Ndoa ya mke mmoja au wengi? Vipi kuhusu talaka? Soma hapa ujue msimamo wa Biblia

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
9,622
20,972
NDOA YA MKE MMOJA AU WENGI? VIPI KUHUSU TALAKA? SOMA HAPA UJUE MSIMAMO ULIOPO KWA MUJIBU WA BIBLIA.

"Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote". Hiyo ni ahadi namba 6 ya mwanachama wa CCM. Mimi kama ilivyo wakati wote nitaendelea kutimiza hiyo ahadi. Hii post itajikita kwenye suala zima la ndoa. Je, sisi wakristo tunaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja? Talaka je? Biblia inasemaje? Soma kwa makini aya zinazofuata upate majibu.

Kabla ya kujibu hilo swali lazima tujue kwanza ndoa ni nini ikiwemo historia yake nzima.

Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.

Kibiblia ndoa ni mpango mtakatifu wa Mungu ulioanzia Edeni. Mwanzo 2:18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye". Kama ilivyo kwa sheria ya jamhuri ya TZ basi hata kibiblia tafsiri haijapishana;
Mwanzo 2:24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja".

Kwa kifupi ndoa ni taasisi takatifu iliyoasisiwa na Mungu mwenyewe. Mwanaume na mwanamke wataungana bila kujali kabila, dhehebu wala taifa. Cha muhimu muwe mmejitoa nafsi zenu kwa dhati kabisa kuitumikia taasisi ya ndoa. Ni ruksa mke kuolewa na asiyeamini au mume kuoa asiyeamini (1 Wakorintho 7:12-16). Kwa msisitizo imeandikwa kwenye 1 Wakorintho 7:16 "Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?".. ukipata asiyeamini na mnaelewana biblia imesema msiachane kwasababu anayeamini atamwokoa mwenzake.

Tukisoma biblia zaidi tutaona watu pekee waliowahi kuwekewa masharti zaidi wakati wa kuoa walikuwa ni Walawi. Hawa waliongezewa masharti kwasababu walitengwa kwa kazi maalum ya ukuhani. Waliambiwa hivi;

Mambo ya Walawi 21:7 "Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake".

Mungu hufurahishwa pale watu wanapofunga ndoa badala ya kufanya uzinzi. Lengo kuu la Mungu kwa wanandoa ni kuijaza dunia kupitia vizazi vyao. Tunaona Adam na Hawa waliambiwa zaeni mkaongezeke muijazw dunia na hata baada ya gharika aliendelea kusisitiza watu wazaliane. Ingawa Mungu mwenyewe hufurahi mtoto anapozaliwa bila kujali ni wa ndani ya ndoa au nje ila kasisitiza kabla ya lolote ni vema kufunga ndoa. Mithali 6:32 "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake".

Je, ni sahihi kuoa mke zaidi ya mmoja? Hili swali lina mtego mkubwa kwa sababu hata kwenye biblia tumeona kina Suleman na Yakobo wakioa mke zaidi ya mmoja hivyo kuleta maswali mengi zaidi miongoni mwa wakristo wa leo. Kwa sisi wakristo tukisoma vizuri biblia huku tukizishirikisha akili zetu vizuri tutaona wazi mpango wa Mungu ni ndoa ya mume na mke mmoja na sio mume na wake wengi. Mwanzo 2:18 mkisoma mtaona imeandikwa "nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" na sio wasaidizi. Hata mwanzo 2:24 imeandikwa "mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja". Kwahiyo hadi hapo tumeona point ilikuwa ni "mume na mke" na sio "mume na wake".

Marko 10:2-12 tumeona pia Yesu akiwasisitiza mafarisayo kwamba ndoa ni ya mke na mume tu. Mtume Paulo nae alieleza umuhimu wa kuwa na mke mmoja akitaja uzinzi kama sababu kuu. 1 Wakorintho 7:2 "Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe". Hata sisi tunaona kwamba mume mmoja na mke mmoja ni bora zaidi hasa nyakati hizi ili kuepuka maradhi. Hivyo wakristo tuelewe kwamba mpango mzima ni mume na mke mmoja tu.

Je, vipi kuhusu talaka? Kwa kifupi talaka haikuwa mpango wa Mungu kabisa. Na wanandoa wanapoachana ni huzuni kubwa hadi kwa muumba mwenyewe. Mpango wa Mungu ni wanandoa watenganishwe na kifo tu na sio sababu nyingine. Yesu anasema alichokiunganisha Mungu basi binadamu asitenganishe (Marko 10:9)

Kama ilivyokuwa kwa mafarisayo enzi za Yesu bado kuna wengi tunajiuliza mbona kwenye agano la kale tunaona Musa aliwaruhusu waisrael kutoa talaka? Soma Kumbukumbu la torati 24:1-4 uone maelekezo waliyopewa. Yesu alijibu swali hili vizuri sana kwa kutuambia "Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. " (Mathayo 19:8 na Marko 10:5).. ni kwamba waisrael waliruhusiwa mambo ya talaka kwasababu walikuwa walalamishi mno. Hawakuwa wakiridhika hata wafanyiwe kitu gani. Kule jangwani ilibidi Mungu kupitia Musa atunge sheria ndogondogo nyingi sana ili aweze kwenda nao sawa. Baadhi ya sheria ndo hizi ambazo SDA wanalazimisha tuzifuate hadi leo hii.

Pia tujue kwamba sababu pekee inayokubalika mbele za Mungu kwamba inaweza kusababisha talaka ni uzinzi (kuchepuka). Mathayo 5:31-32 "Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini". Lakini ili kuonyesha jinsi gani talaka isivyo jambo la kumpendeza Mungu, biblia imeshauri kupitia 1 Wakorintho 7:11 kwamba watu wakiachana yule mwanamke asikimbilie kuolewa bali atafute suluhu na arudiane na mumewe na pia huyo mume asimuache mkewe tena.

Kiukweli ingawa sababu inayotambulika ni hii ya kuchepuka ila hata Mungu mwenyewe anajua mabalaa ya wanawake. Anaweza asiwe anachepuka ila hizo kero ukajikuta uko jehanam hapahapa duniani. Biblia imetamka wazi.. Mithali 21:9 "Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi". Na Mithali 21:19 "Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi".

Pamoja na yote hayo bado mwenyezi Mungu ni mtetezi mkuu wa wanawake. Mwanzo 21 tunaona jinsi gani Sara alimkera mumewe Ibrahim ambapo kibinadamu ingeleta shida ila Mungu akamwambia Ibrahim aliyekuwa kakasirika aendelee kumsikiliza mkewe. Kuna visa vingi vya wanawake kupata utetezi lakini kubwa ni pale biblia inapotuambia mwanamke ni kiumbe dhaifu hivyo tunapaswa kuishi nao kwa akili (1 Petro 3:7). Kimsingi wanawake wanatakiwa kuwatii waume zao na waume wanatakiwa kuwapenda wake zao.
 
Amina SoMo nzuri sana, Tuache tabia Mbaya ya kuoa oa hovyo,
Ila changamoto ni kwamba wanawake ni wengi kuliko wanaume, Sasa Hawa wanawake wengine watashugulikiwa na nani?
 
Kipi bora
Kuwa na mke wa ndoa na bibi wa kando mliozaa na mchepuko aliyenasa?! Au kuwa na wake watatu wanaotambulika kimila/kisheria?!
Nashauri
Bora uwe mchawi ili upate muda mzuri wa kufanya shirki kuliko mara upo ibadani ila unawaza umloge sheikh/mchungaji usiku

Bora uwe mnywaji na mla mdudu kuliko kuwa kwenye nyumba ya ibada huku ukijua hakuna unachofanya/unachokipata pamoja na kuattend
 
Siku hizi TABIA MBAYA imekuwa mbadala wa KIFO kwenye kutenganisha wanandoa
Hali ya uchumi kwa mwanaume inapoyumba na uzinzi kwa mwanamke imekuwa ndiyo chanzo kikuu cha kuvinjika kwa ndoa. Wanandoa wa siku hizi hawana uvumilivu licha ya ndoa kufungwa kwa gharama na ufahari wa anasa. Single mother wanaongezeka kwa kasi ya ajabu wala viongozi wa dini hawana ubavu wa kukemea kuachana kwa wanandoa
 
Kuoa single mother nako kumekuwa na changamoto za kuchanganya familia mbili au tatu zenye mama mmoja kwa baba wawili au watatu. Ni ngumu kuishi na mwanamke aliyeachika mara mbili au tatu, hiyo siyo ndoa ni uhuni mtupu. Cha ajabu mwanamke anaachika halafu anaenda kufunga ndoa nyingine kwa harusi huku mume wake wa kwanza au wa pili yuko hai na amezaa nae watoto. Ndoa za namna hii si za kufungwa na kupewa cheti, ni vurugu tupu
 
Umeandika maneno mazito mno. Mimi siku za karibuni nimeona karibu kila mwanamke nikimtaka anakuwa tayari ana mtoto.
 
Hawa wanawake wenye watoto kwa wanaume wao wa mwanzo wakiwa hai ni ngumu kudhibiti mahusiano yao kwa kuwa ni wazazi wenza. Jamaa anaweza kutuma matumizi kwa mtoto wake kupitia kwa mama yake na pengine kuagiza wakutane sehemu akapokee matumizi. Sasa wanaweza wakafanya yao kukumbushiana
 
Wakristo bana, sijui walokole kwani kwenye biblia unayotumia kuna sheria mahususi kwa waisraeli na mahususi kwa binadamu wote? Unazitofautishaje? Mfano kutokula kitimoto ni ya israeli au ya wakristo wote?
 
Sasa hutaki tukumbushie?

Kwani wkt unamuoa hukujua kama ana mtoto na amezalishwa na njemba ingine?

Wanawake wote hawa hukuona ambao hawana watoto uzae nae?

Tutaendelea kukumbushia mpaka mmoja kati yetu atakapotangulia kaburini.
Kumbushieni ila nisijue huo mchezo nitafanya yangu
 
NDOA YA MKE MMOJA AU WENGI? VIPI KUHUSU TALAKA? SOMA HAPA UJUE MSIMAMO ULIOPO KWA MUJIBU WA BIBLIA.

"Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote". Hiyo ni ahadi namba 6 ya mwanachama wa CCM. Mimi kama ilivyo wakati wote nitaendelea kutimiza hiyo ahadi. Hii post itajikita kwenye suala zima la ndoa. Je, sisi wakristo tunaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja? Talaka je? Biblia inasemaje? Soma kwa makini aya zinazofuata upate majibu.

Kabla ya kujibu hilo swali lazima tujue kwanza ndoa ni nini ikiwemo historia yake nzima.

Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.

Kibiblia ndoa ni mpango mtakatifu wa Mungu ulioanzia Edeni. Mwanzo 2:18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye". Kama ilivyo kwa sheria ya jamhuri ya TZ basi hata kibiblia tafsiri haijapishana;
Mwanzo 2:24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja".

Kwa kifupi ndoa ni taasisi takatifu iliyoasisiwa na Mungu mwenyewe. Mwanaume na mwanamke wataungana bila kujali kabila, dhehebu wala taifa. Cha muhimu muwe mmejitoa nafsi zenu kwa dhati kabisa kuitumikia taasisi ya ndoa. Ni ruksa mke kuolewa na asiyeamini au mume kuoa asiyeamini (1 Wakorintho 7:12-16). Kwa msisitizo imeandikwa kwenye 1 Wakorintho 7:16 "Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?".. ukipata asiyeamini na mnaelewana biblia imesema msiachane kwasababu anayeamini atamwokoa mwenzake.

