Mkapa ana matatizo gani? Angalia na hili.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa ana matatizo gani? Angalia na hili....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 27, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  HABARI LEO

  RAIS mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, amesema matatizo ya nishati katika mataifa ya Afrika hayawezi kumalizika kwa kulia, bali kuwa na mikakati maalumu inayotekelezeka.

  "Hata mkilia mpaka Mbinguni, lakini bila kuwa na mikakati bora na utawala bora kamwe hamtamaliza matatizo ya nishati katika nchi zenu," amesema Mkapa katika mkutano wa wakuu wastaafu wa mataifa ya Afrika uliokuwa ukifanyika jijini hapa.

  Akiongoza mjadala kuhusu mustakabali wa kuwa na nishati ya uhakika juzi Mkapa alisema mataifa mengi yanayoendelea yamekuwa yakilalamika kukosekana nishati ya uhakika, lakini bila kufanya chochote cha kuondoa tatizo hilo.

  Alisema pia dhana kuwa sekta binafsi ndiyo suluhisho la tatizo hilo ni potofu kwa kuwa Serikali zinapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tatizo hilo linatoweka.

  "Ni vema serikali zikawa na mipango mizuri kuanzia uzalishaji wa nishati mathalan umeme, usambazaji na upatikanaji wake wa watumiaji," alisema Mkapa.

  STORI NZIMA HAPA


  My Take:
  Yeye kwa miaka 10 aliyokaa madarakani alifanya nini zaidi ya yeye naye kulialia? Hivi Mkapa wakati anauza makampuni yetu kama njugu alihakikisha vipi kuna nishati ya kutosha wakati makampuni yanafufuliwa au alifikiria watatumia nishati ya kuni?
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  kiwira keshaisahau?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Huyu ni MWIZI tu ambaye ameamua kubwabwaja kila anapopata nafasi lakini wizi alioufanya kupitia ununuzi wa rada, uuzwaji wa nyumba za Serikali, Kukwapua Kiwira, ununuzi wa ndege ya Rais akiwa kabakisha miezi mitatu tu kumaliza awamu yake, wizi kupitia netgroup solutions, ununuzi wa helicopters na magari ya jeshi na hadi hii leo hataki kuzungumzia kuhusu ni nani aliyekuwa anafanya naye biashara alipokuwa Ikulu.
   
 4. k

  kaka miye Senior Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sikiliza alichosema kwani aliyofanya mtu mwaka jana na leo yanalingana na hata hivyo ameshauri namna ya kuondokana na tatizo wewe badala ya kukubaliana nae na kumsapoti unapiga kelele njoo na njia yako ya kumaliza tatizo la nishati.

  Maana unapokosoa mtu toa na wewe ufumbuzi wa tatizo. Hii ndio tabu yetu watanzania kukosoa bila kutoa ufumbuzi.
   
 5. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji kweli unamchukia mkapa!

  Mambo mengi sana we huwa unakua msitari wa mbele kutaka tujadili hoja tusiwajadili watu, lakini ikifika kwa mkapa....mmh!

  Hebu niambie, kasema uongo?, aliyo sema hayawezekani? (simply kwa vile yeye hakuyafanya?)
   
 6. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni kweli asemayo Mkapa.

  Kulia na kulalamika hata kumuomba Mungu hakuwezi kuwa suluhubali kuwakamata akina Mkapa na kuwawajibisha kwa uovu waliolitendea taifa.

  Kimsingi Mkapa, kutokana na kujisahau na kulewa madaraka anawaona watanzaniakama wavivu wa kufikiri kiasi cha kuwatia madole machoni akijua hawatamfanyakitu. Wakati wa kuwakamata akina Mkapa na washirika zake na mkewe umefika ililiwe somo kwa waliopo.

  Kuna haja ya watanzania kuamka na kuwashughulikia mafisina mafisadi wenye madaraka
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Iwapo Mkapa angejitahidi kufanya hivyo ila mazingira yaliyokuwapo yakamfanya ashindwe kutimia azma yake, kweli ningemsapoti sana katika hoja hii. Tatizo ni pale yeye alikuwa akifanya mambo kinyume kabisa na hayo anayozungumza leo.

  Ni kama vile amejifunza kuwa alifanya makosa baada ya kutoka madarakani au wakati akiwa madarakani alikuwa hatumii akili kabisa.
   
 8. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,972
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aliweka mikakati gani yeye alipokuwa madarakani? Hili nalo ni kubwa jinga tu.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Binafsi, naamini hajakubali makosa aliyoyafanya. Ni kana kwamba anaamini kuwa watu wanamuonea na hawamshukuru.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Katafute post zangu za nyuma kuhusu ufumbuzi wa matatizo ya nchi yetu badala ya kukurupuka.

  Mkapa hana jipya alipewa madaraka akayachezea na kuingiza nchi katika mikataba ambayo haina maslahi kwa Watanzania.

  Wabunge wakiwemo wa CCM walipokuja juu kutaka kuiona mikataba hiyo wakati Mkapa akiwa madarakani akasafiri haraka sana kwenda Dodoma kukutana na wabunge wa CCM katika kikao cha siri na hivyo kuwanyamazisha wasiendelee na madai yao ya kutaka kuiona mikataba ile.

