Mkapa above the law?: Allegations

Hivi huko Mtibwa wakati akiwa RAIS si ndiko alipeleka FFU kuwatwanga wafanyakazi wakiwa wamegoma hili waache mgomo?

Huyu Mzee nafikiri inatakiwa asurubiwe tena mbele ya watanzania, hivi si ndiye aliyeleta Netgroup Tanesco na akaweka FFU wawalinde hili waingie ofisini?

Nafikiri huyu mzee alifanya uhalamia wa kutosha, sasa ni zamu ya Watanzania kumsurubu. Mimi nafikiri inatosha. Sheria ichukue mkondo wake, hivi hilo shamba box yake nini? TUsije kukuta pia ni magogoni.
 
Mkapa hana tatizo zaidi ya RUKSA iliyoanzia kwa Mzee ruksa mpaka kuvunja miiko ya uongozi ya JKN.

Hilo ndio chimbuko na KIRUSI kilichomuingia Mkapa na kitakachomtafuna mpaka siku ya mwisho wa maisha ya dunia hii.

Ingawa:

Anaweza kuja mbele ya jukuwaa na kusema kama nilivyosema hapa na kuoamba msamaha.

Haikuwa nia yake. BALI ALIKUWA ANATEKELEZA AZIMIO LA ZANZIBAR!

NDIO: situations and all circumstances...zilizojengwa na kiongozi kabla yake ..na kuhitimishwa na azimio la zanzibar...hata hawa wana JF ..wanaolalama hapa ..wengi wangeteleza... Alipo Rasi wetu Mstaafu!

Mkapa anashindwa kuja kujieleza tu! He did a good Job kuja kutekeleza Azimio la zanzibar kwa VITENDO..Kalisome then utaona kuw aMkapa hakuwa na Tatizo zaidi ya kulitekeleza azimio hilo!!

Kutoka enzi ya Azimio la arusha... na kuingia utandawzi....Na falasa ya RUKSA..Those factors ....vimechankia sana kuvuruga Fikra za Mkapa na kumuingiza ..hapo alipo...!

Mkapa just come forward ..and tell all ...nini hasa kilikushwashi..wewe..Mr Clearn...Mpaka hapo ulipo...There must be obviouse contributing factors....

Mkapa njoo mbele yetu fafanua....usijifiche....!! Ulikuwa Mtiifu Kwa azimio la zanzibar Tu!!!

All what Mkapa did NI UTEKELEZAJI WA AZIMIO LA ZANZIBAR..sijui anapata kigugumizi gani....AJE ASEME!!! The tuanza mjadala mwingine wa kina.

Nani haoni hivyo???
 
kwa serikali iliyopo hata tuandike mara mia jamani hili bwana wala halioni na
hakuna kupya wala atakae mgusa....ila tusikate tamaa uwezi jua...
OBASANJO akaleta matumaini nchini kwetu
 
Mkuu Field 80
Huyu Mama Wala Msimsingizie Huyu Alijiibia Kivyake Ila Jamaa (ben)
Ndugu Zake Walimwambia Mbona Mama Anamali Nyingi Na Wewe Una Nini Akaona
Huu Ujinga Akaanza Kuiba Ovyo Bila Kusoma Nyakati Na Haya Ndio Matokeo Yake .....akujua Yule Mama Anaiba Kwa Adabu..ille Jengo La Ilala Kasahauza Kwa Jamaa Wa Imaleseko..mkapa Kila Anaetaka Kumuuzia Heka Za Mtibwa Anaogopa ....baba Nkapa Hilo Unaloo Utoki Mzeee.....hata Uende Kwenu Kuzindika
 
Kuna bwana moja anaitwa Tambwe Hiza,aliandika makala ndefu sana kuhusu "ujasiriamali" wa mzee Mkapa;akiusifu,hauna tatizo!
Itapendeza akitolea maelezo mengine kutoka pale Lumumba kwenye ofisi ya propaganda ya CCM.
 
Kimsingi sioni shida kwa mzee Mkapa ku-own shamba, na kama katiba au maadili ya uongozi yanamzuia kufanya hivyo nadhani hizo instruments ndio zenye matatizo na zinapaswa kurekebisha.

Kinachoudhi ni kwamba umiliki unafanywa siri na kumekuwa na upendeleo kwa sababu ya influence ya madaraka aliyokuwa nayo. Kwa mfano ni kwa nini yeye halipi michango kwa Association ya wakulima kama wakulima wengine?
 
Mkuu mimi nafikiri tumezidi ,kila kitu kulaumu laumu tu hakusaidii

Mkapa kumiliki Mtibwa ama shamba si tatizo na ni haki ya kila mtanzania labda kama kuna sheria inayosema ukishakua Rais basi hutakiwa kumiliki biashara yoyote hapo itakua sawa lakini kama haipo tatizo la mkapa lipo wapi??

Mimi nafikiri sisi watanzania tuna wivu,roho ya korosho na wavivu wa kufikiri,kwanini yani mfano ukianzisha leo kibanda cha kuuza nywere pale mwenge na watanzania wakakuona unapata fedha utaona mwingine naye analeta kibanda chake palepale ulipo na yeye anaanza kuuza nywere cha ajaabu zaidi badala ya kukubali ushindani yeye ataanza kukulaumu tena wewe kuwa unamnyang'anya wateja.

Kama ni mashamba yapo mengi tu na lunch zipo nyingi tu na zimekufa zimegeuka pori na wala hatuzipigi kelele ,wewe unayepiga kelele kuhusu shamba la mkapa nawewe katafute shamba ulime harafu uoombe uhisani na mtibwa .

Leo hii mashamba yaliyogeuka mapori yapo mengi tu wakiambiwa wanaachi wayachukue walime hakuna hata mmoja atayejitokeza lakini Kikwete ama Lowasa ama Azizi ama Amani akijitokeza na akaamua kuyaendeleza na akafanikiwa kwa wivu na kinyongo tulicho nacho tutajitokeza na kuanza kuhoji jinsi alilivyolipata shamba hilo.

Acheni kuogopesha watu na neno UFISADI wewe chukua basi nenda Tanga ,chukua basi uelekee mwanza ,chukua basi uelekee tunduma utaona mashamba mengi yaliyo kufa na kugeuka pori ,luch nyingi zilizokufa nazo utaziona.Ukiona cha elea usifikiri ni chepesi kimeundwa

Ubinafishaji ulikua na lengo nzuri sema kila jambo lazima liwe na hasara zake na wajanja kujipenyeza kufanya mambo yao hilo haliepukiki.

Kabla ya ubinafishaji kagera sugar,mwatax,mutex viwanda vyote vya nguo ukitoa urafiki vilikua vimekufa.

Yale mashirika ya mikoa sijui RTC yako wapi? leo hii mtu akiyarudisha na yakabinafisishwa watu wataibuka na kuhoji.

Viwanda vingi,mashirika mengi kabla ya mkapa yalikua yamekufa,kabla ya mkapa Shule nyingi ziliteteleka waalimu waliaacha kazi na kufanya biashara wafanyakazi serikalini walikimbia kazi zao wakawa wafanya biashara.

Tatizo la la Tanzania ni tatizo kua mWatanzania .
 
Ndio maana nimesema tena na kurudia kuwa mkapa alitekeleza Falasafa ya RUKSA iliyochimbuko la AZIMIO LA ZANZIBAR lililorekebisha AZIMIO LA ARUSHA.

Mkapa hahitaji kujificha na kunyaama..Aje atoe DARASA ZITO KABISA..Ili tufungue ukurasa mpya!
 
Single D,
Asante kwa kutukumbusha ya Askofu na nguo ya ndani ya padiri! Lakini kwa ufisadi wote huu tunaousoma ambao tunaambiwa ulitokea wakati wa Rais Mkapa kama ni kweli basi ni wazi kwamba wananchi tuliachwa bila 'nguo za ndani' za kiuchumi. Mkapa has a case to answer! Wakati mwingine nashindwa kabisa kuamini kwamba mtu aliyeaminiwa sana na Mwalimu wake wa darasani na wa kisiasa aliweza kufanya yote yanayoorodheshwa. Kama Mwalimu anaona haya yote nadhani anajisikia vibaya kweli kweli kwa kumpigia debe 'Rais wake'!
 
Bw. Yahya alizidi kudai kuwa Bw. Mkapa, kama walivyo wakulima wengine wa nje wa Mtibwa, ni mkulima halali anayelipa makato yake kama wakulima wengine isipokuwa ameingia mkataba wa kibiashara kwa kuhudumiwa shamba lake na kiwanda.

Source:http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/06/07/115999.html

Mmhh!!! Hivi babangu Jidulamabambasi anaweza kuingia mktaba na MWATEX ili shamba lake la pamba lihudumiwe na kiwanda??? Yayaa, bagosha. Mie naenda zangu kujinywea pingu sasa nisijue tena kinachoendelea hapa duniani
 
Tamaa nyingine bwana mtu kesha zeeka lakini bado tu anachuma hivi hiyo 80% aliona kama haita mtosha mpaka akaingia majaribuni kama hivi?
Dah hii kali sana.Anajidhalilisha mwenyewe kwa tamaa za mzee fisi.

Mafisadi kamwe hawatosheki!
 
Sio tatizo mkapa kumiliki shamba lakini akilimiliki kwa gharama za watanzania masikini hapo ndo tatizo linaanzia hapo, huyu mtu ni mchafu sana, kwani hata kagera sugar na kwenyewe kuna minongono kuwa yumo sisi tutege masikio siku moja tutapata ukweli, wananchi wangapi wanaweza kupata huduma ya kuangaliziwa mashamba yao, labda bwana yahya atuambie mpaka sasa ni wakulima wangapi wanaoangaliziwa mashamba yao na kiwanda?

Wanajitajirisha kwa gharama ya wananchi na watu hata hapa JF wanamtetea kuwa hakuna tatizo kwa yeye kumiliki shamba, ili shamba lisiwe ni gharama za wananchi, Mwalimu Nyerere alilima mashamba yake watu wote wanaona hakukuwa na siri kwanini yeye awe na shamba kwa siri mpaka yamkae kooni ndo viongozi wa kiwanda wamtete.
 
Mkuu mimi nafikiri tumezidi ,kila kitu kulaumu laumu tu hakusaidii

Mkapa kumiliki Mtibwa ama shamba si tatizo na ni haki ya kila mtanzania labda kama kuna sheria inayosema ukishakua Rais basi hutakiwa kumiliki biashara yoyote hapo itakua sawa lakini kama haipo tatizo la mkapa lipo wapi??

Mimi nafikiri sisi watanzania tuna wivu,roho ya korosho na wavivu wa kufikiri,kwanini yani mfano ukianzisha leo kibanda cha kuuza nywere pale mwenge na watanzania wakakuona unapata fedha utaona mwingine naye analeta kibanda chake palepale ulipo na yeye anaanza kuuza nywere cha ajaabu zaidi badala ya kukubali ushindani yeye ataanza kukulaumu tena wewe kuwa unamnyang'anya wateja.

Kama ni mashamba yapo mengi tu na lunch zipo nyingi tu na zimekufa zimegeuka pori na wala hatuzipigi kelele ,wewe unayepiga kelele kuhusu shamba la mkapa nawewe katafute shamba ulime harafu uoombe uhisani na mtibwa .

Leo hii mashamba yaliyogeuka mapori yapo mengi tu wakiambiwa wanaachi wayachukue walime hakuna hata mmoja atayejitokeza lakini Kikwete ama Lowasa ama Azizi ama Amani akijitokeza na akaamua kuyaendeleza na akafanikiwa kwa wivu na kinyongo tulicho nacho tutajitokeza na kuanza kuhoji jinsi alilivyolipata shamba hilo.

Acheni kuogopesha watu na neno UFISADI wewe chukua basi nenda Tanga ,chukua basi uelekee mwanza ,chukua basi uelekee tunduma utaona mashamba mengi yaliyo kufa na kugeuka pori ,luch nyingi zilizokufa nazo utaziona.Ukiona cha elea usifikiri ni chepesi kimeundwa

Ubinafishaji ulikua na lengo nzuri sema kila jambo lazima liwe na hasara zake na wajanja kujipenyeza kufanya mambo yao hilo haliepukiki.

Kabla ya ubinafishaji kagera sugar,mwatax,mutex viwanda vyote vya nguo ukitoa urafiki vilikua vimekufa.

Yale mashirika ya mikoa sijui RTC yako wapi? leo hii mtu akiyarudisha na yakabinafisishwa watu wataibuka na kuhoji.

Viwanda vingi,mashirika mengi kabla ya mkapa yalikua yamekufa,kabla ya mkapa Shule nyingi ziliteteleka waalimu waliaacha kazi na kufanya biashara wafanyakazi serikalini walikimbia kazi zao wakawa wafanya biashara.

Tatizo la la Tanzania ni tatizo kua mWatanzania .

MkamaP,

Kuna mambo mengi labda hujaelewa kwenye hili suala la Mkapa, kwanza ni juu ya hilo la kufanya biashara ikulu, maadili yanakataza na kibaya zaidi kuna conflict of interest nyingi zinaingiliana.

Pili ni hilo la kutumia connections zake kujinufaisha, anachotakiwa kufanya Mkapa ni kununua shamba lake kiwazi, kulima kiwazi na kuingia mikataba na makampuni yoyote kiwazi. Kila ninaposoma siamini Mkapa alifanya hivyo, ni kama yeye anatumia connections zake kuhakikisha watu wengi wanamfanyia kazi. Matokeo yake mazao yake yanapambanishwa na mazao ya wakulima wengine ambao wametumia juhudi zao. Hapo bei haiwezi kuwa fair, ni kama shamba la Mkapa liko subsidized .

Kila ukisoma unaona jinsi conflict of interest inavyojichanganya kila sehemu. Sio fair kwa wananchi wa kawaida. Ukienda ndani si ajabu jamaa hata kodi halipi inayostahili na mambo mengine kadhaa.

Tusipoangalia haya mambo ya conflict of interest kwenye biashara za viongozi wetu, jua tunaenda kubaya. West walipata matatizo makubwa kwenye haya mambo ndio maana kila siku wanazidi kubana sheria za conflict of interest. Ni hulka ya binadamu kuwa mchoyo, ndio maana kuna sheria ili kuzuia uchoyo wa mtu mtu usiwe na madhara kwa wengine. Hao wakulima wengine wanahitaji a level playing ground na sio mmoja anachezea kwenye carpet wakati wengine kwenye matope.
 
Mkapa hana njia ya kukwepa lazima awafuate wakina chiluba haiwezekani tumwache hivi hivi tutalaaniwa na historia itatuhukumu. kama serikali ya CCM haitamshughulikia yeye na wengineo basi Kikwete afute usemi wake wa kupambana na rushwa na ufisadi na aseme anaendeleza na kuwalinda ili tuelewe moja. Imani na matumaini yetu kwake yameshatoweka tunamsubiri tumfanyie hitimisho 2010.
 
MkamaP,

Kuna mambo mengi labda hujaelewa kwenye hili suala la Mkapa, kwanza ni juu ya hilo la kufanya biashara ikulu, maadili yanakataza na kibaya zaidi kuna conflict of interest nyingi zinaingiliana.

Pili ni hilo la kutumia connections zake kujinufaisha, anachotakiwa kufanya Mkapa ni kununua shamba lake kiwazi, kulima kiwazi na kuingia mikataba na makampuni yoyote kiwazi. Kila ninaposoma siamini Mkapa alifanya hivyo, ni kama yeye anatumia connections zake kuhakikisha watu wengi wanamfanyia kazi. Matokeo yake mazao yake yanapambanishwa na mazao ya wakulima wengine ambao wametumia juhudi zao. Hapo bei haiwezi kuwa fair, ni kama shamba la Mkapa liko subsidized .

Kila ukisoma unaona jinsi conflict of interest inavyojichanganya kila sehemu. Sio fair kwa wananchi wa kawaida. Ukienda ndani si ajabu jamaa hata kodi halipi inayostahili na mambo mengine kadhaa.

Tusipoangalia haya mambo ya conflict of interest kwenye biashara za viongozi wetu, jua tunaenda kubaya. West walipata matatizo makubwa kwenye haya mambo ndio maana kila siku wanazidi kubana sheria za conflict of interest. Ni hulka ya binadamu kuwa mchoyo, ndio maana kuna sheria ili kuzuia uchoyo wa mtu mtu usiwe na madhara kwa wengine. Hao wakulima wengine wanahitaji a level playing ground na sio mmoja anachezea kwenye carpet wakati wengine kwenye matope.

Mtanzania
Nimekupata ,lakini mimi Nafikiri hiyo conflikti ya interesti inabidi iangaliwe kwa kwa mapana yake.

Ukiangalia hilo shamba la Mkapa mimi bado sijaona sehemu panapoenyesha kanunua lini nilichoana ni kua amelimiki zaidi ya miaka kumi iliyopita.

Pili sijaona mahala kua hilo shamba kalinunua kutoka kwa mtu binafsi ama lilibinafisishwa kutoka serikalini .Na hata hivyo kama alinunua kwa kufuata sheria huo mimi nafikiri ni moja ya njia ktk uwazi ,kinachoshawishika hapa ni kua kwanini alipolinunua shamba hilo hakuenda ktk vyombo vya habari na kuwatanganzia watanzania sasa anamiliki shamba Fair point

Mtanzania nimekuelewa ila hoja yetu hapa wengi tunaunganisha kuhudumiwa kwa shamba hilo ni ufisadi hapa nachelea kusema wenda tunakurupuka kupita kiwango.

Mfano kama kaka yangu ni mwalimu si lazima mimi niwe mwalimu eti kwa vile tumemelewa malezi sawa.Hapa nasema hivi mkulima Mkapa Terms na konditions walizotiliana saini na mtibwa si sawa na terms za wakulima wengine.

Mimi ktk hili bado sina data za kutosha za kuanza kumlaumu Mr X-Presd , Ila ujumbe niliopata na wewe mtanzania naamini umeupata kutokana na somo hili la Mkapa kua kumbe
Mtanzania , mimi na yule tunaweza kwenda kujenga vyuo vikuu tanzania na tukaingia ubia na serikali wa kutunza vyuo vikuu hivyo.

Alamski <<<==== Binulu
 
Tuhuma za ufisadi dhidi ya Mkapa

2008-06-08 12:26:22
Na Simon Mhina

Familia ya Baba wa Taifa marehenu Mwalimu Julius Nyerere, imeelezea kusikitishwa na `mikasa` ya ufisadi na kufanya biashara akiwa Ikulu zinazomkabili rais mstaafu Bw. Benjamin Mkapa, ambaye kutokana na `usafi` wake baada ya kifo cha muasisi huyo wa Taifa hili, alipewa hadhi ya kuwa mwanafamilia wa ukoo huo.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, ambaye pia ni mtoto wa Mwalimu, Bw.

Charles Makongoro Nyerere alisema wanatamani mambo hayo yamalizike.

Bw. Makongoro alikuwa akizungumzia madai yanayotolewa na wananchi kwamba Bw. Mkapa avuliwe `hadhi` aliyopewa ya kuwa miongoni mwa familia hiyo, kutokana na kuvunja miiko ya hayati Baba wa taifa, ikiwemo kufanya biashara akiwa Ikulu.

Hata hivyo Bw. Makongoro alisema haitakuwa rahisi kumuondolea Bw. Mkapa hadhi hiyo, kwa sababu ya tuhuma ambazo hazijathibitika.

Alisema hata kama tuhuma dhidi yake zitathibitika, ukoo ni kitu cha kimila, ambacho kinajumuisha wema na wabaya.

``Hata kama wanasema amekosea amevunja miiko, ni vugumu kumuondoa kwenye familia, kwa vile hata akiondoka, hata waliosalia wengine huenda wana madhambi kibao,``alisema.

Lakini alisisitiza kwamba Bw. Mkapa hakupewa hadhi ya kuwa mwanafamilia ya Nyerere kutokana na sababu za usafi wake pekee bali heshima hiyo ilitokana na kuwa karibu na familia hiyo.

Alipoulizwa kwamba kama ni suala la `ukaribu` pekee lililofanya Rais huyo mstaafu apewe hadhi hiyo, ni vipi Rais wa awamu ya pili mzee Alli Hassan Mwinyi hakuwezeshwa, Bw. Makongoro aliguna kisha akacheka.

``Unajua bwana kuwa mwanafamilia au mwana ukoo kwetu sisi Wazanaki ni kitu cha kawaida, ndio maana hata mtoto aliyezaliwa kikeni, anaweza kuamua kwa hiari yake kujiunga na ukoo wa upande wa kiumeni, kwa hiyo hili la Mkapa sio jambo la kuumiza watu vichwa,``alisema.

Pia alipoulizwa kuwa kama si sababu za `usafi` pekee zilizomfanya Bw. Mkapa awe mwanafamilia wa Nyerere, sababu zingine ni zipi, Bw. Makongoro alisema hafahamu sababu hizo, na kwamba siku ya `kumteua` yeye hakuwepo kwenye kikao.

Katika hatua nyingine, Bw. Makongoro alisema ni vema suala la kuruhusiwa au kutoruhusiwa biashara Ikulu likawekwa kwenye sheria.

Alisema kwa sasa yeye anaamini kwamba maneno ya mwalimu kukemea kufanya biashara Ikulu yalikuwa mawazo yake binafsi.

``Wakati fulani nilikuwa nazungumza na watu kule Afrika Kusini wakauliza kama Tanzania kuna sheria yoyote inayomkataza mtu kufanya biashara akiwa Ikulu, sikupata jibu sahihi nikabaki naduwaa,``alisema.

Alikumbusha kuwa Baba wa taifa alitoa mawazo mengi, yakiwemo ya kutaka wagombea binafsi waruhusiwe lakini akasema haelewi kwanini hilo linapuuzwa.

Hivi karibuni viongozi wa kambi ya upinzani wamekaririwa kwa nyakati tofauti wakisema kutokana na kufanya biashara Ikulu, Bw. Mkapa hastahili kuendelea kuwa mwanafamilia ya Mwalimu, heshima aliyopewa mara baada ya kifo cha baba wa taifa.

Bw. Mkapa anatuhumiwa kununua `kimagendo` Mgodi wa Kiwira, kuanzisha kampuni ya ANBEN na kutumia ofisi za Ikulu kwa ajili ya kampuni hiyo.

Pia anatuhumiwa kumiliki mahekalu ya kifahari na mashamba huko Morogoro, ambavyo vyote anadaiwa kuvipata kwa kutumia madaraka yake.

SOURCE: Nipashe
 
Wamiliki wa Mtibwa ndio wale wanaomiliki pia Kagera Sugar na ndio wale waliochukua mkopo mkubwa about $60m from commercial banks kwa guarantee ya serikali (case kama ya mkopo wa Mzindakaya na kiwanda chake cha nyama). sinahakika kama mikopo hii imelipwa na BOT na hivyo kuhamishia madeni hayo rasmi kwa walipakodi.

Kwahiyo, it is ok kuzungumzia conflict of interest. Hata hivyo nakubaliana na Mkamap (sounds like Mkapa!!) kwamba tusi-conclude kuwa huu ni ufisadi mpaka at least tuestablish kwa kiwango cha kutosha kwamba one or more of these is true:-
-shamba alipewa bure au alinunua kwa bei ya kutupa,
-mkataba wa kutunziwa shamba unampa an unfair advantage,
-wakulima wengine wa kawaida hawawezi kutunziwa mashamba yao kama ilivyo kwa Mkapa,
-anayo arrangement kama hiyo pia kule Kagera,
-etc.
 
Wamiliki wa Mtibwa ndio wale wanaomiliki pia Kagera Sugar na ndio wale waliochukua mkopo mkubwa about $60m from commercial banks kwa guarantee ya serikali (case kama ya mkopo wa Mzindakaya na kiwanda chake cha nyama). sinahakika kama mikopo hii imelipwa na BOT na hivyo kuhamishia madeni hayo rasmi kwa walipakodi.

Hii issue Lowassa alikuwa akiitetea sana baada ya kushindwa kurudisha on time. Sijui alikuwa na maslahi gani maana almost guarantee yote ya serikali kwa sekta binafsi ($60 out of $70 billion)waliwapa kwa favour hawa jamaa na kuwasahau wazawa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom