Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Tunasema kuwa Mwalimu, hakuwa mfisadi, lakini hakuwa na tatizo na mafisadi waliokuwa wakimsujudia, Mkapa included, kusema Mwalimu, hakumjua Mkapa ni very naive thinking kama sio kujua what makes siasa na wanasiasa, to be politicians, siasa sio dini wakuu au charity, siasa ni utawala na power ndani yake, na pia tukumbuke kuwa power siku zote huwa ina-corrupt hata wachungaji kina Mtikila!Quoted from FMES

Ninadhani tulio wengi hatukuelewa falsafa zake huyu mzee , ninamnukuu" Pale Asia pale serikali inaweza ikampa tenda ya ujenzi wa barabara mwana wa mfalme ,ktk hali hiyo fedha italiwa lakini na barabara itaonekana lakini si hivyo kwa waswahili,watakula hela na barabara hakuna.J.K.Nyerere 1995.

Mchango wangu ni huo Mwalimu
 
Ninadhani tulio wengi hatukuelewa falsafa zake huyu mzee ,


Mkuu FDR,

Heshima mbele, you might be right kuwa huenda wengi hatukumuelewa huyo mzee, lakini one thing tunaelewa ni kuwa alituachia fisadi Mkapa, that we know much na ninachokataa ni lame story ya kwamba eti hakumjua Mkapa, no alimjua isipokuwa Mwalimu, hakuwa malaika na kwenye siasa kuna kitu kinaitwa the devil you know and the devil you do not ndio maana US wanamkumbatia Kibaki, the devil they know!
 
Correct!! Hivyo ndivyo ilivyo; vipimo vya uadilifu vya Nyerere vilikuwa shallow sana. Kwa hiyo ilikuwa ni rahisi sana kwake kuwa spoofed na wanafiki kama Mkapa na mawaziri wengi aliofanya nao kazi!

Lakini, siyo kweli kuwa alimweka Mkapa pale akifahamu kuwa atafanya madudu haya aliyofanya; hakujua kuwa Mkapa atafanya vile.

Sio kwamba Nyerere alimuona Mkapa ni lesser devil ukilinganisha na washindani wake by then?

Nafikiri nikubaliane pia na Nyani kwamba tuachane na habari za Nyerere. Kuna mtu aliwahi kuniambia kwamba "let's heal the past and live the present", sasa haya mambo ya kulaumu the past tu on our present woes ni fake. Mkapa tunaye tena hana hata majeshi sasa hivi, tunashindwa nini kwenda kumchukua pale Lushoto na kumleta Dar es Salaam ajibu mashtaka? Tena pale Tanga kuna mahakama, sasa si asongezwe tu pale? kwa nini hatumlazimishi Kikwete kuchukua hatua? Wapiga kura wamwambie Kikwete kwamba usipomchukulia Mkapa hatua tutakunyima second term 2010, uone kama atakaa kimya.

Adhabu ya mwanasiasa ni kunyimwa kura (my roginal quote, you can quote it without necessarily citing me!).
 
Nina uhakika Muungwana naye akitoka madarakani tutaendelea kumlaumu Mwalimu(RIP) kisa Alimweka Mkapa na Mkapa kamweka Kikwete...
Kelele nyingi tukifika kwenye box la kura ndio wa kwanza kuweka tiki kwa mgombea wa CCM.
 
Kuna siku... yatayumika hata mawe kuwaponda mafisadi.
 
Mwenyezi mungu atupe roho za subira waungwana,this is dangerous.

Mkuu Jr,
Naomba nipingane na maombi yako, naomba Mungu aiondoe hiii roho ya subira ili tufanye kweli, kwani hii roho ndo imetufikisha hapa tulipo!

Unajua hata Mungu mwenyewe kasema Tusiwe wapole kupita kiasi! Watanzania tumezidi upole ndo maana mafisadi wanakula bila kunawa na tunabaki kuwashangilia kwamba wana akili na wamejaliwa!

Natamani ombi letu watanzania wote liwe kuondolewa huyo roho wa subira na kutupa mwamko wa kupigania/kudai iliyo haki yetu!
 
Jamani eeh...sasa tuache kumlaumu Nyerere kwa kila kitu. Hata kama Nyerere alimu-endorse na kumpigia debe Mkapa ni sisi wananchi ndio tuliomchagua. Nyerere hakutushikia bunduku kichwani na kutulazimisha kumchagua Mkapa. Tulikuwa na haki sawa ya kuwachagua wengine waliogombea uraisi mwaka huo.

Tutaacha lini kumlaumu huyu mzee wa watu jamani? Sio haki kabisa kumrushia lawama mtu ambaye hayuko hai kujitetea mwenyewe. Mzee wa watu aliaga dunia mwaka 99. Mwaka uliofuata tukamchagua tena Mkapa. Najua kuna mtakaosema alianza ufisadi katika muhula wake wa pili. Sawa, hiyo labda ni kweli. Sasa kama tunajua hivyo ndivyo ilivyokuwa na kama inavyosemwa ushahidi wa ufisadi wake upo tena mwingi tu, ni nini sasa kinachotuzuia kumchukulia hatua za kisheria au hatua zingine zozote zile zinazofaa? Au tunamsubiri Nyerere afufuke ndio aje amchukulie hatua yeye?

Watanzania kweli bado hatujajua jinsi kuwajibika kwa matendo yetu. Tunapenda sana kutumia njia rahisi na za mkato na kulaumu wengine...ooh wakoloni hivi...wakoloni vile..Nyerere hivi...Nyerere vile...CCM hivi...CCM...vile...wapinzani hivi...wapinzani vile....viongozi wetu hivi...viongozi wetu vile...lakini hata siku moja husikii sisi wananchi tukiwajibika kwa makosa yetu. Mkapa bado tunaye...sasa kinachotuzuia sasa hivi ni nini? Halafu nikisema Miafrika Ndivyo Tulivyo mijitu inanibishia...saa ingine nataka sana niseme shauri yenu..au shauri letu..

Umeshamsikia M-Zanzibar analaumu utawala wa Sultani? Wa-Malawi wameacha kumsema Banda. WaZambia wameacha kumsema Kaunda. WanyaRwanda yakitokea makosa watamlaumu Kagame. Nchi hizi haziangalii nyuma sana kwa sababu walifanya complete change. Na nafasi hizi haziji mara kwa mara.

Tulikuwa na nafasi na 1995 Mchonga alitunyang'anya na hilo ndio kosa la kubwa sana kwa maoni yangu mimi. Na tutaendelea kuloloma about that.
 
Nafikiri kabla ya kuanza kujibizana humu ndani ya JF tungeanza na kuangalia awamu zote za uongozi tangu ya kwanza hadi hii, ane then tuweke vigezo (variables) kwamba tunaposema awamu hii ilikuwa FISADI tunatumia vigezo vipi. Maana mksema Nyerere aliwa fisadi au Mkapa au Kikwete au Mwinyi tunaangalia nini kati ya mali wanazomiliki, kuwakumbatia watendaji fisadi au kuwa na uongozi wa kishkaji au nini hasa!!!

Nawasilisha tu
 
Mafisadi walikuwepo toka enzi za JKN na vilevile alilifahamu nafikiri mnakumbuka maskendo ya Gapex n.k. Tatizo la Nyerere ilikuwa siyo mafisadi ila watu wenye tofauti na mitizamo yake kisiasa. Sikumbuki watu waliofungwa kwa sababu za ufisadi kama wapo ni wchache sana. Ila watu waliopigwa chini au kukimbilia uhamishoni kwa sababu za kisiasa ni wengi. Sokoine alipojaribu kuwasaka mafisadi wote tunajua yaliyomkuta. Hizo kampeni za Mr. Clean na za kuwakandamiza akina Lowasa na Malecela ilikuwa ni janja yake ya kumweka mtu wake kwa vile AHM alishamsaliti by then.

