Mkandarasi achota 3bn advance akimbia! Alipewa kujenga km 26 za lami wakati hana ujuzi wowote...

Bora hata angepewa Nyanza road hata akichakachua na kujenga chini ya kiwango lakini ni wa hapa hapa

Umesema jambo la msingi sana. Kampuni hii haingeshindwa kujenga 26km hata kidogo. Na fedha ambazo ingelipwa bado zingekuwa zinazunguka humuhumu. Lakini ndio hivyo nchi hii wazawa hawatakiwi kabisa kuendelezwa.



Sent from my iPad using JamiiForums
 
Miaka ya 70 ni CCM wenyewe wamejenga, sasa unafiki wa nini? Watu wamefanya shughuli na Serikali imewaachia.

Ila kwenye ndege na Gas, hapo wanatembeza ubabe hata JWTZ wanaitwa waje wapige watu. Nani MNAFIKI?

Hata kama hakujenga, wewe Waziri unaenda kuongoza magari ya kumwaga vifusi, na jitu kama wewe linaona jamaa anafanya kazi. Kwanza hajasomea hiyo kazi. Pia hana kofia ya kufanyia kazi Site (Helmet) na wala nguo za usalama kazini. Pia analeta tu Stress kwa wafanyakazi kuwepo kwake na lundo la waandishi wa habari kama wewe na mwisho mnaishia kupewa vibahasha muje muuze sura yake na kumtetea kama vile mmeshikishiwa akili zenu na Magufuli.

Chezea bahasha za KAKI wewe................................

Nimekupa like mkuu. Hawa ndio "chumvi" kwenye supu ya ujinga wa Mtanzania.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Ndugu wanaJF,

Waziri John Magufuli alipokuwa akisoma bajeti ya Wizara yake alisema contractor wa barabara ya kutoka KIA kwenda Mererani amefukuzwa kutokana na utendaji mbovu. Hakuendelea na detail yeyote ile kuhusu huo mradi, huenda hakutaka watu wajue zaidi au yeye mwenyewe hajui kilichotoekea.

Ukweli ni huu:
Kampuni iliyopewa kazi ya kujenga hiyo barabara inaitwa Strada International iliyoonyesha ina Makao Makuu yake UK. Ukubwa wa mradi ulikuwa ni km 26 za kiwango cha lami na gharama za mradi jumla ni 26bn.

Contractor alipewa advance payment ya takribani 3bn (am not sure ila ni kati ya 2.5 mpaka 3.2). Baada ya kupewa hiyo pesa contractor huyu ambae asili yake ni singa singa hakufanya chochote toka mwezi wa 5 mwaka jana mpaka mwezi wa kwanza mwaka huu. Zaidi alisafisha barabara mita 600 tu ambayo ni hatua ya mwanzo kabisa. Hata kujenga camp yake alishindwa, na mbaya zaidi hakuwa na vifaa vya kufanyia kazi. Alinunua grade 2 za kichina na hela hakumalizia kulipa. Mradi ulitakiwa kuwa na zaidi ya tipper 25 lakini alikuwa na tipa 2 za kukodi. Pamoja na kampuni ya usimamizi ya LEA kutoa vielelezo toka mwezi wa 10 kwamba Contractor hana uwezo wa kufanya kazi, aliendelea kulelewa mpaka mwezi January alipokimbia.

UFAKE WA KAMPUNI HII
Inashangaza kuona kampuni ya kigeni ambayo ni ya kisanii imepewa tenda ya kujenga km 26 za rami ambazo ni sh 26bn wakati kampuni hii haijawahi kujenga hata mita 5 za changarawe. Hii kampuni haijawah kufanya mradi wowote wa barabara, lakini walisubmit Company Profile iliyoomyesha wamejenga barabara Sudan, Ghana, Msumbiji, Ethiopia, Qatar, UK na Namibia. Kabla ya kupewa huu mradi kwa kuwa ni kampuni mpya tanroads huwa na utaratibu wa kujiridhisha kwa kupeleka wajumbe baadhi ya nchi kwwnda kuona miradi iliyofanywa na hiyo kampuni. TANROADS ilituma wajumbe ghana na msumbiji, na wajumbu hao walirud na report ya kuonyesha kwamba ni kweli walifanya na mbaya zaidi walirudi mpaka na ripoti za idara na mamlaka za barabara ktk nchi husika kwamba hiyo kampuni ilifanya kazi huko (Kitu ambacho si kweli, wajumbe walihongwa na kuchakachua report zote za Msumbiji na Ghana kwamba kampuni ilifanya kazi huko na kukamilika).

HASARA KWA SERIKALI

Serikali imepata hasara kubwa katika maeneo makuu matatu:

1. Adnvace pyament ya 3bn. Serikali imeambulia grader 2 za kichina zisizo na thamani ya zaid ya milioni 200.

2. Gharama za kumlipa mhandisi msimamizi kwa zaidi ya miezi sita aliyokaa. Ambapo ni zaidi ya million 700.

3. Kuandaa tender upya ambapo gharama za mradi lazima zipande kutokana na kupanda kwa maisha. Maana 26bn ni tender iliyotangazwa mwaka 2012.

NINI KILITOKEA MPAKA STRADA IKAKIMBIA

Katika hali ya kusuasua alikokuonyesha, serikali ilianza kuichunguza hii kampuni kwa undani zaidi maana hata wale waliokuwa wamekula hela kwa kuipa kazi hii kampuni ilionekana wanashindwa kuibeba. Serikali ikagundua kumbe hata bank guarantee iliyowekwa ni feki! Hiyo bank ilikana kuijua hiyo kampuni hii na hapo ndipo serikali ilipochanganyikiwa maana mdhamini aliyewekwa ili kama mambo yakiwa sivyo yeye ndo alipe fidia haijui hiyo kampuni. Watu hao hao wa TANROADS waliokula dili hilo wakamshtua mteja wao kwamba serikali imeshtukia mchezo na jamaa akakimbia mpaka leo.

Kuonyesha kampuni ilikua ni ya kitapeli, ilikopa mpaka furniture za ofisi. Vitendea kazi kama computers na printers walikopa duka la Compcat hapo Arusha. Ana deni kubwa la milion ka 200 hivi kutoka kwa NSK. Wafanyakaz wanadai mishahara ya mwezi wa kumi na mbili ma wa kwanza na hapo ni baada ya kugoma kwa wiki nzima na kumtumia mkuu wa Wilaya na mbunge mh Lema kumpigia simu ndipo alilipa deni la mwezi wa 10 na 11.

EXIM WANUSIRIKA

Bank ya Exim ilibakia kidogo tu nayo itapeliwe baada ya hiyo kampuni ku-process mkopo wa milion 450. Katika hali iliyoonyesha bahati kwa Exim, walichunguza kabla ya kutoa hizo hela maana walikuwa tayari wameshajiridhisha kwa asset zilizowekwa ambazo miongoni mwao ndo zile grader ambazo sasa serikali imezizuia kupitia TANROADS Arusha.

KAULI SAHIHI

Ukweli ni kwamba mkandarasi Strada alikimbia mwenyewe na si serikali kumfukuza. Na amekimbia baada ya kuona ukweli kuhusu kampuni yake kufoji vitu umejulikana. Lakini wameondoka na faida kubwa na kuitia hasara serikali. Maana ktk 3bn, alizotumia Bongo hazifiki hata 1.5bn mpaka anaondoka.

NANI WA KUWAJIBISHWA

Kitengo cha Procurement cha TANROADS lazima kiwajibike kwa hili maana walifanya Investigation kwa hii kampuni na kutoa report za uwongo. Maana huwezi kuniambia walivyoenda Ghana na Msumbiji walidanganywa na hizo mamlaka kuhusu kampuni hii. Na pia bank guarantee walishindwa ku-confirm kabla. Hili swala lilifanyika wakiwa wanajua dhahili ukweli kuhusu kampuni hii.

Na ningependa kuona Magufuli akilitolea ufafanuzi swala hili na hatua zilizochukuliwa kwa watendaji waliosaidia kuidanganya serikali. Na pia mbunge husika, Olesendeka na ningependa ajue kuhusu hili maana barabara ipo jimboni mwake.

Nawakilisha.

