Mke wa Lowassa azindua kitabu

Hivi ukiacha Regina, Mwanamama gani mwingine au mke wa kiongozi wa serikali ameandika kitabu! She is getting my attention now! Maudhui ya kitabu yatajadiliwa tutakapo yapata! Lakini cha msingi ameongea kwa sauti yake au ya mumewe! Very interesting!

Pia cha msingi, inawezekana kabisa ilileta patashika ndani ya nyumba ama mahusiano yao. Itakuwa vyema tusubiri tusome mama kasema nini!
 
Sasa nione mshamba mmoja anasema " Lenin alifanya makosa kupiga marufuku dini.."
Choma makanisa, choma misikiti, masinagogi, choma mafisadi ..... ni unyama unyama tu kama wa Mzee Kishoka (kidevu cha Lenin). Hamna cha Sarah au nanihii. Bahati mbaya naota tu, ndoto yangu sijui itakuja kuwa kweli?

Kuna mtu aliuliza ukiwa Rais utafanya nini?
Nafikiri jibu ni KUPIGA MARUFUKU DINI ZOTE. Labda mtu kama anasalia kwenye miti/milima au pango yaani yeye na miungu wake. Mtu akijifanya kuwa eti yeye kafunuliwa, basi tutaona kama ndani ya jeneza atafunuliwa na atoke kutembea.

Nashukuru Lowassa hakufa huko Izrael, maana ingelitokea akafa na kuzikwa na siku ya tatu akafufuka akiwa more powerful, hapo tungelikwisha.
 
"dibaji yake imeandikwa na Monsinyori Julian Kangalawe kutoka Kanisa la Mtakatifu Joseph la Dar es Salaam."
sasa kama mtu anaandika kitabu cha kurasa kumi na tano tu na anashindwa kuandika dibaji ya nusu kurasa hiyo ni hatari kabisa katika taifa ili,
kama msemaji mmoja aliyetangulia kusema kwamba m2 akishafikia kuwa cardinal ni kwamba muda wowote anaweza kuwa papa kwAni yupo kwenye ranki hiyo,
matatizo yote ya UFISADI yanayotokea Tanzania hawa viongozi wa dini wanakuwaga kimya 2, na sisi tunaojua mambo ya dini tuliona ni sahiHi kwani yakaisaRi mwachie kaisari, yaani kutochanganya dini na siasa
kuna mambo mangapi ambayo wananchi wangependa wayasikie kutoka kwa viongozi hao wa dini kusudi yaweze kuwa na nnguvu lakinin wameaamua kunyamazA KIMYA NA KWENDA KUSHABIKIA MAMBO YA UJINGA, KWA KWELI HAWA JAMAA WAMEJISHUSHIA HADHI YAO KABISA
 
Nashukuru Lowassa hakufa huko Izrael, maana ingelitokea akafa na kuzikwa na siku ya tatu akafufuka akiwa more powerful, hapo tungelikwisha.

Ha! ha! sicheki kwenye swala la kifo rather the context is funny! God wish him this guy the long life, maybe he will write his own book someday for us to understand how his mind works.
 
Sawa, wafanye kama Zakayo mtoza ushuru. Nusu ya mali kwa masikini na waliyoipata isivyo halali wairejeshe! Huko ndiko kuokoka/kukutana na Yesu. Vinginevyo ni usanii tu!
 
hiyo hela ni ndogo sana. hapa tumlaumu Lowasa kwa kula hela, ila mkewe hana kosa. mkewe ana kosa gani? mwizi ni mumewe, yeye amefanya nini? namfagilia kwa kwenda israel nchi ambayo mimi naipenda na kuithamini kuliko hata tanzania.

- Duh! bonge la point la kusaidia masilahi ya taifa letu, saafi sana mkuu na ubarikiwe!

FMEs!
 
Suala: nani anamtumia mwenzie? Lowassa anawatumia wakuu wa dini au wanamtumia yeye?

Pili: Nani aliyenufaika katika hili, Mr. au Mrs. au wakuu wa dini au waumini?!

