Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Kama serikali au BWMmwenyewe hawatachukua hatua zozote, hii ya kuzomewa yaweza kuwa mwanzo tu....labda atapigwa mawe au vinginevyo.
Angalao yeye ana nafasi ya kujitetea kwamba hakujiuzia Kiwira, hajui kuhusu EPA n.k. Wanaochomwa moto na wananchi wenye hasira hawapati nafasi hiyo!
 
Mheshimiwa Pinda anakosea anaposema serikali haitakubali Mkapa aendelee kudhalilishwa.

Mheshimiwa Mkapa alipoukwaa uraisi kama si mwaka na ushei hivi alianza kuvaa "bullet proof" na tayari mitaani watu hawakuwa na imani nae kutokana na kauli zake za kinyonga au undumi la kuwili.

Mbona hatukuwahi kumuona mheshimiwa Alhaj Ali H Mwinyi akivaa jacket hilo?. Ni kwamba alikuwa mkweli na watu walimwamini.

Sasa mheshimiwa Pinda nae anataka kujidhalilisha mwenyewe?

Mwisho wa siku ni wananchi wenyewe wataoishinikiza serikali kwamba Mkapa ni lazima afikishwe mahakamani ili ajibu tuhuma za hujuma na ufujaji wa mali ya umma akiwa madarakani.
 
"katika kuzingatia utawala wa sheria, hatuwezi kama serikali kuruhusu watu wamzomee rais mstaafu ama yeyote yule, kama kuna makosa yatashughulikiwa kwa taratibu zinazostahili na kwa hili la Mkapa linashughulikiwa".

Halisi;

Pinda anasema Serikali hairuhusu mtu kudhalilishwa kwa sababu kuna njia nyingine za kisheria za kufikisha yale yanayo kukera. Hiki kitu Pinda kakitoa wapi? Sheria gani hiyo? Hiyo sheria inawezaje basi kuruhusu kiongozi adhalilishwe kwa kuchorwa picha za dhihaka magazetini?

Hayo mambo ni Majira ndio ilibidi wapate majibu. Huu ndio uozo wa Media Tanzania. Lakini maadam wewe umemuelewa Pinda labda unaweza kunisaidia na maswali hayo.
 
Huyu Pinda nae ndio nini au nae kwa kuwa ameshaingia kwenye chungu chenye minofu ya ufisadi kwa hiyo anataka kutetea madudu.....Vitakuja kumgeuka very soon. Kama anataka kumtetea Ben nina uhakika anaanza kujipunguzia credit kwa wa-tz.

Huyo fisadi wa siku nyingi kila mtu anajua then anataka kumtetea.. Hajui kuwa watu wanahasira nae na wamemchoka so ili kupunguza hasira juu yake wanaamua kumzomea?? Atazomewa sana tu badooo aendelee kujifichaficha tu hivyo hivyo asije kushangaa watu wengine wamepinda wakamtupia hata mayazi yaliyooza hata wakikamatwa lakini ujmbe umefika....
 
Kama serikali haiwafikishi mahakamani kwa kisingizio cha uchunguzi basi wananchi ruksa kuwa zomea mafisadi mpaka haki itendeke.
 
Mimi nilijua tuu ni wale wale tuu.. Hakuna cha Pinda wala Kunyooka hawa ni wale wale tuu. hadi hapo CCM itaondoka kwenye madaraka ndio nchi hii itabadilika... Kwani Ufisadi wote ulianza wakati upi? kwa hiyo lazima kweli awajibike lakini nani wa kumfunga paka kengele?
 
Pinda hakusema kwamba BWM ni msafi, ila alisema asizomewe wakati bado hajashitakiwa. Hivyo anatuchagiza kwamba tuendelee kushinikiza BMW apate haki yake...mahakamni.
Kumbekeni pia BMW alikua Bosi wa MPP kwa muda mrefu....
Ila Mhe. MPP anasahau kitu kimoja....kwamba kuzomewa kwa BWM ni matokeo ya hasira za watu dhidi yake...amekataa mwenyewe kukana (au kukubali?) tuhumu zote dhidi yake.
Mapambano yaendelee.....

Unajua hakuna mtu atakuja kumshtaki BWM hata kama atakuwa na hatia.. Nani atasimama amshtaki? Hao wooote wakina Pinda na wengineo ni kizazi cha BWM sasa nani ataweza kumgeuka baba yake?
Walau tumzomee tuu aone aibu .... hakuna cha kufanya
 
Two wrong don't make right!
Sasa watu walitaka Pinda aseme kuzomewa jamaa ilikuwa sawa.People don't make it personal ie..........may be Pinda moyoni anaona poa Mkapa kuzomewa (I just saying) ila kama kiongozi anazungumuza kufuata sheria zinasemaje.
 
Sijathubutu kutomwamini Pinda. Kwa hiyo nakataa kuamini maneno yake

Sijui kama Pinda ni mtu wa kusema neno kama hili. Tuangalie ukweli kama katumwa au vipi?
Na kama katumwa, Je katumwa na nani? Na kuna mission ganikwenye kutumwa huku?

Bado naamini kuwa mfumo ulivyokaa haujjiandai kumlinda Mkapa. Ninashawishika kuwa kumlinda Mkapa ni ghali kwa JK kuliko kumwachia justice imshughulikie.

Kaka yangu Pinda: Kwa kuwa ninakuamini ninakataa kuyaamini maneno uliyoyasema kuwa HUTAKUBALI MKAPA ADHALILISHWE. (My words)
Ninaamini kuwa hii ni charging back paces.
Yamkini Pinda anaplay game ya kuwaongezea wananchi jazba dhidi ya BM ili presha ya kumshughulikia iongezwe, maan hata mimi naridhika kuwa bado presha haitoshi kuilazimisha serikali kumwachia BM.

Till Then
 
Obasanjo denies power corruption

_44610372_obj226ap.jpg

Olusegun Obasanjo said the probe
could scare off potential investors

Former Nigerian President Olusegun Obasanjo has denied any responsibility for the failure of the country's power generation industry.
In a 5,000 word written submission to a parliamentary investigation panel, he said his administration had increased the amount of power generated. He denied any personal responsibility for the corruption the panel said it had found in the industry. The panel said $16bn had been spent without improving power supply. Mr Obasanjo declined the panel's invitation to appear in person.

He said he chose not to attend because the invitation letter was signed by a subordinate to the investigating panel chairman Ndudi Elumelu. Many Nigerians rely on personal petrol-fuelled generators and a huge number live without any power at all. Large industry has been virtually destroyed by the poor power supply. The House of Representatives investigation alleged that Mr Obasanjo's government had paid millions of dollars to 34 "non-existent companies".

The committee visited the sites where power stations were meant to be built. It found no work had been done at some sites after several years.

Denials

Defending his record, Mr Obasanjo said his government had inherited 18 years of neglect in the power generation industry, and had done well to more than double power supply. Gas pipeline vandalism had hampered power generation. One damaged pipeline took two years to repair, he said. To "the uninitiated" it would seem like no work had been done on the power stations, but the reality was that millions of dollars had been "invested", he said. But he said the investigation into the power sector may actually hamper improvement, and jeopardise Nigeria's development. Private partners were being chased away by the probe because they feared being "criminalised".
The former president also said the figure spent on building power stations was much lower than the $16bn the panel claimed. "One year is already lost, we cannot afford to lose another year without dire consequences in the coming years," said Mr Obasanjo.

String of investigations

Referring to a string of investigations into his tenure, he said the legislature should not work against the interests of the Nigerian economy. "Theatrical or circus shows will provide fun and, maybe, hurt some people but the reality will remain," he said. He called for the panel to prosecute anyone who they had concrete evidence of fraud against, but said: "Most of the contractors and suppliers are companies with tremendous reputations and most of their management and staff are men of honour and dignity." He said under his administration, generation had risen from 1,500 MW to 3,500 MW of electricity. But the country still has a long way to go, Mr Obasanjo said. According to him, Nigeria will need to generate 100,000 MW to provide enough for its 140 million population and to support the industry it needs to improve their standard of living.