Haingii akilini mwangu kusikia kuwa Mkapa alikuwa na account ya US$ 1000 na 5 million Tshs baada ya kuwa balozi UN na waziri wa nje kwa muda mrufu. Kama hayo ni kweli basi inabidi leo hii aje atueleze watanzania katika miaaka kumi ya mwisho amewezaje kutajirika 1000x wakati akiwa katika nafasi nzuri ya utumishi serikalini kwa muda mrefu alishindwa.

Kwa vile usanii na mazingaombwe ya CCM yataendelea kutufanya WTZ tuzidi kulala nafikiri itatuchukua karne nzima kuamka. WTZ wote wanafahamu uwezo duni wa JK lakini anachaguliwa kwa 80%.
 
Nafikiri kabla ya kuanza kujibizana humu ndani ya JF tungeanza na kuangalia awamu zote za uongozi tangu ya kwanza hadi hii, ane then tuweke vigezo (variables) kwamba tunaposema awamu hii ilikuwa FISADI tunatumia vigezo vipi. Maana mksema Nyerere aliwa fisadi au Mkapa au Kikwete au Mwinyi tunaangalia nini kati ya mali wanazomiliki, kuwakumbatia watendaji fisadi au kuwa na uongozi wa kishkaji au nini hasa!!!

Nawasilisha tu

Mkereketwa:

Hayo ndio matatizo ya waafrika. Kila kukicha tunataka kuweka vigezo (variables).

Tunaleta uendeshaji wa maisha ya jadi vijijini katika kuongoza serikali ya sasa.

Katika mambo ya jadi mtu akifumaniwa, mkutano utaitwa chini ya mwembe. Wazee watajadiliana siku nzima na pombe watakunywa na mkutano ukiisha aliyefanya makosa anakubaliwa katika jamii kama vile hakufanya kosa lolote.

Kuna viongozi wengi tu Tanzania ambao ni masikini lakini wamefuja pesa za serikali kwa kufanyia ufilauni. Na ukichukua kigezo cha kipimo cha mali kama ni uaminifu basi viongozi wa namna hii pia wataonekana ni wazuri.
 
Icadon,

..nafikiri watu wanamlaumu Mwalimu leo hii kwasababu wakati yuko madarakani walishindwa kutoa madukuduku yao.

..Mwalimu alipenda kuzungumza halafu akasema, NDIYO. Hakuna aliyekuwa na uwezo wa kuhoji baada ya hapo.

Bin Maryam,

..yuko ndugu wa Mwalimu Nyerere aliyedai kwamba Waziri Mkuu wa JMT alimjengea nyumba mdogo wa Mwalimu Kiboko Nyerere[rip]. Nauliza, pesa alitoa wapi? Je hiyo haiwezi kuwa aina ya ufisadi?

..kuna viongozi walikuwa na watoto 20,30, na hata 50. walikuwa wanatoa wapi fedha za kuhudumia familia zao? je, hawakuwa mafisadi?

..miaka hiyo kiongozi akitembelea mikoani alikuwa akifungashiwa chakula mpaka mifugo[ngombe,mbuzi,..]. Ukizingatia hali ya maisha ya wananchi vijijini, huo siyo ufisadi?

Kitila Mkumbo,

..Watanzania tumekuwa na utawala uliofeli tangu ule wa Mwalimu.

..CCM kama chama kiondoshwe madarakani. Chama hicho kimeshindwa kutuletea uongozi wenye manufaa Tanzania.

..Watanzania msitegemee atatokea Mikail Gobachev ndani ya CCM.
 
