ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,060
- 49,748
Wote tunafahamu kwamba Vijijini ndiko kunafanyika shughuli za Kilimo na hivyo msimu wa mazao Barabara za huko Huwa busy sana.
Sasa Tarura eti wanajenga km 19.25 za lami Kwa Bilioni 9.86 sawa na wastani wa 500/Km. Hivi hizi lami za Tarura ni lami kweli au mzaha?
Mbona TanRoads wanajenga 1km/1.3-2.2bln kutegemeana na aina ya lami?
--
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Igwachanya - Itulahumba yenye urefu wa kilometa 19.25 itakayogharimu Sh. Bilioni 9.86 kwa kiwango cha lami kuanza kazi kwa wakati na kuikamilisha katika muda uliopangwa kwenye mkataba.
Dugange ametoa agizo hilo wakati akishuhudia makabidhiano ya mkataba baina ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na mkandarasi kampuni ya Summer Communication Ltd itakayoanza kujengwa Desemba, 5 mwaka huu katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.
Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Igwachanya na Itulahumba waliojitokeza katika tukio hilo, Dk. Dugange amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi hicho cha fedha na kumtaka mkandarasi huyo kuzingatia thamani ya fedha pamoja na kujengwa kwa kiwango bora kwa kuwa ni barabara muhimu itakayoifungua wilaya hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Claudia Kitta ametoa rai kwa mkandarasi wa mradi huo kutoa fursa ya ajira kwa wananchi wa eneo hilo badala ya kutoa ajira kwa wananchi wa maeneo ya mbali.
Naye, Meneja wa TARURA Wilaya ya Wanging'ombe, Boniface Kasambo amesema mradi huo utakamilika ndani ya miezi 20 na kukamilika kwake kutarahisisha usafiri kwa abiria na mazao, kuimarisha kipato cha wananchi pamoja na kuifungua Wilaya hiyo.
My Take
Hawa ndio wanasababisha Tanzania kuwa ya Mwisho Kwa Ubovu wa Barabara Duniani.
View: https://www.instagram.com/p/Cz6ojIUIOdK/?igshid=NmJiYWZiY2E0Mg==