Sasa wenzake wanajibu shutuma yeye kwa sababu anafikiri WTZ bado ni mbumbumbu anataka serikali ya CCM ambayo ndiyo imeibuka na hii tabia ya kuwatetea mafisadi wamsaidie na kufumbia maovu aliyoyatenda alipokuwa madarakani.

WTZ hatukumchagua aende kujitajirisha wala kufanya biashara Ikulu, sheria lazima iwe msumeno hizi sheria hazikuwekwa kwa walipa kodi na walalahoi peke yao, na wala hata siku moja hatukusema kutakuwa na wafalme ambao wana sheria zao. Pinda hukuchaguliwa kuwa waziri mkuu kuwatetea Mafisadi.
 
Pinda anajipendekeza? anaogopa? hajiamini? ni kilaza? kalewa madaraka? anajua dhamana ya uongozi? anajua maana ya demokrasia? anajua maana ya uhuru wa mawazo? Majibu anayo. Ni kwa nini asijiuliza Mwalimu baada ya kuachia ngazi ya Urais alishawahi kuzomewa? Je mzee wetu wa Ruksa Mwinyi alishawahi kuzomewa? mawaziri wakuu waliopita kabla ya Richimondulilowasa kuna aliyewahi kuzomewa? JAMANI HATUNA WAZIRI MKUUU!! NI KILAZA asiyejua kufanyia mambo uchambuzi kabla ya kuropoka hadharani. Wacha wazomewe ili liwe funzo kwao na wasnaofuata mkumbo wao. hizo mali walizoiba basi wakati wanazifuna wajifiche. tukiwaona tu ZOMEAZOMEA na ikibidi mawe!!! hatuwachinjiii ng'ombe ng'o!! Na nyie mlioko madarakani tutawazomea tu unless tuone mnachukua hatua madhubuti ya kuondoa kero za wana wa
TUMENYANYSWA KIASI CHA KUTOSHA
TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA
TUMEIBIWA KIASI CHA KUTOSHA
TUMEFISADIWA KIASI CHA KUTOSHA
TUMEDANGANYWA KIASI CHA KUTOSHA
TUMEHAADAIWA KIASI CHA KUTOSHA
SASA NI ZOMEA ZOMEA TU. hayoo mafisadi, hili lifisadi linapita!!! lione!!! linapasuka mali za wizi Hilo!!!

pIndA silaha yetu wanyonge ni sauti zetu. Tutawazomea tu mpaka mkome, wacha kujipendekeza. kwa kufanya hivyo uwaziri mkuu umekushinda!! rudi ikulu.
 
Unajua hakuna mtu atakuja kumshtaki BWM hata kama atakuwa na hatia.. Nani atasimama amshtaki? Hao wooote wakina Pinda na wengineo ni kizazi cha BWM sasa nani ataweza kumgeuka baba yake?
Walau tumzomee tuu aone aibu .... hakuna cha kufanya

As long Chama Cha Mbebano ( CCM) kinashika hatamu tusitegemee BWM kufikishwa mahakamani hiki chama ni family kama mafia
 
haya ndio yaliyowakuta vijana waliomzomea BWM

sasa utawatumia waanze kujifunza kitachowakuta
Waliomzomea Mkapa wakiona cha moto
Adam Hussein na Heri Shaabani

VIJANA waliokamatwa hivi karibuni kwa madai kuwa walimzomea Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa kumuita fisadi maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, wamesema licha ya kuachiwa kwa wenzao watano, bado wanazidi kusumbuliwa wakilalamika kwamba polisi wamevunjiwa kijiwe chao ambacho wamekuwa wakikitumia kutafuta riziki.

Wakizungumza na DarLeo, vijana hao wamesema wametakiwa kuondoka eneo hilo kwa madai kwamba kijiwe chao kiko karibu na nyumba hiyo ya rais mstaafu wa awamu ya Tatu. Wamekiri kwamba ni kweli kuna watu walimzomea lakini sio rahisi kwao kujua ni akina nani hasa.

"Huyu Mzee (Mkapa) nyumba yake iko pale jirani na anapita hapa mara kwa mara. Inawezekana mtu mmoja tu alimuita fisadi kwa sababu penye wengi hasa sehemu kama hii lolote linaweza kusemwa, "akasema kijana mmoja ni dereva wa teksi.

Waliosombwa wamesema kwamba baada ya kukamatwa kwenye msako huo uliofanywa muda mfupi baada ya msafara wa rais huyo mstaafu kupita, walikamatwa, wakapelekwa kituo cha polisi Oysterbay na kupekuliwa kishenzi na maafisa wa polisi.

Wakasema kwamba mbali na hilo pia waliulizwa maswali kibao huku wakipigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole maarufu kama finger point.

"Sisi hatukupiga mtu wala kuua lakini tunashangaa tunazidi kunyanyaswa na polisi, kibaya zaidi katika kijiwe chetu hakuna mtu ambaye amemzomea Mkapa.Tunaomba tusiondolewe katika eneo letu kwani tumekaa kwa miaka mingi kabla ya Mkapa kuwepo eneo hilo,"amesema mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe kwa kuhofia mkono wa dola.

Amesema inasikitisha kuona hata wale ambao walikuwa wakisubiri usafiri siku ya tukio wakiwa hawana hili wala lile walichukuliwa na kupelekwa polisi wakati hawana makosa yoyote kwa kuwa Mkapa mwenyewe alikuwa amekwishaondoka.

Katika eneo hilo la kituo cha daladala Masaki, vijana wengi wakiwemo madereva wa teksi, wapiga debe na wengine wanaojishughulisha na biashara nyingine ndogondogo wamesema kwamba wanatumia eneo hilo kupata riziki na kwamba wakiondolewa itakuwa ni sawa na kuwaonea.

"Tukiondoka eneo hili ni sawa na kufukuza zaidi ya watu 300 kwani tunafamilia ambazo zinatutegemea kwa kila kitu.Pia kuna mwanajeshi ambaye amekuwa akija kijiweni na kuanza kutpiga makofi na kudai sisi ni wezi,"amesisitiza kijana mwingine.

Mei 5 mwaka huu vijana watano walikamtwa na kusekwa polisi kwa madai kuwa wamemzomea Mkapa wakisema fisadi huyo! fisadi huyo! .Vijana hao waliokamatwa ni Ayubu Masoud, Kasungi Shukuru, Hassan Ramadhani, Juma Rashid na Peter Stiven.

Baada ua kukamatwa walifunguliwa kesi ambayo ilikuwa na RB namba OB/RB/8201/2008 ikieleza bayana wanatuhumiwa kutumia lugha ya matusi dhidi ya kiongozi mstaafu.

Kamanda wa Polisi Kinondoni Jamal Rwambow alikanusha kukamatwa kwa watu waliomzomea Mkapa akidai kwamba walikamatwa katika msako wa kawaida wa kipolisi.

SOURCE: dARLEO
 
Unajua hata Mugabe anafanya the same thing kwa wananchi wake huko Zim
 
Hey Mwafrika, itabidi utengeneze bango kubwa saana halafu usimame nalo pale salender bridge huku ukicheza souja boy....au walk it out
 
Hey Mwafrika, itabidi utengeneze bango kubwa saana halafu usimame nalo pale salender bridge huku ukicheza souja boy....au walk it out

Nakuambia nimeshanunua uniform mpya na nimekata bonge la kitop kwa my kid sisterz....... ninawasiliana na jamaa wa Bose wanitengenezee audio system ya nguvu ili nikiweka souja boy .... jiji la Dar lizizime!

Just watch this space for updates!
 
Back
Top Bottom