Mke kaniweka njia panda, naombeni ushauri

Mke wako alichepuka..
Kama unapenda mfe wote mapema na kuacha watoto bila wazazi.. basi kuwa mjinga

Mnunulie matoi umsaidie muyachezee.. kumfikisha bila wewe kupata hayo..

Pole na kila la kheri, anatishia kujiua labda aliyempatia ni mtu wako wa karibu.. ndio maisha jipende..

Jua hawezi kujiua bali anatumia kama njia ya kutokukuambia ukweli.. huku yeye na wake wanajua. Au labda alikuwa analala na wengi wampe maraha na pesa na hajui yupi alimpa
Kabsaa anapaswa amwambie mwenzie ukwel na sio kutishia kujiua akat anajua alipoutoa kama alibakwa au nn aseme mwenzie ajue!
 
Chukua hatua acha uzembe kisa papuch upate ngoma, wakat yeye kaenda kuitafuta mwenyewe na wewe unampokea unataka muipige wote acha kutuaibisha kama anataka kujiua mwambie atakua kapunguza mzigo
 
Mimi ni mwanaume wa miaka 35, nilioa mwaka 2009 kabla ya kuoana tulipima na wote tulionekana tupo salama.

Tukazaa watoto wawili, mwaka 2013 mke alianza kuumwa, alikuwa anatibiwa homa inarudia rudia, baada ya hali kuzidi akashauriwa kupima ukimwi mwaka 2015 na ndipo akagundulika kuwa ameathirika, na mimi nikapima zaidi ya mara tatu nikaonekana ni negative.

Kwa muda wote huo tumekuwa tukitumia mipira katika tendo la ndoa kimsingi tangu nilivyooa sikuwahi kuchepuka shida niliyonayo mimi kwa sasa najawa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi nimepungua kiukweli, sioni radha yoyote kwenye tendo, sipati msisimko wowote kwake moyo umekufa kabisa.

Nikiwa nae karibu ndio najawa na mawazo, sioni mapenzi yoyote kwake kibaya zaidi hajawahi kuniambia alipataje na nikimuuliza anaanza kulia hadi kuchukua sumu kutishia kujiua ninashindwa nifanyaje nikijiangalia na umri wangu bado mdogo.

Naomba ushauri wenu wadau nifanyaje kwa sababu yeye anaonekana ana njaa kubwa ya tendo la ndoa na mimi hali ndio hivo.
Duh...kama ni kweli unachosema nakushauri usimwaache kwa kuwa mlipima kabla ya ndoa na mlikuwa salama maana yake alikuwa anachepuka; hivyo basi usimwambia mshauri aendelee na huyo jamaa au watu wengine kimahusiano ila usimfukuze mtunze kama kawaidi bali aendelee na hao wanaume wake.
 
Kinachoua watu kwenye ukimwi, ni ujinga kuhusu ukimwi. Hicho ndicho kinachoongoza kuua, kwa maelezo ya awali uliyoyatoa pamoja na ushauri uliotolewa unaonyesha kiwango cha ujinga kuhusu ukimwi.

Kwenye ukimwi kuna watu wanabeba vimelea vya ukimwi na wao kutokuonyesha wala vidudu kuonekana wakati wa kupima, hawa watu ndio wanasayansi wanatafuta kujua jinsi gani ya kupata vimelea walivyonavyo na kuwawekea wengine ili kuwa ni kinga ya kila mtu, hivyo kunekana kwako kuwa huna inawezekana na wewe ni kati ya watu wenye vimelea hivyo naturally.

Kuna familia moja mume ni mwenye VVU kwa muda mrefu na mke anazaa naye lakini mke wake hajawahi wala hajapata hivyo vijidudu.

Kwa hiyo ndugu yangu inawezekana huo ushauri wa kwenda kwa mwingine ni wa kukuambia kawaambukize wengine.

Huyo mke wako atakufa haraka sio kwa VVU bali kwa mawazo yanayotokana na masimango, masimango hayo chanzo chake ni kufikiria kupata kwake ukimwi kumetokana na kuchepuka kisa wewe huna, hivyo kifikra kapata kwingine.

