Mkandarasi achota 3bn advance akimbia! Alipewa kujenga km 26 za lami wakati hana ujuzi wowote...

Bora hata angepewa Nyanza road hata akichakachua na kujenga chini ya kiwango lakini ni wa hapa hapa

Umesema jambo la msingi sana. Kampuni hii haingeshindwa kujenga 26km hata kidogo. Na fedha ambazo ingelipwa bado zingekuwa zinazunguka humuhumu. Lakini ndio hivyo nchi hii wazawa hawatakiwi kabisa kuendelezwa.



Sent from my iPad using JamiiForums
 

Nimekupa like mkuu. Hawa ndio "chumvi" kwenye supu ya ujinga wa Mtanzania.


Sent from my iPad using JamiiForums
 

Wenye kumsifia Pombe waje hapa wajionee wenyewe....Chini ya CCM tutaendelea kuwa shamba la bibi milele daima...hawa jamaa hakuna wanaloliweza, kilimo, mifugo, viwanda, madini, nishati, afya, elimu, usafiri na usafirishaji ...Vyote ni (-v)... = 0
 
3. Unababaisha na kujichanganya au umbulula? ....

Na wewe unajichanganya ile mbaya. Unajifanya kuandika kama third party lakini siku za mwizi wala siyo arobaini. Mfano hapo chini
4. Ujenzi wa Camp: Ni kweli tulianza kujenga camp kwa asilimia 20 lakini haikumalizika tukafukuzwa

Hapo kwenye red una maana kuwa wewe ni mmoja wa wahusika kwenye hiyo kampuni.

Ni nani huwa anajenga camp? Wewe? Kama nani?

cc. SUMLEY
 
kwa maconsultants makini hivi huwa vinachekiwa mwanzoni wakati wa contract negotiations .... kosa ni la watendaji wa TANROADS hapa pamoja na consultants wa mradi (kama walikuwepo)

kama Magufuli ni msanii, ina maana hata aliyemteua ni msanii pia!


Mimi nilishaacha kumwamini Magufuli baada kugundua ni mtu wa show off na mwenye kutaka tu sifa kwa umahiri wa kukariri km za barabara na majina ya barabara

na mimi naomba kuuliza!! je magufuli ni injinia??? na kama sio je kapewaje hii secta?? sawa wenda ujuzi hawajali katika kuteua waziri, lakini ni lazima ifike sehemu kila secta wapewe wataalamu na sio mtu kisa mbunge ndio apewe!!
 
Je na wewe ni mmoja wa wahusika wa hii kampuni??

Kwanza ujenzi wa camp unatakiwa ukamilike ndani ya miezi mitatu baada ya kusaini mkataba. Maana ipo ndani ya mobilization period ambapo wao kimsingi asilimia ilitakiwa kukamilika mwezi wa 8. Sasa wao mpaka miezi 9 imepita wamefanya 20 percent. Kuna kampuni hapo?
 
na mimi naomba kuuliza!! je magufuli ni injinia??? na kama sio je kapewaje hii secta?? sawa wenda ujuzi hawajali katika kuteua waziri, lakini ni lazima ifike sehemu kila secta wapewe wataalamu na sio mtu kisa mbunge ndio apewe!!

Profesa Philemon Sarungi aliyewahi kuwa Waziri wa Afya je unakumbuka madudu aliyofanya afya wakati ni bingwa wa mifupa? Hoja yako haina mashiko!
 



Huyu incorruptible amejiunga hapa 19th April 2014.
Hawa wenye ID nyingi humu JF ndio wala nchi. Sasa hivi atakuwa ameenda kutengeneza ID nyingine.
Awali nilikuwa najiuliza, iweje ana information kiasi hiki lakini hakuwahi kuzitoa hapa jamvini mpaka alipoona posti ya SUMLEY?
 

Hivi kaka yangu kwanini kupoteza muda na wale waliotayari kula hata bila kunawa.Kutetea UOVU wa aina yoyote ili mradi atapata kitu fulani.Kwa ID yake hakutakiwa kumtetea MGENI huyo bali kuionea huruma NCHI yake na jamii yake.Achana naye akija jua wapi amekosea atajutia,lakini mpaka hapo atakuwa amekuelewa mbivu na mbichi.
 
kwa maconsultants makini hivi huwa vinachekiwa mwanzoni wakati wa contract negotiations .... kosa ni la watendaji wa TANROADS hapa pamoja na consultants wa mradi (kama walikuwepo)

kama Magufuli ni msanii, ina maana hata aliyemteua ni msanii pia!


Mimi nilishaacha kumwamini Magufuli baada kugundua ni mtu wa show off na mwenye kutaka tu sifa kwa umahiri wa kukariri km za barabara na majina ya barabara

Profesa Philemon Sarungi aliyewahi kuwa Waziri wa Afya je unakumbuka madudu aliyofanya afya wakati ni bingwa wa mifupa?!

aiseee...
Hoja yako haina mashiko
je unadhani kwa hii sample space yako moja ni kigezo cha kusema huu uzembe ulioandika hapa una maana?
 
Wengine wanaweza kuona dawa ni kuchukua mtutu na kuingia mtaani. Huu ni ulafa usiokubalika. Ccm oyeeeee.
 

Kwa uswahili wa mtanzania kila sehemu hatuwezi, awe mwanasheria, muhandisi,doctor au mwanasiasa wote ni ubabaishaji tupu, je kuna kampuni yoyote ya kitanzania inayojenga barabara nje ya nchi? kwa wanaojua tafadhari mnifahamishe, kama hakuna basi wacha tuendelee hivi hivi na hivyo kuthibitika kwa ongezeko la wajinga nchini.
 
..................... mimi ni mzalendo na nimefuatilia sakata hili mpaka lilipo sasa kwa kuwa ninadai malipo yangu kwa mkandarasi huyu........

Uzalendo wako una mashaka makubwa sana......na inaonyesha upo kwenye "circles" za ulaji/ufisadi.....kwa sababu zifuatazo


  1. Umekuwa na taarifa ya upuuzi wa muajiri wako.....na umekuwa kimya hadi habari imewekwa hapa JF....Uzalendo unaodai uko wapi....
  2. Umeonyesha wazi kuwa maslahi yako binafsi kwanza pamoja na upuuzi wote huo wa huyo Mkandarasi wako
  3. Umeonyesha kukubalina na Poor Performance ya Mkandarasi wako unayemdai.....ulitegemea mpewe muda gani ili muweze kukamilisha kambi yenu
  4. Umeonyesha kutokuwa na upeo wa kuona HOJA YA MSINGI ya mleta mada...na kuanza kumu-attack pasipo kuwa na sababu yeyote ya msingi
  5. Hukuonyesha kwa namna yeyote ya kihoja kuelezea/kulaani/kukataa upuuzi uliotokea

Kufanyika kwa due diligence...taarifa kamili na za uhakika zinatakiwa awe nazo Client na vyombo vinavyotoa udhamini na si vinginevyo.......

The fact of the matter ni kuwa Mkandarasi amekuwa terminated....na madudu mengine yanafumuka....ikiwemo ya udhamini....kwa jinsi ulivyojibu hoja za mleta mada...nachelea kusema knowledge yako kwenye hayo mambo bado sana........

Back to the hoja ya msingi ya Mada
Kufuatia upuuzi kama huu CEO wa TANROADS inabidi aachie ngazi pamoja na maofisa husika kwa upuuzi wote huu....ifike mahala tusioneane huruma......that is where I miss "Fagio la chuma"......
 
mkuu hapa siwezi kukujibu, ila hata kama hamna je ndio sababu ya kutopewa tenda hizi za ndani?? je unaamini hatuwezi kiasi hiki?
Hata kama vifaa hawana.. siamini kama nchi yote hii inashindwa kuwapa asset chini ya erb na kwa kutumia vifaa hivyo vya serikali wakafanya hizi kazi???
 
mkuu hapa siwezi kukujibu, ila hata kama hamna je ndio sababu ya kutopewa tenda hizi za ndani?? je unaamini hatuwezi kiasi hiki?

Mkuu kampuni za Kitanzania zenye uwezo wa ujenzi zipo na hata huko miaka ya nyuma zilikuwepo.....Kuna kipindi nilikuwa Uganda, DRC na Kenya nilikutana na kampuni za Kitanzania zikichapa mzigo......

Hivi sasa BRN na Private Sector Association wameishauri Serikali ku-review Procurement Act ili kuwawezesha zaidi wazawa na kushiriki miradi mbali mbali ya maendeleo......one of their point ni kwamba......ili kuendeleza ubunifu kwa wazawa na kulinda ubinifu wetu inabidi kipa umbele wapewe wabunifu wazawa wenyewe......its debatable though!
 
Nachojua mkandarasi yeyote akipewa site lazima alipwe advance payment hiyo ndo mikataba ya kimataifa i.e FIDIC swala la how alipewa advance payment kabla hajafanya kazi si sahihi hapa!


Wakuu hapo juu...ni vizuri mkafafanua kuhusu hiyo "Advance Payment (AP)"......neno "lazima" litumike kwa uangalifu kidogo.......kwa sababu "lazima" ina conditions zake kwenye hili suala.....

Kwanza, kabisa ni lazima iwe (AP) stated kwenye Mkataba/Contract i.e. Appendix to Tender and kama Contractor anahitaji AP (maana sio Contractors wote wanataka AP) ni lazima awakilishe Advance Payment Guarantee (APG).

Pili, ieleweke kuwa AP is an interest free mobilization loan from the employer (excluding provisional sums)

Tatu, and in short Mkandarasi hatalipwa/pewa Advance Payment endapo:
  1. Hataomba kulingana na relevant sub-clause (in this case 14.3 FIDIC red book)
  2. Hata wakilisha Performance Security kulingana na relevant sub-clause (in this case 4.2 FIDIC red book)
  3. Hata wakilisha APG kulingana na relevant sub-clause (in this case 14.2 FIDIC red book)

Items hizo tatu hapo juu ni mandatory kabla ya kuidhinishwa by the Engineer kwa AP.......
 
aiseee...

je unadhani kwa hii sample space yako moja ni kigezo cha kusema huu uzembe ulioandika hapa una maana?

nafikiri unafahamu vizuri constitution yetu ina allow yote haya .... mtendaji mkuu wa wizara ni katibu mkuu na huyu ndie anayetakiwa kujua kila kitu ndani ya wizara kiutendaji kwa kusaidiwa na wakurugenzi wa kila idara ... waziri na naibu waziri ni viongozi wa kisiasa na hutakiwa kusimamia policy kulingana na ilani ya serikali iliyopo madarakani ... kwa katiba yetu ndio maana unaona mawaziri wanarushwa ovyo ovyo tu kwenye wizara mbali mbali ... wako wachache kama marehemu Mgimwa ndio alikua waziri stahiki wa wizara ya fedha kwa sababu alikua amesomea mambo hayo

shida ya tanzania ni system na mara nyingi sio viongozi waliopo .... system sio imara ndio maana inaruhusu hata viongozi wa ovyo kufanya madudu
 
Mkuu Sumley heshima yako mkuu.

Hili suala zima linaonyesha lilichezwa na baadhi ya watu kule TANROADS ambao ndio waliona hio pesa inanukia kupitia huo mradi.

Taarifa nilizo nazo kuhusu kumbukumbu za makampuni, Strada Internatinal ni kampuni iliosajiliwa Uingereza yenye namba 07546113 na ina ofisi zake maeneo Wilaya iitwayo Middlesex na anuani yake ya posta ni 170 Draycott Avenue, Kenton, Middlesex, HA3 0BZ UK.

Kampuni hii haina simu ya ofisi,tovuti, wala barua pepe na haina mtu maalumn kwa kuwasiliana nae, ingawa inaonyesha inafanya shughuli za ukandarasi.

Pia rekodi zinaonyesha kwamba kulikuwa na watu wawili ambao ndio wanaonekana ni waendeshaji wa kampuni ambao wanaitwa G. Burji na F. A. Malik, E.S. Isingo na B. Kahan ambae ni mwanamke ambao wote wa sasa wanaonekana wameondokana na kampuni hiyo(inawezekana baada ya kugawana ile pesa)

Pia kuna mshiriki mwngine anaetambulika kwa majina ya K.S. Mudan ambae taarifa hazisemi kama bado yupo au la.

Kwahio wa kuchambua hapa ni huyo bwana E.S.Isingo kwamba ni mtanzania au ni raia wa wapi.

Nafikiri haka kataarifa katafaa kwa Iasi Fulani kuchangia mada yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…