Mkakati: Lowassa kuhamia UKAWA

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa waliofukua Uzi huu,bahati mbaya wengi wamebadili ID zao,ila baadhi waliobaki tumewajua walivyo wanafiki,ni heri ya DK Slaa aliyekomaa na msimamo wake maana huko nyuma Alikuwa akimpinga EL,ila leo Hii anashambuliwa na wasio na msimamo na wanafiki wakubwa.

Endeleeni kufukua nyuzi tujue rangi zao halisi hawa jamaa. Ila hatushangai sana kama safu yote ya uongozi wa CDM walimsema EL ni fisadi miaka kibao halafu wakamkubalia kumpa nafasi ya kugombea uraisi,ni dhahiri kuna biashara nzuri ilifanyika.

Kwa mwanaume yeyote ambaye ni kidume mwenye msimamo ilitakiwa uachane na siasa au uhamie upande wowote unaouona nafuu kwako. Badala yake wakashambuliwa waliopinga ujio wa EL na kuitwa wasaliti.

Kweli wanafiki ni wengi sana nchi hii.
 
Binafsi nafahamu wana-CHADEMA wawili hapa JF ambao hawajapata kuyumba ktk hili; kuna MTAZAMO na meningitis... anyway, I know wapo wengine lakini hao ndo nina uhakika nao! Hawa wengine; hamna kitu... wamejaa mayowe tu na ndio kuna cku nilishawahi kuwaambia hapa; hata cku JK huyu mnayemuita fisadi, cku akiingia CHADEMA, kila atakopita watampokea kwa shangwe na mashada ya maua! Unafiki ulioje!
 
Lowasa akija UKAWA mimi natoka , amechafuka , hana na wala hajawahi kuwa na fikra mpya , ndio maana hadi leo anaamini kwamba rushwa itampeleka ikulu .
Hivi bado uko Ukawa Mkuu?
Hii kitu ngumu kumeza.
 
hatutaki viongozi waliowahi kuliingizia taifa hasara ndo waje huku never on earth, labda awe mwanachama wa kawaida tu na sio kugombea nafasi yoyote ya uongozi vinginevyo arudi huko huko kwa chama chake cha mashetani
Haya sasa uliyemwita shetani ndo mkuu wa nyumba hivi sasa...
Una la kusema au ushaufyata?

Unavyosema "hatutaki" unamaanisha wewe na nani?
Unadhani maoni yako yana umuhimu ai uzito wowote huko kwa 'makamanda?'

Hivi huko 'chama cha demokrasia' kuna mwanachama yeyote aliyeulizwa katika kikao rasmi na kutoa maoni yake 'kidemokrasia?'

Taarifa kamili ni kuwa Lowassa alitambulishwa kwa kamati kuu (kuwa ndo boss mpya) usiku hotelini...

Hili game halitaki hasira hata kidogo ha ha ha.
 
Usikurupuke na kuandika jambo ambalo halipo, hebu weka ushahidi wa pale ambapo nilimeza maneno yangu. Lowassa kwangu mimi bado ni fisadi na hakustahili kukaribishwa CHADEMA.
Mkuu rudisha kisu alani.
 
Reactions: BAK
Mkuu hizo ni jazba sasa. Wacha dawa iingie kidogo kidogo. Utapona tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…