Mkapa ana matatizo gani? Angalia na hili....

HATA MKILIA MPAKA MBINGUNI ??INA MAANA YEYE HALII AU

mkuu bana yaani anazeeka VIBAYA MBAYAAAAA
 
Hana tofauti na wale waeneza dini wanaosema fuateni maneno yangu na sio matendo yangu....what a joke.....
 
sikiliza alichosema kwani aliyofanya mtu mwaka jana na leo yanalingana na hata hivyo ameshauri namna ya kuondokana na tatizo wewe badala ya kukubaliana nae na kumsapoti unapiga kelele njoo na njia yako ya kumaliza tatizo la nishati.

Maana unapokosoa mtu toa na wewe ufumbuzi wa tatizo. Hii ndio tabu yetu watanzania kukosoa bila kutoa ufumbuzi.

wakati amekabidhiwa jiko alishindwa kupika chakula kizuri ambacho kingewafanya watanzania wafurahi leo hii anatoka anatoa ushauri je kipindi ameshika makali hakuyaona haya au alihishia kusign mikataba na kujiuzia migodi
 
Mkapa.JPG


HABARI LEO

RAIS mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, amesema matatizo ya nishati katika mataifa ya Afrika hayawezi kumalizika kwa kulia, bali kuwa na mikakati maalumu inayotekelezeka.

"Hata mkilia mpaka Mbinguni, lakini bila kuwa na mikakati bora na utawala bora kamwe hamtamaliza matatizo ya nishati katika nchi zenu," amesema Mkapa katika mkutano wa wakuu wastaafu wa mataifa ya Afrika uliokuwa ukifanyika jijini hapa.

Akiongoza mjadala kuhusu mustakabali wa kuwa na nishati ya uhakika juzi Mkapa alisema mataifa mengi yanayoendelea yamekuwa yakilalamika kukosekana nishati ya uhakika, lakini bila kufanya chochote cha kuondoa tatizo hilo.

Alisema pia dhana kuwa sekta binafsi ndiyo suluhisho la tatizo hilo ni potofu kwa kuwa Serikali zinapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tatizo hilo linatoweka.

"Ni vema serikali zikawa na mipango mizuri kuanzia uzalishaji wa nishati mathalan umeme, usambazaji na upatikanaji wake wa watumiaji," alisema Mkapa.

STORI NZIMA HAPA


My Take:
Yeye kwa miaka 10 aliyokaa madarakani alifanya nini zaidi ya yeye naye kulialia? Hivi Mkapa wakati anauza makampuni yetu kama njugu alihakikisha vipi kuna nishati ya kutosha wakati makampuni yanafufuliwa au alifikiria watatumia nishati ya kuni?

Jua hilo ndo kakumbuka blanketi! Alivyokuwa uwanjani hakuliona hilo sasa anatafuta kuwa mshangiliaji bora!:sleepy:
 
Hiyo mikakati kama angeianzisha 1995 leo after 17 years tatizo la nishati lingekuwa ni historia. Hatusemi kuwa anachokisema ni ukweli ila tunachoshangaa ni yeye kutokuyajua haya wakati akiwa madarakani. Hivi Mkapa anafikiri kuwa tumeshasahau kama alikuwa Rais wa nchi hii miaka saba tu iliyopita?? Hivi anafikiri tumesahau kuwa tatizo la umeme limekuwa kubwa mara tu ya yeye kutoka madarakani?? Ningemuelewa kamaangesema mikakati yake ilikuwa A,B,C na alimuachia JK mafaili yote ila hakutekeleza hapo ningemuelewa. Siyo hili longolongo.................. Mbona hiyo Kiwila alijiuzia mpaka leo hatuoni huo umeme................???
 
Jua hilo ndo kakumbuka blanketi! Alivyokuwa uwanjani hakuliona hilo sasa anatafuta kuwa mshangiliaji bora!:sleepy:


Mwnkjj wewe ndo humwelewi Mkapa. Mwenzio anataka mabilioni ya MO Ibrahimu ya Rais mwenye kutoa kauli zenye tija baada ya kushidwa uongozi wenye tija. Nami ningekuwa na fursa ningempigia kura.
 
Mkapa ni janga la kitaifa, pia ni boriti inayomtafuna Kikwete kiana.

1. Mandela katika hotuba yake iliyofanyika bandarini, alimwonya mkapa kutouza mashirika ya uma hasa yale ya msingi na faida kwa nchi. Alijiuzia Ticts kwa miaka 15, halafu akajiongezea mingine 10 kinyemela na Kina karamagi. Pamoja na speech anayodaiwa kusifiwa humu (SA), Mandela hakuhudhuria na hakutaka kuonana na Mkapa tena fuatia jitihada za Mkapa kutaka aonane naye.

