Mh. Phillemon Mikael,
Nadhani uko right kwa mambo mengi uliyoyasama ikiwa ni pamoja na kuwa hakuna miiko ya viongozi. Lakini kusema kwamba kampuni iko wazi, naona hapo hujaweka wazi huo uwazi na ukweli ulikuwa wapi? Je, tokea mwaka 1999 alipoanzisha hiyo kampuni nani alijua kabla ya THISDAY kuandika? Je, alipokopa Benki nani alijua? Sumaye alipokopa milioni 50 mpaka leo ameandamwa Ben leo amekopa mamilioni kwa mamilioni (USD 500,000+ 250m/-), shamba la Sumaye la Mvomero na lile alilokodi ekari 7 Kibaigwa, limekua kelele na hakuna aliyewahi hata kuandika undani, leo Mkapa ana mashamba na kadhalika, tunasema ana haki. Jamani tujiulizeni, hawa walitangaza mali 1995, leo vipi? Wametangaza mali baada ya kuondoka? jamani hii kampuni ofisi zake zilikua wapi? Hebu tueleze kama wewe unajua unaposema hakufanya siri? alifanya siri na aliweka jina lake kwa kuwa alikua na kiburi na akijua hakuna wa kumgusa. (Hiyo ni mada mpya). Mkapa alifanya hivyo akijua Tanzana hakuna waandishi. Aliwahi kusema Waandishi wa Tanzania ni uchwara na hawajui kuandika wala kuchunguza. Alikua na haki kwani hakuna aliyeweza kupita anga zake. HAKUNA UHALALI WOWOTE NDIO MAANA COWI Counsult waliacha kupangisha kwa pale Sea View mara Mkapa alipoichukua nyumba. Wa Denish walisema hawawezi kumlipa Rais kodi ya nyumba. Walilipa kodi mara moja tu then wakahama