Anyway, nawashukuru kwa ushauri wenu wadau, kuna watu wamesema nimsamehe maisha yaendelee, Kama umenisoma vizuri utaona tangu 2015 hadi leo ni muda umepita, kimsingi nilimsamehe na kukubali hali iliyopo. Lakini kwa nini sasa na kwa nini nauliza ushauri kwa wadau ni kwamba nimeona zipo Dalili kuwa bado anawasiliana na watu wake. Wiki mbili zilizopita nilichukua simu yake alipokuwa kuoga asubuhi saa 12, nikaona meseji ya kimahusiano toka kwa mtu, sikumuuliza ile asubuhi,,, jioni nikaangalia simu yake nikaona ile sms ameifuta ila alimjibu kuwa "nitakupigia my" na mengine na ni kweli calls zake inaonekana alimpigia. Nilimuuliza aniambie ni nani alimtumia sms asubuhi na aniambie ilisemaje, alikataa kata kata kuwa hakutumiwa meseji yoyote ile,,, sasa hapo kabla ya ile sms alikuwa anaongea na mtu mwingine usiku kama saa nne hivi usiku mimi nikiwa sebuleni yeye chumbani maongezi yao niliyashitukia, nilipomuuliza alikuwa anaongea na nani na walikuwa wanaongea nini alinijibu sio lazima nijue kila anachoongea. Sasa hapo ndipo msamaha niliokuwa nimeutoa kabla natafakari ndio njia panda ilipo wapendwa.