BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Bubu,
Aliyofanya Mkapa (1995-2005)
A: Positives
1. Kukusanya kodi
2. Daraja la Mkapa
3. Kufufua EA Community
4. Ujenzi na ukarabati wa barabara (various-Dar, Moro,Bkb-Mtkul)
5. Elimu-MES & MEMKWA
6. Afya- Health Sector Reforms (Basket fund n.k)
7. Kufutwa kwa madeni ya nje HIPC
8. Kuongezeka Foreign Direct Investment- Gold Minig etc
9. Ubinafshaji loss making Parastatals
10. Muafaka wa CUF na CCM
Ukiangalia huyu bwana pia kuna aliyofanya mwema kama wajibu- pia ana mapungufu! Je historia itasema BWM ni raisi aliyeshindwa au aliyefanikiwa? Hata Brair, Bush, Kibaki, Howard..kuna waliyojitahidi na pia wana mapungufu!
To be fair- shilingi ina pande mbili- hii ndiyo hoja yangu.
1. Ukusanyaji kodi. Ndio kweli katika awamu yake makusanyo ya kodi yaliongezeka. Je Watanzania walinufaika vipi? Bado wanafunzi walikuwa wanakalia matofali, mahospitali yetu yalikuwa hayana vifaa muhimu na madawa pia yalikuwa hakuna. Asilimia kubwa ya makusanyo hayo ilitumika kulipa madeni ya nje. Kwa kifupi Watanzania hawakunufaika na ongezeko hilo. Ni kama Baba anayetamba mtaani kwamba yeye ana mshahara mkubwa kuliko baba yeyote pale mtaani lakini watoto wake wanadhoofika maana mshahara wote unaishia nyumba ndogo na kwenye mabar.
2. Daraja la Mkapa hili ni fedha za mkopo na misaada ambapo yeyote yule angeweza kusimamia ujenzi huo.
3. Kama ulivyoona kwa kishindo kikubwa Watanzania hawalitaki shirikisho la EA, labda baadaye. Kwa sasa asilimia 76 wamesema NO na muungwana kasema atakeshimu matakwa yao.
4. Mabarabara ni machache mno yaliyotengenezwa. Asilimia kubwa ya barabara zetu bado hazipitiki na ni zile za mwaka 47. Angalia foleni ya Dar leo hii. Safari ya 15 to 20 minutes inaweza kukuchukua hata masaa mawili hata zaidi. Ikinyesha mvua kubwa kwa saa moja tu basi barabara nyingi hazipitiki. Hili pia kwa mtazamo wangu na Watanzania walio wengi sioni mafanikio yoyote!
.Elimu hili sioni mafanikio yako wapi kwani ukianzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu kuna matatizo chungu nzima na yamesemwa na hata na haki elimu ambayo Mkapa aliipiga vita na hata kuifungia na sasa pia wanawekewa mikwara chungu nzima. Asilimia kubwa ya Watanzania sidhani kama waliona mafanikio yoyote katika elimu enzi za Mkapa.
6. Sera za afya katika awamu ya tatu zilikuwa ni mbovu sana na hadi hii leo bado zinasikitisha sana. Mifano ni mama wajawazito kati ya watano kushare kitanda kimoja!!!! na wengine kulala chini!! vitendea kazi hakuna kabisa na matokeo yake wanasiasa wote hutibiwa SA, Kenya, UK na hata USA. Sijui unazungumzia mafanikio yapi!!! 😕
7. Madeni hayakufutwa kwa sera za Mkapa. Pamoja na hayo Watanzania hawakuona wala hawajaona mafanikio ya kufutwa kwa mikopo hiyo. Maisha ya dhiki kwa Watanzania wengi hayajabadilika hata chembe!!!
8. FDI imeongezeka ndiyo lakini madini yetu yanachukuliwa bila Watanzania kufaidika na chochote. Nadhani umeshasikia kelele chungu nzima kuhusiana na mikataba ya madini iliyo siri hadi leo hii. Sijui hili ongezeko la FDI limewasaidia vipi Watanzania.
9. Breweries na Sigara hawa walikuwa wanapata faida kubwa tu lakini nao wakabinafsishwa sijui Mtanzania alifaidika nini. Mashirika mengi yaliyouzwa yaliuzwa kwa bei karibu na bure na Watanzania hawakufaidika chochote na mengi ya mashirika yaliyouzwa sasa hivi hayafanyi biashara au uzalishaji wowote.
10. Mmmmhhh! Muafaka wa CUF na CCM ambao mpaka leo hii hatujaona lolote la maana katika muafaka huo. Juzi juzi tu kulikuwa na habari kwamba CUF wanataka kujitoa katika mazungumzo hayo!!! Au kuna muafaka mwingine ambao labda hatuujui!!!! 😕
Sioni mafanikio yoyote ya Mkapa zaidi ya kujitajirisha yeye na familia yake na kuacha kashfa chungu nzima ambazo inaelekea anaogopa kuzijibu maana kila kukicha linaibuka bomu jingine la awamu ya tatu!!!