Mimi nitajumuisha maelezo ya wengi humu kuunda hoja moja ambayo nitapenda sana tuitazame kwa uzito wake....
Kuna waliosema kuwa siasa sio dini - nakubaliana na hilo kwa mantiki ya tofauti za kuamini na kuabudu Mungu. Lakinii wakati huo huo siasa na dini vyote hivi hujengwa na IMANI na huwepo wajumbe wa hizi nadharia ambao kazi yao ni kuvuta watu kuamini kile wanachoamini wao kuwa ndio njia pekee ya Ukombozi.
Nyerere kama mtume wa siasa alikuja na hiuo siasa zake na kati ya watu alowachagua kuwa wafuasi (swahaba)wake ndio tunamkuta Mkapa and the gang....
Sasa kama alivyokosea Yesu ama Muhammad ktk machaguzi ya hawa wafuasi sidhani kama ni busara kwetu kutomwani ama kumshushia lawama Yesu ati kwa sababu tu alikuwepo swahaba YUDA msaliti. Ama kwa waislaam kumlaumu Muhammad kwa sababu kulikuwepo maswahaba walokuja badilisha ama kutengua baadhi ya mafundisho yake. Leo hii kuna hata Masheikh na Mapadre ambao tunawaona wakiyafanya mabaya kinyume cha vitabu vyao vya dini sawa sawa kabisa na hawa kina Mkapa and the gang washeikh wa Uongo ambao wamekumbatia biblia yetu KATIBA, hali wanapingana ama hawaamini kabisa baadhi ya mafundisho ya sura za biblia yetu.
Hii ina maana moja tu kuwa hawa watu hawakuwa waumini wa kweli wa UHURU wetu na malengo kamili ya Uhuru huo. Na kama alivyosema Njabu ni jukumu letu sisi leo hii kuwaondoa watu hawa ktk uongozi na pengine kuwachukulia hatua tusahau habari za kulaumu mjumbe aliyetangulia.
Nyerere sio Mtume wala hakuwa na ukaribu wa aina yeyote kumfananisha na mitume kwa hiyo swala la kufahamu mtu mara nyingi huwa ni ktk mafundisho yaani kama mwalimu anavyomwamini mwanafunzi wake darasani kuwa ana kichwa lakini inapofikia matendo ya huyo mwanafunzi hiyo tena ni kazi mpyaaa!..Nina hakika hata walimu wa JK leo hii wamejishika tama wakiuliza kama ndiye mwanafunzi waliyemfundisha ama waliye mjua wakati ule.

Mwisho nadhani tumepata fundisho la kutosha toka Mkapa kwani wengi wa wafuasi wa Nyerere wamejitokeza kuwa ni wapinzani wakubwa wa Uhuru wetu na ndio maana tunawaita Watawala weusi...yaani wameturudisha ktk kuamini shetani la kutawaliwa.
 
...ili ajibu tuhuma mbali mbali zinazomkabili za ufisadi

Tuna shaka na Mkapa
Tanzania Daima

JUMAPILI iliyopita, tuliandika tukimuomba Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, avunje ukimya wake, ajitokeze kuzungumzia kashfa kubwa ya upotevu wa mabilioni ya fedha za Watanzania zilizochotwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati akiwa kiongozi mkuu wa taifa letu.
Tulieleza imani yetu kwamba, Mkapa ndiye mtu muhimu, ambaye kauli yake inapaswa kusikika sasa akizungumza kuhusu kile anachokijua katika kashfa hii ya upotevu wa sh bilioni 133 kutoka Akaunti ya Kulipa Madeni ya Nje (EPA).

Tulieleza zaidi kuwa, pamoja na kutambua msimamo wa Mkapa tangu alipoondoka madarakani zaidi ya miaka miwili iliyopita sasa, wa kutotaka kuzungumza mambo yaliyotokea wakati akiwa madarakani, katika hili la upotevu wa mabilioni ya EPA, tulishauri kuwa anapaswa kubadili msimamo wake huo.

Kwamba ajitokeze, azungumze ili kulinda heshima yake na kuondoa shaka iliyoanza kujengeka dhidi ya wengi kuwa mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha urais wake ni kiini macho.

Kinyume chake, Mkapa amekuwa kimya, mengi yanazungumzwa dhidi yake na wenzake aliokuwa nao madarakani, lakini hakuna maelezo yaliyotolewa ya uhakika kuhusu hayo yanayozungumzwa.

Ukimya huu wa Mkapa umetufanya tuwe na shaka kwamba huenda haya yanayozungumzwa kuhusu yale aliyoyafanya wakati akiwa madarakani, yana chembe chembe za ukweli.

Shaka yetu hii inatokana na ukubwa wa tuhuma zinazomuandama, ambazo tunasema kwa kujiamini kabisa kuwa hazitofautiani sana na zilizowahi kuwaandama viongozi wengine wa Afrika, tukimtaja haraka Frederick Chiluba wa Zambia kama mfano wa kwanza, ambaye sasa anakabiliwa na mashtaka mahakamani.

Kwa sababu hiyo, tunapenda kueleza kuwa, ukimya wa Mkapa unatufanya tuwe na shaka kuwa, huenda tuhuma zilizotolewa kwamba wakati akiwa Ikulu alianzisha kampuni yake ya biashara inayotajwa kwa jina la ANBEM akishirikiana na mkewe, Anna Mkapa, ni za kweli.

Awali hatukutaka kabisa kuamini tuhuma hizi dhidi ya Mkapa, kwa kuzingatia kuwa sifa kubwa kwa kipindi kirefu akiwa madarakani, alikuwa akijulikana kama Mr. Clean, achilia mbali mkewe Anna ambaye alikuwa akitajwatajwa kujihusisha na biashara za hapa na pale.

Hatukuamini kwa sababu Mkapa alikuwa mwanafunzi mzuri wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye kwa kutumia ushawishi wake, alifanikisha Mkapa kwenda kukaa Ikulu baada ya kuwaaminisha Watanzania kuwa ndiye kiongozi aliyekuwa akifaa kwa wakati huo, kuongoza mapambano ya kuwakomboa Watanzania kutoka katika maisha magumu waliyokuwa nayo na kuelekea katika maisha yenye neema.

Shaka yetu inaongezwa na tuhuma kwamba mbali na kufungua Kampuni ya ANBEM, Mkapa huyu huyu, akishirikiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, walisajili kampuni binafsi iitwayo Tanpower Resources na akaisimamia kununua asilimia 85 ya uliokuwa mradi wa umma wa makaa ya mawe, Kiwira mkoani Mbeya.

Kwamba, mbali na kufanya hivyo, Mkapa alikwenda mbali zaidi, alitumia wadhifa wake wa urais kuhahakisha kampuni yake hiyo inapata mkataba wa kuliuzia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) megawati 200 za umeme katika gridi ya taifa.

Hizi ni tuhuma nzito sana kuelekezwa kwa kiongozi wa taifa la Tanzania, tena aliyeingia madarakani kwa msaada wa Baba wa Taifa hili, ambaye historia yake imetukuka kwa uadilifu.

Kwa dhati kabisa tunatamka kwamba, tuhuma hizi zinamfanya Mkapa kuwa rais wa kwanza katika historia ya taifa letu kufanya biashara akiwa Ikulu, mahali ambako palitajwa na Baba wa Taifa kuwa sehemu takatifu.

Hivyo basi, tunapenda kumshauri Mkapa kuwa iwapo ataendelea kuwa kimya, bila kujali ukubwa wa tuhuma zinazomkabili, na bila kujali heshima yake na heshima ya Baba wa Taifa aliyewaomba Watanzania wampe ridhaa ya kukaa Ikulu kwa sababu ni muadilifu, hakika, heshima aliyoondoka nayo madarakani inaweza kufutika kabisa.
 
