Mke anaweza kukuharibia mafanikio maishani

Mke anaweza kukuharibia mafanikio maishani

Sijui kwako, ila naona wengi sikuhizi tunaajiri wasaidizi wa ndani, sikuhizi MTU akipata mtoto tu analeta house girl kumsaidia mama kulea, zamani hiyo haikuwepo, mama analea watoto kibao na shamba anaenda
Housegirl analipwa na nani?
Kua kwanza unaongea tu.
 
Babu yaaani hata hela ya kula naacha kwa taabu sana, nilifungua duka kashindwa sasa kumuacha nikifikiria watoto itawaathiri.

Yaani ni mvivu balaa na mimi kakipato kangu hakatoshi kabisa kusave
ulichagua urembo mkuu....tumia akili yako mkuu.
 
Kijana chunga sana mtu unayemuoa. Kuna baadhi yao wanaweza kukuharibia malengo yako. Usifuate wezere tu.
#vijana wengi wanavutiwa na uzuri wa nje wa mwanamke .siyo mbaya lkn ongeza na sababu ya pili.ndani yake(spiritual and physical) roho yake.ana hofu ya mingy.anaupendo wa dhati.

Tafuta mwanamke ambae ni type yako.ukipagawa kwa tako na sura nzuri my friend umekwisha.
 
Sasa mbona hata akiwepo housegirl bado mnalalamika kuwa mke anamuachia kazi zote housegirl?? Na mnaenda mbali zaidi na kutembea na hao mahousegirl kwa kisingizio cha kuwa wanafanya majukumu yote anayotakiwa afanye mke??

Sasa hebu nikuulize wewe unaona ni sawa mume na mke wote wanatoka asubuhi lakini mke ndiyo afanye usafi na aandae chai halafu wote mnarudi usiku ila mke ndiyo aingie jikoni kupika na kuosha vyombo wakati huo wewe umekaa tu?? Halafu bills zikija mnalipa pasu kwa pasu na ada za watoto mnalipa pasu kwa pasu hiyo kwako unaona ni sawa??
Binafsi naona si sawa,kama mke anawajibika vizuri hadi kwenye kipato..naona kusaidiana kazi za ndani fresh kabisa ila sipendi kufua na kuosha vyombo so ntanunua mashine ya kufulia na ye aoshe vyombo ,ila kupika na usafi mwingine sioni shida japo siwez kupika kila kitu na kila siku
 
Back
Top Bottom