Mke kaniweka njia panda, naombeni ushauri

Mke kaniweka njia panda, naombeni ushauri

Mimi ni mwanaume wa miaka 35, nilioa mwaka 2009 kabla ya kuoana tulipima na wote tulionekana tupo salama.

Tukazaa watoto wawili, mwaka 2013 mke alianza kuumwa, alikuwa anatibiwa homa inarudia rudia, baada ya hali kuzidi akashauriwa kupima ukimwi mwaka 2015 na ndipo akagundulika kuwa ameathirika, na mimi nikapima zaidi ya mara tatu nikaonekana ni negative.

Kwa muda wote huo tumekuwa tukitumia mipira katika tendo la ndoa kimsingi tangu nilivyooa sikuwahi kuchepuka shida niliyonayo mimi kwa sasa najawa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi nimepungua kiukweli, sioni radha yoyote kwenye tendo, sipati msisimko wowote kwake moyo umekufa kabisa.

Nikiwa nae karibu ndio najawa na mawazo, sioni mapenzi yoyote kwake kibaya zaidi hajawahi kuniambia alipataje na nikimuuliza anaanza kulia hadi kuchukua sumu kutishia kujiua ninashindwa nifanyaje nikijiangalia na umri wangu bado mdogo.

Naomba ushauri wenu wadau nifanyaje kwa sababu yeye anaonekana ana njaa kubwa ya tendo la ndoa na mimi hali ndio hivo.
Pole pole hakikisha usinase kamdudu
 
Mke wako alichepuka..
Kama unapenda mfe wote mapema na kuacha watoto bila wazazi.. basi kuwa mjinga

Mnunulie matoi umsaidie muyachezee.. kumfikisha bila wewe kupata hayo..

Pole na kila la kheri, anatishia kujiua labda aliyempatia ni mtu wako wa karibu.. ndio maisha jipende..

Jua hawezi kujiua bali anatumia kama njia ya kutokukuambia ukweli.. huku yeye na wake wanajua. Au labda alikuwa analala na wengi wampe maraha na pesa na hajui yupi alimpa

Update 27/9 22:25hrs
Hii update ya mleta mada ameiandika humu.. inasikitisha sanaaaa[emoji1427][emoji1427][emoji1427]
Mhm mbn machungu
 
Mimi ni mwanaume wa miaka 35, nilioa mwaka 2009 kabla ya kuoana tulipima na wote tulionekana tupo salama.

Tukazaa watoto wawili, mwaka 2013 mke alianza kuumwa, alikuwa anatibiwa homa inarudia rudia, baada ya hali kuzidi akashauriwa kupima ukimwi mwaka 2015 na ndipo akagundulika kuwa ameathirika, na mimi nikapima zaidi ya mara tatu nikaonekana ni negative.

Kwa muda wote huo tumekuwa tukitumia mipira katika tendo la ndoa kimsingi tangu nilivyooa sikuwahi kuchepuka shida niliyonayo mimi kwa sasa najawa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi nimepungua kiukweli, sioni radha yoyote kwenye tendo, sipati msisimko wowote kwake moyo umekufa kabisa.

Nikiwa nae karibu ndio najawa na mawazo, sioni mapenzi yoyote kwake kibaya zaidi hajawahi kuniambia alipataje na nikimuuliza anaanza kulia hadi kuchukua sumu kutishia kujiua ninashindwa nifanyaje nikijiangalia na umri wangu bado mdogo.

Naomba ushauri wenu wadau nifanyaje kwa sababu yeye anaonekana ana njaa kubwa ya tendo la ndoa na mimi hali ndio hivo.
Nakushaur kapime tena usje kuwa umenasa km ujanasa ukimwi usishilik naye tendo la ndoa tena had mpate ushaur kwa watalam wa afya
 
Nimepata hasira sana juu ya hilo lijinianamke, na nimekuhurumia sana na kuumia moyoni mwangu brother. Na inaonekana una hekima ya juu sana na upole, nikupe pole na kukushauri wewe achana naye mkuu, huyo ni mnyama sio wa kawaida. Mwache kabisa mkuu atakupa maradhi na akishafanikiwa kukupa tu, thamani yake kwako inaisha anataka mfanane na mjute kwa pamoja. MWACHE AENDE ZAKE
 
We only live one take care au una mtegemea mwanamke kuendesha maisha yako?
 
Huyu jamaa atakua bwege au hakunyonya akadhiba vizuri kwenye ziwa la mama yake mtimue yani kma mbwa huyo demu wako ni malaya ataenda kukuua
 
hawa watu wanatuumiza sana mioyo na hawana hata sababu za misingi za matendo yao
 
Mmmh... Kwa hali ilivyokaa achana na huyo mwanamke... Tena muachie kila kitu uende ukaanze maisha upya... Hana nia njema kwako
 
Inatisha hali kama hii maana kukosekana kwa uaminifu ndio chanzo cha familia kuteketea kwa magonjwa na kuacha watoto wakiteseka
 
Mimi nafikiri suala la kukosa uaminifu na kwenda kuzini au kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje, kazi ya kufanya maamuzi ni yako. Mimi mwanamke mzinzi sina majadala naye, namsamehe kwakuwa kanikosea lkn ni lazima nimtaliki ili awe huru.
 
Sijui ni ujinga, sijui ni mahaba, sijui ni kutokujitambua. Naona unataka kuacha wanenu yatima wakiwa wadogo mno.

Chakukusahuri ni acha ujinga, lea watoto achana na mapenzi yasioleweka na huyo mkeo!
 
Hivi ni kweli huyu jamaa hajui cha kufanya😡😡😡😡 Kimsingi uamuzi ni wa wako ila ushauri wangu ni kuwa upo kwenye tundu la simba.
Kimbia acha hata nguo kaanze maisha upya.
Hatari ni hizi 1.kwanza kafanya uzinzi na ushahidi upo wazi 2.umekuta sms za my wake 3. anaongea na huyo my wake .Fanya maamuzi ya kiume
 
Hili lipo nje ya uwezo wangu kutoa ushauri....naona watu wanaandika magazeti utadhanimama terry
 
Dogo bado unawivu pamoja janga uliyonayo?
Ebu mpe ruksa ale good time na ikiwezekana aolewe kabisa na aliyempa Ugonjwa kama kweli ameupata kwa njia ya ngono. Lakini fanya utafiti pengine wakati wa kuzalishwa kulijitokeza matatizo ya afya km vile kuongezewa damu nk.
Anza kumjenga kiakili akuache huru maana kama katika hali aliyonayo bado anaendeleza kuchepuka ni hatari kwako na hasa watoto watabaki yatima kama wote mtaingia kwenye mtego .
 
Alafu huwa wakali kupitiliza , watu wa kypanic kukasirika ovyo !! ...
 
Back
Top Bottom