Kupima mwanzoni mlipima kujua kama mnavyo au la lakini hamkupima kama kuna mbebaji asiyedhurika au kuonyesha amebeba.

Utakapokwenda kwenye kikao cha familia usishangae watano kati ya kumi uliowaita kwenye kikao nao ni waathirika wanaotumia dawa ila hawajakuambia.

Kuna magonjwa mbalimbali yanayotumia dawa kila siku, kisukari, moyo, heartitis B na mengine kwa wagonjwa wote hao niliowataja wanaotumia dawa hao watakuwa wa kwanza kufa kabla ya mkeo kama wote wataendelea kutumia dawa kama walivyoshauriwa. Mwambie mkeo atumie dawa na wewe usiwe sehemu ya kumnyanyasa.
Safi sana umemaliza kila kitu
 
Ushauri wa dhahabu huu

Tafuta mke mwengine
ila huyo,usimuache kumuhudumia
kwasababu ni Mama watoto wako
anaweza akawa ameupata kwa njia tofauti na ngono

SI KILA ALIEAMBUKIZWA UKIMWI,ALIUPATA KWA NJIA YA NGONO

mtunze ndg
tuna na watt wako
ila tendo la ndoa.....noooooooopp
Unajua wengi wanamshauri wamuache ila ukigeuza upande wa pili huyo ni mke na ni mama watoto, watu wanajifikiria wao binafsi bila kufikiri mustakabadhi mzima wa watoto watakaoish mbali na baba yao. Na hata akioa mwanamke mwingine hawezi kushangaa chanzo cha yote ni yeye.
 
Inakuwaje tangu 2013 hadi 2015 apime yeye awe na tatizo;halafu wewe huna.Kwa kipindi hicho chote wewe ulikuwa na mahusiano na nani?
 
Kama muislam oa mke wa pili, muhimu usimnyanyapae tu. Mjali, mthamini ila akili kichwani ukimuendekeza huyo kichwa asie na ubongo utaumia, haja zako zitimize kwingine umri wako bado usijidhulumu lakini pia fikiria ingekuwa wewe unao yeye hana ungependa afanyeje..
 
Inawezekana mlipopima kabla ya ndoa mke wako alikuwa kwenye window period kwa vile vipimo vya zamani mngepima tena baada ya miezi mitatu angejulikana.

🏾Nenda nae kwenye kitengo siku ya clinic yake na uombe kuongea na daktari wake nyinyi wawili tu. Kwasababu ndiye anaemuelewa magonjwa wake atakupa majibu ya maswali yako mengi.
Window period si miezi mitatu na kitu hivi??..huyo possibility kubwa kauleta baada ya ndoa
 
Sijawahi kusikia binadamu wa aina yako, wala sikutarajia. Umewahi kujiuliza, ungekuwa wewe ndio muathirika, yeye hana huo ugonjwa angekuwa bado yupo kwako??

Yaaani Kondomu ya tsh 500 ndio unaamini inaweza kukukinga na ukimwi ambao mkeo anao na unafahamu??

Binadamu tumeumbwa tofauti, na hakika wewe ni wa tofauti.

Subiri akuambukize ndio utaona kama anataka kujiua kweli au anataka mfanane.

Naomba niseme (kwa mtazamo wangu binafsi) wewe ni binadamu MJINGA kweli kweli.

Sina ushauri mkuu
 
Anyway, nawashukuru kwa ushauri wenu wadau, kuna watu wamesema nimsamehe maisha yaendelee, Kama umenisoma vizuri utaona tangu 2015 hadi leo ni muda umepita, kimsingi nilimsamehe na kukubali hali iliyopo. Lakini kwa nini sasa na kwa nini nauliza ushauri kwa wadau ni kwamba nimeona zipo Dalili kuwa bado anawasiliana na watu wake. Wiki mbili zilizopita nilichukua simu yake alipokuwa kuoga asubuhi saa 12, nikaona meseji ya kimahusiano toka kwa mtu, sikumuuliza ile asubuhi,,, jioni nikaangalia simu yake nikaona ile sms ameifuta ila alimjibu kuwa "nitakupigia my" na mengine na ni kweli calls zake inaonekana alimpigia. Nilimuuliza aniambie ni nani alimtumia sms asubuhi na aniambie ilisemaje, alikataa kata kata kuwa hakutumiwa meseji yoyote ile,,, sasa hapo kabla ya ile sms alikuwa anaongea na mtu mwingine usiku kama saa nne hivi usiku mimi nikiwa sebuleni yeye chumbani maongezi yao niliyashitukia, nilipomuuliza alikuwa anaongea na nani na walikuwa wanaongea nini alinijibu sio lazima nijue kila anachoongea. Sasa hapo ndipo msamaha niliokuwa nimeutoa kabla natafakari ndio njia panda ilipo wapendwa.