BWM ni mwerevu kiasi fulani... when he saw it coming his way, he claimed to be retired politician. Nahisi huu ni mwanzo wa mengine mengi na BWM hataongea, anasubiri hukumu ya wananchi.
 
Kwani mkapa kuwa muwekezaji kuna tatizo gani??? Mbona mbowe ana mapesa na ni tajiri sana?? Diallo je?? Lowassa nae?? Kama ni mafisadi tuwazungumze kwa ujumla wao sio mojamoja. yaonekana kama watu wanamaliza hasira zao kwa huyu mzee mstaafu. Huwa siamini sana kama sheria inahakikisha haki inatendeka, lakini hata kwa kufuata sheria ni wapi kunamfunga rais kuwa mfanza biashara?? jambo la msingi hapa,ni kama alipindisha mchakato halali ktk kujianzishia hizo biashara na kupata kazi. lawama tu kuwa eti kaanzisha ANBEM au ana 85% kiwira mine si jambo la msingi sana. Kwani mlitaka makaburu wawekeze pale ndio mngejua mambo yanaenda kihalali?? Nyie watanzania msio na akili nani amewaroga???? Kuhusu sehemu ya mabilioni yaliyochotwa BoT kwenda CCM, Mkapa karejea tu yaliyowahi fanywa na nyerere na mwinyi!!! tofauti tu ni kuwa yeye karidhia uchotwaji wa mabilioni kukifadhili chama tawala kipindi cha mult-party system wakati wenzake walichota kipindi chama chashika hatamu!!! pengine tu sheria inamfunga, lakini hatuishi kwa sheria bali kwa imani. dhambi ni ileile!!!

Nawahi lindo jamani, c u neksti taim!!!!
 
Kwani mkapa kuwa muwekezaji kuna tatizo gani??? Mbona mbowe ana mapesa na ni tajiri sana?? Diallo je?? Lowassa nae?? Kama ni mafisadi tuwazungumze kwa ujumla wao sio mojamoja. yaonekana kama watu wanamaliza hasira zao kwa huyu mzee mstaafu. Huwa siamini sana kama sheria inahakikisha haki inatendeka, lakini hata kwa kufuata sheria ni wapi kunamfunga rais kuwa mfanza biashara?? jambo la msingi hapa,ni kama alipindisha mchakato halali ktk kujianzishia hizo biashara na kupata kazi. lawama tu kuwa eti kaanzisha ANBEM au ana 85% kiwira mine si jambo la msingi sana. Kwani mlitaka makaburu wawekeze pale ndio mngejua mambo yanaenda kihalali?? Nyie watanzania msio na akili nani amewaroga???? Kuhusu sehemu ya mabilioni yaliyochotwa BoT kwenda CCM, Mkapa karejea tu yaliyowahi fanywa na nyerere na mwinyi!!! tofauti tu ni kuwa yeye karidhia uchotwaji wa mabilioni kukifadhili chama tawala kipindi cha mult-party system wakati wenzake walichota kipindi chama chashika hatamu!!! pengine tu sheria inamfunga, lakini hatuishi kwa sheria bali kwa imani. dhambi ni ileile!!!

Nawahi lindo jamani, c u neksti taim!!!!

Jambo la msingi si mtu kuwa na mali, ila mtu awe na mali ambazo ni legitimate. Kama BWM ni tajiri asione aibu, asema "mimi BWM (na mke wangu)tunamiliki nyumba na kule Lushoto, Kiwira,........ na tulivipata kwa nia halali kama ifuatavyo......"
Nakumbuka PM wakati wa BWM aliwahi kukataa kumiliki shamba ila baada ya kubanwa akasema ni la mke wake.
BWM alitangaza mali zake wakati anaingia, alipaswa kurudia punde alipomaliza muda wake.
 
Hivi mlishawahi sikia Peninsula hotel musoma ni ya nyerere????

Watafungwa wengi!!!!
 
Back
Top Bottom