Mke na mume sio ndugu, lakini uhusiano wao ni mkubwa na una nguvu kushinda uhusiano wa ndugu wa kuzaliwa

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,154
33,366
Haya ni mawazo yangu.

Mume na mke sio ndugu kabisa, ni Aina ya uhusiano wa kipekee kabisa,uhusiano wa Hawa watu wawili ni uhusiano wenye nguvu na mkubwa Sana kushinda uhusiano wa ndugu wa kuzaliwa tumbo moja.kushinda uhusiano wa baba na mtoto,au marafiki wawili. Lakini pamoja na uzito wa uhusiano huu bado unaweza kuvunjika.

Hali hii ya kuvunjika inaweza kutokea kwa uhusiano mwingine wowote. Mfano Kaka na mdogo wake,baba na mtoto,mama na mtoto,Kaka na dada ama ndugu wengine ama marafiki, wanaweza kufarakana na wasiongee Wala kuwasiliana milele. Uhusiano wa mke na mume unaweza kufuatiwa na uhusiano wa mtoto na mzazi. Uhusiano wa mume na mke unapata nguvu kwa sababu zifuatazo.

Mke na mume katika mahusiano yao wanafanya Mambo mazito kuliko Mambo ambayo yanfanywa na uhusiano wa watu wengine. Mfano kulala uchi pamoja, Kufanya tendo la ndoa,kitendo Cha kufanya mapenzi ni Jambo kubwa Sana na la ajabu Sana.

Unaweza ukamuona mtu unaemheshimu Sana akiwa njiani ama kazini,mfano mwalimu wako ,waziri Fulani,mkuu wako,ama kiongozi wako wa dini akiwa katika hali yake ya kawaida,anaonekana mtulivu ama mkorofi,lakini lakini muonekano huo ni tofauti kabisa na akiwa anafanya mapenzi.

Anayejua hali anayikua nayo mmoja wa wawili Hawa ni mwenza wake ,yaani mume wake ama mke wake.Baba,mama,ndugu na wengine hawajui hali anayikua nayo akiwa katika dimbwi la mapenzi.

Hali hi ndio inafanya uhusiano wa wawili Hawa kuwa wa kipekee kabisa. Kuuguzana wakati wa magonjwa makubwa na madogo, Kuvumilia shida katika maisha yao. Kuna hali anakua nayo mmoja wa watu Hawa akiwa katika changamoto ama shida ama magonjwa,hakuna mtu mwingine awezae kujua hali hiyo zaidi ya mke ama mme. Kuuguzana.wazazi,Ndugu jamaa na marafiki wanaweza kusaidia tu,lakini mateso yote ya kuuguzana wanayapata wenyewe.

Kufurahia raha katika maisha yao, Hakuna awezae kujua kiwango Cha raha Kati ya wawili Hawa.

Furaha ya kupata watoto,

Kupeana raha nyingine,

Kutiana moyo wakati wa shida,

Kugombana na kupatana,

Kujuana mapungufu katika maisha, Mfano wakati wakiwa wamelala,baadhi ya watu huonesha tabia za ajabuajabu Sana,lakini mke na mme huhifadhiana. Uhusiano mwingine unaofuata uhusiano huu ni wa:_

Mzazi na mtoto,

Ndugu kwa ndugu,

Marafiki na

Jamaa.

Natanguliza shukurani.
 
Haya ni mawazo yangu.

Mume na mke sio ndugu kabisa,ni Aina ya uhusiano wa kipekee kabisa,uhusiano wa Hawa watu wawili ni uhusiano wenye nguvu na mkubwa Sana kushinda uhusiano wa ndugu wa kuzaliwa tumbo moja.kushinda uhusiano wa baba na mtoto,au marafiki wawili.
Lakini pamoja na uzito wa uhusiano huu bado unaweza kuvunjika.
Uko sahihi kabisa mkuu..ndoa ni taasisi
 
Yaaani mume na mke ni zaidi ya ndugu kwasababu ni kitu kimoja (mwili mmoja) sawa sawa na maandiko.
Lakini mke au mume na ndugu zake ni vitu viwili ambavyo ni tofauti

Tatizo linakuja watu wengi wanatumia akili zao kuchagua badala ya Mungu, hawa wenza halafu mtu anakuja kwa biti kubwa.Eti usioe au kuolewa
 
Bado hujaingia ktk kifungo Cha Ndoa ukauona Moto wake, mke na mume si ndugu kabisa, umezungumzia upande wa Ndoa changa ya kilokole

Nenda Ndoa za kimila, za mitala mwenye wake wengi ndio utaona Moto, wake zako kukuzunguka kuletewa watoto wa nje. Au mke kuhamisha Mali na kupeleka kwao km nyumba au gari kwa pesa yake kumpa baba yake kwa sababu tu wewe Marioo

Ndugu wa damu hawaachani asilani, usimuone mkeo kagombana na nduguze ukasema hawapatani, hebu mnyime asiende msibani kwao km hakutoroka, au nenda naye km hukusikia kijana aliyefariki ni mtoto wa kwanza wa mkeo, ndugu zake walikuficha.

Kua uyaone damu nzito
 
Mume na mke sio ndugu kabisa, ni Aina ya uhusiano wa kipekee kabisa,uhusiano wa Hawa watu wawili ni uhusiano wenye nguvu na mkubwa Sana kushinda uhusiano wa ndugu wa kuzaliwa tumbo moja.kushinda uhusiano wa baba na mtoto,au marafiki wawili.
Ndivyo inapaswa kuwa, lakini uhalisia mara nyingi huwa kinyume kwa sababa ya kutoaminiana
 
Waluguru wanasema undugu wa mume na mke ni wa Shuka. Akimaanisha pale mnapofanya tendo la ndoa. Shuka likitoka hamna kitu.
 
Back
Top Bottom