Duh pole sana

Uamuzi ni wako.. ila ndio maisha hayo.. kuna binadamu wana roho ngumu.. hakupendi huyo..
 
Duh...kama ni kweli unachosema nakushauri usimwaache kwa kuwa mlipima kabla ya ndoa na mlikuwa salama maana yake alikuwa anachepuka; hivyo basi usimwambia mshauri aendelee na huyo jamaa au watu wengine kimahusiano ila usimfukuze mtunze kama kawaidi bali aendelee na hao wanaume wake.
Hii Ni hatari zaidi kuliko kuamua kuishi kila mtu nyumba yake.
Mwanamke akiamua kubadilika Ni mnyama.
Anaweza kukuua any minute.
Wakae wakubaliane tu namna nzuri watatunza watoto.
Hakuna haja ya kuishi nyumba moja kila mtu anarudi muda anaoutaka kutoka kwenye mishe zake.
 
Mkuu kupata "ukimwi" siyo mwisho wa maisha, tena siku hizi kuna ARV'S basi imekuwa rahisi sana kukabiliana na hili gonjwa. Ushauri wangu kwako usimwache mkeo, mpende, mtunze, muheshimu. Fahamu kwamba "rehema"(huruma) ni kitu muhimu sana, tena sana.

Kwetu sisi tuliofundishwa dini, imeandikwa hivi; "rehema itaizidi hukumu"... tena kuna mahali pia imeandikwa hivi; "sitaki sadaka bali nataka rehema". Maana yake ni kwamba Wanadamu tunatakiwa kuwa na huruma kuliko chochote kile.

Mkuu muhurumie Mkeo hata kama ameleta ugonjwa ndani ya nyumba, huwezi kujua nani kati ya wewe au yeye atakayetangulia. Anaweza akawa na Ukimwi lakini wewe ambaye ni mzima ukafa kwa sababu zingine tu na kumuacha yeye akiendelea kula maisha.


Msamehe, Mhurumie tena mhurumie kabisa. Kuna njia ya kufanya naye tendo la ndoa pasipo wewe kuambukizwa, tumia njia hiyo na mpende mkeo mpaka kifo kitakapo watenganisha.

Msaidie aanze kutumia dawa za ARV'S mapema kabisa, tena uwe unahakikisha amemeza hicho kidonge kimoja kila siku. Mtangulize MUNGU mbele na siku zote itegemee "imani" ya YESU KRISTO na hakika maisha yenu wewe na mkeo yatakuwa sawa tu. Narudia tena, ukimwi siyo mwisho wa maisha, bali ni mwanzo wa maisha mapya kati yenu.
 
Angalia sana maamuzi yako.

1. Huyo ni mke wako, mpende na umthamini.

2. Kama una wasiwasi na uaminifu wake, muwekee app ya kutrace calls zake na message. Mambo ya kuulizana ili upate ukweli ni mambo ya kizamani.

2. Japo yeye ni HIV positive, lakini unaweza ukatangulia kufa na kumwacha. Mtreat vizuri, usije ukashangaa siku unaumwa hata chooni huwezi kwenda lakini akawa ndiye msaada wako.

3. Kacheck status za watoto kama wapo ok au vipi.

4. Huu ndiyo muda wa kutengeneza future ya watoto na uache kulalamika na kuwaza, mshukuru Mungu kwa kuepusha na hayo matatizo.
 
Back
Top Bottom