  Huyu ni mwizi tu ambaye anatafuta umaarufu asiokuwa nao na kuchagua nini cha kuongea huku akiwa kalitia hasara Taifa la Tanzania kwa pesa chungu nzima alipokuwa madarakani.
   
 11. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Yanayowezekana kukiri anakiri, kwa mfano katika mkutano wa kimataifa uliofanyika Mliman City, alikiri kwamba ubinafsishaji haukwenda vizuri kama ilivyotakiwa. We ulitaka asimame aseme nakiri nilikosea kujiuzia Kiwira sio?, mambo hayaendi hivyo katika dunia hii. Kiongozi yeyote anapopewa kashfa/tuhuma halafu asijitetee specifically kwa hiyo kashfa huwa anakua amekiri tayari. Ofcoz yapo mengine huwa anasingiziwa na pia ni kweli kwamba mazuri yake hayasemwi.

  Nani kama mkapa katika awamu hizo 2. kabla na baada?
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Katika hali ya kawaida, tatizo la nishati ni tatizo nyeti sana hata kwa nchi ya dunia ya kwanza seuze sie wazee wa stone age tunaotawaliwa na wachumia tumbo wene upeo usiozidi pua zao bapa?

  Nishati ina-link moja kwa moja na maendeleo ya viwanda na bei ya bidhaa, hata kukiwa na miundombinu bora (ambayo haipo) bila ya nishati ya uhakika ni kazi bure. And worse wanasiasa wetu uchwara wameigeuza Tanesco ni goldmine yao na mikataba ya kina chifu Mangungu kwene mambo ya gesi na mafuta imeshika kasi.
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mie kanifurahisha tu kupanda kizimbani kumtetea Mahalu, ati anawashangaa waliompeleka mahakamani (serikali) kwa sababu kila kitu kilikuwa approved!

  Siku hizi usishangae ya Mussa wala ya Firauni, kuna ya CCM!
   
 14. g

  gpluse JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 394
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 80
  Mfa maji! Alishinikiza Net Group Solutions ili kumsaidia kuiba. Kwa muda wote aliokuwa madarakani hakukuwa na uwekezaji kwenye sekta ya nishati. Leo hii ati analiona tatizo. Kweli watanzania amkeni kuondoa unyonyaji na ujinga vinginevyo hadithi zitaendelea kwa zaidi ya miaka 50 mingine na hakutakuwa na jipya.
   
 15. M

  Masabaja Senior Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu ni mwizi anatoa ushauri gani na wakati alipokuwa rais alileta kampuni ya kihuni kuongoza tanesco ikala pesa na miaka yote kumi akuwekeza kwenye umeme akawa anakula pesa, akuishia hapo mwizi huyu akajibinafshia kiwira, akanunua rada feki leo chenji imerudi AIBU, akaja na dege bovu, akaingia mikataba ya kinyonyaji ya madini leo hii tunalia sasa huyu mwizi anakuja na pumba kama hizi yeye alikuwa kiongozi halafu anatuambia hata tukilalamika kwa nini tusilalamike kwa kuwa yeye alikuwa kiongozi hakufanya kitu zaidi ya KUTUIBIA MWIZI MKUBWA ANYAMAZE KIMYA ASUBIRI KUSHITAKIWA SIKU SERIKALI MAKINI IKIINGIA MADARAKANI
   
 16. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  kubwa jinga tu hili. si ni yeye aliyejiuzia kiwira ili taifa lisiwe na vyanzo vyake vya nishati? anahubiri nini sasa
   
 17. U

  Uswe JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwenye kigoda cha mwalimu Mkapa alisema, hata kama kuna makosa ya kimaamuzi alifanya wakati wake, suluhisho ni kulalamika tu? akahoji, ''hata kama ni kweli naambiwa niliuza mashirika ya umma, mbona sijaona kiwanda hata kimoja kilichoanzishwa toka nimeondoka?'' - MM, hata kama hatutaki, hapa kuna hoja!

  Ni kweli kuna makosa ya kimaamuzi na ufisadi wakati wa mkapa, lakini toka braza achukue nchi ni mwaka wa saba sasa, mkapa alipaswa awe amewajibishwa toka 2005 baada ya kutoka madarakani na sasa tungekua tunaongelea mambo mengine.

  My Take:
  Kama Mkapa ni Tatizo, Kikwete ni Tatizo kubwa zaidi
   
 18. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  amekiri kuwa kubinafsisha hakusaidii na akakiri bila utawala bora hakuna kitakachoendelea.

  ANAUNGANA NA SISI KUWA KUIONDOA CCM MADARAKANI NDIYO DAWA.
  WALIOBINAFSISHA KILA KITU NI CCM,WANAOKUMBATIA MAFISADI KATIKA KILA SEKTA NI CCM.
   
 19. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2012
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mzee Mwanakijiji, nanukuu Habari Leo "Alisema pia dhana kuwa sekta binafsi ndiyo suluhisho la tatizo hilo ni potofu" nadhani huku ni kukubali makosa aliyoyafanya, indirectly. Mzee unataka rasmi kwenye TV?

  Vyama vya siasa, kila mmoja waonyeshe mipango ya kudhibiti suala la nishati. (energy policy). Nadhani kuna watu humu bongo wenye uwezo wa kuplani and kutekeleza ufumbuzi.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kampuni ipi iliyokuwa ina uhai aliyoiuza? usitake kuaminisha watu yasiyo ya kweli.
   
Loading...