Mke wa Lowassa azindua kitabu

Mke wa Lowassa azindua kitabu

Jamani nachokiona hapo ni kutaka sifa,haya na huyo Mwakasege anaposema yeye ndo aliwashauri kuwa wakatembelee Israeli alikua na maana gani? Na hao maaskofu wanasema watu siku hizi wanasulubiana pia ana maana gani?Kwamba EL hakutendewa haki au? Nijuavyo aliyoyapata anastahili,na wala hakusulubiwa na mtu ni yeye mwenyewe aliyoyafanya ndo yalomsulubisha alijitundika mwenyewe,kingine nachokiona hapo ni kama vile kupigana vijembe kwa sababu anaposema watu wanasulubishana ina maana kuna watu fulani hapo wanasemwa ki-aina fulani,na huo ni usengenyaji kwa nini usimfate mtu live na kumwambia kuwa wewe acha kusulubisha wenzako kuliko kuanza kurusha maneno kwenye zinduzi kama hizo,Swali,walienda kuzindua kitabu au ndo walipata sehemu ya kutoa madukuduku yao?

Natatizika na kauli zao.

...walienda kupiga mipasho (siasa za bongo)
 
15 page book, that is a book with 7-8 leaves(sheet of paper),...ndio mkusanyiko wote huo?.... Kweli imani imekua pesa sikuhizi. Wangeitwa kwenye harambee ya albino nyalugusu si ajabu kila mmoja wa hao viongozi wangetoa udhuru na kutuma muwakilishi...

Maana ni kama chain, alianza wa zanzibar kwenye salamu za pasaka, maneno ya askofu shayo kuhusu mafisadi yanakuachia maswali mengi, kana kwamba hajui nchi hii inaendeshwa kishikaji na kwa kulindana. Huyu Lowassa anataka kucheza mchezo hatari sana wa karata ya dini. Watanzania tuwe macho. Mwalimu alituasa ukishaanza kula nyama ya binadamu hautaacha. Nanukuu "wao wabara sisi wa visiwani" halafu "wao wapemba sisi waunguja" halafu "wao wazanziBARA sisi wazanziBARI".
 


Ni mtizamo wako. Tukifikia hapo pa kutohoji lolote wafanyalo kwa kuwa tu wao ni viongozi wa dini, basi hata uumbaji aliyoifanya Mungu utakuwa hauna maana. Yafaa nini basi kujitofautisha na ng'ombe au hayawani mwingine?

Nakubaliana na wewe kabisa, kuhoji ni lazima kama binadamu, ila tusihukumu na kutukana kwenye hoja zetu.
 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. “Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo,” alisema.

.

Maneno mazito haya..ningependa Pengo atufafanulie anamaanisha nini. Maana kama nielewavyo kama Yesu hangesulubiwa akina sisi tusingepona. Sasa wasiposulubiwa watu wokovu utapatikana wapi? AU na yeye ameshakula ya mbuzi?
 

Mhubiri maarufu mwenye makazi yake mjini Arusha, Christopher Mwakasege, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema ni yeye aliyetoa wazo kwa Lowassa na mkewe kutembelea Israel baada ya matatizo yaliyowakuta.

COLOR]


Huyu naye inabidi atueleweshe hadi tuelewe, ni motive gani iliyomfanya awashauri waende kutembelea mahali patakatifu?
 

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, aliwahimiza watu kujenga moyo wa kupendana ili kujenga nchi yenye maelewano.


Maelewano hayana dili kama watu wanakwiba fedha za wanyonge halafu hawafanywi kitu, wanatunga vitabu vya uwongo na kweli, na mafarisayo wanakuja kuvibariki.
 


Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.

EL umepata matatizo gani? hebu tukumbushe. Kweli unaonekana hujatubu. Tuliopata matatizo ni sisi wavuja jasho kwa uroho wako.
 
Kwa atakayepata hiyo ripoti ya Israel naomba atuwekee hapa tuisome na sisi tupate kujua yaliyojiri huko mji mtakatifu!
 
GOD`S TRUTH IS MARCHING ON.


