Kwanza mkataba huu ni wa kifisadi na unazinyima haki ya kibiashara radio za jamii. TBC ni redio ya umma na ina vyanzo vingi vya mapato ikiwa na pamoja na kodi zetu hivyo kuipa hati miliki hiyo siyo haki kabisa kwa radio binafsi ambazo pia zingependa kuwapa uzoefu watangazaji wake na kuongeza mapato.
Pili katika maeneo mengi ya mikoani usikivu wake siyo mzuri na mengine haisikiki kabisa hivyo wananchi hutegemea redio za jamii.
Tatu inapotokea shughuli za kitaifa kuwa muda mmoja na mechi TBC hutoa umuhimu katika shughuli na kuhamishia matangazo ya mpira TBC FM ambayo ni hafifu sana katika kuisikiliza.
Nne mkataba huu unawanyima haki wafanyabiashara wa mikoani kutangaza biashara zao na hasa katika mechi za mikoani ambako ingekuwa rahisi kwao kutangaza kupitia redio za jamii ambazo zinasikika vizuri.
Kwa hoja hizi chache na nyingine nyingi ambazo zijazitaja nashauri TFF kupitia upya mkataba huu ili ikiwezekana kila mechi ipate mkataba wake wa kuitangaza na hasa mechi za mikoani.