Mkanye mkeo nakwambia!

Akili mu Kichwa. 1: Kuwa mtulivu. 2: Mfuatilie Huyo Bibie ujue anaishi wapi 3a: Mfuate siku nyingine ili akupe ABC. 3b: Anza kufuatilia nyendo za mkeo 4:iwapo Bibie atakufafanulia ukweli wa tuhuma zake, zifanyie kazi kwa utulivu mkubwa bila kusukumwa na hisia. 5: Fanya maamuzi ya Busara (iwapo ni kweli kwanini ametoka nje? Je chanzo ni wewe au ni tamaa tu) 6: Kama ni tamaa tu, Kaka PIGA CHINI FASTA
Nakupa TANO Mkuu........................
Nilikuwa nasubiri jibu la aina hii.........................
 
Mtambuzi...
natambua uwepo wako...
hii iko kihisia zaidi...na inategemea GLANDS gani zitatangulia kutoa homoni gani siku iyo na zitanituma vip...
 
Uko kwenye mizunguko yako maeneo mbali na nyumbani kwako, mara ghafla anakutokea mwanamke usiyemjua kabisa na anakwambia kwa sauti kiasi cha kuwavuta wapita njia wengine waliokuwa wakipita na shughuli zao kusimama na kusikiliza kinachoendelea.

Mwanamke huyo anakwambia……, “Wee baba we, nakuomba sana umkanye mkeo kutembea na bwana angu, la sivyo nitamfanya kitu ambaccho hatakuja kukisahau maishani mwake…..Mwambie asisahau kama mie ni mzaliwa wa Tanga. Kama humtoshelezi, si akatafute wanaume mwengine huko, kuliko kutembea na mabwana za watu, mpaka anataka kunihatarishia uchumba angu, mwambie akome tena akome kama alivyokoma kunyonya titi la mama yake……………..” mwanamke huyo anaondoka huku akiendelea kubwabwanya na njia kwa maneno yenye kukera.

Hebu niambie kama ni wewe unachukua hatua gani ………..?

Atakuwa kakosea kwa kuwa mke wangu ni marehemu
 
Kwanza ujue kuwa uko kwenye anga za wenye muji!!

Pia utambue kwamba imekula kwako (iwe ni kweli au la)....Mambo yameshakuwa si mambo.

Dawa hapo ni kufanya maamuzi magumu...Kwa wajinga kama mie, ningeamua kuishi kwa matumaini!!

Babu DC!!
 
Mmmmh!!!!!!!! unampotezea kisha unafanya ukachero maana mambo mengine siyo ya kukurupuka inaweza kuwa janja ya nyani kula mahindi mabichi

  • :embarassed2:
 
Ila Babu kama ni wewe kuwa tu mkweli tukupe ushauri wa kupita kwenye supu ya pweza jioni, haingii akilini bibi atange na njia kiivo, hapo hata huyo mwanamama naye utampitia ili umonyeshe kuwa we ni rijali hahahahahaaaaa.........
 
Ila Babu kama ni wewe kuwa tu mkweli tukupe ushauri wa kupita kwenye supu ya pweza jioni, haingii akilini bibi atange na njia kiivo, hapo hata huyo mwanamama naye utampitia ili umonyeshe kuwa we ni rijali hahahahahaaaaa.........
Ingekuwa ni mimi wala nisingeficha...............Kwani hujui kwamba mficha uke huwa hazai?
 
Utulivu na busara ndio za muhimu sana katika kufikia maamuzi na wala sio papara na hasira maana utaharibu kila kitu
 
Hapo inabidi busara itumike, kwa maoni yangu huyo mwanamke ni mhalibifu tu hivyo yakupasa kujiuliza mara mbili kabla ya kuchukua hatua, maana kama angekuwa mtu mwema angekuita faragha na kukiueleza dukuduku lake na siyo mbele ya kadamnasi
 
Hii hainihusu mimi jamani......................! Nawasilisha tu.

Kiongozi mbona unajitetea!
Hii kali ya mwaka, Hapo inahitaji tafakuri ya nguvu!! Lazima utafute ukweli wa Habari, Kama ni Uzushi au kweli Linahitaji uchunguzi wa kina.Ila aibu Kiongozi!! Mh mbele za watu, Aibu kwako na aibu kwake!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom