Mkanganyiko katika majina ya sayari

Mkanganyiko katika majina ya sayari

Astronomy kiswahili si ni unajimu?

Pia, tunatenganisha vipi astronomy na astrology? Au astrology ndiyo unajimu? Nakumbula kusoma kitabu cha nadharia za LaPlace kuhusu mfumo wa jua ulivyoumbwa, darasa la saba, kwa Kiswahili, astronomy tuliita unajimu. Elimu ya anga la juu na vilivyomo.

Kuna watu wanasema hao Wagiriki nao walipata hiyo elimu Misri, kwamba Wamisri walijua mambo mengi sana ambayo hawakutaka kuweka wazi na mengine yamepotea mpakaleo.

Ukifuatilia mfano wa Erasthotheses, mtu wa kwanza aliyerekodiwa kupima mzingo wa dunia, alijua habari hizokutoka Misri. Yaani jamaalilikaa chini tu likatumia geometry,kivuli kinachotokana na jua na akili zake kujua mzingo wa dunia nzima. Huyu kazaliwamiaka 276 kabla ya Yesu kuzaliwa.

Hata Pythagoras aliyegundua "Pythagoras Theorem" alijifunza maengi sana Misri.

Eratosthenes - Wikipedia

Hapana, Astronomy si unajimu, maana neno "unajimu" linatumika katika kutabiri maisha ya watu kutokana na mipangilio ya nyota, lakini hiyo haina misingi ya sayansi.
Kwa hiyo imebidi kuunda neno lingine kwa ajili ya kueleza somo la kisayansi ya nyota na anga za juu. Neno tulilokubaliana "Astronomia" tumelitohoa kutoka Kiingereza.

Astrology ni utabiri wa maisha ya watu kwa kuangalia mipangilio ya nyota. Na hiyo tunaita "unajimu"

Ni kweli kuwa Pythagoras na Erastosthenes wamejifunza mengi kutoka kwa wa Misri na tamaduni zingine za wakati huo.
 
Hii elimu ya nyota inasomewa wapi?
Kwa sasa hapa kwetu hatuna programu maalum ya elimu ya nyota, ila infundishwa katika somo la Fizikia shuleni hadi katika vyuo.
 
Hapana, Astronomy si unajimu, maana neno "unajimu" linatumika katika kutabiri maisha ya watu kutokana na mipangilio ya nyota, lakini hiyo haina misingi ya sayansi.
Kwa hiyo imebidi kuunda neno lingine kwa ajili ya kueleza somo la kisayansi ya nyota na anga za juu. Neno tulilokubaliana "Astronomia" tumelitohoa kutoka Kiingereza.

Astrology ni utabiri wa maisha ya watu kwa kuangalia mipangilio ya nyota. Na hiyo tunaita "unajimu"

Ni kweli kuwa Pythagoras na Erastosthenes wamejifunza mengi kutoka kwa wa Misri na tamaduni zingine za wakati huo.
Naona wameelezea vizuri sana hapa Unajimu - Wikipedia, kamusi elezo huru

Nilikuwa najiuliza sana kamaKiswahili tunatofautisha Astronomy na Astrology,hasa kwa sababu vitabu vingi vya shule ya msingi viliandika astronomy kama unajimu.
 
Ok. Pale katika KUNDI ORION BELT KUNA HORSEHEAD NEBULA

HII NENO NEBULA NDO GIMBA KWA KISWAHILI HORSE-HEAD KWA KISWAHILI INAITWAJE?

TUPE UFAFANUSI DOCTOR

Nebula si gimba maana kuwa gimba linaundwa na maada iliyokusanyika kwa karibu.

Nebula ni kama wingu, lakini ni wingu lililo undwa na gesi joto za Hidrojeni na Heli (Helium) pamoja na vumbi na utegili (plasma) na zimekusanywa kwa kani-mvuto ya graviti. Hapa ndani ya nebula ndiyo hutokea maeneo ambako magimba yatatokeza baada ya maada kukusanyika kwa karibu sana hadi kusababisha kuunda gimba la jua na magimba ya sayari zake.