2. Mkapa ameongelea utawala bora, kibaya zaidi ni kuwa yeye akiwa kama Rais alishindwa kufanya hilo. Alifungua kampuni binafsi na mkewe akiwa ikulu (AnnBen), kinyume na sheria za utawala bora. Alizuia wachina kupewa Kiwira kwa bei ya juu, matokeo yake akajiuzia kwa bei chee mgodi ule, huku akiingia mkataba na tanesco wakulipwa mamilioni kwa siku, ukiacha mabilioni aliyopewa kwa dhamana ya serikali kwa ishu hiyo tu.

3. Ndege aliyojinunulia, rada chakavu iliyowekwa cha juu ni vitu ambavyo watanzania hawakuwa na umuhimu navyo, ndiyo ilikuwa dira yake, hapa siongelei Net-Group Solution ambayo mwane Nc alikuwa mmoja wa wakurugenzi waliokuwa wanalipwa siyo chini ya 20m kwa mwezi, na hapakuwa na lolote. Achilia mbali kuwa makampuni mengi ya nishati yanayo tunyonya yalisainiwa wakati wake.

Kinachokera watu hapa ni kuwa, anachohubiri siyo alichokifanya na matokeo ya aliyoyafanya ndio maana leo Tanzania ina matatizo ya umeme, madini, gesi, maji n.k! Tuzo ya Rais bora ambayo hutolewa kila mwaka na MO-Ibrahm, haijawahi kuona kutukuka kwake na huwa anaiotga. Hiyo nchi ya bondeni wana haki ya kumpa tuzo watakayo kwani, Tanzanite yetu wao ndio yao, alishawapaga migodi na haki zote. NBC aliyokuwa anaipigia debe iuzwe huko bondeni, imechoka na tayari ishauzwa kwa benk ingne.

Kwa swala la nishati, madini, maji NKapa hatakiwi kunyanyua mdomo wake, kwa hata Transparency International, walimwambia Jakaya katika jitihada zake za kurudisha migodi kwa wananchi au kuwepo na uwiano wa mapato, kuwa hana cha kufanya bkoz mtangulizi wake Ben, alishafunga loki zote.

Kibanga Msese
 
Mkapa ana-enjoy freedom ya muda aliyopewa na mwizi mwenzie,lakini akae akijua Nchi hii itakakuja ongozwa na mtu makini,mzalendo,anayefuta sheria na kuzitekeleza basi ajue hizi jokes zake ataziongelea jela.
 
Mkapa na dalali,muuza nchi Balozi Mpungwe ndio waliliangamiza Taifa la Tanzania.Yaani kama nchi hii inapata kiongozi wa mfano wa Sokoine,hawa jamaa wanaozea jela.
 
Sikiliza alichosema kwani aliyofanya mtu mwaka jana na leo yanalingana na hata hivyo ameshauri namna ya kuondokana na tatizo wewe badala ya kukubaliana nae na kumsapoti unapiga kelele njoo na njia yako ya kumaliza tatizo la nishati.

Maana unapokosoa mtu toa na wewe ufumbuzi wa tatizo. Hii ndio tabu yetu watanzania kukosoa bila kutoa ufumbuzi.
Kashauri nini huyu? kama kweli angekuwa anajuwa thamani ya nishati na maana yake asingeiuwa kiwira hebu watanzania tufikiria na kuacha ushabiki anaongea hivyo na wakati yeye kaharibu hadi kero we mgodi wa 4 billion unauza kwa 700 m??? Ukitaka kujuwa alichofanya huyu mzee kaitembelee kiwira mine then uone now ilivyo
 
Aichoongea Ndugu Mkapa ni sahihi.Kwa kipindi alichokuwa madarakani amefanya mengi na hapa sina haja ya kuyataja.Na wengine waendeleze pale alipoishia.Mkapa hangeweza kufanya kila kitu kwa kipindi hicho cha miaka kumi.Waliopo nao waonyeshe mikakati yao ya kukabiliana na tatiozo la nishati.Ni dhahili kabisa nchi haiwezi kuondokana na tatizo la umeme kwa kulalamika majukwaani.hatua za dhati zichukuliwe kumaliza tatizo hilo.Tatizo letu watanzania ni kuchapa siasa na kukosa uzalendo na nchi yetu.


Sahihi kwa lipi? Mbona mnakua na maono finyu sana kwa ujinga alofanya mkapa? Au sababu anajua kuongea ndo hata hamuoni maujinga yake? Huyu mzee hana maana hata kidogo akafie huko.... LAZY PUMPKIN huyu
 
Kampuni ipi iliyokuwa ina uhai aliyoiuza? usitake kuaminisha watu yasiyo ya kweli.


Kupenda kwingine taaaabu... Hivi NBC ilikuwa imekufa ndiyo ikauzwa kwa makaburu? Tanesco je, mpaka leo hawajapona majeraha ya Net Group Solutions
 
Mkapa alisimamia vipaumbele vyake vizuri katika utawala wake. Kila amabacho alinuia kufanya alikifanya na kikaonekana. Miundombinu ya barabara kilikuwa kipaumbele chake kikubwa, elimu na sekta ya fedha, afya na viwanda. Suala la umeme halikuwa la uhakika lakini halikuwa tatizo kubwa kulinganisha na wakati wa 2005-2012. Hivyo basi mikakati yake ilikuwa katika vipaumbele vingine. Utakumbuka hata bei za vyakula ilikuwa ya kawaida na serikali ilikuwa na fedha za kutosha za kujiendesha.Pamoja na mapungufu yake alijitahidi. Tulitegemea awamu hii ya utawala kuanzia pale alipoishia na kuendeleza sekta nyingine ikiwemo hii ya nishati. Lakini tumeona nchi imezidi kurudi nyuma kimaendeleo kwa kasi ya ajabu isivyotarajiwa. Utasema Mkapa hakuwa na vision? Je na Kikwete? tuache chuki na tuuone huu ukweli. Ninaamini Mkapa anakijua anachokiongea na ana maanisha. Kama aliacha mpango wa ujenzi wa nyumba za watumishi mawilayani na hela yake ilitengwa basi naamini mpango wa nishati ulikuwepo lakini hakuwa na muda wa kuutekeleza na sasa hivi anatoa ushauri (sio vibaya kutoa ushauri). Mtoa ushauri huwa anasema kulingana uzoefu wake katika sekta hiyo au kushindwa kwake katika kutimiza wajibu katika sekta husika n.k. Hivyo tusimbeze Mkapa bali tuchukue ushauri wake.
 
Aichoongea Ndugu Mkapa ni sahihi.Kwa kipindi alichokuwa madarakani amefanya mengi na hapa sina haja ya kuyataja.Na wengine waendeleze pale alipoishia.Mkapa hangeweza kufanya kila kitu kwa kipindi hicho cha miaka kumi.Waliopo nao waonyeshe mikakati yao ya kukabiliana na tatiozo la nishati.Ni dhahili kabisa nchi haiwezi kuondokana na tatizo la umeme kwa kulalamika majukwaani.hatua za dhati zichukuliwe kumaliza tatizo hilo.Tatizo letu watanzania ni kuchapa siasa na kukosa uzalendo na nchi yetu.

KATITU nakuunga mkono 100%, Mkapa had vision, alipoiingia madarakani alikuta uchumi umekufa kwa hiyo kitu cha kwanza ilikuwa ni kuinua uchumi kitu ambacho alifanikiwa kwa kiasi kikubwa na uchumi ni pamoja na miundo mbinu ambalo pia alianza vema sana, sasa aliyefuata ilibiidi aanzie pale alipoishia. Sasa successor wake alipoingia tu akagawa billion moja kila mkoa ambazo alitoa asante kwa waliompigia kampen coz nasema hivi hata ukimuuliza atoe impact ya zile hela hawezi kujibu chochote.
Hata tuseme Mkapa he did his best and he need to be congratulated and let rest. He is and was my president
 
aliweka mikakati gani yeye alipokuwa madarakani? Hili nalo ni kubwa jinga tu.

tumemzoea ni mtaalam wa kukanusha!
Ukisikia kuzeeka vibaya ndo hii ya mkapa!
10 yrs ikulu, alaf wajaongeo upuuzi!
Na baada ya kutambua, anaisadiaje nchi yake!
 
Viongozi was kiafrica ndivyo walivyo, wakiwa madarakani hawasikilizi wala hawashauriki, wakitoka madarakani ndo anajifanya anawajua mahitaji ya Taifa! Sinema ya mwisho mtaiona Vasco da Gamba akitoka madarakani-atapinga sana rais atakae kuwepo kusafiri hata mara moja kwa mwaka!
 
Nacho jaribu kufocus hapa ni kwamba nyani siku zote huwa haoni kundule,anachofanya ni kutaka huruma ya Watanzania,lakini anasahau yeye ndiyo chanzo cha matatizo yote na hakwepi suala la kuiiza nchi kinyemela bila ridhaa ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom