Ni wazi kabisa kwamba baad ya kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na kuteuliwa kwa baraza jipya kufuatia ripoti ya Dr.Mwakembe kamati ya kuchunguza ubadhirifu wa BOT ivunjwe nayo kwani tayari kuna watuhumiwa wawili mule ambao watavuruga mchakato mzima na kutuletea taarifa kuwa "utapeli wa BOT haukuwa na madhara kwa taifa" kama walivyofanya kwa Richmond. Hawa watu wawili Hosea na Mwanyika ni wazi wanapaswa kuondolewa kwenye ile kamati ili sio tu kuonekana haki imefanyika bali watu tuione kuwa inatendeka.
Wakuu mnaonaje wazo hilo la Dr. Slaa mie naliunga mguu kabisaaa
2008-02-09 08:39:47
Na Mary Edward, Dodoma
Kambi ya upinzani, imependekeza kuwa, Rais mstaafu Bw. Benjamin Mkapa achukuliwe hatua kwa madai ya kushiriki ufisadi na kujimilikisha mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.
Walimtaka Rais Jakaya Kikwete, aache kumtetea kwa kauli za `mwacheni Mkapa apumzike amestaafu` kwa kuwa hakuna sheria inayomlinda Rais aliyestaafu kushtakiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Naibu Kiongozi wa Upinzani, Dk. Wilbroad Slaa, alisema Bw. Mkapa amejimilikisha asilimia 85 za mradi wa Kiwira, ujasiri alioupata akiwa Ikulu.
``Tutamshtaki Mkapa na sheria ya kumshtaki ipo, hana kinga kisheria,`` alisema kiongozi huyo.
Alisema baadhi ya taarifa alizoandika kwenye Ofisi ya Msajili wa Kampuni (BRELLA) zinaonyesha kuwa, alijisajili kama Ben Mkapa, mjasiriamali. ``Tutamshtaki kama mjasiriamali, si kama Rais,`` alisema.
Katika hatua nyingine, kambi hiyo ya upinzani imetaka maamuzi ya Baraza la Mawaziri yasifanywe kwa siri.
Kiongozi wa kambi hiyo, Bw. Hamad Rashid Mohamed, alisema katika mkutano huo kuwa, wakati umefika yanayoamuliwa katika baraza hilo, yakafahamika kwa wabunge na wananchi walioiweka serikali madarakani.
Alisema taarifa ya kamati ya Richmond imebainisha kuwa, maamuzi ya baraza hilo, yalivunjwa na kulisababishia taifa hasara, lakini kama yangekuwa yanafahamika kwa wabunge, suala hilo lisingekubalika kwani kila hatua ingekosolewa.
``Katika kikao cha Baraza la Mawaziri, iliamuliwa kuwa, TANESCO itafute mzabuni wa kuzalisha umeme wa dharura, lakini Wizara ya Nishati na Madini, ikapuuza agizo hilo kwa shinikizo la Waziri Mkuu aliyejiuzulu na kuvunja agizo la baraza hilo ambalo Rais wa nchi ni kiongozi.``
Akizungumzia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alisema Watanzania hawana imani nayo kwa vile msimamizi wa hazina ya Taifa, amevunja imani ya wananchi kwa kuandika barua na kufungua akaunti ya Richmond licha ya benki za nje kama Citi Bank kukataa kwa vile Richmond ni matapeli.
Alisema miswada ya nishati inayoletwa bungeni, haikubaliki kwa vile imelenga kuwahalalisha vigogo kuendelea kuinyonya TANESCO kwa staili ya Richmond ambayo inalipwa Sh. milioni 152 kwa siku.
``Kampuni ya uzalishaji umeme ya Aggreco, IPTL, Songas na Alstrom huchota kutoka TANESCO jumla ya Sh. bilioni 244 kwa mwaka,`` alisema Bw. Mohamed.
Alisema upinzani utashangaa kama mafisadi watateuliwa katika baraza jipya.
``Hatutamuelewa Rais endapo waliotajwa na kamati kwa namna moja au nyingine kuhusika na Richmond watateuliwa,`` alisema mbunge huyo wa Karatu (CHADEMA).
Walionya kutocheleweshwa kufikishwa Bungeni taarifa ya Ernst & Young inayohusu ufisadi wa BoT na kwamba itakuwa jinamizi kwa serikali na kusisitiza baraza jipya liiwasilishe ripoti hiyo na uchunguzi ufanyike kikamilifu.
