Ili kuweza kupata ladha ya kabumbu ligi ya NBC, vitu vifuatavyo lazima vifanyiwe kazi

Aug 4, 2014
20
36
NDUGU WANAJAMVI ILI KUWEZA KUPATA LADHA YA KABUMBU VITU VIFUATAVYO LAZIMA VIFANYIE KAZI

  • Usajili wa wachezaji bora
  • Benchi la ufundi bora na lililokamilika
  • Maandalizi ya msimu/ pre season
  • Viwanja bora vya kuchezea mpira
  • Vifaa bora na vya kutosha vya kurushia matangazo kutoka kwa mdhamini
  • Maandalizi ya waamuzi
  • Ratiba ya ligi

  • USAJILI
Huu ni wakati muhimu kwa vilabu kuhakikisha vinapata vipaji bora kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa bora katika msimu unaofuata na sio wakati wa kusajili wachezaji wa kuja kuongeza idadi ya wachezaji katika timu zao. Vilabu pia inabidi vikumbuke kupandisha under 20 kwenye timu zao ila sio kupandisha tu bali kupandisha kwenye timu kubwa kwa wale wanaostahili mfano mzuri mtibwa au geita

Sio lazima kwa vilabu kusajili wachezaji 30 kama kanuni inavyowataka ila vinapaswa kuacha nafasi kadhaa kwa ajili ya kufanya maboresho kipindi cha dirisha dogo ili kuepuka gharama ya kuvunja mikataba ya wachezaji.

Benchi la ufundi

Ili uweze kupata timu bora lazima uwe na benchi la ufundi bora hivyo basi kwa muktadha huu ni muhimu kwa bodi za vilabu kuhakikisha wanakuwa na wataalamu sahihi katika kila idara ili kupata kitu kilicho bora. Ni lazima timu ziwe na kocha bora wa viungo, kocha wa makipa, mtaalamu wa kusoma mechi (match analyst), kocha wa fisrt team na msaidizi wake n.k Hawa ni viuno muhimu kuhakikisha malengo ya timu yanafikiwa

Coaches must remember always their position is hot anytime they can be fIred

Maandalizi ya msimu(pre-season)

Maandalizi bora huleta matokeo chanya. Hapa ni wakati wa makocha wa viungo kutengeneza physic ya wachezaji na kocha mkuu kuweka mbinu zake. Kwa kuangalia tu timu za ligi kuu zina week tano hadi sita kwa kujiandaa na kivumbi cha NBC ni rai yangu watumie muda huu kuandaa mpango mkakati wa namna ya kucheza kwa duru ya kwanza ya ligi.

Ni muhimu kupata Zaidi ya mechi tano za majaribio kwa kuanza na timu zilizo level ya chini kwenda level ya juu kwa ajili ya kuhakikisha mifumo na falsafa za mwalimu zinawaingia wachezaji kabla ya kivumbi kamili cha ligi.

Viwanja

Ili mpira uchezwe lazima kuwe n eneo la kuchezea yaani kiwanja. Tatizo kubwa kwa ligi yetu ni vilabu kutomiliki viwanja hivyo viwanja vingi wakati ligi haichezwi vinakuwa vimetelekezwa na pia vinakosa matunzo bora. Rai yangu ni wakati wa timu na wamiliki wa timu kufanya marekebisho ya viwanja kuanzia kwenye pitch, majukwaa, dressing room, vyoo, press conference room, medical room na technical and substitute bench. Viwanja lazima viwe na nyasi bora na zinazoruhusu mpira kutembea ili kuruhusu mpira kuchezwa kwa aina zote na pia hii inapelekea ubora wa picha kwa mwenye haki ya matangazo ambae ni AZAM TV.

Kufungiwa kwa viwanja kuna waumiza mashabiki, AZAM TV na vilabu kwa ujumla kwa kuongeza gharama zisozo za maana. Pia kwa msimu uliopita changamoto nyingine ilikuwa kwenye viwanja vyenye taa kwa kukosekan kwa mwanga bora mfano kaitaba na majaliwa. Pamoja na kuwa ni msaada kutoka azam ila vilabu na wamiliki wajiongeze kwa kuongeza japo tower moja ya taa ili mwanga ujitosheleze uwanjani.

AZAM TV

Ni kampuni bora na ya mfano ila changamoto kwao kwa msimu uliopita ni kutokuwa na vifaa vya kutosha vya kurushia matangazo yaan camera za kutosha. Kurusha matangazo kwa camera zilizopo kwenye angle mbili inapunguza ubora wa picha na ladha ya mpira kwa mtazamaji anashindwa kuona kwa uangavu wachezaji na matukio mbalimbali. Changamoto nyingine ni kukatika katika kwa matangazo wakati wa urushwaji. Natumaini wameliona hili ni rai kwao waboreshe katika haya.

Waamuzi

Huwezi kupata mechi bora bila kuwa na waamuzi waliobobea na wenye weledi. Niwapongeze kwa msimu uliopita waamuzi wetu walijitahidi sana kutofanya makosa mengi ila hata hivyo bado wanahitajika kuongeza ufanisi ili ligi yetu izidi kuwa bora na bora Zaidi. Tatizo la waamuzi kutolipwa kwa wakati ni wakati muafaka kwa TFF na bodi ya ligi kulipatia ufumbuzi kwa kutafuta mdhamini ambae atakuwa anatoa fedha kwa ajili ya waaamuzi. Kwa kumvutia mdhamini TFF wanaweza kupitisha sheria kwenye viwanja vyote vya NBC Premier league mabango ya mdhamini huyo yawekwe kwenye kila mechi na waamuzi fulana zao ziwe na nembo ya mdhamini husika. Waamuzi wapangiwe mechi kwa mtiririko unaofaa ili usiharibu ubora wao.

Ratiba ya ligi

Kwa kuhakikisha shindano linakuwa bora basi ni wakat muafaka kwa kutafuta namna bora ya kupanga ratiba ili kuepusha uchepushaji wa mechi wa mara kwa mara. Ni vyema bodi ya ligi wakaandaa ratiba kwa team kucheza weekend kwa weekend (ijumaa hadi jumapili) na mara chache jumatatu. Bodi ya ligi na TFF isikubali mapendekezo ya hovyo ya kubadilisha tarehe za mechi

HITIMISHO

  • KWA LIGI YETU ILIPO SASA BODI YA LIGI INAPASWA KUWA CHOMBO HURU NA SIO KAMATI YA TFF
  • BODI YA LIGI IONGEZE JITIHADA ZA KUSHAWISHI WADHAMINI WENGINE KWENYE LIGI
  • TFF ISIFUMBIE MACHO MASWALA YA RUSHWA IFANYE UCHUNGUZI WA KINA
  • VIWANJA VYOTE VIWEKWE MABONGO YA WADHAMINI KUZUNGUKA PITCH YOTE ILI KUNOGESHA ENEO LA KUZECHEZEA KWA WATIZAMAJI
  • MATUMIZI BORA YA FEDHA KWA VILABU NA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO

  • utalia sana wewe jikaze tu
 
Ongezea section ya Fedha, Hela maana bila financing appropriation matokeo chanya tutayasikia tu
 
FACT
 
Pia bodi ya Ligi iache ratiba za upendeleo. Simba na Yanga nazo zicheze saa nane namchana jua kali.
 
Back
Top Bottom