Horeshead ni neneo lililotokana na umbo la nebula ambayo katika darubini inaonkeana kama kichwa cha farasi. Angalia http://www.constellation-guide.com/wp-content/uploads/2014/01/Horsehead-Nebula.jpg

Kwa hiyo kwa Kiswahili tutaweza kuita nebula hii nebula ya kichwafarasi.
 
Tunategemea kuondoa mkanganyiko huo sasa na kutenga unajimu na sayansi ya Astronomia
Astronomia iloitakiwa ipewe jina lake linalofanana na unajimu, kama astrology inavyofanana na astronomy.
 
Astronomia iloitakiwa ipewe jina lake linalofanana na unajimu, kama astrology inavyofanana na astronomy.
Kwa sasa astrology inapigwa vita sana kwa vile inpigwa debe kwa vile watu wanadhani utabiri wa maisha ya watu unategemea nyota, kumbe siyo kweli. Moja ya sababu ya kuendelea kwa tatizo hili ni ukaribu wa majina hayo, kwa hiyo watu wanadhani astrology pia ina misingi ya sayansi kumbe si kweli.

Kwa hiyo tumefanya vizuri kutenga kabisa majina ya unajimbu kuwa mbali sana na Astronomia.
 
Formula ilikuwaga inaitwa ZE,ZU,DU,MI,SU,SA,ZO,KA,U

ZEBAKI
ZUHURA
DUNIA
MIHIRI
SUMBURA
SATANI
ZOHARI
KAUSI
UMBURA
Hii formula naona chaka, wataalamu wanasema Sayari ya kwanza ni Utaridi
 
Dr, Jiwaji umefika wakat wa kampen ya kahamasisha watu kuujua UTALII WA ANGA kutoka hapo ulipo. Pia imefika wakat wa kaunzisha group la whatsaap la wana asrtonomy. Zingatia hilo. Asante
 
Dr, Jiwaji umefika wakat wa kampen ya kahamasisha watu kuujua UTALII WA ANGA kutoka hapo ulipo. Pia imefika wakat wa kaunzisha group la whatsaap la wana asrtonomy. Zingatia hilo. Asante

Anga yetu ni hazina ya kitalii maana haijachafuka kwa nuru kali ya taa za mijini
iliyoakisiwa na angahewa (light pollution). Hali ya hewa pia inavuta watu watoke nje na kuona maelfu ya nyota yakin'gaa katika giza zito. Zaidi ya hiyo, kwa vile tupo jirani na Ikweta nyota za kaskazini na kusini zote zinaonekana kwa wakati mmoja. Tunajiandaa kutoa kozi kwa tour guides wanaowaongoza watalii kufahamu anga yetu kwa undani.

Kuhusu kundi la wnaopenda astronomia, tumeweza kusajili chama cha astronomia karibuni tu na tunajipanga kuwaalika watu wanaopenda kufuatilia mambo ya nyota na anga za juu kujiunga.
 
Dr, ulisema utatunganisha na whatsApp ,usisahau
 
Dr liwe km group kwani mengi sana yapo yakujifunza kupitia kwako.

Mf. Nina swali hapa. Je, katika galaxy yetu ya milky-way jumla kuna makundi mangapi?

Je,sie wanadamu tuliopo ndani ya solar system na jua letu tunaishi na kumilikiwa ktk kundi lipi la nyota?
 
Makundi ya nyota ni ya kinadharia tu kwa vile makundi hayo ni nyota zilvyojipanga tu angani na haziko pamoja. Kwa hiyo makundi ya nyota hayaundi mfumo halisi. Mfumo wa Jua ni mfumo tunaoishi na galaxy yetu ya Milky Way in mfumo ambamo upo mfumo wetu wa Jua. Nitumie barua pepe kwa id yangu ya ntjiwaji at yahoo dot com
 
Back
Top Bottom