Wiki ya jana tulichangia mada inayohusu baadhi ya vingozi wa majumba ya ibada,leo tunashuhudia matokeo yake ni ya uwazi kabisa wanatumiliwa kutumia kivuli za dini kuficha maovu yao na maovu ya wanaowatumili na sio kufanya kazi za Mmungu kama wanavyodai :
Nilikuwa nasoma kijarida cha mwanakijiji hivi juzi kuna mahali aliandika kwa kusema hapa namnukuu moja kati ya makundi ndani ya CCM ni(Kundi ambalo limejikita katika sera za ubepari na wao neno ujamaa ni kinyaa kwao. Hawa wana nguvu moja kubwa nayo ni pesa. Wana uwezo wa kushawishi mtu yeyote wa makundi yale mawili ya mwanzo na wakiamua kutishia maslahi ya mtu huyo (aidha bungeni au vinginevyo) kundi hilo haliwezi kusita kufanya hivyo. Ni kundi ambalo kwa watu wengine tunaweza kusema ndilo lililoiteka nchi! )hapa binafsi naugana nae tumeshuhudia mara kwa mara watu wa aina hiyo kukimbilia nyumba za ibada. ukisoma maelezo ya maskofu hao utapatwa na hisia zitakazo kufanya kuamini hawa ni miongoni mwa wale rubuniwa kipesa au kimawazo, jinsi walivyo simama kidete kuwatete direct or indirect .kwa tarifa zenu ndugu wote hapa tusije tukashangaa siku moja kuona baadhi ya viongozi wa nyumba za ibada wakatowa kauli kama zile zinazotolewa na baadhi ya nchi za magharibi zinazowatete mashoga kuwa viongozi ndani ya majumba ya ibada na kusema madhali anamtumika mungu basi likubalike au kulifanya jambo hilo ni sehemu ya maisha yetu ,kusema hivyo inatoka na kile nilichokiita kubuniwa kwao kimawazo au kifedha, tuwe macho sio kila wanachokisema wao binafsi tukubaliano nao, hayo ni mawazo yao wenywe lakini jee ndani ya dini wanazozitumikia zinaamrisha nini inapofikia maswala kama hayo?
 
Last edited:
Mke wa Lowassa azindua kitabu

Na Mwandishi Wetu,
MTANZANIA, Aprili 15, 2009.

Watu mbali mbali jana jioni walimiminika nyumbani kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kushuhudia uzinduzi wa kitabu kilichotungwa na mkewe Regina, uliofanywa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Regina aliandika kitabu hicho wakati akiwa katika matembezi binafsi inchini Israel, siku chache baada ya mumewe kujiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka jana kutokana na sakata la Richmond.

Kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kiitwacho “Walk The Path With Diary in Israel, The Holy Land” kina kurasa 15 na dibaji yake imeandikwa na Monsinyori Julian Kangalawe kutoka Kanisa la Mtakatifu Joseph la Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. “Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo,” alisema.

Mhubiri maarufu mwenye makazi yake mjini Arusha, Christopher Mwakasege, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema ni yeye aliyetoa wazo kwa Lowassa na mkewe kutembelea Israel baada ya matatizo yaliyowakuta.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, aliwahimiza watu kujenga moyo wa kupendana ili kujenga nchi yenye maelewano.

Mbali na Mlasasusa, Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ni Pwani, Elinaza Sendoro, pia alihudhuria hafla hiyo, na akatumia nafasi hiyo kuwashawishi watu kutembelea Israel kujionea namna watu wa dini tofauti wanavyoishi.

Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.
Mungu wangu siamini ninayoyasoma...
 
X: Darling i want to write a 15 page encyclopedia

Y: Dont worry swty heart just do it i have money and i dont know where to spend it..

🙁
 
Halafu mambo haya yanafanyika katika wiki ya kumuenzi mwalimu....shame on you!!!
 
Naelekea kufikiri Fedha ni kama Mbolea hivi,.....ukairundika na kuiacha pahala pamoja kwa muda mrefu basi hutoa harufu mbaya sana,ila ukaitawanya sehemu mbaliX2 matokeo yake ni ustawi maradufu!
Tuwe waangalifu sana na huyu Bwana EL,he knows Tanzania is the only place in the World where Everything is Possible!!
 
safi sana, Mungu ibariki Israel, Mungu saidia kuwamaliza maadui wa Israel woooote. amin.
 
hiyo hela ni ndogo sana. hapa tumlaumu Lowasa kwa kula hela, ila mkewe hana kosa. mkewe ana kosa gani? mwizi ni mumewe, yeye amefanya nini? namfagilia kwa kwenda israel nchi ambayo mimi naipenda na kuithamini kuliko hata tanzania.
 
Back
Top Bottom