Mkanganyiko baada ya roho kuachana na mwili

Mkanganyiko baada ya roho kuachana na mwili

Gefu ni sahihi kabisa kitu ni hichocho bali kwa maelezo mengine hasa kulingana na imani ya kikristo. Nenda pale Muhimbili wodi ya Sewa Haji wale wagonjwa wa kinywa na koo wanatamani kunywa lakini tone moja kupita kooni ni ishu! Unajua haya mambo tunaishi nayo ni kwa kuwa tu tumezingwa na changamoto za kidunia.

We mzee wee! Kwa hiyo wale wagonjwa wa kinywa na koo ni roho za marudio zimo mule ili wataabike?
 
Mtu akifa amekufa hawezi kujua neno lolote hapa duniani wala kaburini (kuzimu) hivyo roho hutoka na nkisema roho maana yake ni pumzi, so hii pumzi haiendi pepon wala haiwezi kuingia kwa mtu yeyote wala hawezi kuzaliwa mtu na kuwekewa pumzi hyo, hivyo basi YESU anaporudi mara ya pili watu wote waliotenda mema watafufuliwa kwa ajili ya uzima na wale waliotenda maovu watasubiri ufufuo baada ya miaka elfu nao watafufuliwa kwa ajili ya mauti, ile kusema roho ilazwe mahali pema peponi ni mafundisho potovu na hayatakiwi kuendekezwa!
 
Haya mambo bado yanachanganya wengi kwamba roho inaenda wapi baada ya kuachana na mwili
1.Je inaenda kuzimu?
2.Je inaenda peponi?
3.Je inazaliwa upya?
4.Je inawayawaya na kutangatanga huku na kule?

Maswali yote hapo juu yana majibu yanayofanana, kuwa roho zipo na zinakuwa kote huko kulikotajwa kutegemeana na kwenye uhai wake kidunia zilibeba/ zilifanya nini? Hebu twende moja baada ya jingine.

Kwanza, dini zote zinahimiza matendo mema na maisha baada ya kifo; hata wapagani pia. Hivyo basi, japokuwa maelezo yanatofautiana, lakini msingi unabaki kuwa ule ule wa roho kuwa sehemu husika.

1.Je, roho inaenda kuzimu? Jibu ni ndio

Kwamba bila kujali unaamini nini lakini jehanam iko hapahapa duniani , roho iliyotenda mabaya duniani baada ya kutoka katika mwili uharibikao huingia kwenye mwili mwingine uliojaa mateso tabu na mahangaiko mengi! Kumbuka ili roho iweze kubeba hisia za mateso na maumivu lazima zipate jumba/ mwili!! Hiyo ni jehanam au kuzimu.

2.Je, roho huenda peponi? Jibu ni ndio

Pepo iko hapahapa duniani, roho iliyoishi kwa kutenda mema hubaki mahali kwenye dunia hii ikiwa iko live lakini domant ikiwa haihisi wala kufanya chochote na kama ikibidi kupata mwili huingia kwenye mwili ambao haujui shida za dunia hii kila kitu kwake ni mteremko tu mpaka mwili husika unapochoka na kuharibika/ kufa!! Hii ni peponi.

3.Je, roho inazaliwa upya? Jibu ni ndio japo kimsingi sio kuzaliwa upya bali ni kupata makao/ makazi mapya hapa ndio penye dhana nzima ya reincarnation, ambapo sasa hutegemea matendo ya nyuma Kwahiyo yaweza kuwa kwenye mwili mzuri au mbaya refer pepo na kuzimu.

4.Je, roho zinatangatanga? Jibu ni ndio
kwanza roho huwa hazifi bali kuna wakati hukosa makao mapya/mwili baada ya zamani kwisha na kuharibika
Haijulikani hasa nini hutokea lakini hizi ni roho zenye matatizo makubwa na ndio hizi huwa mashetani majini vinyamkera na viumbe vya ajabu ajabu. Ni roho hizi hizi ambazo huweza kuingia kwenye familia kikundi au mkusanyiko wowote na kuleta mirafaruku mikubwa tu ambayo mingine huleta maafa makubwa.

