Mr. Mangi
JF-Expert Member
- Sep 21, 2014
- 1,512
- 772
Wapi niliposema uongo?? Kuhs elimu?Nadhani una tatizo la uelewa...Neno kinasema hivi ...nchi na VYOTE viijazavyo ni mali naam mwanadamu na WOTE wakaao ndani mwake...hayo mafundisho yote ambayo mimi nayaita ni chukizo mbele za Mungu asili na chanzo chake ni pale Eden na mwanzilishi wake ni shetani ambaye ndio alikuwa malaika mkuu kabla ya kuasi...na ndio maana neno pia linasema hakuna jipya chini ya jua/mbingu yote yaliyokuwepo yaliyopo na yajayo ni mambo yalikwisha tabiriwa enzi na enzi...kila kitu kiwe kibaya ama kizuri vyote ni uumbaji wake
Kuhusu elimu umeongopa ndugu yangu... Mungu hawezi kukwambia ukatafute sana elimu wakati elimu unayo mkononi mwako umeishika...si kweli hata kidogo...!Yeye alimaanisha Alichosema fullstop
Kuna vitabu viwili sana kwenye Biblia takatifu 1.kitabu cha Mwanzo 2.ufunuo wa Yohana...watu wengi hukimbilia kusoma mwanzo kwakuwa kwanza no kama historia ni mambo yaliyopita na yanaeleweka LAKINI wengi hukimbia kusoma UFUNUO kwakuwa kwanza ni mambo magumu hata kuyasoma tu na kuyaelewa achana na kutafsiri, pia ni mambo 'yaliyofunuliwa'
Kwahiyo ndugu yangu naelewa ninachokiandika na nina hakika nacho na sipingani na Biblia takatifu
Ubarikiwe mtu wa Mungu, maana umesema haupingani na biblia hivyo tofauti zinazooneka ambazo zinapingana na biblia ni dhahiri hujadhamiria
Ila kwa kuwa umesema hupingani na biblia unaelezea kwamba roho haifi biblia inasema mtu anapokufa ni sawa na mtu alielala usingizi mzito usio na ndoto kama ulishawahi fanyiwa upasuaji ukapigwa nusu kaputi utakuwa umejifunza kitu cha pekee mi nshafanyiwa Mhubiri 9:5, 10 Ayubu 3:13-19 ukipitia hapo utagundua kwamba kifo kinaelezewa kwamba mtu anapokufa anarudi ktk hali aliyokuwa nayo kabla hajazaliwa hivyo roho zote ovu ama laa hupumzika kimya kama ilivyo kuwa kabla ya kuzaliwa hadi ile ahadi ya UFUFUO itakapotimia maana Yesu aliahidi atarudi tena kuziamsha hizo roho kisha zitahukumiwa alihaidi atarudi kuwachukua washindi na roho za waovu zitaangamizwa Mathew 25:31-46
Hivyo ndugu yangu mtu anapokufa hulala usingizi kabisa hata Yesu alipokufa hakwenda popote ndo maana alipofufuka wakati alipomtokea Maria Magdalena alimwambia usinishike maana sijaenda bado kwa Baba Yohana 20:17 na muda ulipofika alipaa mbinguni na atakaporudi kwa staili ile ile roho zilizomwamini na kufa ktk haki zitapaa kwenda mbinguni pamoja na Yesu kwa staili ile ile