Mkanganyiko katika majina ya sayari

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
279
202
Tutakuwa hewani katika kipindi cha RADIO ONE - Kumepambazuka-Kiswahili kesho Jumamosi tarehe 8/Jul/17 pamoja na BAKITA kuelezea mkanganyiko katika majina ya sayari katika lugha ya Kiswahili.

Kipindi kinaanza saa 1:30 aaubuhi hadi saa 3 na tutapewa nafasi humo.

Ni kipindi kutoa mchango wako na kutoa mawazo na maoni yako.

Unaweza kufuatilia kipindi hicho katika mtandao kwa kutumia:

Listen to Kumepambazuka Kiswahili online
Kumepambazuka Kiswahili

======

We will be on air in the radio program Kumepambazuka - Kiswahili this Saturday 8th August, 2017 with BAKITA to discuss the confusion in planet names in Kiswahili. The program runs from 7:30 am to 9 am so we will get a slot within that time.

It is a call in program so listen in and give your contributions and opinions also.

Regards,

Jiwaji

Listen to Kumepambazuka Kiswahili online

Kumepambazuka Kiswahili
 
Tuko nao. Ndiyo maana tunatoa hii mada kwa umma ilituelewane kwa pamoja.
Kwahiyo mnataka kutushirikisha wananchi ili tuyapigie kura majina ya sayari ili mchukue yatakayo shinda ?
Mi nadhani jukumu lenu ni pamoja na kuyachagua majina sahihi ya kibantu ili yatumike kuziita hizo sayari.
Na vigezo vya kuyaita vinaweza kuwa vya kitaalamu, kwa mfano mnaweza kuchukua kwa kichagua majina katika Lahaja au mizizi ya kibantu, badala ya kuchukua majina yenye matamshi (sauti) za kiarabu.
Jambo hili naona linahitaji utafiti wa kitaalamu zaidi na sio maoni ya watu.
 
Lugha ni matumizi, na maneno yana mazoea ya kutumiwa. Kwa hiyo tutaweza kuelewa mazoea ya kutumia majina hayo, na kama kuna matumizi ambayo hatuyaelewi na kama kunamisingi ya matumizi ya maneno hayo, tutatumia michango hiyo kuwashauri BAKITA.
 
Malkia wa yamini ya Benin, wekundu wa Zebaki
Kwako najiamini,sintohama nitabaki
Mrembo mwendo Zuhura, mpole usofura
Na kwa kudura una sura umefungasha mpaka chura
Wote wa dunia, wanakuhudumia
Wewe hariri bunia, wao busati la gunia
Mahiri vita Mhiri, si jamvi la mshihiri
Mama wanisitiri, kiroho na kimwili
Roho unasumbua, Dar mpaka Bujumbura
Nikupe bamvua kama za miezi ya Sambura
Kwa kani ziso fanani, sina budi kughani
Nikuvike pete kama za kwenye Saratani
Wewe tunu johari, nikupige zumari
Na utulivu wako kama sura ya Zohari
Bi Tausi, nyara kama Kausi
Ubaridi wa Utaridi wewe mwisho wa kamusi.

Mercury - Zebaki
Venus - Zuhura
Earth - Dunia
Mars - Mihiri
Jupiter - Sumbura
Saturn - Saratani
Uranus - Zohari
Neptune - Kausi
Pluto - Utarid
 
Kwahiyo mnataka kutushirikisha wananchi ili tuyapigie kura majina ya sayari ili mchukue yatakayo shinda ?
Mi nadhani jukumu lenu ni pamoja na kuyachagua majina sahihi ya kibantu ili yatumike kuziita hizo sayari.
Na vigezo vya kuyaita vinaweza kuwa vya kitaalamu, kwa mfano mnaweza kuchukua kwa kichagua majina katika Lahaja au mizizi ya kibantu, badala ya kuchukua majina yenye matamshi (sauti) za kiarabu.
Jambo hili naona linahitaji utafiti wa kitaalamu zaidi na sio maoni ya watu.
Kuna utamaduni wa WaSwahili waliokuwa mabaharia na walishatumia majina ya sayari 5 zinazoonekana angani usiku kwa macho kavu. Walitumia nyota mbali mbali pamoja na kudinyota na fungunyota kupata mielekeo wakiwa katika uwazi wa bahari, mbali na nchi kavu. Huo ni msingi mkubwa wa kuzingatia katika kuamua majina ya sayari na nyota.
 
Malkia wa yamini ya Benin, wekundu wa Zebaki
Kwako najiamini,sintohama nitabaki
Mrembo mwendo Zuhura, mpole usofura
Na kwa kudura una sura umefungasha mpaka chura
Wote wa dunia, wanakuhudumia
Wewe hariri bunia, wao busati la gunia
Mahiri vita Mhiri, si jamvi la mshihiri
Mama wanisitiri, kiroho na kimwili
Roho unasumbua, Dar mpaka Bujumbura
Nikupe bamvua kama za miezi ya Sambura
Kwa kani ziso fanani, sina budi kughani
Nikuvike pete kama za kwenye Saratani
Wewe tunu johari, nikupige zumari
Na utulivu wako kama sura ya Zohari
Bi Tausi, nyara kama Kausi
Ubaridi wa Utaridi wewe mwisho wa kamusi.

Mercury - Zebaki
Venus - Zuhura
Earth - Dunia
Mars - Mihiri
Jupiter - Sumbura
Saturn - Saratani
Uranus - Zohari
Neptune - Kausi
Pluto - Utarid
Asante sana kwa shairi tamu. Inaonesha umuhimu wa kuelewana majina ya sayari.
 
Mercury - Zebaki
Venus - Zuhura
Earth - Dunia
Mars - Mihiri
Jupiter - Sumbura
Saturn - Saratani
Uranus - Zohari
Neptune - Kausi
Pluto - Utaridi
Wewe umenikumbusha mbali hivi vitu tulivisoma primary enzi hizo ila nilisahau, ahsante kunikumbusha.
 
Kuna utamaduni wa WaSwahili waliokuwa mabaharia na walishatumia majina ya sayari 5 zinazoonekana angani usiku kwa macho kavu. Walitumia nyota mbali mbali pamoja na kudinyota na fungunyota kupata mielekeo wakiwa katika uwazi wa bahari, mbali na nchi kavu. Huo ni msingi mkubwa wa kuzingatia katika kuamua majina ya sayari na nyota.
Nakumbuka kusikiliza hadithi za kipindi cha "Mama na Mwana" miaka ya themanini ya mwanzo.

Kulikuwa na hadithi ya sayari ya Zuhura.

Haya si majina yaliyotungwa jana, mengine yana mizizi katika safari za biashara kati ya fukwe za Afrika Mashariki na za Uarabu na Uajemi.
 
Back
Top Bottom