Mkanye mkeo nakwambia!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Uko kwenye mizunguko yako maeneo mbali na nyumbani kwako, mara ghafla anakutokea mwanamke usiyemjua kabisa na anakwambia kwa sauti kiasi cha kuwavuta wapita njia wengine waliokuwa wakipita na shughuli zao kusimama na kusikiliza kinachoendelea.

Mwanamke huyo anakwambia……, "Wee baba we, nakuomba sana umkanye mkeo kutembea na bwana angu, la sivyo nitamfanya kitu ambaccho hatakuja kukisahau maishani mwake…..Mwambie asisahau kama mie ni mzaliwa wa Tanga. Kama humtoshelezi, si akatafute wanaume mwengine huko, kuliko kutembea na mabwana za watu, mpaka anataka kunihatarishia uchumba angu, mwambie akome tena akome kama alivyokoma kunyonya titi la mama yake…………….." mwanamke huyo anaondoka huku akiendelea kubwabwanya na njia kwa maneno yenye kukera.

Hebu niambie kama ni wewe unachukua hatua gani ………..?
 
Hii hainihusu mimi jamani......................! Nawasilisha tu.
 
Waulize kina Lulu Facebook!


QUOTE=Mtambuzi;3682373]Hii hainihusu mimi jamani......................! Nawasilisha tu.[/QUOTE]
 
Kwa kawaida mwanaume unatakiwa kuwa na busara sana! Yale ni maneno yanayokera, ila huna uhakika na huyo mama kwa alichokisema. Unaweza kuchukua tu kama taarifa za kuzifanyia kazi. Unaweza kukuta katumwa aje abomoe ndoa yako. Kwanza yeye anaongea mabwana! sio mume? anaweza akawa changu huyo. Mambo kama haya hayahitaji hasira, unaweza kuongea kwa taratibu na mkeo kumweleza mkasa ila bila ya kumlaumu coz huna ushaidi wowote. yeye atasema anachofikiri na wewe unaweza kuchuja mbivu na mbichi.
 
Ni busara tu ndio inayotakiwa ichukuwe nafasi hapo kwani hakuna ushahidi wa tuhuma hizo, fanya uchunguzi.
 
hahah Mtambuzi umepatikana kama ndo wewe uliambiwa haya..
Sijui utaanzaje kumkanya mama watoto..
am kidding !
 
Hahaha hahaha,

Pole sana baba yangu!

Huyo mwanamke mcharuko wenda ikawa ana lake kwann asipambane na mumewe!!!

BTW,Hapo nikunyamaza tu bila kujibu maana anaweza akakujazia watu na kuendelea na safari yako then ufanye uchunguzi kimya kimya mpaka ujue ukweli.
 
i nitamwambia "njoo kwangu nikwambie kitu, tuyaongee kiutu uzima" and you know what will follow....
Khaaaaaaaaaaaa!
Big shem ni wewe au kuna mtu kaiba pasiwedi!!!

Epushia mbali Sisy asipite mitaa hii maana naimajin huyo mwanamke akubali na kutaka kuambatana nawe kwao mkaongee kiutu uzima!!!
 
Unatakiwa kutuliza akili na kufanya uchunguzi wa kina. Isije kuwa katumwa kuja kuvuruga ndoa yenu maana hii dunia ina watu wasio wema wengi wa kutosha!
 
Akili mu Kichwa. 1: Kuwa mtulivu. 2: Mfuatilie Huyo Bibie ujue anaishi wapi 3a: Mfuate siku nyingine ili akupe ABC. 3b: Anza kufuatilia nyendo za mkeo 4:iwapo Bibie atakufafanulia ukweli wa tuhuma zake, zifanyie kazi kwa utulivu mkubwa bila kusukumwa na hisia. 5: Fanya maamuzi ya Busara (iwapo ni kweli kwanini ametoka nje? Je chanzo ni wewe au ni tamaa tu) 6: Kama ni tamaa tu, Kaka PIGA CHINI FASTA
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom