....kitila Mkumbo Una Akili Sana ...wala Haikuwa Ajabu Pale Ulipopewa Nafasi Ya Kufanya Kazi Pale Udsm ..mara Tu Baada Ya Ku Graduate....
Nafikiri Umetoa Mwelekeo Wa Namna Tunavyotakiwa Kuyachambua Mambo Hapa Jf.........maana Wengi Hapa Wanapenda Tu Kusema ...mkapa Hakufanya Kitu!!!....au Mkapa Sio Fisadi !!!
Naomba Wachambuzi Mfuate Msingi Alioleta Kitila Ili Hii Mada Ichambuliwe Kitaaluma Zaidi.....naomba Kuwasikia Wachambuzi Maarufi ..kama Rev Kishoka ,kichuguu,fmes,....na Wengine.....woote!!
Sina haja ya kwenda kumuuliza yoyote kuhusiana na 'mazuri' ya Mkapa. Hao wafanyakazi unaowataja wamejaa tele hapa JF na sijasikia hata siku moja wakimtetea fisadi Mkapa. Wewe unayemtetea labda ulinufaika kwa namna moja au nyingine na ufisadi wa Mkapa, lakini Watanzania walio wengi hawakunufaika na chochote.
Nimeuliza mazuri aliyoyafanya fisadi Mkapa ni yepi? Je, yanaweza kuwekwa hapa? 😕
Ooh! Kamuulize huyu kamuulize yule! Nyerere ameng'atuka miaka 23 iliyopita pamoja na kuwa alikuwa na makosa yake lakini leo hii ukiuliza Watanzania wengi mazuri aliyoyafanya Nyerere basi hawatapata kigugumizi na kukwambia labda nenda kawaulize watu wa Butiama au wale waliokuwa Ikulu wakati alipokuwa madarakani. Toka kona moja ya nchi mpaka kona nyingine ya nchi Nyerere mazuri yake hayajifichi pamoja na kuwa mengine hayakuwa na mafanikio makubwa kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake kama kupigwa vita na mataifa ya magharibi kwa kufuata siasa za ujamaa na pia kupanda kwa bei kubwa ya mafuta duniani mwaka 1973, vita dhidi ya nduli Idi Amini 1979, na ukame mkubwa ulioikumba Tanzania mwaka 1975.
Sasa uliza matatizo ya Mkapa yote yamesababishwa na wizi na ufisadi wake na sera ambazo zilitowa upendeleo dhahiri kwa wageni wachukuaji badala ya Watanzania.
Kwa Watanzania wengi Mkapa ni fisadi tu na wengi tungependa afikishwe Mahakamani kushtakiwa dhidi ya wizi alioufanya na hatimaye kufilisiwa. Sheria za nchi ni lazima ziwabane wote bila upendeleo wowote wa kujali wana utajiri mkubwa kiasi gani au walikuwa na wadhifa mkubwa kiasi gani ndani ya chama au serikali.
mkandara,
upande niliosimama mie ni kutaka kuona wale wote wanaohusika na ufisadi wafikishwe kunako chombo cha haki (sijui kama hili linawezekana). sina hata chembe ya nia ya kumtetea fisadi yeyote yule.
naafikiana nawe kwamba ufisadi wa bot haukuanza na awamu ya nne bali toka enzi ya bwm ulikuwepo. na nina hakika upekuzi wa kina ukifanyika utavumbua mengi zaidi hadi yale yaliyopelekea benki kuu kuunguzwa na moto.
ndio maana nimesema kama hoja ni kurutubisha mchenguo wa wanayoendelea sasa basi namuombea mzee butiku mafanikio (na sio kejeli bali ni maombi ya dhati). ila wasiwasi wangu pia ni uwezekano wa hoja zake kukwamua uhusiano wa bot na uchaguzi na awamu ya nne na kulengesha fikra za watu kwa bwm. sasa haya ni mawazo tuu na yaweza kuwa kweli au yasiwe na ukweli binafsi naomba sana mawazo yangu yasiwe na ukweli.
mazuri nimekuorodheshea lakini kwa vile una jibu tayari ndio inakua vigumu kuyaona.
1.ametia uhai elimu iliyokua inaelekea kuzimu.
2.ameanza kuajili walimu walikua wamepigwa lumba kali zaidi ya miaka 5bila ajira
Ndio walianza which has nothing to do with being paid on time!3.Wafanya kazi walianza kulipwa mishahara kwa wakati
kwa miaka kumi ameshindwa kulipatia ufumbuzi suala la wastaafu wa Afrika ya Mashariki. Leo hii mstaafu wa Tanzania yuko nyuma sana katika malipo wakati chini ya utawala Rais mstaafu akajitengenezea kipackage chake cha kustaafu!4.wafanyakazi walianza kulipwa malimbikizo yao
Haya siyo mafanikio, hili ni jambo ambalo lilitakiwa kufanyika na hata hivyo bado kuna kazi kubwa sana katika kulipa watumishi wa serikali hasa walio mbali na mabenki na makao makuu ya wilaya.5.wafanya kazi walisogezewa huduma kwa kuletewa mishaharra katani na si kuzifuata wilayani zaidi ya mile 50.
Natural increase.6.wanafunzi waliongezeka mashule kwa ailimia 90%
Wangali walifaulu na kuendelea na wangapi walielemika. Chini ya utawala wake illiteracy level ilifikia asilimia 31!7.karibu kila mtoto mwenye kwenda shule alikwenda
of course.. do you really want to know why?10.amerudisha hali ya watanzania kupenda kuajiliwa na kuitumikia serikali yao
Absolutely, wao wenyewe kuheshimiana na kuoneana aibu!11.amerejesha heshima ya serikali
The best spin.. uchumi umekua in relation to uchumi wa nani? Unajua sasa hivi ni maskini zaidi kuliko tulivyokuwa miaka mingi iliyopita. Kukua uchumi siyo sawasawa na kuondoa umaskini!12.amekuza uchumi kwa 6%
Kwa kujiuzia yeye mwenyewe mengine na kuwaacha wezi waje waibe viwanda vyetu mbele ya macho yetu. Ni chini ya mkapa TTCL, NBC, ATC.... zote zilifufuliwa!13.amefufua viwanda na makampuni yaliyokufa
Mkamap,
Mkuu nashinda hata kuelewa ulichosimamia hapa..
Umezungumzia viwanda kuwa makazi ya nguchiro kama utani ama una uhakika wa hilo maanake kusema rahisi sana!.. Imekuwaje viwanda hivyo viendelee kuzalisha bila wawekeshaji kuweka mashine mpya!.. Na vile vilivyouzwa vingine baadhi mashine kung'olewa na kusafirishwa Kenya ambako na kuuzwa kama vipuri, kisha walionunua viwanda kutumia viwanja hivyo kuanszisha miradi mipya.. Je walichouziwa ni kiwanda kukiendeleza ama ilikuwa kuondoa taka!..Umemsikia mwenyewe Mizengo Pinda akilaumu kuhusu Reli, tazama ATC, NBC bado kitu gani unataka hasa kutuelezea hapa!..Kuna shirika hata moja ambalo limefikia hata kiwango cha juu wakati wa mwalimu?
Kama alivyosema Jasusi, siku zote kizuri kujiuza!
Mkuu kama Mkapa alifanya lolote bora ingeonekana manufaa yake. Mchango wa vitu hivyo vyote alivyouza ktk mfuko wa Taifa % umepungua kuliko wakati wowote ule!... hili ni somo mojawapo..
Kama kweli kuna mazuri sii myaseme? kuonyesha ubovu wa vitu vilivyokuwepo haiwezi kudhihirisha UBORA ikiwa hakuna matunda ya kufanya hivyo!..
Hata mguu unapopata matatizo makubwa na kuanza kuharibika, unaweza kuondolewa ikiwa kuondolewa kwa mguu huo utasababisha kupona kwa mtu huyo, lakini ni ujinga mkubwa kuondoa mguu wa mtu bila kutazama replacement za mguu huo! kuzama ndani kiutaalam na kupata jibu sahihi la maradhi ya mguu huo kabla hujaondolewa.
Kichekesho cha mfumo wa Mkapa ni kwamba mguu huo ulioondolewa umeenda kutumiwa na mtu mwingine mwenye maradhi kama yetu na umefanya kazi....tulichofanya sisi mkuu ni kutoa donation ya kiungo chetu. Hii ndio lugha mnashindwa kuifahamu kwa sababu upeo wenu wa kutazama unaishia pale mguu ulikuwa una matatizo ya tulishindwa kutembea... Hivyo kata hakuna haja ya kumwona daktari..Hii ndio taabu ya WANASIASA wanapoingilia UCHUMI..
IMF ni soko la kukusanya hizi organs kwa hiyo mawazo yao kwanza yatakuwa kuwaponyesha kina Trump kabla hawajakufikiria wewe ngozi ya tako..
Mawazo ya Mkapa yahana tofauti na Mhindi anayetoa organ yake kuiuza kwa sababu hana kazi nayo....
Hayo mazuri uliyoyataja unaweza kutupa takwimu zake maanake tunarudia mada iliyokwisha siku nyingi..unavuta vitu ambavyo nina hakika huwezi kuvielezea zaidi ya kuandika juu juu..
Mkapa is the best president.
Ila kosa lake tu nikuongoza Taifa bovu kama Tanzania.
Ngoja nitoke nje ya maada kidogo
Kama wa marekani na waingereza wangekua werevu kama Watanzania
BREA,BUSH mwana na BABA leo hii wangekuwa wananyea SEGELEA ama GWATANAMO.
Mkapa is the best president.
Ila kosa lake tu nikuongoza Taifa bovu kama Tanzania.
Ngoja nitoke nje ya maada kidogo
Kama wa marekani na waingereza wangekua werevu kama Watanzania
BREA,BUSH mwana na BABA leo hii wangekuwa wananyea SEGELEA ama GWATANAMO.
Mkamap,
Blea na Bush wanatazama maslahi ya nchi zao kwanza.. Ubaya wao ni mtazamo wa haki za kibinadamu lakini wanachokitaka Iraq, Iran, Venezuela Korea na kwingineko kote ni faida kwa nchi zao..
Tatizo kubwa linalowakaribiri watu hawa ni gharama ya kuvipata vitu hivyo!..hili ndio somo kubwa Marekani na Uingereza!
Bush wala Blea hakuna mwizi kati yao na wasingechukua hata siku 100 Ikulu kama wangekuwa na mfano mdogo tu wa Mkapa..
Mkuu umeshindwa kuitazama picha na nini wana JF wanakizungumza hapa.
Tanzania sio mbovu ila wabovu ni watanzaniaMkapa will always remain a fisadi, corrupt leader and very selfish who did nothing to benefit Tanzanians. Na Tanzania kwa taarifa yako si Taifa bovu bali tuna viongozi wabovu na mafisadi kama fisadi Mkapa na wengineo wengi.
Tanzania sio mbovu ila wabovu ni watanzania
Mkapa is the best president.
Ila kosa lake tu nikuongoza Taifa bovu kama Tanzania.
Mkamap,
Umeniacha hoi hapa - hebu elezea kidogo una maana gani na Taifa bovu. Halafu huo ubovu wa taifa unasababishwa ama umesababishwa na nini. Kama Mkapa alikubali kuwa president wa taifa bovu na hakuweza kuikwamua kutoka kwenye ubovu, atakuwaje Best President. Hakika hapo unajikanganya.
which includes you, me and mkapa!
Mfano wako mzuri sana mkuu tena hapo nakupa pongezi..Mkapa
kama naye angekuja na kukumbatia hizi nyumba za nguchiro na kuacha madini yakae ardhini mpaka Watanzania wapate elimu leo hii TZ ingekua moja ya mahala pa ajabu sana duniani saizi palivyo ni infinity ahueni.
Kwa maana elimu inayosubiliwa isingekuwepo wala kuja maana walimu tayari walikua wamenza kukimbia.
Filosofia nzuri ni-
Kama wewe ni kibabu cha miaka 80 huwezi shika jembe na huna mtaji wala jinsi ya kuishi na wajukuu wako 10 walio na miaka chini ya 5 wanakutegemea wewe .Na hapo hapo wewe kibabu unashamba la hekali 100.
Sasa wewe kama una akili nzuri ni kumtafuta mtu mwenye uwezo wa kulilima na kumwambia bwana chukua shamba hili bure lima hili shamba lakini ktk mavuno utakayopata wewe nipe mavuno yatakayo niwezesha kula mwaka mzima na wajukuu wangu pia vijisenti vidogo vya matibabu na kuwawezesha hawa wajukuu kwenda shule.