Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mbona Nick alikuwa akimuona dingi wake kuwa mnoko tu! Na yeye kakubali dili hili! Au wametumia jina lake na mwenyewe hana habari?

Nadhani BM inabidi ajitokeze kujitetea sasa. Kama anadhani ataweza kuuchuna mpaka wananchi wasahau basi anafanya makosa sana.
Rada, Gulfstream, NBC, Netgroup, Barrick, Bank M, Mwananchi Gold, Kiwira, TRC-Rites, Simu 2000, SAAFI...ataweza kuhimili vishindo vya skendo??

Mwanagenzi,
Mbona pia watu hawaibui mema aliyofanya BWM? Ila tuweze kuwekea mizani, maanake sijaona mtu ameibua jema alilitetea na kupigania!
Shilingi ina upande wa Nyerere na Mwenge!
 
Nadhani kwa mwendo huu, tutayajua mengi. Lakini kinachosikitisha ni kwamba raia karibu million 40, tumekosa azma ya kuijenga Tanzania yenye neema kwa kila raia na vizazi vijavyo. Hivi jamani, hawa viongozi wetu wapewe nini kusudi waweke maslahi ya wananchi na taifa mbele? naombeni mwenye mawazo anipe. Tuwape nini? Pension ya wanasiasa Tanzania ni kubwa kuliko popote, maisha yao ni ya neema mno (kulinganisha na hali ya wanaowaongoza), sasa jamani tufanye nini? Ama kweli kama jamaa alivyosema ITS ALL ABOUT IQ, IQ, IQ ya mwafrika akiwa Africa! Zaidi ya hili, utaelezeaje huu ufedhuli wa hawa viongozi wetu (wengi wao wakiwa na utumishi uliotukuka nje ya nchi, lakini baada ya kurudi nyumbani wamekuwa majuha?)

Naomba wanaforum humu na watanzania, tusiwe wepesi wa kusahau, kila anayepita humu, ayaweke na kuyatunza haya madudu ya hawa wazee kichwani, 2010 tusidanganywe tena. Tafadhali sana, maana ugonjwa wa watanzania ni kusahau haraka. Kashfa za hawa wazee zimezidi mno, na madhara ya hizi rushwa ndo tunayaona, kipindupindu ambacho hakiishi kilometa mbili toka nyumbani kwa mkuu wa nchi, uchafu na ukosefu wa huduma za msingi kabisa ambazo binadamu inabidi azipate kwa kuwa raia! si mara mia wangekuwa wanakula lakini wanawamegea wananchi wao? Taifa kama taifa tukae chini tutafute mstakabali wa hili taifa, tuache theories na ndoto za kutumia usomi wetu kuihujumu nchi na hawa raia wake wanaotambulika kwa namba na idadi tuu za kuombea misaada. Tutafanya hivi kwa kila mtu kugundua wajibu wake kama kiumbe aliyepewa utashi na Mungu wa kuamua mema na mabaya. Tuna silaha moja nayo ni KURA (its our last democratic right in Tanzania), Hii ikiondolewa, basi we shall be banished in the dustbin of history.

THISDAY have played their part, wewe na mimi je? ukitaka kuwaita wenye majungu, or whatever name, wewe ndo mwamuzi.
 
Mwanagenzi,
Mbona pia watu hawaibui mema aliyofanya BWM? Ila tuweze kuwekea mizani, maanake sijaona mtu ameibua jema alilitetea na kupigania!
Shilingi ina upande wa Nyerere na Mwenge!
Hayo mema alikuwa anatimiza wajibu wake kama kiongozi na haya madudu tunayoelezwa hayaweza kuwa diluted na mizani yoyote. Tunasubiri kuona kama sheria inafanya kazi au inachagua.
 
Mwanagenzi,
Hata kama unamwona dingi wako mnoko huwezi kukataa ulaji.
 
hiyo inaitwa mjenga nchi ni mwananchi na muuwa nchi ni mwananchi,wimbi,upepo huko huko,mbele kwa mbele,Imagine hawa ndio tuliwaaminini tukawapa heshima ya kutuongoza.Kasema Dr Ongala,nchi inateketea,wamepewa madaraka wakayatumia vibaya.
 
Wenzetu wa Uganda wameshtuka......(Source monitor 2/8/2007)




PARLIAMENTARIANS on Tuesday ordered the minister of Energy, Daudi Migereko to make public all oil exploitation agreements the government signed with oil companies.

The legislators said the minister should lay on the table all the agreements between Tullow Oil and Heritage Oil that are exploring oil in Lake Albert area in Bunyoro Kingdom.
Rich oil deposits were confirmed in the western Uganda districts of Hoima and Buliisa in 2006.
 
maana huo ugonjwa sasa unaingia Tanzania football federation
 
Kwa watanzania hili suala sio muhimu kwao kama kutafuta kula ya siku,kama wangekuwa na uwezo wa kujua kesho atakula nini basi mambo yangekuwa tofauti.
 
...for the cost of 14.5m USD/month,kwa mwaka hiyo cost ni almost 160m USD..kwa utaalam wangu hiyo ni cost ya kujenga mtambo mpya kabisa wa kuzalisha umeme wa 150MW...tunaibiwa sana wananchi na waliosema wabunge ni sifuri nimeamini au nafikiri vichwani akili yao kiuwezo ni ndogo sana
 
Mtanzania,

Mkapa ana watoto wawili Steve na huyu Nico, Peter ni mtoto wa mama,

so far habari za ndani ni kwamba mama watoto amekuwa akimtaka Mkapa aende kwenye media kujibu mapigo, lakini washauri wengi wanamshauri asiende,

ila jamaa ana hasira na Kulikoni/Thisday, na hafichi anadai iko siku atawafundisha adabu, mimi ninaomba kuwauliza maapologists wa Mkapa kina Mzee Moshi, Philemon, na wengineo ambao mara kwa mara mme mtetea huyu Mkapa kuwa anatumia tu mishahara yake na marupurupu ya kazi,

Je kwenye hili mnasemaje, au bado ni mshahara wake tu una-cover kote huku?
 
Kuna watu mnatia aibu!!Hii tabia ya kusema mbona hatuangalii mazuri aliyofanya ni upuuuzi mtupu.Ina maana tuhalalishe upuuzi wa mtu kwa vile amefanya baadhi mazuri???.Waanapoomba urais hawaombi kwenda kutuibia,kula rushwa,kutufungisha mikataba ya kuifilisi nchi,kuwalinda wala rushwa nk,wanaomba ili watufanyie mazuri ili kuiendeleza nchi na kuwaletea maisha bora watanzania.Sasa tuwasifie kwa kitu gani,wakati ni wajibu waliouomba kuutimiza.Pale watakapofanya miujiza ndipo tutawasifia.Lakini kwa sasa hawajaweza fanya zaidi ya walichoomba na wanachotakiwa kukifanya. Hawastahili sifa. Wanabomoa kwa kasi kubwa zaidi kuliko wanvyojenga. Tunawalaumu kwa kuwa wameshindwa kufanya kile wanachostahili kukifanya tena kwa makusudi.
 
Kutenda mazuri kwa ajili ya maendeleo ya Taifa si ni WAJIBU wao sasa iweje leo kutendewa mazuri na viongozi wetu tulipie kwa kuibiwa na kufanyiwa ubadhirifu wa hali ya juu?
 
Mwanagenzi,
Mbona pia watu hawaibui mema aliyofanya BWM? Ila tuweze kuwekea mizani, maanake sijaona mtu ameibua jema alilitetea na kupigania!
Shilingi ina upande wa Nyerere na Mwenge!

Mema kama yapi!? Hebu yataje basi ili tuone kama kweli yalikuwa mema au ni madudu tu!! Aliwezesha kukusanya kiasi kikubwa cha kodi ambacho asilimia kubwa akaishia kulipia madeni yetu ya nje, vinginevyo sioni jema lolote!! Kama unalijua liweke hapa tulijadili kwa mapana na marefu. Huyu Mkapa ataendelea kujificha mpaka lini!? Makashfa kibao dhidi yake na wale walio karibu naye hasa kutoka familia yake.
 
Bubu,
Watu bwana! Mara Nyerere alitifikisha pabaya early 80s, mara Mwinyi alifungulia milango mno, mara BWM naye skendo kibao, mara JK msanii!
 
NImeishi kusini, lakini sijapata kuona Mmakonde mlafi na asiye muadilifu kama huyu Ex Muheshimiwa. Thanks to Baba wa Taifa...!!!
 
