Mke na Mumewe wanafanana.... Kuna ukweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke na Mumewe wanafanana.... Kuna ukweli?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SG8, Oct 14, 2011.

 1. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Wakuu natumaini wote muwazima wa afya!!!!

  Leo naomba wataalam wa mahusiano na saikolojia mnisaidie kuondokana na utata huu!

  Ni muda sasa nimekuwa nikisikia kuwa Wana ndoa wakiishi pamoja baada ya muda fulani hufikia kiwango cha kufanana (kwa sura). Nimesikia mara kadhaaa na mimi nahisi kama kuwa watu ninao wafahamu wanaofanana (wana ndoa).

  Lakini cha ajabu zaidi ya watu watatu nao wameniambia "wewe (Mimi) umefanana na Mkeo", nikashtuka sana. Inakuwaje nifananane na mtu ambaye nilikutana naye akiwa mtu mzima tayari? Na ndoa yenyewe ndio kwanza ina miaka mitano tu?

  Wataalam naomba mnijuze nini kinasababisha watu (wana ndoa) waonekane kama wanafanana? na je dhana hii ni ya kweli au ni upofu wa macho yetu tu?
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,097
  Trophy Points: 280
  hakuna saikolojia au jingine ila maelekezo ya Muumba ya kuwa wakiooana wanakuwa mwili mmoja.........................na mwili mmoja ni lazima ufanane kifikra na kimatendo..........wakishindwa kuwa hivyo......................basi migongano huanza na mwishowe wake wanaachana.........

  ingawaje wapo wanaosema..............ya kuwa wapenzi hupenda kuolewa na wale wenye sura zinazofanana na za wazazi wao........................upo huo ukweli ingawaje siyo wote.....................wapo ambao wanasema kutokana na watoto watu huanza kuona sura za wazazi zinashahibiana....................tough call
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye mstari umesema kweli kabisa. Kwa kawaida watu wanavutiwa na watu wanaofanana kwa sura au tabia na wazazi wao au na ndugu zao (kaka/dada). Sura za aina hiyo zikijitokeza inakuwa kama sumaku mbele ya chuma. Inakuwa rahisi sana kujenga uhusiano na watu wa aina hiyo. Kimantiki, wale wanaofanana wa wazazi wetu mara nyingi wanafanana na sisi pia kwani sisi tunakuwa tumerithi mengi kutoka kwa wazazi wetu vikiwemo sura na hata tabia.
   
 4. Matango

  Matango JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli japo kwa ushahidi wa uzoefu wa maisha. Unavutiwa na mwanamke au mwanaumme bila ya wewe kujua kuwa kilichokuvutia ni maumbile fulani mnayofanmana ninyi wawili. Na kadiri mtakavyoishi kuna tabia zitakuwa moja yaani mtafanana hata kwa aina fulani za tabia.
   
 5. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wanakuja kufanana kimawazo tu, sio sura.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,097
  Trophy Points: 280
  kuna jamaa yangu wa karibu sana huwa nikimwangalia yeye na mkeo ninaonakama kaka na dada yake.........................huwa ninajiuliza hivi hii imekaaje? Lakini kabla dunia haijaumbwa hizi safari ambazo huwa tunazililia kumbe Muumba alitupangia kabla kuwa ni lazima tuzipite........
   
 7. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Khaaaa! sina hakika kama kuna ukweli hapa hasa kwa upande wangu. Kuhusu watoto ajabu ni kwamba wote waliosema mimi nafanana na My Wife wangu tunafanana hawajawahi kumwona mtoto wangu hii inakaaje?
   
 8. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  oooh! God.....ina maana nitakuja kufanana na huu mpapule ulo lala pembeni yangu??
   
 9. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  hiyo ni kweli hutokea na ni sababu za kawaida kabisa za mtu kujipenda mwenyewe
  1) Mara nyingi mtu huwa anajijua Sura yake ama kwenye picha ama Kioo, sasa anapokutana na mtu mwenye sura kama yake anagerate ile hali ya kujipenda mwenyewe (na kuona yule mwenzie ni kama yeye)

  2) Mwenza kufanana na ndugu wa karibu wa mwenzie (Baba, Mama, Kaka nk)
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Rejea Thead hii, yaweza kujibu swali lako:

  https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/160484-mabinti-hawa-huolewa-na-baba-zao.html
   
 11. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  dah mkuu....god forbid asije akagundua huo ndio wasifu wake ulimtunuku.
   
 12. a

  alph Member

  #12
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mbona wewe pua yako ndefu na ya kwake fupi? labda mmefanana mawazo tu,
   
 13. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Labda kwa kuwa wanaonekana pamoja muda mwingi na akili ina uvivu wa kupembua inaamua ku conclude A=B.

  Ni sawa na watu wanaosema wachina wanafanana wakati in real sense hawafanani ila ni hulka yetu ya kurahisisha mambo. Hata mapacha hawafanani ila hatutaki kuangalia tofauti; ukiuliza marafiki wa mapacha watakwambia wanawatofautisha bila shida yoyote.
   
 14. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inasemekana kua wanaume wenye upendo mkubwa kwa mama zao wanavutiwa na wanawake wenye kumfanana mama. Na kama wewe na mama yako mmefanana basi inakua hivo. kufanana huko kutaendelea kadri unavo zidi kumsifia kila akivaa/akijiremba kama vile mama yako. Ila sio rahisi kwako kutambua kua ni sababu kamfanana mama ndio amependeza.
  The opposite is also true, maybe unamfanana baba yake na anakupa compliments kila ukisema au ukivaa kama baba yake. with time wewe na yeye mnafanana...
   
 15. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Hapo nakubaliana na wewe kabisa!
   
 16. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Haya wajameni naona mitazamo mbalimbali, japo kwangu ni bila bila
   
 17. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  makuuubwa!
   
Loading...