Mkanganyiko wa biashara ya kamari: Mitandao vs vyombo vya habari

Uislamu umetangulia mbali sana kimikakati ya uchumi.Kamari haramu kabisa.Watu wafanye kazi sio kudowea dowea.

Museveni nilisikia aliwahi kushtukia ujinga huu.Sijui na yeye aliishia wapi.

Betting hazifai
 
Jana nimebet Wasafibet, zile live match, nimechagua zinazoongoza nika stake laki moja kwa Odds 28,
Na saizi Kuna sehemu naelekea nikapate Supu niondoe hangover.

Sasa huu Uzi sijui nauelewa vipi, Kila nikijilazimisha kukubali lakini akili za usiku zinakataa.

Hela inatosha breakfast ya wiki nzima, Petrol ya wiki nzima,na nikitoka narudi na mtungi wa gesi mkubwa mnaniambiaje?

Kwenye betting Kuna terms and conditions, pia kustake kiasi unachomudu , la mwisho na kubwa zaidi UWE NA AKILI TIMAMU
Narudia tena UWE NA AKILI TIMAMU.

Huo n ulevi kama ulevi mwingine na mwisho wake ni mbaya
 
Bongo Kuna vitu Halali ukivifanya vinakua na ushuru mkubwa hadi mtu anakata tamaa lkn Mambo ya ovyo wanayaacha ili Hali Yana madhara makubwa kwa kizazi
Tulipokosea ni pale tulipoipa siasa hadhi kubwa kuliko taaluma
 
Kwani ulishasikia betting ipo kwa sababu ya kuendeleza nchi? Tatizo ni kuwa watu mnajaribu kutatua tatizo complex kwa njia rahisi.

Betting kukimbiliwa na vijana wengi ni matokea ya sera na utekelazji mbovu wa serikali kushindwa kufanya kazi. Tatizo litaondoshwa kwa ku-fix tatizo. Hata kama zitawekwa sheria au kuonda kabisa betting leo hii, tatizo litahamia sehemu nyingine na linaweza kuwa kubwa na hatari kuliko betting.

Jiulize kwanza china waliwezaje kuwa taifa kubwa ndani ya miaka michache,hiki tunachofanya kinazidi turudisha nyuma
 
Nchi ya Uchumi wa bodaboda na michezo ya kamari.

Bodaboda zinabeba hadi mbao wanaburuza tu barabarani.
Ukiuliza wanakuambia ajira kwa vijana.

Hivi kuna nchi nyingine duniani wanafanya mambo ya hovyo kama Tanzania?
 
Linapokuja suala la betting mchezaji anapoteza zaidi ya anavyopata. Mtu yoyote mwenye avarage iq ataliona hilo kupitia set ups za odds, unless hapa unafanya marketing kwa malipo basi jua utapoteza zaidi ya utakachokipata kadri unavyocheza.

Hii michezo haikupaswa kuwa promoted. Ilitakiwa ibaki kuwa burudani tu kwenye maeneo ya starehe.

Atleast umeongea vema
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
1. Bahati ya KUUAGA UMASKINI imegonga hodi leo. Njoo ushinde pesa BWELELEE na Tigo Ishi Kistaa sehemu ya Tsh 6,200,000. Tuma neno STAA kwenda 15633 kujiunga.

2. BAHATI YA MTENDE imekuangukia 255XYZXYZXYZ UMOO kwenye DROO ya Tsh 1,500,000 na sehemu ya Tsh 6,000,000. Jiunge CHUKUA USHINDI sasa tuma neno STAA!

Very unfortunate namba inayotuma hizo sms ukijaribu kui-block haiblokiki! Mamlaka husika mtusaidie to get rid of such nonsenses; sio kila mtu anapenda hizo takataka.

N kwl
 
Habari kila mmoja,

Ndugu wapendwa kiuhalisia kama jamii tunaelekea kwenye eneo ambalo sio sahihi hasa jinsi palivyoshamiri michezo hii ya betting au kubahatisha.

Ukiangalia nchi kama china miaka 40 au 30 nyuma haikua na kiwango hiki kikubwa cha uchumi ila serikali na watu wake waliamua kuwekeza kweny uzalishaji na teknolojia kiujumla ili kuweza kwenda mbele,ukija huku kwetu ni tofauti kabisa,sasa hv mpka tv na redio ya serikali inachezesha betting(ajabu kabisa).

Kuna mengi ya kujiuliza hv kweli huku ndo tumeona kama njia sahihi ya kutufikisha kwenye maendeleo ya kweli, jibu ni hapana bali ni kuendelea kuukuza umaskini na kuwanenepesha mabepari!

Jambo hili linasikitisha sana kiuhalisia.
Ulaya ndio maisha yao yenye pesa za maana
 
Jana nimebet Wasafibet, zile live match, nimechagua zinazoongoza nika stake laki moja kwa Odds 28,
Na saizi Kuna sehemu naelekea nikapate Supu niondoe hangover.

Sasa huu Uzi sijui nauelewa vipi, Kila nikijilazimisha kukubali lakini akili za usiku zinakataa.

Hela inatosha breakfast ya wiki nzima, Petrol ya wiki nzima,na nikitoka narudi na mtungi wa gesi mkubwa mnaniambiaje?

Kwenye betting Kuna terms and conditions, pia kustake kiasi unachomudu , la mwisho na kubwa zaidi UWE NA AKILI TIMAMU
Narudia tena UWE NA AKILI TIMAMU.
Angalia ubaya wake ulivyo.Yaani wewe hukuzalisha chochote.Umekula jasho la wenzako ambao kwa hizi pesa ulizowachukulia wanalia.
 
Dah nimeumia ukitaja kamari juzi muhindi kanipiga 200k ya parizi shamba gemu ya southamptom vs man city
Ushahidi wa uharamu ni huu.Mhindi kachukua laki mbili zako bila jasho.Laki moja kampa JACK DANIEL amebakiwa na laki 1 anakwenda kula urojo bila kutoka jasho.
 
Kila ukionacho kina umuhimu wake, hakuna mtu anayelipa kodi kama mcheza kamari, na kwenye kamari kodi wanazotozwa ni kubwa kweli kamari ni chanzo kikubwa sana cha mapato serekalini, kamari ni mtego, una access ya fedha nyingi inabalone equation, huna fedha huwezi kucheza na kupata ni 2/100 by chances, so akili kichwani mwako tu.
Ningefurahi siku moja likaulizwa swali bungeni juu ya kamari huchangia kiasi gani kwenye pato la Taifa nadhani itastaajabisha kwa wingi wa mapato, endapo kama hakuna ujanja ujanja wa watendaji.
KAMARI HUCHANGIA UCHUMI WA AMERIKA KWA 15%.
 
Back
Top Bottom