Bubu,
Watu bwana! Mara Nyerere alitifikisha pabaya early 80s, mara Mwinyi alifungulia milango mno, mara BWM naye skendo kibao, mara JK msanii!

Kwa hiyo wewe Kashfa zote hizi za Makaburu wa Net Group, uuzwaji NBC na nyumba za serikali kiholela, Simu 2000, ununuzi wa (rada, ndege ya Rais, helicopters za jeshi, magari ya jeshi) kufanya biashara akiwa Ikulu, kuwapa watu ukurugenzi wa kiwira watu alio karibu nao pamoja na mwanae, kuwalazimisha TANESCO wasaini mkataba na Kiwira ambao hauna maslahi kwa Watanzania n.k., kashfa zote hizi wewe unauona na hadithi za pwagu na pwaguzi!!!!? Yeye alijiita mr msafi na awamu yake ya uwazi na ukweli, sasa huo usafi na uwazi na ukweli uko wapi!? mbona anaendelea kujichimbia!? au hayasikii makelele ya Watanzania yanayoongezeka kila kukicha kuhusu kashfa chungu nzima dhidi yake na familia yake!? Kumbuka panapofuka moshi hapakosi....
 
Bubu,
Hebu angalia posts zangu- sijatetea mabaya- ila nimesema tuwe na utamaduni wa kuangalia pande zote za shilingi! Wengi wamesema mazuri ni wajibu kwa wapiga kura hence wanajikita tuu kwenye mabaya!
Kuna posts kwa mfano iliyozungumza BWM kupendekezwa Chancellor Makerere!
Haya mapungufu yapo- BWM, EL, Sumaye, n.k na tunayapigia kelele kila siku!
 
Bubu,
Hebu angalia posts zangu- sijatetea mabaya- ila nimesema tuwe na utamaduni wa kuangalia pande zote za shilingi! Wengi wamesema mazuri ni wajibu kwa wapiga kura hence wanajikita tuu kwenye mabaya!
Kuna posts kwa mfano iliyozungumza BWM kupendekezwa Chancellor Makerere!
Haya mapungufu yapo- BWM, EL, Sumaye, n.k na tunayapigia kelele kila siku!

Watanzania kwa mtazamo wangu wana utamaduni wa kuangalia pande zote za shilingi kabla ya kufikia tamati ya mtazamo wao. Katika post yangu moja nilikupa nafasi ya kuyaleta mazuri ya Mkapa toka 1995 mpaka 2005. Nakupa tena nafasi hiyo ili tuyajadili kwa maslahi ya nchi yetu.

Hilo la kupendekezwa kuwa Chancellor mimi sioni kama lina maslahi yoyote kwa Watanzania bali Mkapa kama mtu binafsi na wala halifuti kashfa nyingi zinazomwandama Mkapa. Na kama waliompendekeza wangezijua kashfa dhidi yake sidhani hata jina lake kama lingetamkwa. Haya tunasubiri utuletee mazuri aliyoyafanya Mkapa.
 
Bubu,

Aliyofanya Mkapa (1995-2005)

A: Positives
1. Kukusanya kodi
2. Daraja la Mkapa
3. Kufufua EA Community
4. Ujenzi na ukarabati wa barabara (various-Dar, Moro,Bkb-Mtkul)
5. Elimu-MES & MEMKWA
6. Afya- Health Sector Reforms (Basket fund n.k)
7. Kufutwa kwa madeni ya nje HIPC
8. Kuongezeka Foreign Direct Investment- Gold Minig etc
9. Ubinafshaji loss making Parastatals
10. Muafaka wa CUF na CCM

B: Mapungufu
1. Mikataba mibovu- Gold, NBC n.k
2. Kuongezeka kwa Rushwa
3. Biashara Ikulu
4. IPTL
5. Kuongezeka kwa utegemezi wa wafadhili
6. Mpasuko wa Zanzibar- haukukamilika
7. Mauaji Mwembechai 1998 na Pemba 2001
8. etc
9. etc
10. etc

Ukiangalia huyu bwana pia kuna aliyofanya mwema kama wajibu- pia ana mapungufu! Je historia itasema BWM ni raisi aliyeshindwa au aliyefanikiwa? Hata Brair, Bush, Kibaki, Howard..kuna waliyojitahidi na pia wana mapungufu!
To be fair- shilingi ina pande mbili- hii ndiyo hoja yangu.
 
Back
Top Bottom