KERO Mke amfungia Mume ndani amnyima Matibabu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Habari ndugu zangu, katika pitapita zangu ndugu yenu leo nimekutana na jambo ambalo kibinadamu siyo la kawaida.

Katika mtaa wa Chem Chem maeneo ya Uyole inapatikana familia ya Mzee SIMONI ROMANUS PELLA .
Mzee SIMONI ROMANUS PELLA anasumbuliwa na ugonjwa ambao umemfanya ashindwe kutembea na kujikuta tangu mwaka jana mwezi wa 12 kuwa ndani tu.

Mwanzoni mzee anadai aliwahi kupata matibabu katika hospital ya Rufaa ya kanda ya Mbeya ambapo alifanyiwa operation ya kibofu cha mkojo na kuwekewa mpira kwaajili ya haja ndogo,lakini baada ya hapo hajawahi kupata matibabu tena mpaka leo hii.

Kinachosikitisha sasa nikwamba mzee wakati akiwa na afya njema alikuwa anamiliki duka katika soko la Uyole jijini Mbeya na ilo duka kwa sasa linasimamiwa na mke wake.
Sasa huyo mwanamke pamoja na watoto hawataki kabisa kuhusika na matibabu ya mzee huyo na kila akijaribu kuomba msaada mke wake hataki.

Mbaya zaidi hawataki mtu yeyote aende kumtembelea wala kutoa msaada wowote kwa mgonjwa
Walijitokeza wasamalia wema kutoka kanisa la KKKT DAYOSISI YA KONDE usharika wa Uyole kwaajili ya kumsaidia kwa kutoa pesa za Matibabu lakini wakamta mke wake akasimamie matibabu hayo hospital kama mtu wa karibu lakini alikataa na kudai hana muda .

Mateso anayopitia mzee huyu ni makali sana muda wote anahaki pekee yake ndani bila msaada wowote.
Wanamuachia chakula mezani huku akiwa na ndoo yake ya kujisaidia pindi akipatwa na haja pembeni
Ndugu zangu mzee huyu anapitia magumu mengi, yaani duka lake lipo ila hawataki kutoa pesa za Matibabu
Kwa leo mwanongwa naomba niishie hapa ila kesho nitakuja na maelezo ya majirani wanaosaidia mzee SIMONI ROMANUS PELLA.

View attachment 3557969View attachment 3557970View attachment 3557971
Kama ni Wakinga usihangaike nao. Wanajua kinachoendelea, masharti ya biashara.

Achana na kabila hili, utajiri wao ni wa mateso kama hayo tu
 
Hana ndugu ama nae kipindi mzima na mpunga anao alikua hawajali ndugu...maana km anaongea ni kupiga simu moja tu ndugu wanajaa pale yule mama na wanae wataondoka na nguo walizo vaa tu yaan ingekua mm huyo mwanamke angekua sijui wapi
 
Habari ndugu zangu, katika pitapita zangu ndugu yenu leo nimekutana na jambo ambalo kibinadamu siyo la kawaida.

Katika mtaa wa Chem Chem maeneo ya Uyole inapatikana familia ya Mzee SIMONI ROMANUS PELLA .
Mzee SIMONI ROMANUS PELLA anasumbuliwa na ugonjwa ambao umemfanya ashindwe kutembea na kujikuta tangu mwaka jana mwezi wa 12 kuwa ndani tu.

Mwanzoni mzee anadai aliwahi kupata matibabu katika hospital ya Rufaa ya kanda ya Mbeya ambapo alifanyiwa operation ya kibofu cha mkojo na kuwekewa mpira kwaajili ya haja ndogo,lakini baada ya hapo hajawahi kupata matibabu tena mpaka leo hii.

Kinachosikitisha sasa nikwamba mzee wakati akiwa na afya njema alikuwa anamiliki duka katika soko la Uyole jijini Mbeya na ilo duka kwa sasa linasimamiwa na mke wake.
Sasa huyo mwanamke pamoja na watoto hawataki kabisa kuhusika na matibabu ya mzee huyo na kila akijaribu kuomba msaada mke wake hataki.

Mbaya zaidi hawataki mtu yeyote aende kumtembelea wala kutoa msaada wowote kwa mgonjwa
Walijitokeza wasamalia wema kutoka kanisa la KKKT DAYOSISI YA KONDE usharika wa Uyole kwaajili ya kumsaidia kwa kutoa pesa za Matibabu lakini wakamta mke wake akasimamie matibabu hayo hospital kama mtu wa karibu lakini alikataa na kudai hana muda .

Mateso anayopitia mzee huyu ni makali sana muda wote anahaki pekee yake ndani bila msaada wowote.
Wanamuachia chakula mezani huku akiwa na ndoo yake ya kujisaidia pindi akipatwa na haja pembeni
Ndugu zangu mzee huyu anapitia magumu mengi, yaani duka lake lipo ila hawataki kutoa pesa za Matibabu
Kwa leo mwanongwa naomba niishie hapa ila kesho nitakuja na maelezo ya majirani wanaosaidia mzee SIMONI ROMANUS PELLA.

View attachment 3557969View attachment 3557970View attachment 3557971
NDOA NI UTAPELI, KATAA NDOA
 
Yote kwa yote kwenye hizi ndoa kesho inatengenezwa na leo nikimaanisha aina ya maisha wanayoishi mke na mume kila siku.

Tunaweza msema huyo Mama vibaya weee lakini si ajabu kukuta msingi wa yote hayo ameujenga huyo Mzee mwenyewe kipindi anadunda.

All in all pole kwake nadhani vyombo husika vikipata hizi taarifa vitamsaidia.
 
Back
Top Bottom