Wenye kumsifia Pombe waje hapa wajionee wenyewe....Chini ya CCM tutaendelea kuwa shamba la bibi milele daima...hawa jamaa hakuna wanaloliweza, kilimo, mifugo, viwanda, madini, nishati, afya, elimu, usafiri na usafirishaji ...Vyote ni (-v)... = 0
 
3. Unababaisha na kujichanganya au umbulula? ....

Na wewe unajichanganya ile mbaya. Unajifanya kuandika kama third party lakini siku za mwizi wala siyo arobaini. Mfano hapo chini
4. Ujenzi wa Camp: Ni kweli tulianza kujenga camp kwa asilimia 20 lakini haikumalizika tukafukuzwa

Hapo kwenye red una maana kuwa wewe ni mmoja wa wahusika kwenye hiyo kampuni.

Ni nani huwa anajenga camp? Wewe? Kama nani?

cc. SUMLEY
 
kwa maconsultants makini hivi huwa vinachekiwa mwanzoni wakati wa contract negotiations .... kosa ni la watendaji wa TANROADS hapa pamoja na consultants wa mradi (kama walikuwepo)

kama Magufuli ni msanii, ina maana hata aliyemteua ni msanii pia!

Maconsultants katika mradi huu ni LEA, lakin hawastahili lawama yeyote kwa maana ktk hali utaratibu usio sahihi contractor alisaini mkataba na kuanza kazi mwezi mei 2013 wakati consultant alisaini na kufika site mwezi wa 9 2013. Na huwa sio kazi ya consultant kujua contractor kapataje mradi na ana sifa gani huko nyuma. Yeye kazi yake ni kuhakikisha contractor anafanya kazi na vitu vyote as per contract.

Mimi nilishaacha kumwamini Magufuli baada kugundua ni mtu wa show off na mwenye kutaka tu sifa kwa umahiri wa kukariri km za barabara na majina ya barabara

na mimi naomba kuuliza!! je magufuli ni injinia??? na kama sio je kapewaje hii secta?? sawa wenda ujuzi hawajali katika kuteua waziri, lakini ni lazima ifike sehemu kila secta wapewe wataalamu na sio mtu kisa mbunge ndio apewe!!
 
Je na wewe ni mmoja wa wahusika wa hii kampuni??

Kwanza ujenzi wa camp unatakiwa ukamilike ndani ya miezi mitatu baada ya kusaini mkataba. Maana ipo ndani ya mobilization period ambapo wao kimsingi asilimia ilitakiwa kukamilika mwezi wa 8. Sasa wao mpaka miezi 9 imepita wamefanya 20 percent. Kuna kampuni hapo?
 
na mimi naomba kuuliza!! je magufuli ni injinia??? na kama sio je kapewaje hii secta?? sawa wenda ujuzi hawajali katika kuteua waziri, lakini ni lazima ifike sehemu kila secta wapewe wataalamu na sio mtu kisa mbunge ndio apewe!!

Profesa Philemon Sarungi aliyewahi kuwa Waziri wa Afya je unakumbuka madudu aliyofanya afya wakati ni bingwa wa mifupa? Hoja yako haina mashiko!
 

4. Ujenzi wa Camp: Ni kweli tulianza kujenga camp kwa asilimia 20 lakini haikumalizika tukafukuzwa
Je na wewe ni mmoja wa wahusika wa hii kampuni??

Na wewe unajichanganya ile mbaya. Unajifanya kuandika kama third party lakini siku za mwizi wala siyo arobaini. Mfano hapo chini

Hapo kwenye red una maana kuwa wewe ni mmoja wa wahusika kwenye hiyo kampuni.
Ni nani huwa anajenga camp? Wewe? Kama nani?
cc. SUMLEY


Huyu incorruptible amejiunga hapa 19th April 2014.
Hawa wenye ID nyingi humu JF ndio wala nchi. Sasa hivi atakuwa ameenda kutengeneza ID nyingine.
Awali nilikuwa najiuliza, iweje ana information kiasi hiki lakini hakuwahi kuzitoa hapa jamvini mpaka alipoona posti ya SUMLEY?
 