``Kwa kilichotokea BoT, hatuna imani na kamati ya uchunguzi, hivyo Rais atafute wataalam wengine hata ikiwezekana kutoka nje na wanaoteuliwa watajwe kwa majina ili tujue namna ya kuwawajibisha,`` alisema.
Mwanasheria Mkuu ndiye Mwenyekiti wa Tume inayochunguza ufisadi wa BoT, na wajumbe ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali na Jeshi la Polisi.
SOURCE: Nipashe
Mie nadhani imetosha.muacheni Mkpa apumzike na mdili na uchaguzi wa kiteto.Msipoangalia mtasindwa vibaya.na hili suala la kumng'oa Lowassa limewasaidia sana Chama tawal katika Kampeni zao.Wapinzania hawatashinda tena."Muacheni Mzee apumzike."Jakaya kikwete
Mie nadhani imetosha.muacheni Mkpa apumzike na mdili na uchaguzi wa kiteto.Msipoangalia mtasindwa vibaya.na hili suala la kumng'oa Lowassa limewasaidia sana Chama tawal katika Kampeni zao.Wapinzania hawatashinda tena.
Tatizo wapinzani wamekosa sear nzuri na wanatumia makosa ya viongzoi wa CCM kama seara ya kuwapandisha juu,hii haitawasaidia sababu CCM wameshagundua hili.,wakiona mnang;angania jambo wanafanya kama mnavyotaka na wataendelea kupeta.
angalia sula la kumpa zitto kamati ya MAdini,ni kumpoza tu.na analipwa posho kubwa sana
PCCB walisema kuwa hawana ubavu wa kumchunguza Mkapa; Waoa hao hao wakasema kuwa utoaji wa mkataba wa Richmond haukuvunja sheria. Nasubiri wakati utapowadia tukianza kumrarua Mkapa kwa ujasiriamali.
PCCB walisema kuwa hawana ubavu wa kumchunguza Mkapa; Waoa hao hao wakasema kuwa utoaji wa mkataba wa Richmond haukuvunja sheria. Nasubiri wakati utapowadia tukianza kumrarua Mkapa kwa ujasiriamali.
Kwenye suala la Mkapa, tusiende kichwa kichwa kwa ajili ya ushabiki au unazi kuwa "asulubishwe, auawe'.
It is important that the opposition "strike while the iron is hot"
This is the best time to hold Kikwete to his oath and his presidential accountability. My only fear is Kikwete is toothless to prosecute Lowassa, let alone Mkapa, since he himself is implicated.
Bubu,Mkuu, hakuna anayeenda kichwa kichwa. Mkapa kafanya ufisadi ndio maana hayuko tayari kuzungumzia ufisadi alioufanya. Kama utakumbuka yeye alituita Watanzania wavivu wakufikiri na tukimuona mtu amekuwa tajiri tu basi tunashabikia kwamba kachukua rushwa. Wakati ule aliposema haya tulikuwa hatujui kwamba the so called mr clean alikuwa si msafi chochote! alikuwa ni mchafu wa hali ya juu.
Bubu,
Suala si kuwa hatujui kuwa Mkapa ni fisadi, suala ni kuwa je kuna ushahidi wa kufungika na kufilisiwa mali?
Hili linanijia ukiangalia Tokomile alilocheza Lowassa na Muungwana kwenye Richmond. Lowassa kawajibika kisiasa na kupoteza kazi, lakini ripoti ya Mwakyembe haionyeshi kuwa kuna ushahidi wa wizi au yeye Lowassa kunufaika kifedhaau kimali.
Ndio maana nasema tusiende kichwa kichwa maana CCM na mafisadi wana turufu mpya ya Ubangusilo ambayo huishia kuaibishwa hadharani lakini kesi hamna, ushahidi hautoshi na hivyo MWafisadi kuendelea kupeta kula walivyochuma.
Trust me I would like to see every one of the mafisadi gets trivial time at Mahakama Kuu kivukoni, serve time in Ukonga and loose everything kwa kufilisiwa. Lakini compromises za kichama ambazo huwa ni adhabu kwa uzembe au kutokuwa makini hazina vifungo au kufilisiwa!
That is where I have a beef that kelele za "asulubiwe' zitaishia kuwa kelele na hakuna atakaye kwenda Golgota!