Kwahiyo roho zipo na zipo sana na kamwe hazifi wala hazipotei jehanam, na pepo zao zipo hapahapa duniani na kwenye kila nyanja ya maisha yetu ikiwemo JF.
Mkuu Mshana Jr; Asante kwa uzi huu. Naamini Mungu yupo kwa maana ya mapokeo. Kwa umri huu, najua kuna kufa lakini hakuna kufufuka, kwa maana kwamba hakuna maisha ya baadaye, wala hakuna moto wa milele; aidha, hakuna roho hai baada ya kifo. Binadamu akizaliwa, anakuwa hai then, kifo. Mengine yote ni ujanja, wizi, uhuni na kutishana tu. Kikubwa, ni kwamba watu waishi kwa amani na kuiacha amani ikiendelea. Mengine yote ni ubinafsi. Dini is a social activity ambayo baadhi huitumia kuishi kwa kutiishia watu na kutajirika. Maisha ni haya na mwisho wake kifo.
 
Hujawahi fika mbinguni wala kuzimu wala ukiwa unazaliwa hukumbuki ilikuwaje, utajifikilisha nini hapo, hata watafiti popote wana reference, ni wapiga ramli tu ndo hupaswi kujua reference Wa Yale wanayoyasema, hivyo reference ni za msingi

Mleta mada anakusihi ukalitumie ubongo ulo nao kufikiri...kwa mapana na marefu, husizishirikishe vitabu na vingine, ukweli unao mwenyewe, husiwe mvivu wa kufikiri wala husikubali kuzuiwa na yeyote kufikiri.

Salam kutoka Kenya.
 
Uhangaishe nini akili yako wewe kuhusu "soul", na hiyo aya laiti ungeliijuwa kwa Kiarabu ungeona raha sana.

Hicho kipande cha mwisho kilichotafsiriwa kama "And mankind have not been given of knowledge except a little." Kina maanisha ni watu wachache waliopewa ilm hiyo na pia imetolewa kwa uchache wake hiyo ilm yenyewe.

Sitegemei hiyo ilm uwe nayo mtu kama wewe, kwani wenye ilm hiyo huwa hawaulizi.

Wenye ilm hiyo hutwa wana Ilm Kishti wa Ruh.

Watu kama weye ndiyo mnaowatisha watu mkitumia vitabu na dini za ajabu ajabu,wasiweze kutumia akili zao kufikiri wenyewe kwa mapana.

Potelea mbali.
 
projectmano post: 16415293 said:
soma biblia! achana na mitazamo!

mwisho wa siku ukweli unabakia katika kitabu cha Mungu! ukweli ndio huo! ukifa unakwenda sehemu uliyo jiwekea tayali ukiwa bado unaishi duniani yaani kuvuna unacho panda!

Dhibitisha kama ni kitabu cha mungu.
 
Mkuu kwa kweli hapa natetemeka mno hii mada haiepukiki duuh Roho ikiacha mwili inarudi ilikotoka kusubiri malipo ya mambo ya huku DUNIANI huko kunaitwa mbinguni, sasa maamuzi ni ipi inastahili kwenda wapi ni Hukumu ya mungu yaani balaa mkuu nasikia roho ya dhambi itakula mkong'oto mwanzo mwisho asubuhi jioni kipigo tu sasa ndio maana naogopa mno mkuu
 
Haya mambo bado yanachanganya wengi kwamba roho inaenda wapi baada ya kuachana na mwili
1.Je inaenda kuzimu?
2.Je inaenda peponi?
3.Je inazaliwa upya?
4.Je inawayawaya na kutangatanga huku na kule?

Maswali yote hapo juu yana majibu yanayofanana, kuwa roho zipo na zinakuwa kote huko kulikotajwa kutegemeana na kwenye uhai wake kidunia zilibeba/ zilifanya nini? Hebu twende moja baada ya jingine.

Kwanza, dini zote zinahimiza matendo mema na maisha baada ya kifo; hata wapagani pia. Hivyo basi, japokuwa maelezo yanatofautiana, lakini msingi unabaki kuwa ule ule wa roho kuwa sehemu husika.

1.Je, roho inaenda kuzimu? Jibu ni ndio

Kwamba bila kujali unaamini nini lakini jehanam iko hapahapa duniani , roho iliyotenda mabaya duniani baada ya kutoka katika mwili uharibikao huingia kwenye mwili mwingine uliojaa mateso tabu na mahangaiko mengi! Kumbuka ili roho iweze kubeba hisia za mateso na maumivu lazima zipate jumba/ mwili!! Hiyo ni jehanam au kuzimu.

2.Je, roho huenda peponi? Jibu ni ndio

Pepo iko hapahapa duniani, roho iliyoishi kwa kutenda mema hubaki mahali kwenye dunia hii ikiwa iko live lakini domant ikiwa haihisi wala kufanya chochote na kama ikibidi kupata mwili huingia kwenye mwili ambao haujui shida za dunia hii kila kitu kwake ni mteremko tu mpaka mwili husika unapochoka na kuharibika/ kufa!! Hii ni peponi.

3.Je, roho inazaliwa upya? Jibu ni ndio japo kimsingi sio kuzaliwa upya bali ni kupata makao/ makazi mapya hapa ndio penye dhana nzima ya reincarnation, ambapo sasa hutegemea matendo ya nyuma Kwahiyo yaweza kuwa kwenye mwili mzuri au mbaya refer pepo na kuzimu.

4.Je, roho zinatangatanga? Jibu ni ndio
kwanza roho huwa hazifi bali kuna wakati hukosa makao mapya/mwili baada ya zamani kwisha na kuharibika
Haijulikani hasa nini hutokea lakini hizi ni roho zenye matatizo makubwa na ndio hizi huwa mashetani majini vinyamkera na viumbe vya ajabu ajabu. Ni roho hizi hizi ambazo huweza kuingia kwenye familia kikundi au mkusanyiko wowote na kuleta mirafaruku mikubwa tu ambayo mingine huleta maafa makubwa.

Kwahiyo roho zipo na zipo sana na kamwe hazifi wala hazipotei jehanam, na pepo zao zipo hapahapa duniani na kwenye kila nyanja ya maisha yetu ikiwemo JF.
Namshukuru Mungu kwamba chanzo cha habari ni wewe mwenyewe wala hauna rejea yoyote ya maandiko matakatifu

Hivyo ndugu wanaJf alichoandika huyu ndugu hakina maana yoyote hususani ktk mitazamo ya kibiblia hivyo kama utayaamini maneno yake ujue umeamini ktk mtazamo wake na ktk biblia haipo hivyo
 
Gefu ni sahihi kabisa kitu ni hichocho bali kwa maelezo mengine hasa kulingana na imani ya kikristo. Nenda pale Muhimbili wodi ya Sewa Haji wale wagonjwa wa kinywa na koo wanatamani kunywa lakini tone moja kupita kooni ni ishu! Unajua haya mambo tunaishi nayo ni kwa kuwa tu tumezingwa na changamoto za kidunia.
Ushauri; unapotaka kuongelea jambo lenye mizizi ktk maandiko matakatifu jitahidi uwe umekisoma kitabu husika Quran ama bible vinginevyo unapoteza roho za wengi na hizi roho unazozipeleka mbali na Mungu utadaiwa na kama usipotubu na kuungama adhabu yako itakuwa kubwa mno, kumbuka Mungu yupo na siku ya hukumu inakuja
 
Naamini kama ungekuwa msomaji mzuri wa Biblia na kuelewa usingekuja na hoja kama hizi
Mungu alipotuasa tukatafute na kuishika elimu alikuwa na maana kubwa sana kwakuwa nje ya Bible pia kuna elimu nyingine...sasa Unapokuwa mtu wa Misahafu tu bila maarifa mengine shida huanzia hapo
 
Unaposoma ktk biblia "mshike sana elimu usimwache aende zake" haina maana ya elimu unayoijua ww wala hii elimu ya leo tunayosoma ya evolution, rain formation, continental drift etc usidhani ni vitu vyenye kumpendeza Mungu wala kumtukuza hivyo kwa mujibu wa biblia iliyoandikwa kwa lugha ya kiebrania elimu inayoongelewa sio elimu unayoijua ww ila elimu ya kumjua Mungu na kumtumikia pekee, hata Paulo anaandika ni aibu baadhi ya watu hawamjui Mungu 1Wakorintho 15:34

Elimu yeyote nje ya biblia kama inapingana na biblia haifai, elimu ya biblia yenyewe inajitosheleza kwa kila kitu

Na kingine hekima itokanayo na elimu yeyote ambayo inapingana na maandiko ya Mungu hiyo elimu haina maana hivyo hiyo elimu nyingine unayoiongelea kama haina mizizi ktk biblia ama inapingana na Mungu hiyo elimu matokeo yake ni uharibifu mtupu
 
Mkuu Mshana Jr; Asante kwa uzi huu. Naamini Mungu yupo kwa maana ya mapokeo. Kwa umri huu, najua kuna kufa lakini hakuna kufufuka, kwa maana kwamba hakuna maisha ya baadaye, wala hakuna moto wa milele; aidha, hakuna roho hai baada ya kifo. Binadamu akizaliwa, anakuwa hai then, kifo. Mengine yote ni ujanja, wizi, uhuni na kutishana tu. Kikubwa, ni kwamba watu waishi kwa amani na kuiacha amani ikiendelea. Mengine yote ni ubinafsi. Dini is a social activity ambayo baadhi huitumia kuishi kwa kutiishia watu na kutajirika. Maisha ni haya na mwisho wake kifo.
Si kweli Mungu yupo na mapokeo hayo ni yakukufanya wewe ujifunze zaidi juu ya Mungu inaweza kuwa umeishi kwa muda mrefu na hujapata kuamini juu ya uwepo halisi wa Mungu na kwamba yeye ndie alieumba dunia hii na vyote vilivyomo ila sasa ni wakati wako wa kumjua Mungu.

Mungu yupo na ukiamini atajidhihirisha kwako fanya hivi mwombe Mungu atende jambo lolote ambalo unahisi ama unaliona kwa ajili za kibinadamu haliwezekani na ambalo likitokea utaamini ni Mungu kalitenda mwombe kwa dhati atalifanya ili upate kumwamini kwamba yupo na siku ya hukumu ipo na wafu wote watafufuliwa kuhukumiwa

Ila pamoja na ilo na kushauri soma biblia walau kidogo tu hasa kitabu cha mwanzo utajifunza mengi juu ya uwepo na kuu wa Mungu, ubarikiwe
 
Haaaaah
Kwakweli Science inahitaji kufundishwa kwanguvu zote mashuleni kwetu, Kwa imani hizi za ajabu ajabu
 
Unaposoma ktk biblia "mshike sana elimu usimwache aende zake" haina maana ya elimu unayoijua ww wala hii elimu ya leo tunayosoma ya evolution, rain formation, continental drift etc usidhani ni vitu vyenye kumpendeza Mungu wala kumtukuza hivyo kwa mujibu wa biblia iliyoandikwa kwa lugha ya kiebrania elimu inayoongelewa sio elimu unayoijua ww ila elimu ya kumjua Mungu na kumtumikia pekee, hata Paulo anaandika ni aibu baadhi ya watu hawamjui Mungu 1Wakorintho 15:34

Elimu yeyote nje ya biblia kama inapingana na biblia haifai, elimu ya biblia yenyewe inajitosheleza kwa kila kitu

Na kingine hekima itokanayo na elimu yeyote ambayo inapingana na maandiko ya Mungu hiyo elimu haina maana hivyo hiyo elimu nyingine unayoiongelea kama haina mizizi ktk biblia ama inapingana na Mungu hiyo elimu matokeo yake ni uharibifu mtupu
Nadhani una tatizo la uelewa...Neno kinasema hivi ...nchi na VYOTE viijazavyo ni mali naam mwanadamu na WOTE wakaao ndani mwake...hayo mafundisho yote ambayo mimi nayaita ni chukizo mbele za Mungu asili na chanzo chake ni pale Eden na mwanzilishi wake ni shetani ambaye ndio alikuwa malaika mkuu kabla ya kuasi...na ndio maana neno pia linasema hakuna jipya chini ya jua/mbingu yote yaliyokuwepo yaliyopo na yajayo ni mambo yalikwisha tabiriwa enzi na enzi...kila kitu kiwe kibaya ama kizuri vyote ni uumbaji wake
Kuhusu elimu umeongopa ndugu yangu... Mungu hawezi kukwambia ukatafute sana elimu wakati elimu unayo mkononi mwako umeishika...si kweli hata kidogo...!Yeye alimaanisha Alichosema fullstop
Kuna vitabu viwili sana kwenye Biblia takatifu 1.kitabu cha Mwanzo 2.ufunuo wa Yohana...watu wengi hukimbilia kusoma mwanzo kwakuwa kwanza no kama historia ni mambo yaliyopita na yanaeleweka LAKINI wengi hukimbia kusoma UFUNUO kwakuwa kwanza ni mambo magumu hata kuyasoma tu na kuyaelewa achana na kutafsiri, pia ni mambo 'yaliyofunuliwa'
Kwahiyo ndugu yangu naelewa ninachokiandika na nina hakika nacho na sipingani na Biblia takatifu
 
Kaka m
Kwa kifupi mtoa mada unapotosha watu. Mtu akifa kinachofuata ni hukumu tu soma waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu. Hapo unaona pia hakuna habari za toharani muda wa kutengeneza mambo ni hapa duniani ukiwa hai basi.

Ni vema ukaokoka hata ukifa uwe salama huko uendako.
-----------------------
Kaka binafs nikipata shida kuelewa huo mstar..But Roho Mtakatifu ni mwema akanifanya niulewe kwa namna hiiii....
Nilikuwa najiuliza inamaana mtu akifa tu ni hukumu(Eb 9;27)Nikasema na ile hukumu ya mwisho atakua kundi lipi sasa?
Ufunuo 21 inaonyesha bhr itawatoa wafu,ardhi itawatoa wafu wakubwa kwa wadogo then watahkumiwa.
Nikapata shida juu ya mkanganyiko..wa baada ya kifo n hukumu na hukumu ya watu wote.
Ni kijiuliza je hkm ipo mara mbili...
Nikaja pata jibu..
Kwamba Baada ya kifo hakutakuwa na nafasi nyngne ya toba/rehema/msamaha..yaani itakuwa ni kusubiri hukumu ya mwsho ya watu wote..wale watao fufuka na wale wataokutwa hai.
Wote kwa pamoja hakuta kua na nafasi ya kusema subiri ama nirudishe nikatubu..kwanza...
Kam vile ulivyozaliwa mara moja..umeona uzuri au ubaya wa dunia.ni ngumu kumwabia Mama..nirudishe tumboni Mama.No mpk ngoma uzeen mpk kaburi.
Ndivyo nilivyoelewa maana ya baada ya kufa ni hukumu.
Barikiwa na ww.

Kaka mm nilipata tabu kuelewa huu mstari..lkn Roho Mtakatifu ninmwema
 
Back
Top Bottom