Njoo na hoja sio unakuja na kauli za mtu kutumika mara nna taarifa za kutosha. Mara nimekufundisha mambo mengine ya mradi ulikua hujui. Sioni nafasi ya hizi kauli kwa swala la msingi kama hili Ukiwa sahihi ntakwambia uko sahihi na siko kwa ajili ya kubishana ili mradi tunabishana ndo maana nimekujibu kila kitu ulichojengea hoja. Kwa great thinker kuja na majibu mepesi kama haya si sahihi. Naanza kushawishika kuwa wewe ni mmoja wa waliosaidia udanganyifu huo maana unadai we umefanya kazi mradi ule. Maana waliofanya kazi mradi huu mpaka leo wanadai mishahara ya mwezi wa 11 na january 2014.

Sasa hapo umejibu kitu gani, nimejibu hoja zako zote 10 then unakuja na kauli hizi. Ila nadhan wana jf watapembua vizur na kujua.

Hivi unajua kwamba strada inadaiwa na
1. NSK zaidi ya milion 100- huyu alikua ni supplier wa diezel.

2. Compucat zaidi ya milion 50- huyu alisupply office equipments na computers

3. Kodi ya nyumba alioifanya ofisi pale boma.

4. Hotel ya snow view ya boma- ambapo ilibid mhandisi mshauri amlipie engineer wake maana strada alikuwa halipi deni mpaka likafika milion 7. Mwanzo alilipa nayo kwa mbinde.

5. Kampuni ya kukodisha magari ya serena ambayo baada ya kushindwa kununua gari alilopaswa kumpa msimamiz wa tanroad arusha ilibid wakodishe kweny kampuni ya serena.

6. Kampuni ya ujiji ambayo mwanzo ilimkodishia tippers na roller baada ya kuona hawalipwi wakachukua mashine zao.

7. Wafanyakazi wote wanaodai mishahara ya mwezi wa 12 na 1.

Hii kweli ni kampuni class 1? Na kumbuka hapo ameshapewa 3.25bn..... Sasa hii kampuni hiyo hela ya advance ilifanyia nini kama kila sehem alikopa? Hii kampuni lengo lake lilikua nini? Watanzania tuwe na huruma na nchi hii.

Hivi kaka yangu kwanini kupoteza muda na wale waliotayari kula hata bila kunawa.Kutetea UOVU wa aina yoyote ili mradi atapata kitu fulani.Kwa ID yake hakutakiwa kumtetea MGENI huyo bali kuionea huruma NCHI yake na jamii yake.Achana naye akija jua wapi amekosea atajutia,lakini mpaka hapo atakuwa amekuelewa mbivu na mbichi.
 
kwa maconsultants makini hivi huwa vinachekiwa mwanzoni wakati wa contract negotiations .... kosa ni la watendaji wa TANROADS hapa pamoja na consultants wa mradi (kama walikuwepo)

kama Magufuli ni msanii, ina maana hata aliyemteua ni msanii pia!

Maconsultants katika mradi huu ni LEA, lakin hawastahili lawama yeyote kwa maana ktk hali utaratibu usio sahihi contractor alisaini mkataba na kuanza kazi mwezi mei 2013 wakati consultant alisaini na kufika site mwezi wa 9 2013. Na huwa sio kazi ya consultant kujua contractor kapataje mradi na ana sifa gani huko nyuma. Yeye kazi yake ni kuhakikisha contractor anafanya kazi na vitu vyote as per contract.

Mimi nilishaacha kumwamini Magufuli baada kugundua ni mtu wa show off na mwenye kutaka tu sifa kwa umahiri wa kukariri km za barabara na majina ya barabara

Profesa Philemon Sarungi aliyewahi kuwa Waziri wa Afya je unakumbuka madudu aliyofanya afya wakati ni bingwa wa mifupa?!

aiseee...
Hoja yako haina mashiko
je unadhani kwa hii sample space yako moja ni kigezo cha kusema huu uzembe ulioandika hapa una maana?
 
Wengine wanaweza kuona dawa ni kuchukua mtutu na kuingia mtaani. Huu ni ulafa usiokubalika. Ccm oyeeeee.
 
Ni lini tanzania itaanza kuwaamini na kuwatumia mainjinia wazawa!? Hata kama vifaa hawana.. siamini kama nchi yote hii inashindwa kuwapa asset chini ya erb na kwa kutumia vifaa hivyo vya serikali wakafanya hizi kazi??? Na ingekua ni rahis sana kuwabana kama ingetokea uhuni wowote!! Na waibe tu..aghghghg.hhh..

Kwa uswahili wa mtanzania kila sehemu hatuwezi, awe mwanasheria, muhandisi,doctor au mwanasiasa wote ni ubabaishaji tupu, je kuna kampuni yoyote ya kitanzania inayojenga barabara nje ya nchi? kwa wanaojua tafadhari mnifahamishe, kama hakuna basi wacha tuendelee hivi hivi na hivyo kuthibitika kwa ongezeko la wajinga nchini.
 
..................... mimi ni mzalendo na nimefuatilia sakata hili mpaka lilipo sasa kwa kuwa ninadai malipo yangu kwa mkandarasi huyu........

Uzalendo wako una mashaka makubwa sana......na inaonyesha upo kwenye "circles" za ulaji/ufisadi.....kwa sababu zifuatazo


  1. Umekuwa na taarifa ya upuuzi wa muajiri wako.....na umekuwa kimya hadi habari imewekwa hapa JF....Uzalendo unaodai uko wapi....
  2. Umeonyesha wazi kuwa maslahi yako binafsi kwanza pamoja na upuuzi wote huo wa huyo Mkandarasi wako
  3. Umeonyesha kukubalina na Poor Performance ya Mkandarasi wako unayemdai.....ulitegemea mpewe muda gani ili muweze kukamilisha kambi yenu
  4. Umeonyesha kutokuwa na upeo wa kuona HOJA YA MSINGI ya mleta mada...na kuanza kumu-attack pasipo kuwa na sababu yeyote ya msingi
  5. Hukuonyesha kwa namna yeyote ya kihoja kuelezea/kulaani/kukataa upuuzi uliotokea

Kufanyika kwa due diligence...taarifa kamili na za uhakika zinatakiwa awe nazo Client na vyombo vinavyotoa udhamini na si vinginevyo.......

The fact of the matter ni kuwa Mkandarasi amekuwa terminated....na madudu mengine yanafumuka....ikiwemo ya udhamini....kwa jinsi ulivyojibu hoja za mleta mada...nachelea kusema knowledge yako kwenye hayo mambo bado sana........

Back to the hoja ya msingi ya Mada
Kufuatia upuuzi kama huu CEO wa TANROADS inabidi aachie ngazi pamoja na maofisa husika kwa upuuzi wote huu....ifike mahala tusioneane huruma......that is where I miss "Fagio la chuma"......
 
Kwa uswahili wa mtanzania kila sehemu hatuwezi, awe mwanasheria, muhandisi,doctor au mwanasiasa wote ni ubabaishaji tupu, je kuna kampuni yoyote ya kitanzania inayojenga barabara nje ya nchi? kwa wanaojua tafadhari mnifahamishe, kama hakuna basi wacha tuendelee hivi hivi na hivyo kuthibitika kwa ongezeko la wajinga nchini.
mkuu hapa siwezi kukujibu, ila hata kama hamna je ndio sababu ya kutopewa tenda hizi za ndani?? je unaamini hatuwezi kiasi hiki?
Hata kama vifaa hawana.. siamini kama nchi yote hii inashindwa kuwapa asset chini ya erb na kwa kutumia vifaa hivyo vya serikali wakafanya hizi kazi???
 
mkuu hapa siwezi kukujibu, ila hata kama hamna je ndio sababu ya kutopewa tenda hizi za ndani?? je unaamini hatuwezi kiasi hiki?

Mkuu kampuni za Kitanzania zenye uwezo wa ujenzi zipo na hata huko miaka ya nyuma zilikuwepo.....Kuna kipindi nilikuwa Uganda, DRC na Kenya nilikutana na kampuni za Kitanzania zikichapa mzigo......

Hivi sasa BRN na Private Sector Association wameishauri Serikali ku-review Procurement Act ili kuwawezesha zaidi wazawa na kushiriki miradi mbali mbali ya maendeleo......one of their point ni kwamba......ili kuendeleza ubunifu kwa wazawa na kulinda ubinifu wetu inabidi kipa umbele wapewe wabunifu wazawa wenyewe......its debatable though!
 
Nachojua mkandarasi yeyote akipewa site lazima alipwe advance payment hiyo ndo mikataba ya kimataifa i.e FIDIC swala la how alipewa advance payment kabla hajafanya kazi si sahihi hapa!

