Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,227
Profesa anajidhalilisha. He makes this look personal, lakini anatakiwa kujua kuwa it is the war against graft, of which Mkapa is part of it. Kumfikisha Mkapa peke yake hakuwezi kung'oa mzizi, anyway ndio siasa za majukwaani.
Yupo sawa kabisa huwezi kuwalinganisha wahusika wengine na Mkapa ,tatizo mlilonalo ni ufahamu wa kinachozungumzwa na kina chake.
Sidhani kama Lipumba haelewi kuwa Mkapa ana kinga kwa kiasi fulani Mkapa hawezi kufikishwa mahakamani kama wengine kumbuka Mkapa alikuwa ni Jemedari na mkuu wa Nchi(Raisi) ,Lipumba hapa anapigania sheria kuwa Raisi nae aweze kufikishwa mahakamani pindipo Mkapa akifikishwa mahakamani basi na Raisi aliekuwepo au atakaekuwepo watajumuika katika kuwajibika na sheria hii na hivyo hata Mwiny nae anaweza kufunguliwa mashtaka.
Inaonyesha unapata tabu kuwasikilza watu wenye uzoefu wa kutoa Lecture.
Kwanza Lowasa then Mkapa tunakaribia mfupa nyama inakuwa tamu zaidi
Mkuu kichuguu,
Wako tayari wakupe Mkapa sababu ndiye unayemtaka,ila swali la kujiuliza unamtaka mkapa ili ushitaki kw amashtaka yapi?
Unajua tunaongea sana kuhusu haya ila we are missing one Point behind,Yes inawezekana alishiriki ila siyo rahisi kiivyo kujua kama alihusika ama laah
Kwa sababu ziko sehemu moja tu katika ulimwengu wa Sheria na Katiba Tanzania, mara nyingi ukisema "kinga za Ibara ya 46" unaeleweka unazungumzia nini. Ikisemwa "kinga za Ibara ya 46" tunamaanisha ibara za Katiba. Isitoshe kulikuwa na clue ya wazi kabisa, niliposema hapo juu kwamba Bunge haliwezi kupingana na Katiba.
Sasa maana ushajua tunaongelea Katiba, rudi basi ka point out "umahoka" wa chochote nilichokisema.
Asante kwa ufafanuzi na sasa maelezo yako yanaleta maana halisi. I just wanted to make sure tunaelewa unachoelezea kwani yawezekana kueleweka vinginevyo. Thanks
FYI Its a must to mention ni sheria ipi unaitaja kwa ibara pindi unapoweka au ku-quote au kuitaja ibara na kifungu chake pia kusema ni sheria ipi ama katiba, ama sheria ya ardhi ya mwaka 1999, sheria ya ndoa ya mwaka 1972, national park ordinace cap (year) etc. I mean you have to mention the law and year in which was enacted or put in force. It is a must and not just mentioning ibara is not enough to detail. Sheria ni ngumu anyway kwa kuwa inahitaji umakini. Hata kama ni Jaji anapo-refer au ku-qoute lazima ataje ni sheria gani na ya mwaka gani na ibara ipi n.k.. OKEY!!! Kila mtu kumbuka anapaswa kujua sheria ili asivunje sheria. Thanks Kuhani once again for clarification
Naona umeongeza hicho kipande kwenye posti yako ya awali baada ya kuona nimekubali ile soft response yako ya kwanza. Sasa unaanza lugha za "for your information" sio ? Kukushukuru imekuwa tabu ?
Sikia we mtu:
Kwenye masuala ya Katiba na Sheria nikisema "Article 46 Immunities" mwenye macho haambiwi ona!! Inajulikana na wanaojua kwamba tunaongelea kinga za Rais za Kikatiba!!
Na hatuongelei sheria as legislative acts hapa, ambazo ndio huwa zinatajwa details zote za mwaka na vipengele. Unaponukuu Katiba hutaji mwaka kilichopitishwa hicho kipengele cha Katiba!
Sasa hizo ni cosmetics. Tuje kwenye subtantive issue at hand. Naomba unionyeshe ni wapi katika nilivyo elezea zile immunities nimeandika "umahoka" ? Mbona hujibu ?
Sioni kinga yeyote ya kikatiba dhidi ya wizi alioufanya MH Mkapa akiwa rais wa nchi.
Ni vema kutaja vifungu vya katiba vinavyomlinda Rais mtaafu, pia ni vema kuchambua makosa ya jinai yaliyofanywa na MH Mkapa hatua kwa hatua ili kutoa utata unaojitokeza wa kudhani Rais Mtaafu anakinga ya kikatiba pale anapotumia madaraka kujiuzia shirika kwa bei ya kutupa na kushindwa kabisa kulipa 100% ya bei hiyo.