Kadhiya hii inatupa taswira, kuwa kwa kiasi kuna mafungamano baina Wakuu wa dini na wakuu wa siasa, hata ikabidi watetewe katika hali ya UFISAD na kutokua madarakaniI!
 
- Guys lets get on na the real ishu hapa, Regina ameandika kitabu chenye kurasa 15 baada ya mumewe kukimbia shutume tu za ufisadi ndani ya bunge, lets say ameandika kwa nia njema hiki kitabu ambacho uzinduzi wake umejumuisha wakuu wa taifa wa dini.

- Nia na madhumuni ilikuwa njema, swali je huyu mama amewahi kuandika vitabu vingapi katika maisha yake? Kwamba isiwe ajabu kwake kuandika hiki kitabu!

FMES!
 
..kwani ameandika nini kwenye kitabu chake?

..nadhani tunakuwa na haraka kidogo kuhukumu kabla ya kusoma kitabu chenyewe.
 
Ingekuwa vizuri Mama Regina Lowassa angeandika kitabu kinachoelezea jinsi mumewe alivyoanza ufisadi na ujambazi nchini Tanzania na ni kwa kiasi gani ameweza kuwaibia watanzania na kujitajirisha yeye binafsi na familia yake.

Teh hehe heheh,

Mkuu, labda kaandika kiduchu kuhusu hilo. Tusubiri kitabu hicho kikiingia street!
 
Nimemdharau sana Cardinal Pengo! this is too low kwake yeye kwenda kwa Lowasa kuzindua kitabu chenye kurasa 15 duuu! Ni kama assignments tulizo kuwa tunafanya Muhimbili enzi zileeee! Ametuabisha wakatoliki wote, naomba niweke wazi ile ni kauli yake binafsi muadhama kardinali Pengo " Watanzania waache tabia ya kusulubiana. "Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo haituwakilisi sisi wakatoliki..
 
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. “Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo,” alisema.

Hii ni kauli ya hatari sana kutoka kwa kiongozi wa kidini. Kwa literal interpretation anatuambia mafisadi wakiiibia nchi tunyamaze. This is very dangerous!

Hii kauli ni ya kifisadi. Kiongozi anayesimama kwenye nafasi ya Musa huwezi kutoa matamshi kama haya.

Aibu na fedheha kwa waumini wake!
 
No offense waJemeni:

Kama Mzee Jomo Kenyatta alivyosema. Wakoloni walipokuja waliwaambia waAfrika wafumbe macho, walipofumbua wakoloni wakawa wamechukua ardhi na waaAfrika wamebaki na dini. Sasa hivi macho tunafumbishwa na wenzetu. Remember, religion is the opiate of the masses.
 
Kuna haja ya kutohamaki. Gazeti limeandika "…kilikuwa na kurasa 15". Inawezekana sana kwamba walikosea wakaandika 15 badala ya 150. It would not be the first time. Ni vema kuthibitisha kurasa zake kabla ya kumdharau Mwandishi.

JF mnamsulubu Regina kwa "dhambi" ya Edward. Regina ni Mwanakondoo wa Kardinali Pengo. Ni Mkatoliki anayefuata dini yake kwa jitihada kubwa. Mchungaji Mwema huenda kwenye hafla ya mwanakondoo wake, hata kama hafla yenyewe ni ya kuzindua kitabu kidogo sana. Mnamsulubu Pengo kwa kumtembelea Muumini wake?

Jiulizeni kama aliyeandika dibaji ni mjinga. Lazima kuna kitu kizito sana kwenye hicho kitabu au kijarida.

I would advise caution. Why insult the prelates before knowing anything about what is written in the book, encyclical, poster, letter or whatever? Don't be quick to throw mud at others
 
Last edited:
......JF mnamsulubu Regina kwa “dhambi” ya Edward....
..Kwani hizo fweza alizokwiba Ngoyai hazijatumika na Regina?? Ushasahau sheria inavyosema kuhusu kutumia au kuhusika na mali iliyokwibwiwa?
"Hata shabiki ni mwanamichezo pia"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom