Mkanganyiko wa biashara ya kamari: Mitandao vs vyombo vya habari

Habari kila mmoja,

Ndugu wapendwa kiuhalisia kama jamii tunaelekea kwenye eneo ambalo sio sahihi hasa jinsi palivyoshamiri michezo hii ya betting au kubahatisha...
Uislamu umetangulia mbali sana kimikakati ya uchumi.Kamari haramu kabisa.Watu wafanye kazi sio kudowea dowea.

Museveni nilisikia aliwahi kushtukia ujinga huu.Sijui na yeye aliishia wapi.
 
Jana nimebet Wasafibet, zile live match, nimechagua zinazoongoza nika stake laki moja kwa Odds 28,
Na saizi Kuna sehemu naelekea nikapate Supu niondoe hangover.

Sasa huu Uzi sijui nauelewa vipi, Kila nikijilazimisha kukubali lakini akili za usiku zinakataa.

Hela inatosha breakfast ya wiki nzima, Petrol ya wiki nzima,na nikitoka narudi na mtungi wa gesi mkubwa mnaniambiaje?

Kwenye betting Kuna terms and conditions, pia kustake kiasi unachomudu , la mwisho na kubwa zaidi UWE NA AKILI TIMAMU
Narudia tena UWE NA AKILI TIMAMU.
 
Ni mtazamo wako mkuu wala hujakosea
 
Kwani ulishasikia betting ipo kwa sababu ya kuendeleza nchi? Tatizo ni kuwa watu mnajaribu kutatua tatizo complex kwa njia rahisi.

Betting kukimbiliwa na vijana wengi ni matokea ya sera na utekelazji mbovu wa serikali kushindwa kufanya kazi. Tatizo litaondoshwa kwa ku-fix tatizo. Hata kama zitawekwa sheria au kuonda kabisa betting leo hii, tatizo litahamia sehemu nyingine na linaweza kuwa kubwa na hatari kuliko betting.
 
Wanajuwa kabisa watoto zao
Hawafanyi mambo hayo ya betting,kamali nk
Ndomana hawajali

Ova
Hata kama wanafanya, hawafanyi kama kazi bali ni burudani tu. Mtoto kashapachikwa wizara ya ardhi mzazi ana presha gani na maisha yake.

Wanaoteseka ni watoto wa maskini maana tajiri hawezi kuruhusu mwanae acheze kamari.
 
Jana nimebet Wasafibet, zile live match, nimechagua zinazoongoza nika stake laki moja kwa Odds 28,
Na saizi Kuna sehemu naelekea nikapate Supu niondoe hangover.

Sasa huu Uzi sijui nauelewa vipi, Kila nikijilazimisha kukubali lakini akili za usiku zinakataa.

Hela inatosha breakfast ya wiki nzima, Petrol ya wiki nzima,na nikitoka narudi na mtungi wa gesi mkubwa mnaniambiaje?

Kwenye betting Kuna terms and conditions, pia kustake kiasi unachomudu , la mwisho na kubwa zaidi UWE NA AKILI TIMAMU
Narudia tena UWE NA AKILI TIMAMU.
Linapokuja suala la betting mchezaji anapoteza zaidi ya anavyopata. Mtu yoyote mwenye avarage iq ataliona hilo kupitia set ups za odds, unless hapa unafanya marketing kwa malipo basi jua utapoteza zaidi ya utakachokipata kadri unavyocheza.

Hii michezo haikupaswa kuwa promoted. Ilitakiwa ibaki kuwa burudani tu kwenye maeneo ya starehe.
 
Ijue nguvu ya buku.

Na wew unacheza chota mihela
1. Bahati ya KUUAGA UMASKINI imegonga hodi leo. Njoo ushinde pesa BWELELEE na Tigo Ishi Kistaa sehemu ya Tsh 6,200,000. Tuma neno STAA kwenda 15633 kujiunga.

2. BAHATI YA MTENDE imekuangukia 255XYZXYZXYZ UMOO kwenye DROO ya Tsh 1,500,000 na sehemu ya Tsh 6,000,000. Jiunge CHUKUA USHINDI sasa tuma neno STAA!

Very unfortunate namba inayotuma hizo sms ukijaribu kui-block haiblokiki! Mamlaka husika mtusaidie to get rid of such nonsenses; sio kila mtu anapenda hizo takataka.
 
Uislamu umetangulia mbali sana kimikakati ya uchumi.Kamari haramu kabisa.Watu wafanye kazi sio kudowea dowea.

