sikiliza alichosema kwani aliyofanya mtu mwaka jana na leo yanalingana na hata hivyo ameshauri namna ya kuondokana na tatizo wewe badala ya kukubaliana nae na kumsapoti unapiga kelele njoo na njia yako ya kumaliza tatizo la nishati.
Maana unapokosoa mtu toa na wewe ufumbuzi wa tatizo. Hii ndio tabu yetu watanzania kukosoa bila kutoa ufumbuzi.
HABARI LEO
RAIS mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, amesema matatizo ya nishati katika mataifa ya Afrika hayawezi kumalizika kwa kulia, bali kuwa na mikakati maalumu inayotekelezeka.
"Hata mkilia mpaka Mbinguni, lakini bila kuwa na mikakati bora na utawala bora kamwe hamtamaliza matatizo ya nishati katika nchi zenu," amesema Mkapa katika mkutano wa wakuu wastaafu wa mataifa ya Afrika uliokuwa ukifanyika jijini hapa.
Akiongoza mjadala kuhusu mustakabali wa kuwa na nishati ya uhakika juzi Mkapa alisema mataifa mengi yanayoendelea yamekuwa yakilalamika kukosekana nishati ya uhakika, lakini bila kufanya chochote cha kuondoa tatizo hilo.
Alisema pia dhana kuwa sekta binafsi ndiyo suluhisho la tatizo hilo ni potofu kwa kuwa Serikali zinapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tatizo hilo linatoweka.
"Ni vema serikali zikawa na mipango mizuri kuanzia uzalishaji wa nishati mathalan umeme, usambazaji na upatikanaji wake wa watumiaji," alisema Mkapa.
STORI NZIMA HAPA
My Take:
Yeye kwa miaka 10 aliyokaa madarakani alifanya nini zaidi ya yeye naye kulialia? Hivi Mkapa wakati anauza makampuni yetu kama njugu alihakikisha vipi kuna nishati ya kutosha wakati makampuni yanafufuliwa au alifikiria watatumia nishati ya kuni?
Jua hilo ndo kakumbuka blanketi! Alivyokuwa uwanjani hakuliona hilo sasa anatafuta kuwa mshangiliaji bora!:sleepy:
Binafsi, naamini hajakubali makosa aliyoyafanya. Ni kana kwamba anaamini kuwa watu wanamuonea na hawamshukuru.
Kashauri nini huyu? kama kweli angekuwa anajuwa thamani ya nishati na maana yake asingeiuwa kiwira hebu watanzania tufikiria na kuacha ushabiki anaongea hivyo na wakati yeye kaharibu hadi kero we mgodi wa 4 billion unauza kwa 700 m??? Ukitaka kujuwa alichofanya huyu mzee kaitembelee kiwira mine then uone now ilivyoSikiliza alichosema kwani aliyofanya mtu mwaka jana na leo yanalingana na hata hivyo ameshauri namna ya kuondokana na tatizo wewe badala ya kukubaliana nae na kumsapoti unapiga kelele njoo na njia yako ya kumaliza tatizo la nishati.
Maana unapokosoa mtu toa na wewe ufumbuzi wa tatizo. Hii ndio tabu yetu watanzania kukosoa bila kutoa ufumbuzi.
Aichoongea Ndugu Mkapa ni sahihi.Kwa kipindi alichokuwa madarakani amefanya mengi na hapa sina haja ya kuyataja.Na wengine waendeleze pale alipoishia.Mkapa hangeweza kufanya kila kitu kwa kipindi hicho cha miaka kumi.Waliopo nao waonyeshe mikakati yao ya kukabiliana na tatiozo la nishati.Ni dhahili kabisa nchi haiwezi kuondokana na tatizo la umeme kwa kulalamika majukwaani.hatua za dhati zichukuliwe kumaliza tatizo hilo.Tatizo letu watanzania ni kuchapa siasa na kukosa uzalendo na nchi yetu.
Kampuni ipi iliyokuwa ina uhai aliyoiuza? usitake kuaminisha watu yasiyo ya kweli.
Aichoongea Ndugu Mkapa ni sahihi.Kwa kipindi alichokuwa madarakani amefanya mengi na hapa sina haja ya kuyataja.Na wengine waendeleze pale alipoishia.Mkapa hangeweza kufanya kila kitu kwa kipindi hicho cha miaka kumi.Waliopo nao waonyeshe mikakati yao ya kukabiliana na tatiozo la nishati.Ni dhahili kabisa nchi haiwezi kuondokana na tatizo la umeme kwa kulalamika majukwaani.hatua za dhati zichukuliwe kumaliza tatizo hilo.Tatizo letu watanzania ni kuchapa siasa na kukosa uzalendo na nchi yetu.
aliweka mikakati gani yeye alipokuwa madarakani? Hili nalo ni kubwa jinga tu.