Tukisoma biblia zaidi tutaona watu pekee waliowahi kuwekewa masharti zaidi wakati wa kuoa walikuwa ni Walawi. Hawa waliongezewa masharti kwasababu walitengwa kwa kazi maalum ya ukuhani. Waliambiwa hivi;

Mambo ya Walawi 21:7 "Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake".

Mungu hufurahishwa pale watu wanapofunga ndoa badala ya kufanya uzinzi. Lengo kuu la Mungu kwa wanandoa ni kuijaza dunia kupitia vizazi vyao. Tunaona Adam na Hawa waliambiwa zaeni mkaongezeke muijazw dunia na hata baada ya gharika aliendelea kusisitiza watu wazaliane. Ingawa Mungu mwenyewe hufurahi mtoto anapozaliwa bila kujali ni wa ndani ya ndoa au nje ila kasisitiza kabla ya lolote ni vema kufunga ndoa. Mithali 6:32 "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake".

Je, ni sahihi kuoa mke zaidi ya mmoja? Hili swali lina mtego mkubwa kwa sababu hata kwenye biblia tumeona kina Suleman na Yakobo wakioa mke zaidi ya mmoja hivyo kuleta maswali mengi zaidi miongoni mwa wakristo wa leo. Kwa sisi wakristo tukisoma vizuri biblia huku tukizishirikisha akili zetu vizuri tutaona wazi mpango wa Mungu ni ndoa ya mume na mke mmoja na sio mume na wake wengi. Mwanzo 2:18 mkisoma mtaona imeandikwa "nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" na sio wasaidizi. Hata mwanzo 2:24 imeandikwa "mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja". Kwahiyo hadi hapo tumeona point ilikuwa ni "mume na mke" na sio "mume na wake".

Marko 10:2-12 tumeona pia Yesu akiwasisitiza mafarisayo kwamba ndoa ni ya mke na mume tu. Mtume Paulo nae alieleza umuhimu wa kuwa na mke mmoja akitaja uzinzi kama sababu kuu. 1 Wakorintho 7:2 "Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe". Hata sisi tunaona kwamba mume mmoja na mke mmoja ni bora zaidi hasa nyakati hizi ili kuepuka maradhi. Hivyo wakristo tuelewe kwamba mpango mzima ni mume na mke mmoja tu.

Je, vipi kuhusu talaka? Kwa kifupi talaka haikuwa mpango wa Mungu kabisa. Na wanandoa wanapoachana ni huzuni kubwa hadi kwa muumba mwenyewe. Mpango wa Mungu ni wanandoa watenganishwe na kifo tu na sio sababu nyingine. Yesu anasema alichokiunganisha Mungu basi binadamu asitenganishe (Marko 10:9)

Kama ilivyokuwa kwa mafarisayo enzi za Yesu bado kuna wengi tunajiuliza mbona kwenye agano la kale tunaona Musa aliwaruhusu waisrael kutoa talaka? Soma Kumbukumbu la torati 24:1-4 uone maelekezo waliyopewa. Yesu alijibu swali hili vizuri sana kwa kutuambia "Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. " (Mathayo 19:8 na Marko 10:5).. ni kwamba waisrael waliruhusiwa mambo ya talaka kwasababu walikuwa walalamishi mno. Hawakuwa wakiridhika hata wafanyiwe kitu gani. Kule jangwani ilibidi Mungu kupitia Musa atunge sheria ndogondogo nyingi sana ili aweze kwenda nao sawa. Baadhi ya sheria ndo hizi ambazo SDA wanalazimisha tuzifuate hadi leo hii.

Pia tujue kwamba sababu pekee inayokubalika mbele za Mungu kwamba inaweza kusababisha talaka ni uzinzi (kuchepuka). Mathayo 5:31-32 "Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini". Lakini ili kuonyesha jinsi gani talaka isivyo jambo la kumpendeza Mungu, biblia imeshauri kupitia 1 Wakorintho 7:11 kwamba watu wakiachana yule mwanamke asikimbilie kuolewa bali atafute suluhu na arudiane na mumewe na pia huyo mume asimuache mkewe tena.