Museveni nilisikia aliwahi kushtukia ujinga huu.Sijui na yeye aliishia wapi.
Ila makampuni yote yanamilikiwa na Waislamu wenzenu
 
Hahahahah serikali inapumulia kwenye boda boda na kamari. Wanachukua kodi kubwa huko sasa kwanini wakataze kitu kinachowanufaisha!

Serikali inakataaga mambo yanayoweza kuwaharibia kubaki madarakani tu kama mikutano ya Chadema na katiba mpya.

Au kuisema serikali inakosea kwenye taasisi flani hapo ndipo nguvu yake utaiona. Ila mambo ambayo hayagusi maslahi ya watawala moja kwa moja hapo wewe utakesha unalalamika tu.
 
Tuliandika, tunaandika na tutaandika tena na tena lakini ni kama mamlaka zimetiwa upofu machoni na kuweka nta masikioni.. Ni wazi kuna mfaidikaji/wafaidikaji bila kujali madhara makubwa ya baadae

Nilikaa kwenye hii biashara kwa mwaka mzima... Haya ndio niliyaona
Ni biashara ya faida kubwa
Ni biashara yenye mtandao mkubwa
Ni biashara yenye udanganyifu mkubwa
Ni biashara yenye utapeli mkubwa
Ni biashara yenye wizi mkubwa
Ni biashara yenye makengeza mengi sana

Sasa wafaidikaji ni akina nani?
1. Wamiliki
2. Watendaji wa mamlaka(Commissions na rushwa)
3. Serikali(mapato)
4. Washindi
5. Wachezeshaji
6. Vyombo vya habari(kuuza matangazo nk)

Wakosoaji ni akina nani?
1. Wananchi viona mbali kupitia mitandao ya kijamii
2. Waliofilisika kupitia kamari
3.Waliozimishwa ndoto zao kupitia kamari
4. Wanafunzi na wanachuo waliofeli na kuharibu masomo yao kwasababu ya kamari
5. Wanandoa na wote waliovuruga familia zao kwasababu ya kamari
6. Na wengine wote ambao kupitia kamari makutana na mengi magumu kama kesi, ajali, madawa nknk

Makundi hasa ya vijana yaliathirika na kamari ndio mashuhuda wazuri kwenye hii kampeni ya kupinga na kutoa maonyo mengi kuhusiana na huu mchezo mbaya kabisa

Wenzetu waliokwisha onja shubiri na machungu ya shubiri sasa wameweka sheria kali na ngumu kwenye hii biashara, sisi tunawaona maboya.. Tutakuja kulia kilio kikubwa sana

Serikali iko kimya kwakuwa inapokea mapato ambayo hata hivyo ni kiduchu ... Vyombo vya habari vinaisherehesha hii biashara kwa kuitangaza, kuchezesha na kutangaza washindi kila siku.. Nao wa watangazaji wao wamepata vyanzo vyepesi vya mapato.. Huwaambii kitu

Pengine kwasasa ni tv na radio za kidini tu ndio hawafanyi hii biashara..wengine woote wametekwa huko... Umasikini mbaya sana, hasa umaskini wa fikra uduni wa elimu, na ufinyu wa maono.. Wanachojali ni commision kwenye bukubuku za masikini walalahoi

Kamari kutokana na nature yake sio biashara ya kuhusishwa na mamlaka za nchi imejaa uhuni na udanganyifu mkubwa.. Kwahiyo inahujumu uchumi pakubwa sana, maana hizo bukubuku zinazokusanywa kila siku zinaishia mifukoni mwa wajanja wachache na kuondoshwa nchini kwa njia za kimafia

Kamari inalifilisi taifa
Kamari inawatia ufukara wananchi
Kamari inaangamiza vipaji na vipawa vingi
Kamari ni janga la taifa.. Lakini kuipiga vita kwakuwa washika dau ndio wafaidikaji wakubwa na badala ya kula siha wanaambulia makombo...

Thread 'Udanganyifu unaofanywa kwenye michezo ya kubahatisha na kamari' Udanganyifu unaofanywa kwenye michezo ya kubahatisha na kamari

Thread 'Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho' Kamari: Janga lingine lililofumbiwa macho

Alamsiki Tanganyika!
Katika vitu vinanikereketa nafs k....mk ni hii michezo ya redio ya kamali,.jamaa waongo vibaya kutwa kuibia wananchi
Inskitisha kwa kweli
 
Uongo dhambi, hawa jamaa wanatafuna pesa za wananchi vijana kupita maelezo. Mchongo pesa ndo washenzi kabisaa! Na serikali imeruhusu makampuni ya simu kuhamasisha watu kila siku kwa njia ya meseji

Na siku Zinavyokwenda hali ndo itazidi kuwa mbaya kama hatua hazitachukuliwa
 
Back
Top Bottom