Haina sifa ya kuitwa sayari. Ni kama mawe mengine tu yanayoelea huko angani. Hii ni kwa Mujibu wa maana mpya ya sayari.Sio sayari au ni sayari kibete?
Kwanza kabisa neno kuwa la kiajemi hakulizuii kutoholewa kuwa la Kiswahili,tukumbuke Kiswahili kimetokea Pwani na Washirazi waliotoka Uajemi walichangia sana katikakukikuza Kiswahili.Sasa kama Mshtari ni neno la kiajemi kama unavyosema.
Neno la kibantu la Jupiter ni lipi ?
Au halipo kabisa ?
Sumbula ni nyota gani hiyo kwa unajimuwa Kiingereza mkuu kama unaifahamu?
Lazimaitakuwa nyota maalum mpakakuwa na jina la Kiswahili.
Mimi ningependa kujua majina ya nyota za Betelgeuse, Sirius, Canopus and Alpha Centauri katika Kiswahili kama yapo.
Inawezekana hata baadhi ya haya majina ya Kiingereza yanatokana na majina ya Kiarabu,hiyo Betelgeuse naona kama imetoholewa kutoka Kiarabu hivi.Majina haya yalitambuliwa kutumiwa na WaSwahili mabaharia tangu zamani:
- Sambula ni jina la nyota angavu ambalo kwa kiingereza linajulikana kama Spica ambayo iko katika kundi la nyota Nadhifa (Kiingereza - Virgo)
- Betelguese ni Ibuti la Jauza
- Sirius ni Shira
- Canopus ni Suheli
- Alpha Centauri ni Rijili Kantori
Inawezekana hata baadhi ya haya majina ya Kiingereza yanatokana na majina ya Kiarabu,hiyo Betelgeuse naona kama imetoholewa kutoka Kiarabu hivi.
Yep, guess what? The wiki has it here Betelgeuse - Wikipedia
Astronomy kiswahili si ni unajimu?Ni kweli. Kuna mifano mingi mingine, kwa mfano Algol.
Maendeleo mengi ya astronomia na sayansi waliyapata Wazungu kutoka kwa Waarabu. Na Waarabu pia walihifadhi habari nyingi za kale za kutoka kwa Wgiriki na kuwafikia Wazungu kutoka kwa Waarabu.
Mushtari/Mushtara ni neno lenye asili ya kiajemi.
Kuna harakati za kukifanya Kiswahili kiwe na maneno ya lugha za asili za kibantu zaidi badala ya kutohoa kutoka kiarabu na lugha kama za kiajemi zaidi.
Kwa hiyo inawezekana kabisa kukawa na majina ya kibantu na kiarabu/kiajemi yanashindana.
Na kwa kuwa wewe ni Sheikh wa Pwani, haya mambo ya Malampaka unaweza usiyajue nkoyi.
Aleyo a ba ng'wani bakizaga na mamihayo ga ng'wani doho.
Ateho mna Malampaka komanya mamihayo ga e nyanza yeneye.
Noloo mna ng'wani komanya mamihayo ga kola manumbu. Eteho yeneyo.
Kaka wa ajabu
kwanza: kwa nini unaleta hapa matusi?
Pili: hapana Mshtarii si Kiajemi, asili ni Kiarabu
Tatu: kumbe hutaki maneno yenye asili ya Kiarabu katika lugha?
Nne: basi badilisha lugha, acha Kiswahili.
Tano: mwenyewe unashindwa kuandika mistari michache bila kutumia maneno ya asili ya Kiarabu.
Sita: Kama hujui: Hapo juu nimechora kwa rangi maneno yote uliyotumia wewe ambayo yana asili ya Kiarabu
Mercury - Zebaki
Venus - Zuhura
Earth - Dunia
Mars - Mihiri
Jupiter - Sumbura
Saturn - Saratani
Uranus - Zohari
Neptune - Kausi
Pluto - Utaridi
Sayari zipo nyingi sana kwa sasa, vyomba vya kuchunguza anga za mbali vimekuwa imara zaidi, hizo sayari 9 zilikuwa enzi hizo kwa sasa sayari zinavumbuliwa kila uchwao.
Sawa mkuu mi nilitumia mafundisho ya shule ya msingi niliyosoma zamani kidogo.Sayari zipo nyingi sana kwa sasa, vyomba vya kuchunguza anga za mbali vimekuwa imara zaidi, hizo sayari 9 zilikuwa enzi hizo kwa sasa sayari zinavumbuliwa kila uchwao.
Kilimia ni fungunyota iliyo jirani na kundinyota ya Jabari (Orion).Kundi hili la ilikuwa ikionekana angan wazee wetu wa kale walijua ni msimu wa kulima yaan cha kulimia (Kilimia). Kilimia ni pamoja na Orioni kati ya makundi ya nyota
yanayotajwa mara kadhaa katika Biblia ( Ayubu 9:9 na
38:31; Amosi 5:8).
Ni Sumbula mkuu 'r'Mercury - Zebaki
Venus - Zuhura
Earth - Dunia
Mars - Mihiri
Jupiter - Sumbura
Saturn - Saratani
Uranus - Zohari
Neptune - Kausi
Pluto - Utaridi