Kiukweli ingawa sababu inayotambulika ni hii ya kuchepuka ila hata Mungu mwenyewe anajua mabalaa ya wanawake. Anaweza asiwe anachepuka ila hizo kero ukajikuta uko jehanam hapahapa duniani. Biblia imetamka wazi.. Mithali 21:9 "Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi". Na Mithali 21:19 "Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi".

Pamoja na yote hayo bado mwenyezi Mungu ni mtetezi mkuu wa wanawake. Mwanzo 21 tunaona jinsi gani Sara alimkera mumewe Ibrahim ambapo kibinadamu ingeleta shida ila Mungu akamwambia Ibrahim aliyekuwa kakasirika aendelee kumsikiliza mkewe. Kuna visa vingi vya wanawake kupata utetezi lakini kubwa ni pale biblia inapotuambia mwanamke ni kiumbe dhaifu hivyo tunapaswa kuishi nao kwa akili (1 Petro 3:7). Kimsingi wanawake wanatakiwa kuwatii waume zao na waume wanatakiwa kuwapenda wake zao.
Hakuna mahali Biblia inapokataza mkristo wa kawaida kuoa mke zaidi ya mmoja. Angalizo limewekwa kwa Askofu na Shemasi hawa ndio wameshauriwa kuwa na mke mmoja, wengine wasio na vyeo hivyo ni ruksa kuwa na mke zaidi ya mmoja. 1 Timotheo 3:1-7 na 1 Timotheo 4:1-5

Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja , mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
1 Tim 3:1‭-‬3 SUV

Vivyo hivyo Biblia haijakataza unywaji wa vileo na divai. Askofu hatakiwi kuwa mlevi bali awe mnywaji wa kiasi, vivyo hivyo na shemasi. Katazo hili haliwagusi wakristo wa kawaida ila nao kistaarabu wanatakiwa kunywa kiasi ili waweze kujikontroo.

Ukisoma 1 Timotheo 4:1-5 unaona Paulo anatahadharisha kuwa kutakuwa na wapotoshaji wanaozuia watu kuoa na kula baadhi ya vyakula. Neno ni hili;

Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
1 Tim 4:1‭-‬4 SUV
 
Lakini ili kuonyesha jinsi gani talaka isivyo jambo la kumpendeza Mungu, biblia imeshauri kupitia 1 Wakorintho 7:11 kwamba watu wakiachana yule mwanamke asikimbilie kuolewa bali atafute suluhu na arudiane na mumewe na pia huyo mume asimuache mkewe tena.
Wanakuwa na kiburi na jeuri nyingi
 
Kwa sisi wakristo tukisoma vizuri biblia huku tukizishirikisha akili zetu vizuri tutaona wazi mpango wa Mungu ni ndoa ya mume na mke mmoja na sio mume na wake wengi. Mwanzo 2:18 mkisoma mtaona imeandikwa "nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" na sio wasaidizi. Hata mwanzo 2:24
Unachanganya kidogo kwenye tafsiri. Hakunaga ndoa ya wake wengi inayofungwa mara moja, bali kuna ndoa kati ya mwanamke na mwanaume ambaye ana mke au wake wengine tayari, kwa maana ya kwamba kila mwanamke atapozungumza atasema "mume wangu" na sio "mume wetu".

Ndoa ni makubaliano ya mtu mume na mke, hata waislamu na wakabila ndoa hufungwa kati ya watu wawili tu, hakuna mahali (hata kwenye sheria) watazungumzia wake badala ya mke, maana kila mmoja (kama wapo zaidi ya mmoja) ana ndoa yake, hakuna ndoa ya pamoja.

Kwa mantiki hiyo, huwezi kuona katika biblia panaposemwa atapewa wasaidizi (sababu hawaoi kwa mara moja), inaandikwa msaidizi sababu anayeolewa ni mmoja tu. Hata mtu mume akioa mara nane, wale wanawake wanakua na ndoa moja tu, kati ya huyo mwanamke na huyo mwanaume.
 
Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom