Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,791
Tuliandika, tunaandika na tutaandika tena na tena lakini ni kama mamlaka zimetiwa upofu machoni na kuweka nta masikioni.. Ni wazi kuna mfaidikaji/wafaidikaji bila kujali madhara makubwa ya baadae
Nilikaa kwenye hii biashara kwa mwaka mzima... Haya ndio niliyaona
Ni biashara ya faida kubwa
Ni biashara yenye mtandao mkubwa
Ni biashara yenye udanganyifu mkubwa
Ni biashara yenye utapeli mkubwa
Ni biashara yenye wizi mkubwa
Ni biashara yenye makengeza mengi sana
Sasa wafaidikaji ni akina nani?
1. Wamiliki
2. Watendaji wa mamlaka(Commissions na rushwa)
3. Serikali(mapato)
4. Washindi
5. Wachezeshaji
6. Vyombo vya habari(kuuza matangazo nk)
Wakosoaji ni akina nani?
1. Wananchi viona mbali kupitia mitandao ya kijamii
2. Waliofilisika kupitia kamari
3.Waliozimishwa ndoto zao kupitia kamari
4. Wanafunzi na wanachuo waliofeli na kuharibu masomo yao kwasababu ya kamari
5. Wanandoa na wote waliovuruga familia zao kwasababu ya kamari
6. Na wengine wote ambao kupitia kamari makutana na mengi magumu kama kesi, ajali, madawa nknk
Makundi hasa ya vijana yaliathirika na kamari ndio mashuhuda wazuri kwenye hii kampeni ya kupinga na kutoa maonyo mengi kuhusiana na huu mchezo mbaya kabisa
Wenzetu waliokwisha onja shubiri na machungu ya shubiri sasa wameweka sheria kali na ngumu kwenye hii biashara, sisi tunawaona maboya.. Tutakuja kulia kilio kikubwa sana
Serikali iko kimya kwakuwa inapokea mapato ambayo hata hivyo ni kiduchu ... Vyombo vya habari vinaisherehesha hii biashara kwa kuitangaza, kuchezesha na kutangaza washindi kila siku.. Nao wa watangazaji wao wamepata vyanzo vyepesi vya mapato.. Huwaambii kitu
Pengine kwasasa ni tv na radio za kidini tu ndio hawafanyi hii biashara..wengine woote wametekwa huko... Umasikini mbaya sana, hasa umaskini wa fikra uduni wa elimu, na ufinyu wa maono.. Wanachojali ni commision kwenye bukubuku za masikini walalahoi
Kamari kutokana na nature yake sio biashara ya kuhusishwa na mamlaka za nchi imejaa uhuni na udanganyifu mkubwa.. Kwahiyo inahujumu uchumi pakubwa sana, maana hizo bukubuku zinazokusanywa kila siku zinaishia mifukoni mwa wajanja wachache na kuondoshwa nchini kwa njia za kimafia
Kamari inalifilisi taifa
Kamari inawatia ufukara wananchi
Kamari inaangamiza vipaji na vipawa vingi
Kamari ni janga la taifa.. Lakini kuipiga vita kwakuwa washika dau ndio wafaidikaji wakubwa na badala ya kula siha wanaambulia makombo...
Thread 'Udanganyifu unaofanywa kwenye michezo ya kubahatisha na kamari' Udanganyifu unaofanywa kwenye michezo ya kubahatisha na kamari
Thread 'Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho' Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho
Alamsiki Tanganyika!