Mke kaniweka njia panda, naombeni ushauri

Mke kaniweka njia panda, naombeni ushauri

Pole sana, tunaopenda kuteleza jamani tuache!
 
Hii Ni hatari zaidi kuliko kuamua kuishi kila mtu nyumba yake.
Mwanamke akiamua kubadilika Ni mnyama.
Anaweza kukuua any minute.
Wakae wakubaliane tu namna nzuri watatunza watoto.
Hakuna haja ya kuishi nyumba moja kila mtu anarudi muda anaoutaka kutoka kwenye mishe zake.
sijui bwana..
 
Mimi ni mwanaume wa miaka 35, nilioa mwaka 2009 kabla ya kuoana tulipima na wote tulionekana tupo salama.

Tukazaa watoto wawili, mwaka 2013 mke alianza kuumwa, alikuwa anatibiwa homa inarudia rudia, baada ya hali kuzidi akashauriwa kupima ukimwi mwaka 2015 na ndipo akagundulika kuwa ameathirika, na mimi nikapima zaidi ya mara tatu nikaonekana ni negative.

Kwa muda wote huo tumekuwa tukitumia mipira katika tendo la ndoa kimsingi tangu nilivyooa sikuwahi kuchepuka shida niliyonayo mimi kwa sasa najawa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi nimepungua kiukweli, sioni radha yoyote kwenye tendo, sipati msisimko wowote kwake moyo umekufa kabisa.

Nikiwa nae karibu ndio najawa na mawazo, sioni mapenzi yoyote kwake kibaya zaidi hajawahi kuniambia alipataje na nikimuuliza anaanza kulia hadi kuchukua sumu kutishia kujiua ninashindwa nifanyaje nikijiangalia na umri wangu bado mdogo.

Naomba ushauri wenu wadau nifanyaje kwa sababu yeye anaonekana ana njaa kubwa ya tendo la ndoa na mimi hali ndio hivo.
 
Mkuu ni Thread Umeirudia? au umecopy na Kupaste, Maana niliona uzi huo Jf juzi!
 
Pole sana kiongozi ila kuna dozi ya ARV ambayo imegundulika kua ikitumiwa na mtu aliye kwenye hatari ya kupata maambukizi basi inafanya kazi kama kinga yaani ikitumika mtu huwezi kupata maambukizi. Ningekushauri ufike hospitali ya taifa au wilaya uonane na wataalamu naamini upo kwenye kundi hilo ambalo unatakiwa ujikinge na uwezekano wowote wa kupata maambukizi. Kwa jina nakumbuka nilisikia inaitwa truvada kwenye makala moja ya bbc. Kwa kuanzia tuu huo ndio ushauri wangu kwako.
 
Mimi ni mwanaume wa miaka 35, nilioa mwaka 2009 kabla ya kuoana tulipima na wote tulionekana tupo salama.

Tukazaa watoto wawili, mwaka 2013 mke alianza kuumwa, alikuwa anatibiwa homa inarudia rudia, baada ya hali kuzidi akashauriwa kupima ukimwi mwaka 2015 na ndipo akagundulika kuwa ameathirika, na mimi nikapima zaidi ya mara tatu nikaonekana ni negative.

Kwa muda wote huo tumekuwa tukitumia mipira katika tendo la ndoa kimsingi tangu nilivyooa sikuwahi kuchepuka shida niliyonayo mimi kwa sasa najawa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi nimepungua kiukweli, sioni radha yoyote kwenye tendo, sipati msisimko wowote kwake moyo umekufa kabisa.

Nikiwa nae karibu ndio najawa na mawazo, sioni mapenzi yoyote kwake kibaya zaidi hajawahi kuniambia alipataje na nikimuuliza anaanza kulia hadi kuchukua sumu kutishia kujiua ninashindwa nifanyaje nikijiangalia na umri wangu bado mdogo.

Naomba ushauri wenu wadau nifanyaje kwa sababu yeye anaonekana ana njaa kubwa ya tendo la ndoa na mimi hali ndio hivo.
Duuuh pole mkuu.
 
mwanamke alichepuka uyo ndo mana hatoi jibu anabaki kulia lia tu hapo
 
Acha kurudia rudia uzi
Naona unatuchora
Acha hiyo tabia Mara moja
Naona unataka kukumbatia mzinga wa nyuki mchana
 
Mimi ni mwanaume wa miaka 35, nilioa mwaka 2009 kabla ya kuoana tulipima na wote tulionekana tupo salama.

Tukazaa watoto wawili, mwaka 2013 mke alianza kuumwa, alikuwa anatibiwa homa inarudia rudia, baada ya hali kuzidi akashauriwa kupima ukimwi mwaka 2015 na ndipo akagundulika kuwa ameathirika, na mimi nikapima zaidi ya mara tatu nikaonekana ni negative.

Kwa muda wote huo tumekuwa tukitumia mipira katika tendo la ndoa kimsingi tangu nilivyooa sikuwahi kuchepuka shida niliyonayo mimi kwa sasa najawa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi nimepungua kiukweli, sioni radha yoyote kwenye tendo, sipati msisimko wowote kwake moyo umekufa kabisa.

Nikiwa nae karibu ndio najawa na mawazo, sioni mapenzi yoyote kwake kibaya zaidi hajawahi kuniambia alipataje na nikimuuliza anaanza kulia hadi kuchukua sumu kutishia kujiua ninashindwa nifanyaje nikijiangalia na umri wangu bado mdogo.

Naomba ushauri wenu wadau nifanyaje kwa sababu yeye anaonekana ana njaa kubwa ya tendo la ndoa na mimi hali ndio hivo.
fanya kazi
 
Kwanza pole sana mkuu na mtihani mzito ulioupata, na nisingependa kukutolea maneno makali kwa huo mtihani uliopata kama wenzangu.

Wito wangu kwa wachangiaji wa huu uzi, tuwe wastaarabu na si kutoa maneno makali kwa mtu anaeomba ushauri, kwani si kosa kurudia uzi JF.

Pili, naamini miongoni mwa watu wanaouma pindi wanapopatwa na janga ni wazazi, watoto na mke/mume.

Huyu mwenzetu kaishakiri kua ana "msongo wa mawazo" na mpaka ameathirika kisaikolojia na kimwili, hakika ana mtihani mzito sana, ningependa tumtafutie sababu za kumtetea kwa hilo jambo aliofanya la kurudia uzi, badala ya kumtolea maneno makali.

Ushauri wangu kwako,

Wewe na mkeo mnahitaji msaada wa daktari wa maswala ya saikolojia, ili awasaidie kuwapa ushauri juu ya hilo janga mlilopata na vipi mtauvuka/mtaukabili huo mtihani kimaisha, ili muendelee na maisha yenu ya mbele.

Mkeo pia anahitaji support yako kwanza kimawazo, kifikra na kimaisha, wewe ndio mwenye funguo ya akili na fikra zake kwa sasa, kama utamuongezea mawazo na kusonona kwa kumuuliza maswali magumu, kumtolea maneno makali, au kumtenga kwa muda, basi anaweza akafanya maamuzi magumu yakakuvuruga hata wewe na watoto kisaikolojia zaidi. Cha msingi mtulize kifikra, ili akili yake ikubaliane na tatizo hilo na akubali kupambana nalo maishani. (Akili yake nahisi haitakua imekubaliana na matokeo kamili ya mtihani huo)

Pia mkeo anahitaji ushauri nasaha kwa wataalamu wa maradhi hayo, pia wamuanzishe dose ya dawa na kumpa elimu juu ya hilo tatizo.
 
Wapendwa Mungu awabariki sana kwa ushauri wenu mlionipa, nimepata elimu ya kutosha kabisa juu tatizo langu. Wengi wenu mlitoa ushauri kwa kuchukulia kama ni tatizo lenu na kutoa maoni stahiki, ninawashukuru sana. Kufikia hapa nimeshapata mwelekeo wa ninachotakiwa kufanya. Niwaahidi kuwa naufanyia kazi ushauri wenu, mmenipa dawa kamili kabisa ya kutetea afya yangu na maisha yangu. Mungu awabariki sana, Asanteni.
 
Anyway, nawashukuru kwa ushauri wenu wadau, kuna watu wamesema nimsamehe maisha yaendelee, Kama umenisoma vizuri utaona tangu 2015 hadi leo ni muda umepita, kimsingi nilimsamehe na kukubali hali iliyopo. Lakini kwa nini sasa na kwa nini nauliza ushauri kwa wadau ni kwamba nimeona zipo Dalili kuwa bado anawasiliana na watu wake. Wiki mbili zilizopita nilichukua simu yake alipokuwa kuoga asubuhi saa 12, nikaona meseji ya kimahusiano toka kwa mtu, sikumuuliza ile asubuhi,,, jioni nikaangalia simu yake nikaona ile sms ameifuta ila alimjibu kuwa "nitakupigia my" na mengine na ni kweli calls zake inaonekana alimpigia. Nilimuuliza aniambie ni nani alimtumia sms asubuhi na aniambie ilisemaje, alikataa kata kata kuwa hakutumiwa meseji yoyote ile,,, sasa hapo kabla ya ile sms alikuwa anaongea na mtu mwingine usiku kama saa nne hivi usiku mimi nikiwa sebuleni yeye chumbani maongezi yao niliyashitukia, nilipomuuliza alikuwa anaongea na nani na walikuwa wanaongea nini alinijibu sio lazima nijue kila anachoongea. Sasa hapo ndipo msamaha niliokuwa nimeutoa kabla natafakari ndio njia panda ilipo wapendwa.
Wewe ni fala, sikushauri tena. Endelea na ujinga wako na kama ni jirani yangu tutatumia matatizo yako kujifunza. Hovyo kabisa wewe kijana.
 
nijibu maswali haya mkuu

mkeo ana umri gani?
je watoto wenu mmewapima pia?
huyu mke ni wa aina gani? mvumilivu? mlitafuta pamoja au alikukuta upo vizuri?
ulimtoa katika mazingira yepi? kabla hujafikia uamuzi wa kumuoa?
wewe unahisi huu ugonjwa ameupata ndani ya ndoa?
kwanini ukimuuliza analia?
hata ukipata ushauri kutoka kwa malaika, hautokuwa sawa kama wewe mwenyewe haupo tayari kuzikabili hizo changamoto, na mwisho wa siku unaweza kutangulia wewe kwa mawazo afu yeye akabaki..

mke anaweza kusema yule alikuwa ni mume wangu, lakini watoto watasema yule ni baba yangu..Think Big
 
Back
Top Bottom