Mwanamke aliye kwenye ndoa zaidi ya miaka 5 na bado ana vigezo hivi ama mojawapo ya hivi
Dharau
Majibu ya hovyo
Kiburi
Muongo
Mgomvi
mchawi
Infidel
Hakikisha unakimbia, achana naye maana hakuna anayeweza kumbadilisha zaidi ya yeye mwenyewe kuamua kubadilika. Hakuna lugha nyepesi ninayoweza kuitumia kwenye hili. ACHANA NAYE maana hakika ukiendelea tutakukalia matanga kabla ya umri wa ahadi ya Mungu kwako.
Wanawake wengi siku hizi wamehalalisha kutenda lolote kwa kigezo cha haki sawa, lakini hawajawahi kusema neno kwenye mahari na kodi ya meza. Sheria kibao zinawalinda na wanajua wakijiliza liza basi kila mlango utafunguka.
Unakuta tabia kama hizo mtu anazo ktk uchumba na bado unajipa moyo atabadilika.
Mwenye uwezo wa kumbadilisha mtu ni Mungu na Mungu atambadilisha endapo mtu akajiona ana hiyo shida, mbali na hapo hesabu maumivu mpaka unaingia kaburini.