Ili uwe na mapenzi yenye raha bila msongo wa mawazo fanya haya

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
1. Mtambue uliyenaye hulka zake na tabia zake Usipomtambua mwanaume au mwanamke wako, itaiupa shida kujua nini anapenda, nini apendi au anapenda, tabia zake mbaya na nzuri, udhaifu wake. Hii itakujenga kujua unaishi na zimwi likujualo haliwezi kula ukaisha utakufanya ujue unaishi na mtu siyo malaika.

2. Acha kumchunga mtu mzima achungwi. Kuwa kipasati au askari kanzu wa mapenzi, bwana utapata shida maana mwenye kukusudia ubaya utatenda tu iwe machoni au mbali na macho yako,unapaswa kuishi na mwanamke ama mwanaume wako kama unavyofuga mfugo wako wa nje, uache uende cha msingi urudi bandani. Weka wazi tu misimamo yako ili kama huyo mwenza wako ni timamu atatambua kuwa na mipaka kwa kila afanyalo.

3. Timiza majukumu yako ya kijinsia. Usiwe unategea mwenzio aanze, wewe kama umeingia kwenye mapenzi toa huduma iwe fedha, nguvu, mawazo, mali, mwili na imani yako. Kama ni mwanamke ishi kama mwanamke na kama mwanaume ishi kama mwanaume, pa kukaza kaza na pa kulegeza legeza, ukiwa unataka kufanana na mwenzio kijinsia utafeli.

4. Fanya mawasiliano ya kawaida usiwe addicted (mraibu/mlevi). Piga na tuma ujumbe kwa kujiwekea utaratibu wa kujali muda wako, muda wa mwenzio, majukumu, jinsia, uwezo wako wa fedha, uwezo wako wa kujenga maneno na mazungumzo nk. Unapopiga simu kila dakika kila saa, ndugu wewe binadamu utashindwa siku itakugharimu lawama. Ndio maana tunapaswa kutumia sms fupi yenye kugusa hisia za mtu au maneno machache yenye maana na kujali vitu,hali na muda wa msingi kuwasiliana.

5. Onyesha wewe ni tofauti na jipambanue kwa kuanglia mwenzio nini anataka, nini alikikosa kwa ex, kwao, maisha yake, ndoto zake na kwa hali yake. Kila mru upenda kuwa na mtu mwenye upekee, ndio maana siyo ajabu kuona wewe unamuona furaha ni mzuri ila haolewi wala hapati mke au mwanaume au mwanamke. Kumbe hajiongezi, yupo yupo anatafakuri. Wapo watu ni malaya ila wanaheshima kubwa sana kwa wenza wao/wapenzi wao na huwezi kwenda peleka umbeya ukaaminika.

6. Tumia uwepo wake kutimiza nawe ndoto zako. Usijifanye wewe unapenda sana maendeleo ya mwenzio, na wewe onyesha unaweza kufanya kitu, hata kama ni mama wa nyumbani wewe ni mwenye thamani sana ni wazi ni kiwanda kilichojificha onyesha weledi wako, kama ni mwanaume kipato cha kawaida onyesha kuthamini hicho kidogo unachopata. Onyesha unatamani kukua, kutoka kituo A kwenda B.

7. Usipende kila utakacho kiwe ni kosa utakufa kwa kihoro. Lazima ujue siyo yote yanawezekana kwa muda utakao, kwa kiasi uwazacho, kwa ubinafsi wako, wakati mwingine subira, kujichanga, kuwa na mpango thabiti ni muhimu. Mtu kuwa na pesa haimaanishi atakupa kila utakacho, penda kuwa shukrani na kuacha uoga wa maisha.

8. Thibiti hasira na ubinafsi wako Kuna watu jambo kidogo tu jazba, mnuno, kipigo, matusi, choyo, kufukuza, kufukua makaburi waliyo zika, kusamehe ni ishu nk huu ni ubinafsi na kukosa kujua namna ya kuthibiti hasira zako.

9. Epuka kuweka sehemu zako za siri kuwa dhamana ya mapenzi.Kujifanya uhodari wa mapenzi huku juna jema la maisha na jingine la mapenzi, ni kuziumiza sejdmu zako za siri. Jiongeze uwe romantiki, rafiki, ndugu,mshauri, CEO, kiwanda, uaminike, nk

10. Julikana. Usijifiche ama kujiweka nyuma nyuma, nyuma nyuma utapigwa, siku hizi mapenzi ni kupata siyo kuwahi. Unakaa na mtu muda mrefu hata kwao hawakujui, marafikize hawakujui yaani alafu unasema anakupenda, hapana anayekupenda hawezi kukuficha, watu wanatambulisha michepuko na mahawala sembuse wewe.

Mambo haya yanagusa maisha yako, uwazi na uhakika wa unachokifanya. Ni bora uwe singo au mpweke kuliko kujiingiza katika mahusiano ya ovyo na mtu asiyejua utu wa mtu, huwa ni ngumu kuukubali ukweli ila unapoona penzi lako upo na mtu wa ovyo tofauti na ulivyomtegemea na umefanya jitihada akad sawa na hakai, ni bora kuyaacha hayo mapenzi yaende.

Na mwandishi na mshauri wa mahusiano MMMUHUMBA
#Imarika na mnogeshe View attachment 2472109
IMG_20230106_142726_937.jpg
 
Kuna komenti moja niliikubali sana! Inasema

"Mkuu wewe ishi tu ya dunia ni mengi sana"
 
Mapenzi bhana hayana mwongozo
ukiwa serious sn nakuhakikishia yatakutesa
Ni kweli hakuna njia ya moja kwa moja, ila elimu ya mahusiano unapokuwa nayo inakufumbua macho walau.
DeepPound kuna mahusiano nimeyaokoa kwa vitu vidogo, unakuta me au ke hajawahi pata malezi hayo mpaka amekua yaan kwao mahusiano hajui lolote, ila hiz elimu zinawapa sehemu ya kujitathmin na kuanza upya.
Ushasikia mwanamke mbuzi na mwanaume mbuzi eeh yeyeye bila elimu ya kuwasaidia kuwa romantiki wanauwana na hakuna wa kujiongeza kwa ajili ya mwenzie.
 
Back
Top Bottom