana vingi wamevitapa kwa udhalimu ndipo waanza maisha mapya ya utakatifu. NAsema hivi yaani kila mali walioipata kwa dili chafu wauze maana inawasuta, kama kweli wamemrudia Mungu na waache mali zile ambazoi wanajua haziwasuti na wamezipata kwa halali. Aluta continua JF forum, where we dare to talk freely.
 
wazo zuri kwani ni sehemu ya kuelimisha jamiii na kujenga hamasa kwa wengine kufuata..

EL yupo kwenye toba takatifu na atatufaa sanaa kuwa kiongozi wa siku zijazooo...

hongereni sana lowasa family kwa uamsho na mwamko wenye neemaaa.
 
Kwa mtaji huo wa kurasa15 kuitwa kitabu basi nadhani Mzee Mwanakijiji na kijaliadda chake cha Ckeche Za Fikra kesha andika vitabu vingi sana.

Watu na Adabu zao wanauita mkusanyiko wa kurasa 15 kitabu?????

Du!
 
Nimeamini hii ndo tanzania zaidi ya uijuavyo!! Kijarida cha pg 15 kinakusanya maaskofu na mapadre wote hao! Kweli huu ni wakati wakusafishana kuelekea uchaguzi mkuu. Hivi kweli viongozi wa dini wa namna hii tunawahitaji kweli??? Ndio makanisa na misikiti imeanza kupoteza waumini kwa kasi kubwa hapa Tz, angalia makanisa ya RC, Lutheran na Moravian jinsi yanavyozidi kuwa upu siku hadi siku, these are some of the reasons wana JF!


KWeli Brook inashangaza kuona viongozi wote hao wa dini. LAkini hutakiwi kutafsiri hicho kimkutano kwa siku moja peke yake. Unaweza kutafsiri hicho kimkutano kuanzia mwaka 1995. Baada ya wanamtandao kupigwa stop na Mwalimu walijipenyeza kila mahali ikiwemo kwenye dini mbili kubwa za kikristo na kiislamu. Ndiyo maana wakati wa uchaguzi 2005 JK aliitwa chaguo la Mungu. Na inaonekana kabisa aliyewavuta viongozi wa kikristo kwenye mtandao ni EL (hii ni assumption yangu). Wanamtandao wameingia na JK anaonekana kama yuko upande wa waislamu zaidi (hilo pia ni assumption yangu-lakini imejengwa kutokana na matamshi mbalimbali yaliyotoka kupinga baadhi ya maamuzi ya serikali ya JK kama vile OIC na mahakama ya Kadhi). Kwa hiyo hicho kimkutano kwangu mimi nakitafsiri kama ni warning kwa JK kuwa kama wewe unaendelea na hao wa dini zako, basi sisi tuliokusupport 2005 kwa sababu ya EL tutaendelea kumsupport EL. Kwa hiyo badala ya kusema sijui Lowasa anajisafisha au nini mimi kwangu nazitafsiri hizi kama ni siasa za udini ambazo zimeletwa na wanamtandao. Na sasa hivi tusipojiangalia basi tutawashabikia viongozi hao kwa udini wao. Kwangu mimi wito naoutoa kwa wanaJF ni lazima tukatae hizi siasa ambazo zinataka kuenea hapa nchini. Njia ya kuzikataa ni kupiga kelele kwa nguvu na pia kusema sasa inatosha. Ikifika 2010 JK na kundi lake iwe wametangana au bado marafiki lazima waondoke. Huwezi kujenga nchi Rais anahudhuria maulid tu kwa sababu ni muislamu na waziri mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu kwa ajili ya kashfa anaalika viongozi wote wa kikristo kwa sababu ni mkristo. UFISADI MTUPU. In 2005 we let our country to go to the dogs, but now we should say enough is enough.
 
Back
Top Bottom