Uko sahihi na swala sio kwanin amepewa advance payment. Advance payment lazima apewe, swala ni kwamba kampuni haikua na sifa ya kupewa mradi. Walichakachua kampuni profile, ndo maana mimi nachotaka kuona ni wale waliosaidia kuidanganya serikali wanawajibishwa. Nasisitiza hii kampuni haikuwahi kujenga hata mita 5 ya kiwango cha gravel!

Wakuu hapo juu...ni vizuri mkafafanua kuhusu hiyo "Advance Payment (AP)"......neno "lazima" litumike kwa uangalifu kidogo.......kwa sababu "lazima" ina conditions zake kwenye hili suala.....

Kwanza, kabisa ni lazima iwe (AP) stated kwenye Mkataba/Contract i.e. Appendix to Tender and kama Contractor anahitaji AP (maana sio Contractors wote wanataka AP) ni lazima awakilishe Advance Payment Guarantee (APG).

Pili, ieleweke kuwa AP is an interest free mobilization loan from the employer (excluding provisional sums)

Tatu, and in short Mkandarasi hatalipwa/pewa Advance Payment endapo:
  1. Hataomba kulingana na relevant sub-clause (in this case 14.3 FIDIC red book)
  2. Hata wakilisha Performance Security kulingana na relevant sub-clause (in this case 4.2 FIDIC red book)
  3. Hata wakilisha APG kulingana na relevant sub-clause (in this case 14.2 FIDIC red book)

Items hizo tatu hapo juu ni mandatory kabla ya kuidhinishwa by the Engineer kwa AP.......
 
aiseee...

je unadhani kwa hii sample space yako moja ni kigezo cha kusema huu uzembe ulioandika hapa una maana?

nafikiri unafahamu vizuri constitution yetu ina allow yote haya .... mtendaji mkuu wa wizara ni katibu mkuu na huyu ndie anayetakiwa kujua kila kitu ndani ya wizara kiutendaji kwa kusaidiwa na wakurugenzi wa kila idara ... waziri na naibu waziri ni viongozi wa kisiasa na hutakiwa kusimamia policy kulingana na ilani ya serikali iliyopo madarakani ... kwa katiba yetu ndio maana unaona mawaziri wanarushwa ovyo ovyo tu kwenye wizara mbali mbali ... wako wachache kama marehemu Mgimwa ndio alikua waziri stahiki wa wizara ya fedha kwa sababu alikua amesomea mambo hayo

shida ya tanzania ni system na mara nyingi sio viongozi waliopo .... system sio imara ndio maana inaruhusu hata viongozi wa ovyo kufanya madudu
 
Mkuu Sumley heshima yako mkuu.

Hili suala zima linaonyesha lilichezwa na baadhi ya watu kule TANROADS ambao ndio waliona hio pesa inanukia kupitia huo mradi.

Taarifa nilizo nazo kuhusu kumbukumbu za makampuni, Strada Internatinal ni kampuni iliosajiliwa Uingereza yenye namba 07546113 na ina ofisi zake maeneo Wilaya iitwayo Middlesex na anuani yake ya posta ni 170 Draycott Avenue, Kenton, Middlesex, HA3 0BZ UK.

Kampuni hii haina simu ya ofisi,tovuti, wala barua pepe na haina mtu maalumn kwa kuwasiliana nae, ingawa inaonyesha inafanya shughuli za ukandarasi.

Pia rekodi zinaonyesha kwamba kulikuwa na watu wawili ambao ndio wanaonekana ni waendeshaji wa kampuni ambao wanaitwa G. Burji na F. A. Malik, E.S. Isingo na B. Kahan ambae ni mwanamke ambao wote wa sasa wanaonekana wameondokana na kampuni hiyo(inawezekana baada ya kugawana ile pesa)

Pia kuna mshiriki mwngine anaetambulika kwa majina ya K.S. Mudan ambae taarifa hazisemi kama bado yupo au la.

Kwahio wa kuchambua hapa ni huyo bwana E.S.Isingo kwamba ni mtanzania au ni raia wa wapi.

Nafikiri haka kataarifa katafaa kwa Iasi Fulani kuchangia mada yetu.
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom